SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – V

September 7, 2011

image

Baada ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo kwa misukomisuko, kisha tukaitazama kuzaliwa kwa Wenge Maison Mere ya Werrason, Didier Masela na Adolphe vile ilivyoanza pia. Tuliona jinsi bcbg ilivyoondoka na lundo la wanamuziki wa iliyokuwa wenge musica original na kuwaacha Werrason, Masela na Adolphe wakibaki peke yao labda na jina wenge musica, kazi ya kujipanga upya na kurudi kwa kishindo ikawa ngumu kwelikweli, Pia tuliona jinsi WMMM alivyojipanga na ku recruit wanamuziki wapya kama Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapaya

 

Mpaka hapo bendi ikawa imekamilika na kuanza mazoezi. Ikafanya official show yake ikiendelea kutumia jina la WENGE MUSICA BCBG 4X4, Lakini baadae wakaachana na neno BCBG kwa kuwa lililetwa na kuwa introduced hapo WENGE MUSICA original enzi hizi na Jb Mpiana, Badala yake wakaweka la kwao “MAISON MERE” hivyo ikawa sasa wao ni WENGE MUSICA lakini MAISON MERE sio tena BCBG. Wenge Maison Mere maana yake wakimaanisha Wenge yao ndio Wenge Mama au Wenge Makao makuu ikiwa na makao yake makuu ZAMBA PLAYA ndani ya Kinshasa.

Je hilo jina MAISON MERE lilibuniwa na nani? alikua ni Werrason? jibu hapana, alikua ni Didier Masela? jibu hapana, je alikua Tata Mobitch Adolphe Dominguez? jibu pia hapana. Ukweli ni kwamba jina Maison Mere lilibuniwa na kupendekezwa na Baby Ndombe! Hilo ndio jibu sahihi.

Tukiacha hilo la jina bendi ilianza Rais akiwa Adolphe Dominguez huku Werra de la Forre akiwa makamu wa rais na artistic director pia, Didier Masela akiwa Chef d’orchestre. Baadae  ya muda kidogo ikaonekana Werra ndio awe rais kutokana nadhani na mvuto wake kwa mashabiki ambao tayari walikwishaanza kumshindanisha na Jb Mpiana wa Bcbg. Wakati huo huo JAPONAIS ambae alijiunga akitokea kwa Jb mpiana akapewa cheo cha artistic director alichokuwa nacho Werra akiwa pia makamu wa rais wa bendi.Na maandalizi ya album yao ya kwanza ile FORCE INTERVENTION RAPIDE yakawa yamekamilika, wakairelease hiyo album huku dogo FERRE GOLA akipewa aimbe vocals za Jb Mpiana.

Hapa muhimu kukumbuka kwamba album ya TITANIC ya BCBG Kiukweli ilikua imetayarishwa kwa pamoja na iliyokuwa wenge musica original kwa maana ya kwamba pia kina werrason walishiriki maandalizi ya album hiyo na walishaifanyia mazoezi na pia kupiga show. Kama utatazama nakusikiliza vizuri video hiyo hapo chini ambayo ni moja kati ya live concert za mwisho mwisho za wenge musica original ikiwa pamoja utaweza kusikia mipigo iliyokuja kusikika kwenye titanic baadae, hapa ilichezwa na kina werrason ndani ya wenge original, ukisikiliza vizuri mwishoni mwishoni mwa hii video utausikia mpini ambao baadae ulikuja kusikika kwenye wimbo wa borkinafaso uitwao Serge Palmi unaopatikana kwenye album ya Titanic, hapa Burkinafaso alikuwa anawachezesha kina Werrason huo mpini wake wa solo ambao baadae waliucheza kina Jb kwenye titanic.

 

Kuibuka kwa Bill Clinton

Kwa hiyo kiufupi ni kwamba album ya titanic ilikua iwe album ya wenge musica original ikiifuatia pentagone ambayo ndio album ya mwisho ya wenge musica original kama kundi. Tukiachana na hayo, mwaka 1999 mwimbaji kijana Heritier Bondongo akajiunga na maison mere then wakafanya album yao ya pili wakiita SOLO LA BIEN ambayo kiukweli ilipata mafanikio makubwa sana sokoni huku ikimuibua pia BILL CLINTON na kumfanya awe kipenzi cha mashabiki katika ulimwengu wa wapenzi wa muziki wa Congo kutokana na kazi yake nzuri na style yake ya kipekee ya atalaku aliyokuja nayo ambayo naweza kusema ndio iliyomtoa Tutu Kaludji sokoni na style yake iliyokuwa imekamata sana kabla ya ujio wa BILL CLINTON na pia baada ya kung’atuka Roberto Ekokota kwenye muziki.

Album hiyo pia ikafungua milango kwa maison mere kuanza kupata mikataba minono ya kwenda kupiga shows ulaya ambako walifanikiwa kumrecruit mpiga guitar kiraka PATIENT KUSANGILA ambae kina werra walikua nae wenge musica original lakini alibaki kwa Jb baada ya mgawanyiko lakini baada ya muda mfupi akamtosa Jb baada ya concert ya bcbg kule zenith 1999 baada ya kupewa nafasi finyu ya kupiga guitar kwenye show hiyo kama tulivyoona huko nyuma katika mfululizo wa makala haya. Baada ya kuachana na JB kusangila alibaki Paris akiishi huko ndipo kina werra walipoenda na maison mere wakamkuta na kumshawishi ajiunge nao.

 

Mimiche amrithi Masela kwenye Bass Guitar

imageMambo yakaendelea, wakiendelea kupata kazi nyingi ndani na nje ya africa, badae wakiwa katika tour nyingine Canada CHRISTIAN MABANGA ambae alikua amerithi nafasi ya  DIDIER MASELA (aliyekua amejiondoa kundini baada ya tour ya ulaya) kama Chef d’orchestre akaugua ghafla ikabidi abaki Canada kwa matibabu zaidi, ndipo Ferre Gola akapewa nafasi hiyo, akawa Chef d’Orchestre na wakarelease album ya TERRAIN EZA MINE ikiwa ni album ya tatu ya kundi kabla ya album binafsi ya werrason, ile KIBUISA MPIPA. Baada ya Masela kuondoka kundini ikabidi waanze mpango wa kumsaka mrithi wake katika bass guitar, ndipo wakampata MIMICHE kutoka kwenye bendi ya PEPE KALLE 

 

Patient Kusangira ajitoa WMMM 

Then wakapata deal nyingine ya kusafiri kwenda kupiga paris, lakini kabla ya kuelekea paris walitakiwa kupitia  Congo Brazaville kwanza, wakiwa katika pilikapilika za maandalizi ya safari hiyo, ndipo KUSANGILA akaachana na Maison Mere kutokana na jina lake kuondolewa katika kikosi kitakachosafiri kuelekea Brazzaville na baadae Paris, kitendo ambacho kilionekana na wengi akiwemo Kusangila mwenyewe kama ni adhabu ya kisasi toka kwa werrason kutokana na ugomvi wao wa siku nyingi toka Wenge Musica original uliosababishwa na mwanamama mchezo show pekee wa wenge musica original kipindi hicho NANA SUKALI.

image

Ikumbukwe kuwa Werre alishawahi kufanya jaribio la kumfukuza Kusangila wenge original lakini Jb na viongozi wengine kundini hawakukubaliana na adhabu hiyo kali dhidi ya Kusangila kwa kuwa walikuwa wakifahamu kinachoendelea kati ya watatu hao kundini yani Werra, Kusangila na Nana Sukali, hivyo ikaonekana ni wivu wa kimapenzi tu na badala yake wakapendekeza asimamishwe tu na si kufukuzwa kabisa, hivyo kitendo hiki cha kuachwa katika safari ya ulaya bila ya sababu za msingi kikatafsiriwa na wanaojua historia ya wawili hawa werra na kusangila kama ni muendelezo tu wa ugomvi wao wa siku nyingi sababu ya mwana mama Nana sukali. Pia werra aliwahi kufanya jaribio la kumtimua Tutu Kaludji kwa kutomuheshimu yeye Werra kama kiongozi na badala yake kumheshimu zaidi Jb na Viongozi wengine kundini.

 

WMMM yafanya Show ya Bercy na Aimelia Lyase atambulishwa rasmi kwa mashabiki.

Baada ya kujiondoa Maison Mere Kusangila kwa msaada wa marafiki zake Sam Tshintu na Modogo akarudi zake Paris. Kwa upande wa bendi ya Maison Mere baada ya kumaliza kazi Brazaville wakachukua zao flight kuelekea Paris, na kupiga ndani ya BERCY Show yenye mafanikio makubwa sana na isiyosahaulika miongoni mwa wapenzi wa maison mere, watu walijaa kupita kiasi na ndipo Werra alipopachikwa jina la Le PHENOMENA na Pia ndio siku werra alipomtambulisha Aimelia Lyase Demingongo kama mwanamuziki mpya wa Maison Mere akitokea kwa mahasimu wao wakuu wenge bcbg.

 

Dominguez ajitoa WMMM

image

Pichani ni Dominguez alipiokuja nchini, hapa akibadilishana namba na Steven Kanumba wa Bongo Movie

Baadae mwaka 2001 “Big Tata” Adolphe Dominguez nae akajitoa, bendi sasa ikawa ya Werrason peke yake.Kwa upande mwingine   mwanamuziki “mtata” na mzee wa kuhamahama Ali Mbonda akatimka Maison Mere na kurudi bcbg na baadae mwishoni mwa 2001 akarudi tena Maison Mere, JAPONAIS nae akaondolewa kwenye nafasi kama Artistic Director, nafasi yake ikachukuliwa na fundi, mtaalam wa solo guitar na music arrangement kiujumla Flam Kapaya.

Next kuzaliwa kwa Le Marqius de Maison Mere, nini chanzo cha vijana kufanya uasi huo na kwa nini hawakufanikiwa licha ya kuanza kwa kishindo?, tutajua zaidi.

Natuma salamu kwa Bana Werason wote Mukulu Timothy Banda shukrani sana kwako kwa mchango wako kwenye blog hii, La Suvereign Maghambo, Mukubwa Chizenga, Muddy Saloon, Choki na Nelly nakati ya Kinondoni, Japhet Malya muzee wa Koffi na WMMM, Abdul Tall na wapenzi wote wa Werason.


TOUR EIFFEL; Utunzi wa “Mkaanga Chips” Titina Alcapone

April 15, 2011

Kuna wakati najaribu kuangaliaga mchango wa kila mwanamuziki ndani ya kundi zima la Wenge BCBG si mchezo. wimbo huu ulitungwa na Titina Alcapone ambaye alikuwa akipiga Ngoma na Chants kwa wenge BCBG, huyu bwana baadaye aliondoka Wenge BCBG baada ya  kutofautiana na kiongozi wake JB Mpiana na sasa anapiga muziki kivyake.

Titina alimuimba mpenzi wake kwenye wimbo huu, mpenzi ambaye alikuja kumuoa kwenye harusi ya kifahari (gonga hapa) na hasimu mkubwa wa JB mpiana wakati huo Koffi Charls Olomide ndio aliyekuwa Best Man wa Titina alcapone jambo ambalo pia JB Mpiana hakulifurahia. Titina alitoka kwa JB Mpiana na kujiunga na Koffi Olomide kabla ya kuamua kutoka solo.

Kwenye wimbo huu utawasikia watu kama Aimelia Lyese Doming’ong’o na sauti yake hasa kwenye chorus akiitikia. Pia napenda sana jinsi Afande Allain Mpela anavyopokezana na wenzie, Verse ya allain Mpela naipenda sana jaribu kumsikiliza kwenye 3:20 utaniambia.

Ndio maana tunaoijua Wenge ilikotoka tunalilia kama ingeweza siku moja kuungana. Tofauti kwa wanamuziki mara nyingi zinatumika kuwagombanisha wanamuziki lakini kwa wakati mwingine zinaweza kutumika kama chachu ya mafanikio.

Koffi Olomide akisalimiana na Wageni wengine waalikwa
Mwanamuziki kiongozi wa Wenge Musica BCBG JB Mpiana akiserebuka na Bi harusi Nene, mke wa Titina Alcapone siku ya harusi yao.
Meza ya wageni waalikwa anaonekana JB Mpiana, Alain Mpela (aliyevaa kiarabu), Dadé Mpoko, Papito Mbala, Thitsho Lembe
JB Mpiana na tajiri mtoto PDG Patrick Bolognia, aliyesimama nyuma yao suti nyeusi ni Titina Alcapone. Majina haya wengi wa wapenzi wa Lingala watakuwa wamezoea kuyasikia kwenye kila wimbo na leo kubahatika kuwaona katika picha hizi.

Kwa wanataka tafsiri ya wimbo huu wafatilie hapa chini:-

Na ye epai nayo oyamba nga Anne,Marie nanga nakokomisa botoli nanga, Mwana ya beaute Anne boyome Oyamba nga na esengo mama na Diana
                   
Nimekuja kwako Anne nipokee,nitajitahidi kufanikisha ndoto zangu, Anna msichana mwenye urembo, Nipokee kwa furaha.   
                                          
Ee bolinga ya bomoi bwa lobiko kotianga malasi,tobalana lelo yo na kati ya ndako ya nzambe
  
Mpenzi wa moyoni nipake manukato/marashi ili tuoane leo kanisani(ndani ya nyumba ya mungu)              

Banguna bayoki nkele lokola basambwe,Anne maria mwana mama sophia bolingo ekokola libala ya mamelo molongani na nga kitoko nayo ya Sirene
             
Maadui wasikie na wachukie, Anne maria mama Sophia Penzi liendelee kukua ndoa ya baraka Mpenzi wangu urembo wako ni wa nguva.  
                         

Blaise:
Anne maria annie ya mozele namela yo lokola mayi ya minuit sambo yosilisa nga masumu…..fiance na nga nakomi nasuka                                  
    
Anne maria, rafiki wa mozele Nitakuywa kama maji ya usiku saba uniondolee dhambi zote mungu wangu nimefikia kikomo  
                              
Yaleo mama  cherie nanga kanga motema na baye bainaka  yaka lelo yo pembeni nanga Nazua yo lokola sirene na nga                                    

Mama we Mpenzi wangu kaza moyo dhidi ya maadui njoo leo hii karibu yangu nikubebe kama nguva wangu 
                                                
Bolingo na nga yo okomi konyokolo ngai Motema nanga na pinzoli nga nakokufa Naye epai nayo nazali lokola fololo vraiment mwana mama kitoko nayo bijou ya talo                                            

Mpenzi wangu waanza kuninyanyasa moyo wangu nitakufa kwa kudondosha machozi, nimekuja kwako kama ua Hakika mpenzi urembo wako kama kama kito cha Thamani

Ata tokotikala biso mibale na Mokili tikala Adamu ngai Eva tobota bana                             

Hata tukibaka wawili hapa duniani endeleaa kuwa Adamu mimi niwe Eva tuzae watoto *(hapo kati pana kifaranza balaa sipapati vizuri) Japo imeanza na Lamentation eloba boye= Yaani biblia yasema hakuna kitachoweza kufanyika hakuna kitachowezekana

souverain mukulu,Malu Lubaka                              
Toyaka na Mokili oyo mama mamaa Basusu Babenz, basusu Makolo                     
                  
Tumekuja hapa duniani wengine wana Benz(Mercedes),wengine huenda kwa miguu.            

Rudia Chorus

Shukrani za kipekee kwa Le Beeceebeegeeque nambar one Mwambungu nakati ya Tunduma kwa mtohoo huu.

Salamu kwa BCBGEEQUE wote, Mama Flower kimya sana, Hadji Mukulu, Papaa Maendeka, Muzee ya Airport, Mukullu Julie Babaa na Aneth, Papaa Aaron Meneja Mukulu wa Bakulu ndenge nini Papaa?.

 


Wenge wametoka mbali jamani!

March 30, 2011

Wenge musica the university of music ilianza huku street mpaka kufikia anga za kimataifa,mnawakumbuka hawa? kina nani ,wako wapi  na wanafanya nini kwa sasa? itakua si vibaya kwa wanaojua tukikumbushana majina ya vijana hawa marafiki sana enzi hizo wakiwasha moto wa burudani na kulichemsha jiji la KIN na vitongoji vyake, tizameni video hii vizuri jamani…..watu wanatoka mbali…tumshukuru sana mungu leo tupo hapa ni kwa mapenzi yake,kesho hatujui tutakua wapi,hawa watu naamini wao wenyewe binafsi wanapoitizama video hii wanakua na furaha na pia huzuni.Pata Picha mwenyewe then toa comment yako.

Ukiangalia kwenye Video hii utamuona JB Mpiana, Allain Prince Makaba, Utamuona Engineer Blaise Bulla utamuona Patient Kusangira na wengineo wakongwe. ama kweli watu wanatoka mbali.


Wimbo(Nzembo)-Champion Kapangala

March 23, 2011

Wimbo(Nzembo)-Champion Kapangala , 

Mtunzi (composer)- JB Mpiana ,

Albam- Titanic

Bendi- Wengi BCBG    

 

Kama kawaida wiki hii nawaletea kibao Champion Kapangala ambacho kinapatikana kwenye Albam ya Titanic, Albam hii ilitungwa baada ya kundi la Wenge Musica kumeguka na walipohojiwa kipindi wamekuja nchini JB Mpiana alisema analifananisha kundi lake na wale walionusurika kwenye janga la kuzama kwa meli ya Titanic miaka kadhaa iliyopita. Kwani kumeguka kwa kundi hilo lilikuwa tukio la ghafla na ni janga kama Titanic.

Albam ilikuwa nzuri sana ukiisikiliza hii albamu utawasikia vyema miamba kama Allain Mpela, Aimelia, Tutu Caludji walivyotamba bila kumsahau mzee mzima JB Mpiana.

nisikunyime uhondo anza kudadavua yaliyomo ndani ya mashairi haya mwanana.

 

Yaka Champion po tobima lelo yo ee tolakisa na ba-banda aa ee tosi tolingani yee yango nasengi nayo yozala pene na ngai  tosimba bolingo ya seko na seko kapangala yoka aa nakoloba lisusu trop te po nayebi, e osi okola ozali na mayele ya bomoto kolula lula mabe bilula lula kolo.                                                                                    

Njoo Champion tutoke leo  na kwaonesha  mahasimu wetu namna tunavyopendana  ndio maana nakuomba uwe pembeni yangu  tupendane mpaka milele , Sikiliza kapangala siwezi kuongea sana tena sababu nafafahamu ya kuwa umeshakua na akili ya kiutu uzima (Kibinadamu) kupenda penda ni vibaya                 

Chorus x 2                                                                                                                                                             
Champion Kapangala , Azali kitoko belomme Teint Rose  Pale nga naluli ye se ye ooh se ye ooh                       

Champion Kapangala,  ni mvulana mzuri mwenye weupe  uliochanganywa na rangi ya pinki  nimemchagua yeye tu yeye tu.

 

JB: 

Pasi ya bolingo nakomona nani akozala ata temoin se motema na ngai moko mishonga yoka Denis Mutombo  Michel Osako…….

 Shida ya mapenzi nayoiona nani atakua shaidi najua ni roho yangu nzuri yenye Mishonga sikia Denis Mutombo   

 

Chorus:

Champion Kapangala , Azali kitoko belomme Teint Rose  Pale nga naluli ye se ye ooh se ye ooh                       

Champion Kapangala,  ni mvulana mzuri mwenye weupe  uliochanganywa na rangi ya pinki  nimemchagua yeye tu yeye tu.

                                                                                                                                               

Alain Mpela: 

Namituni na motema  na nga lulu Iyolo  tata wani tata wani Raymond Muludiki Shalai pamba Claude Pirens Gourverneur zindo Juju Mwanga Henry Magie                                                                                                        

Najiuliza moyoni mwangu  Ilulu Iyolo ,Baba yangu, Baba Yangu  Raymond muludiki, Shalai pamba,  Claude Pirens,   Gouverneur Zindo,Juju Mwanga, Henry Magie.                                                                                  

Aimelia;  Eloko Nzambe  apamboli na Mokili nani aboya nani abongola moyi ekoma butu nani achanger mungwa ekoma sucre ezali se yo tata nzambe moto okela Didier Ikoko , Ali Jabir , Annie Dembo,Jules Guyslain nga nalela Gina leleee.

 Nani atabadilisha kitu mwenyezi mungu alibariki hapa duniani nani atabadilisha mchana iwe usiku , nani atabadili chumvi iwe sukari  ni wewe mwenyezi mungu uliyeumba Didier Ikoko, Ali Jabir, Annie Dembo, Jules Guyslain mimi nampenda Gina Lele                                                                                                     

 

Chorus:

Champion Kapangala , Azali kitoko belomme Teint Rose  Pale nga naluli ye se ye ooh se ye ooh                       

Champion Kapangala,  ni mvulana mzuri mwenye weupe  uliochanganywa na rangi ya pinki  nimemchagua yeye tu yeye tu.

 

Wimbo huu umedadavuliwa na Msomaji wetu maarufu Shaibu Mwambungu. Ingawa kuna baadhi ya maneno yameachwa tunaomba anayeweza kutia nyama afanye hivyo. Ila hii ilikuwa Wenge.


Zadio Kongolo Shabiki nambari wani wa JB Mpiana na Wenge BCBG

December 23, 2008
Anaitwa Zadio Kongolo ukipenda muite ZK wengine humuita Sir Joe Kongolo, ni mfanyabiashara wa Kongo anayeishi Uingereza, Huyu ni mpenzi mkubwa wa JB Mpiana na Wenge BCBG kwa ujumla, ni maarufu kwa kutunza pesa, kwenye onyesho moja la JB alimtunza mwanzo hadi mwisho wa nyimbo (kwa nini asiimbwe!!!) kwenye kila onyesho la JB Mpiana Ulaya humkosi huyu bwana, kama anavyoonekana pichani alisafiri kwenda Belgium hii ilikuwa kwenye onyesho la JB Mpiana mwezi uliopita tarehe 3 May Bruxelles.
JB Mpiana humuimba karibia katika kila wimbo lazima atamtaja ni kama vile unavyosikia PDG Ndama, Abdul Tall Omary Tall, Andrew Traders wanavyotajwa kwenye nyimbo za nyumbani, lakini Zadio amekwenda mbali zaidi kwani kwenye Albamu ya JB Mpiana ambayo inatamba sasa ya “Quel est ton probleme” akimaanisha Nini Tatizo lako?. Jb amemtungia wimbo kabisa Zadio unaoitwa Zadio Kongolo – ZK.
Angalia na usikilize hapo chini, pia wimbo huu uwaburudishe wadau wangu PDG Mukubwa Ling’ande, Big Producer Magambo, Papaa Masabo, Mukulu Biloko Zadio wa Darisalama, Papaa Kasapila, Mukubwa Shabani, Ally Tandika – Tajiri mtoto, Batty William Mwafrica na wengine wengi, Mna nini bwanaaa.
Post hii ilikuwepo kwenye Spoti na Starehe ya awali na nimeiweka kwa maombi ya mdau Mwemtsi baada ya ubishi kati yao. hehehehe

%d bloggers like this: