Son MAMOU BY TP OK JAZZ LWAMBO

April 12, 2012

Madilu;Olobaki nini eee eh= unasema nini eee eh, Olobaki nini Mamou eeeh= (unasema nini eeh Mammou), Olobaki ngai nafundaka yo na Mobali nayo= (unasema mimi nafauta mumeo), Olobaki ngai nasalaka kisefe na libala na bino=(unasema mimi huwa nafanya umbea katika ndoa yenu).                              

Lwambo;

Madilu tika ye aloba,loba,loba,loba makambo ye asalaka ayebaka te = (Madilu muache aseme aseme aseme mambo ayafanyayo hayafamu). Ba balabala ye atambolaka bato bamonaka ye = (Barabara/mitaa yote anayopita watu humuona). Na bandako ye akotaka ba plafond ya ndako efundaka ye  = (Na nyumba zote aingiazo dari za nyumba huwa zinashuhudia). Na bacoins nyoso ye atelemaka ba chauffer taxi bamonaka ye = (kila kona anayosimama madereva taxi humuona).  

 Bavedete ye akamataka banaimbwa bamonaka ye = (Kwenye kila meli anayoingia wavuvi humuona). Po yo nini apanza sango alobi yo osalaka kisefe = (kwa nini akufanyie kampeni ati unahatarisha ndoa yao). Ngai moto nakotelaka yo Mamouee = (Mimi ndio mtu nayekulinda Mamouee) Ngai moto nayebi basekele Mamou eeh=(Mimi ndio mtu nafamu siri Mamoueeh). Lelo nakomi moto mabe Mamoueeh = (Leo nimekua mtu mbaya Mamouee).  

Oyebi tango engindaka  Mamou eeh = (Fahamu wakati hubadilika Mamouee) Okokanisa ngai Mamou nakei yeyeye= (Utanikumbuka Mamou acha nijiondokee) . Ata ofingi ngai ndumba Mamoueeh= (Hata ukinitusi mimi malaya Mamou).                                                 

Lwambo Anaoongea;                                                                                                                                                   Oh Mamou, Kindumbu oyo oza kofinga ngai Mamou= (Eeh Mamou huu Umalaya unaonitukania Mamou).       Kindumbu eza mosala provisoire te Mamou=(Umalaya si kibarua cha muda, mamou).

Ngai pe nazalaka na libala nayebi pasi ya Libala= (Hata mimi nilishaolewa nazifahamu shida za ndoa).               Bongo, kindumba oyo oza kofinga ngai mamou =(Sasa,huu umalaya unakufanya unikashifu).                         

Omona ndumba abota bana te ?= (Ulishamuona malaya asiyezaa?)  Omona nanu ndumba amata te? = (Hujamuona malaya aliyefaulu kimaisha).                                                     

Omona nanu ndumba akoma esika ya gateau te? = (Hujawahi kuona malaya amekua mtu muhimu) Te Mamou na souhaiter te = (Hakika Mamou sijataka kuwa Malaya).                                                                     

Na yo pe mokolo ekoma osi okomi na esika oyo ya biso nakotuna yo = (Siku utakapokua malaya nitakuuliza).

Madilu;  &n bsp;         Eloko nini okolukaeeMamou eeehx2= (Kitu gani unachotaka/tafuta Mamoueeh)                                                 Signature osi ozua Mamoueeh = (Mamlaka ya kusaini hundi(cheque) umepewa mamou) Landa nzela ya libala Mamou= (Wajibika katika ndoa yako) Yango ekumisa yo na poto Mamou= (Umefika Ulaya kwa ajili ya Ndoa) Tika kokosa mobali na yo Mamou=(Acha kumdanganya mumeo) Soki atelephoner loba obimaka= (akikupigia simu mueleze huwa unatoka)                                                          

Lwambo; &n bsp;        Mamou yo moko oyebisai ngai mobali nayo atinda yo na poto okende kobokolo bana= (Mamou mwenyewe ulinieleza mumeo alikutuma ulaya ukalee watoto).  

                                                                                                 Mokolo mosusu soki ngungi esui yo = (siku moja mbu alikuuma)                                                                   Olobi mobali nayo atelephonaka yo 2x par jar = (Ulisema mumeo huwa anakupigia simu mara mbili kwa siku)   Kutu apesa yo na carnet ya cheque = (Hata kitabu cha benki amekupa)   

Mamou amona soki mobali naye atelephoner na yo =(Mamou akiona mumewe amempigia simu)                         Sourtout na minuit amoni likolo  ekiti = (Ikifika saa sita Usiku yeye huwa anao kuwa pamekucha)                     Akoti na salle de bain, atuti monzele, abimi na salon = (ataingia bafuni,atajisafisha,atarudi sebuleni)

Akamati kisi ya bangungi apomper,apomper =(Atachukua dawa ya mbu atapulizia ndani) Po tango akobima mwana wana ayeba te que mama azongi =(Atakapotoka na kurudi mtoto asifahamu) 

Akozonga pe lokola nyau, makolo nyamu nyamu = (atarudi kama Paka kwa kunyata) Papa pe kuna atilaki hoo du matin ekoki drrr,drrr = (inapotimu saa sita ya asubuhi anapiga simu drrr,drrr)       Allo nani wana ? Ngai mamou Oyo nayoki azakoloba kuna nani = (allo nani wangu mimi mamou ni nani nayemsikia akizungumza) 

Te ezaa radio radio tata =(Hiyo ni radio tu) Sala attention Mamou = (Tafadhali jihadhari Mamou) Vraiment batela personnalite na ngai kuna oza na poto = (kweli)                                                                                                                                                                                 


Wamkumbuka Bibisiya Mfwengi?

April 12, 2012

Anaitwa Bibiciya Mfwengi huyu aliwahi kuwika sana akiwa na MAison Mere akitokea kwa Mopao Mokonzy Koffi Charls Olomide, kwa sasa Bibisiya amerejea nyumbani kwa Mopao. Mwanadada huyu nakumbuka akiwa bado na Werason alipokuja Dar nilikuwepo kwenye ile show alifanya mambo balaa, naomba umuangalie hapa uone balaa lake.


Kanumba na Lulu waliitana Mopao na Cindy … unajua maana yake?

April 12, 2012

image

Ukifuatilia Tweet Page za Kanumba na Elizabeth Michael aka Lulu utaona kuwa walijaribu kutumia majina ya Mopao na Cindy labda kunogesha chat yao au katika kupoteza maboya wafuasi wao kwenye mtandao huo wa kijamii au labda kujifananisha na nguli ambaye Kanumba mwenyewe aliwahi kukiri kuwa anampenda sana Koffi Charles Olomide Mopao Sakonzy, huku Kanumba akimuita Lulu Cindy na Lulu akimuita Kanumba Mopao.

Kanumba alikuwa mpenzi mkubwa sana wa Bolingo na jina la Mopao ni jina la Koffi Olomide ambaye mashabiki wanamuita Mopao Mokonzi. Koffi amekuwa kwenye uhusiano wa kimapaenzi na muimbaji wake wa kike anayejulikana kwa jina la Cindy Le Coeur ambaye kwa sasa ndiye mke wake kipenzi. Koffi wakati akiaanza uhusiano na Cindy ilikuwa ni siri na iliandikwa sana kwenye vyombo vya habari lakini kila mara walipoulizwa walikana mpaka kwenye Birthday ya Cindy ndipo Koffi alipovunja ukimya na pale alipomzawadia gari aina ya Jaguar baba yake na Cindy (Gonga hapa kuisoma) na mpaka wa leo Cindy ambaye anakuja kwa kasi kwenye wanamuziki wa kike na amejizolea umaarufu kwa nyimbo zake za Koffi Chante Cindy ambapo amekuwa akizirudia nyimbo za taratibu za Koffi tangu enzi hizo.

Sasa baada ya kukueleza hayo soma Tweet za mwisho za Kanumba “Mopao” na Lulu “Cindy”.

image

image

image

Compilation ya Tweet hizi ni kwa hisani ya Shafi Dauda Blog.

Mamaa Cindy Olomide

Nimewachagulia wimbo huu hapo  ambao koffi olomide na cindy wake walimuimbia Mamaa EDITA OMARI BONGO au EDITA SASOU NGUESSO ambae alikua mke wa presidaa OMARI BONGO wa Gabon na pia alikua ni binti wa kumzaa wa Rais DENNIS SASOU NGUESSO wa CONGO BRAZAVILLE, huu ni wimbo wa majonzi baada ya kifo cha maman EDITA. Natumai kwa Post hii nitakuwa nimekujibu mdau wangu  Mkemimi, wa Kigoma ujiji. Shukrani sana kwa kuwa pamoja kipindi hiki cha majonzi.


%d bloggers like this: