Arsenal yagawana pointi na Wigan 2-2, Chelsea yaona mwezi

December 30, 2010

Arsenal imelazimishwa kwenda sare na Wigan ya magoli 2-2.

Wigan wakicheza nyumbani ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Arsenal kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Ben Watson katika dakika ya 18.

WatsonBen Watson

 

Arsenal walikuja juu ya kulisakama lango la Wigan na kuppata mabao mawili ya haraka haraka katika dakika za 39 na 44, kupitia Andrey Arshavin na Niklas Bendtner.

Wakiwa wanaelekea kupata ushindi wa pili mfululizo baada ya kuizaba Chelsea, Arsenal walijikuta wakienda sare baada la mlinzi wa Arsenal Sebastian Squillaci kujifunga, zikiwa zimesalia dakika tisa mpira kumalizika.

SquilacciSebastian Squilacci alijifunga

 

Kwingineko Chelsea ilizinduka na kupata ushindi wake wa kwanza baada ya michezo saba, kwa kuifunga Bolton bao 1-0.

Bao hilo pekee lilifungwa na Flourent Malouda katika dakika ya 61.

MaloudaFlourent Malouda

 

Liverpool nayo ilishindwa kutamba nyumbani baada ya kuchapwa bao 1-0 na Wolves ambao wako mkiani.

Bao hilo pekee lilifungwa na Stephen Ward katika dakika ya 56.

Liverpool ilishindwa kuonesha cheche zake licha ya nahodha Steven Gerrard kurejea uwanjani.

Wolves wamepata ushindi huo kwenye uwanja wa Anfiled ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 26.

LiverpoolLiverpool wamefungwa kwao

 

Ushindi wa Chelsea umeipeleka timu hiyo hadi na fasi ya nne, juu ya Tottenham. Arsenal imesalia katika nafasi ya tatu, huku Manchester City ikiwa nafasi ya pili na Manchester United katika nafasi ya kwanza, licha ya kuwa pointi sawa na City.

 


Jela kwa kushambulia wachezaji wa Togo

December 30, 2010

Na BBC Michezo

Mahakama moja nchini Angola imemhukumu kwenda jela miaka 24 mtuhumiwa wa shambulio la timu ya taifa ya soka ta Togo, mwezi Januari.

Cabinda

Cabinda, Eneo ambalo mauaji yalitokea

 

Mtuhumiwa huyo ni Joao Antonio Puati. Wakili wa mtuhumiwa huyo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa alikutwa na hatia ya kufanya “uasi kwa kutumia silaha”.

Basi lililokuwa limebeba timu hiyo, lilishambuliwa katika jimbo la Cabinda, wakati wachezaji hao wakielekea katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

JenezaJeneza la mmoja wa maafisa waliouawa wa Togo

 

Bw Puati alikana mashitaka hayo, na amekanusha kuhusiana na kundi la waasi ambalo lilidai kuhusika na shambulio hilo.

Mtu mwingine, Daniel Simbai, alifutiwa mashitaka kama hayo, yaliyokuwa yakimkabili.

Alikuwepo

Maafisa wawili wa Togo waliuawa, katika shambulio hilo lililodumu kwa nusu saa, ambalo kundi la waasi la Flec linadai kuhusika nalo.

“Joao Antonio Puati alikuwepo katika eneo la tukio, na uhusiano wake na Flec umeonekana wakati wa kesi,” amesema mwendesha mashitaka mkuu wa Cabinda, Antonio Nito, wakati akizungumza na AFP.

Mwandishi wa zamani wa BBC nchini Angola Louise Redvers amesema mawakili wa upande wa utetezi wamekata rufaa katika mahakama kuu.

CabindaEmmanuel Adebayor akipozwa na mchezaji mwenzake

 

Wamesema ushahidi wa uhusiano na kundi la Flec haukuoneshwa wakati kesi ikiendeshwa, bali ulitokana na taarifa za polisi zilizochukuliwa kutoka kwa Puati wakati akiwa kizuizini.

Wakili wa utetezi Arao Tempo ameiambia BBC kuwa mteja wake aliteswa wakati akiwa jela la kulazimishwa kukiri kuwa anahusiana na Flec.

Kisiasa

Amesema uamuzi wa kumhukumu Bw Puati ambaye ni raia wa Kongo-Brazzaville, na kumuachilia huru mtuhumiwa mwenzake ambaye ni raia wa Angola, ni wa kisiasa.

Amesema hukumu hiyo ni kupeleka ujumbe Kongo-Brazzaville, ambako waasi wengi na wafuasi wa Flec wanaishi na kufanya shughuli zao.

Gerezani

Wiki iliyopita, wanaharakati wanne wa haki za binaadam waliokamatwa kuhusiana na shambulio hilo la mwezi Januari, waliachiliwa huru kutoka gerezani.

Makundi ya haki za binnadam yameituhumu Angola kwa kutumia shambulio dhidi ya timu ya Togo, ili kuhalalisha msako dhidi ya wakosoaji wa serikali katika jimbo la Cabinda.

Flec imekuwa ikipigana kwa miongo mitatu kudai uhuru wa Cabinda, eneo ambalo linatenganishwa na Angola kwa kipande kidogo cha ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Licha ya eneo hilo kuwa na utajiri wa mafuta, ni moja ya maeneo masikini zaidi nchini Angola.

 


Fire burn New Year Countdown at Kijiji Beach Kigamboni

December 29, 2010

Mambo ya Kijiji


You want another Rap 2010? Wimbo wa Museven uliofunga mwaka kwa Top Ten

December 28, 2010

Mwaka 2010 unakwisha huku tukishuhudia wanamuziki wa Kizazi kipya wakipata mafanikio ya hali ya juu, huku wakionyesha kupiga hatua mbali zaidi ukilinganisha na muziki wa aina nyingine.

Pamoja na kupata mialiko ya shoo kadhaa za kimataifa nje ya Tanzania, na wengine kurekodi na wanamuziki wakubwa na wanaoheshimika duniani, safari ya muziki wa kizazi kipya imegusa hata maraisi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Huku Mh. Jakaya Kikwete akiwatumia wanamuziki hao kwenye kampeni zake pia alitoa ahadi kadhaa ili kuwawezesha wanamuziki hao kufikia malengo yao.

Nchini Uganda, ambapo uchaguzi wa urais unatarajiwa kufanyika mapema mwaka 2011, tayari muziki katika siasa umekwisha gonga vichwa vya habari.

Katika moja ya tamasha la chama chake cha NRM wasanii kadhaa maarufu kama vile Eddy Kenzo na GNL Zamba walipamba jukwaa.

Hata hivyo, katika kuzitaka kura za vijana, Rais Museveni mwenyewe amediriki kuimba.

“Hatuna budi kuezi utamaduni wetu” alisema Bw Museveni na kuongeza “tutunze mashairi yetu katika nyimbo zetu ili yasisahaulike. Tunayahitaji mashairi hayo”.

Mashairi

Mashairi anayozungumzia na aliyoyatumia ni ya nyimbo za kitamaduni alizokuwa akiimba wakati akiwa mdogo.

Mashairi hayo baadaye yalichukuliwa na watayarishaji wa muziki, yakachanganywa na midundo ya kisasa na wimbo kamili kutolewa unaojulikana kama ‘You want another rap?.

Wimbo huo umekuwa maarufu nchini Uganda, ukipigwa katika kumbi za starehe na hata kutumiwa kama mlio wa simu.

Katika uchaguzi wa Rwanda na Burundi ambao umefanyika mwaka 2010, muziki hata hivyo haukuwa na nafasi kubwa.

Je Kenya inayotarajia kufanya uchaguzi wake mwaka 2012, itafuata mkondo huohuo wa siasa kutumia muziki?

Ni jambo la kusubiri.

 


Ancelotti awataka Chelsea sasa waamke

December 28, 2010

Na BBC

Meneja wa Chelsea, Carlo Ancelotti, amewaambia wachezaji wake, hawana budi “kuamka” kabla matumaini yao ya kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England hayajayeyuka.

Carlo AncelottiCarlo Ancelotti

 

Chelsea walikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Arsenal na sasa wamecheza michezo sita ya ligi bila ushindi na wameporomoka hadi nafasi ya nne ya msimamo wa ligi.

Meneja huyo Mtaliano amesema: “Kuna machungu mengi kwa sababu kipindi kigumu bado kinaendelea kutung’ang’ania.”

“Tunapoteza nafasi yetu katika msimamo wa ligi. Hatuna budi kuamka haraka iwezekanavyo.”

Meneja huyo alizidi kueleza: “Nadhani tuna uwezo wa kurejea na kuutetea ubingwa wetu, lakini kamwe hayo hayawezekani kwa namna tunavyoceza sasa.”

“Hatutakiwi kuwaza juu ya ubingwa, tunachotakiwa ni kufikiria namna ya kujikwamua na hali hii. Tunahitajika kujiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Bolton na tujaribu kushinda.”

Ushindi wa mwisho kwa Chelsea msimu huu wa ligi, ilikuwa tarehe 10 mwezi wa Novemba dhidi ya Fulham lakini Ancelotti, aliyeiongoza klabu hiyo kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya England na Kombe la FA msimu uliopita, amepuuza kauli kwamba ajira yake imo mashakani.

Alipoulizwa ni kwa muda gani mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich, ataendelea kuwa mvumilivu, Ancelotti alijibu: “Sijui. Kwa vyovyote vile hatakuwa mwenye furaha wakati huu.”

 


Mpira si “kabila” ruksa kubadili timu … hahahahah

December 28, 2010

Arsenal yainyuka Chelsea 3-1

Arsenal imejikita katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya England baada ya kuizaba Chelsea 3-1.

Arsenal 

Fabregas aliandika bao la pili

 

Mabao kutoka kwa Alexander Song, Nahodha Cesc Fabregas na Theo Walcott ndio yalizamisha meli ya mabingwa hao watetezi.

Bao pekee la kufutia machozi kwa Chelsea lilifungwa na Branislav Ivanovic.

Arsenal sasa wamefikisha pointi 35, katika nafasi ya pili, huku Chelsea wakiendelea kusalia katika nafasi ya nne wakiwa wa pointi 31.


  Tumkumbuke Madiluu kidogo

  December 28, 2010

   

  Madiluu Mult System a.k.a. Le Gra Ninja akiwa katika Pozi

  Ni takriban miaka minne sasa toka Madiluu Mult System a.k.a. Le Gra Ninja ambae jina lake kamili la kuzaliwa ni Jean De Dieu Bilau atutoke hapa duniani,tarehe 11 mwezi wa 8 miaka minne iliyopita yani 2007,Kinshasa Congo Africa na Dunia nzima ilipatwa na simanzi kufuatia kifo cha mkongwe huyu ambae muziki wake ulipendwa sana na watu wa tabaka la juu na wanasiasa(viongozi)wa nchi karibu zote za Africa ya kati ambako madilu alikua akipata mialiko mingi ya kutumbuiza kwenye hafla mbalimbali za wakuu wa nchi hizo katika viwanja vya ikulu n.k.mfano hapa utamuona madilu akitoa burudani kwenye sherehe ya Rais wa Gabon wakati huo marehemuOmar Bongo katika makazi ya Rais huyo katika jiji la libreville, Pata uhondo kidogo toka kwa Madilu kwenye Tafrija hiyo Utaona jinsi madilu alivyokua juu anga hizo za wazito.

  Lakini si katika anga hizo tu kwamba jamaa alikua akikubalika lakini pia hata kwa wanamuziki wenzake wakiwamo wadogo zake katika game kina JB,KOFFI na wengine wa aina hiyo madilu alikua mtu wao mshauri wao na kuinganishi pia,naweza kusema mzee huyu alikua ni kama grisi kwenye gari,yani kila palipokua na msuguano madilu alitumika kuwalainisha mahasimu husika.Madilu alikua rafiki wa kila mwanamuziki wa congo,hakuna jukwaa la bendi asilopanda madilu,mfano hapa tunamuona Madiluu akiwa na Koffi Olomide

  Hapa tntamuona  Madiluu akiwa on stage na KOFFI, Utaona mzee mzima koffi akijaribu  “without success” kumchezesha Madiluu “mzee wa Rhumba” sebene la kisanola,binafsi hapo kitu kingine kilichonivutia ni suti kali kwa vigezo vyangu lakini aliyotandika Le Rambow du zaire Koffi Olomide.

  Mimi nimemkumbuka Madilu kidogo kwa style hii,wewe na wengine sijui.

  Merci Mingi Papaa.

  The Romantique – Beeceebeegeeque!!


  %d bloggers like this: