Aifora ya Linex; Melody, Ujumbe, Hisia vimekutana

October 31, 2012

Rafiki yangu Mngoya Ahmedi Juma Lukuta wa Kibanda Kicheba Kwa Semkope Muheza anasema Wali wa Nazi hauhitaji mboga yenye mbwembwe hahahahaha. hii ni misemo ya kiswahili ambayo inahitaji mtu atulie aweze kuelewa mtu anamaanisha nini.

Huyu bwana Linex mi namkubali sana ni mara chache sana kuniona mimi naweka post za Bongo Flava hapa ila kwa wanaojua muziki huu umepigwa kwenye mahadhi ya Afri Zook/Pop na utasikia Solo Gitaa linauongoza huu muziki kwa mbaali.

Linex ni mwanamuziki ambaye mi napenda kwa sauti yake tuu na jinsi anavyoipangilia na kuimba kwa hisia, kijana ametulia sana na anajua ni nini anakifanya ili kuwaridhisha mashabiki wake, kiukweli kijana anatunga sana na anajua kuifikia hadhira, hata kwenye live show stage performance yake sio mbaya “ Imbeni nyimbo zote mnazozijua, lakini najua. kimoyo moyo najua mnakiri kwamba mpaka sasa, Aifora kutoka kwa Linex ndio wimbo bora wa mapenzi kwa kipindi chote hiki cha kufunga mwaka, Nibishieni maana hamkawii….” anasema Henry Mdimu muandishi na mchambuzi makini wa muziki wa Bongo Flava na Habari za burudani wa gazeti la Mwana Spoti. Mdimu anahaki ya kusema hivyo jaribu kuuusikiliza huuu wimbo, ujumbe, melody na sauti kisha niambie mawazo yako.


Fally Alivyopagawisha mashabiki Dubai

October 31, 2012

 

Katika wanamuziki vijana waliotoka Solo na Kufanikiwa mmoja wapo ni huyu Fally Ipupa ambaye amezidi kujizolea umaarufu sio tu Congo ama kwa nchi zinazozungumza Kifaransa bali dunia nzima achilia mbali Africa ya Mashariki ambapo anasemwa kupendwa mnoo.

Fally alikuwa ziarani huko Falme za Kiarabu na hapa ni pale alipopiga kwenye kumbi moja huko Dubai. Fally ambaye alisema anataka kuuingiza muziki wa Congo kwenye soko la Muziki wa Marekani anasema kuwa ipo siku dhamira yake itafanikiwa na muziki huo wa Congo utakubalika na kushika huko America.

Fally alifanya show ambayo ilihudhuriwa na vijana wengi wa Kiafrica wanaoishi na kufanya shughuli zao Dubai alikonga nyoyo za mashabiki wake pale alipopiga nyimbo zake non stop na kufanya club kuwa ndogo. habari zinasema kila mara mashabiki walivamia jukwaa na kuanza kucheza naye na ilibidi mabaunsa wafanye kazi ya ziada kuteremsha munkari wa mashabiki hao lukuki waliokuwa wakimshangilia kila mara.

Fally akiwa amevaa Kanzu akiwa madukani akifanya shopping kabla ya kuendelea na safari yake hivi karibuni.


Breaking News: JB Mpiana Kutua Dar Es Salaam November.

October 31, 2012

JB Mpiana akiwajibika Stejini jijini Dar Es Salaam mwaka juzi. Miwani aliyovaa alizawadiwa na Spoti na Starehe.

 

Mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo JB Mpiana anatazamiwa kuanza ziara ya Afrika ya Mashariki hivi karibuni ziara ambayo itampeleka Kenya, Tanzania na baadaye Zambia.

Kwa mujibu wa habari za ndani JB Mpiana anatazamiwa kuanza ziara yake tarehe 15 November 2012 na baadaye kutimua vumbi jijini Dar Es Saalm katika show moja kabla ya kwenda Lusaka Zambia ambako pia atakuwa na show moja. Hii ni mara ya kwanza kwa JB Mpiana kutoka nje ya Congo takribani miezi 15 akiwa anafanya sho zake ndani ya Congo na kwenye kiota chao cha Crystal Club katikati ya Jiji la Kinshasa mtaa wa June 30.

Pichani Mashabiki wakifatilia show ya JB Blue Pearl, Je atazikonga tena nyoyo??

Bado haijajulikana nani ana ratibu lakini kwa mujibu wa vyanzo nchini Congo ziara hiyo imeshakamilika mipango yote ya awali, usikose kutembelea ukurasa huu kujua zaidi.

Majuzi JB Mpiana alikuwa kwenye ufukwe pekee maarufu wa Mayi ya Pembe ambao unapatikana hukohuko katika viunga vya Kin na tarehe nne ana show ya kuaga mashabiki wake itakayo fanyika Hotel Venus hukohuko Kinshasa.

Mara ya mwisho JB Mpiana aliletwa jijini Dar Es Salaam 2010 kwenye show iliyo ratibiwa na Club E na kutumbuiza pale Ubungo Plaza, ile ilikuwa Le Classico Show ambapo JB Mpiana alitumbuiza pamoja na Tshala Muana na Meje 30 mwanadada ambaye amelelewa na Tshala Muana kimuziki na anasemwa kuiga hadi vituko vya jukwaani vya mwanamuziki Tshala Muana.

Gonga hapa kuona picha za show ya Blue Pearl


Exclusive: Grace Matata hatimaye amtoa mwanaye Hadharani

October 31, 2012

394998

Bi Dada Grace Matata ambaye alitamba na Single yake ya Free Soul baada ya kimya cha muda amemuweka wazi mwananye. Grace ambaye anajulikana kwa kuishi “Low Profile” alijifungua hivi karibuni na alijifungua salama, Tunamtakia ulezi mwema na karibu tena kwenye ulimwengu wa Burudani tunategemea ukirudi utarudi kivingine maana mashabiki wanakumiss.


Adjani na Fabregas waomba kurejea kwa Werasson

October 31, 2012

 

Tangazo lililotoka mwezi wa February likionyesha kuwa Albamu ya Fabregas ingeingia sokoni siku ya wapendanao Feb 14

Wanamuziki waliowahi kuwika na kundi la WMMM Adjani na Fabregas wameripotiwa kutaka kurejea kwenye kundi lao la zamani la WMMM.

habari ambazo zimethibitishwa na mmoja wa mameneja wa WMMM Ibrahim Monca Monib zinasema kuwa maombi yao yamepokelewa na uongozi lakini bado hawajui wanamuziki wengine na mashabiki watapokeaje “tunaliacha mikononi mwa wanabendi wengine na mashabiki ili waamue kuhusu kurejea kwao ama la…” alisema Monib alipoongea na Digital Congo.

Fabregas aliripotiwa kuondoka kwenye bendi miezi kadhaa iliyopita na kuamua kuwa solo artist ambapo alijipanga pande za Matete na kuanzisha bendi yake na kutoanyimbo kadhaa ambayo inasemwa haijapokelewa vizuri sokoni, sio rahisi kukubalika kwenye soko la Congo inategemea na umahiri na mashabiki utakaopata hasa kwa nyimbo kusikika ikipigwa sana redioni, na ndio maana wanamuziki wengi ambao waliwika na bendi hizi kubwa kama Aimelia, Allain Mpella, na wengineo wameshindwa kufanya vizuri huko nje.

Kwa mwanamuziki kama Fabregas ambaye miaka ya karibuni alianza kujenga jina lake ilikuwa mapema sana kuondoka kwenye WMMM.


Msikilize JB Mpiana anavyomlalamikia tajiri kwenye Bolognia ya SOYONS SERIEUX Album

October 30, 2012

Mabanga ni mtindo maarufu sana kwenye muziki wa Congo ambapo mtu mmoja anajitoa na kutoa pesa ili aimbwe kwenye wimbo lakini kwa Sasa nyimbo nyingi zimekuwa ni Mabanga tuu ambapo unakuta wimbo mzima kuanzia jina mpaka wimbo wenyewe unamhusu mtu, mfano ni huu wimbo wa Bolognia ambapo JB Mpiana amemuimba Pendejee na rafiki yake mkubwa Patrick Bolognia ambaye pia amemuoa Marie Olive Kabila ndugu kabisa wa Rais Kabila.

Bolognia ni tajiri na mwaka jana kwenye uchaguzi wa Congo DRC aliwahi kupata kashfa ya kuwanyamazisha wapinzani kwa kuwapa mlungula ili kumpa support Rais Kabila ambapo inasemekana aliahidi kutoa mlungula wa Euro 3000 kwa operation iliyoitwa Kabila Out au “Kabila Dégage !” ambao ni mkakati ulioandaliwa ili kumuondoa Rais Kabila madarakani kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka  jana.

Huyu bwana amekuwa karibu na mwanamuziki JB Mpiana kwa kitambo na JB amekuwa akimuimba sana, katika wimbo huu Bolognia JB Mpiana kuna mahali anasikika anasema “Kama namuamini na kumuogopa Yesu Masia na sijawahi kumuona iweje nishindwe kukuabudu na kukupenda wewe ninayekuona kwa macho yangu, Kama Namuomba Mungu na ananisaidia na sijamuona iweje wewe ninayekuomba na unanisaidia na nisikupende…” yote hii ni katika kuonyesha ni jinsi gani jamaa anamuabudu huyu Mshkaji.


SG ELIOT MONDOBE Katibu Mkuu wa WMMM aliyekimbilia Canada.

October 17, 2012

Tatizo kubwa la Radio Station Zetu ni kupiga muziki wanaoujua tuu na nyimbo nyingine hazipigwi au hazipewi Air Time ya Kutosha. Hii inafanya nyinmbo nyingi kutojulikana kwa wapenzi wa muziki labda kwetu sisi wadadisi ambao tunanunua albamu na kuto forward nyimbo mwanzo mwisho.

Werasson aliondoka Wenge BCBG baada ya mzozo wa pesa na uongozi baina yake na JB Mpiana, alipoondoka alikwenda kuanzisha WMMM na vijana wake akatafuta vijana akawatengeneza wakaiva hatimaye WMMM ikatisha balaa.

SG Eliot Mandobe ambaye alijulikana kama Secretary General, au Le Secrétaire Général de l’orchestre alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na kukubalika ndani ya kundi la WMMM. Lakini kizuri hakidumu jamaa alikimbia bendi kwa kashfa ya Human Trafficking na kukimbilia Canada hasa baada ya Show ya Zamba Playa ambapo alisemwa kuwa alikimbia akiwa na maelfu ya dola ambazo alikusanya toka kwa watu ambao aliwaahidi kuwatafutia VISA ya kwenda Ulaya, Canada na Marekani kupitia mgongo wa bendi.

Suala la Human Trafficking liliwahi kumgarimu Shumbu Wemba Dio Papaa Wemba Miezi kadhaa jela huko Ufaransa na Fellix Wazekwa aliwahi kutandikwa miezi kumi gerezani huko Braxelles kwa kosa kama hilo ambapo kuna wakati VISA za wanamuziki wa Congo zilisumbua kwani Tshengeni iliamua kupitia upya maombi yoote ya VISA toka kwa wanamuziki wa CONGO. Mandobe baadaye alijiunga na familia yake ikiwa ni mke na watoto ambao walitangulia kuishi huko, Nakuacha na kibao hiki ambacho utamuona vizuri Mandobe akikamua akiwa na Tata Mukulu Werrason Ngiama Makanda ndani ya Wenge Musica Maison Merre.

Big up kwa ma people Bahati Nyakiraria wa 90.2 Moshi FM mtangazaji wa kipindi cha Tamba Africa kiukweli napenda sana mpangilio wa vipindi vyako fanyeni mpango wa kwenda Online watu wengi waweze kuwasikiliza, Mercy Mingi Papaa.

p


%d bloggers like this: