“Mayi ya Pembe” Beach maarufu yenye historia kwa wanamuziki wa Congo

April 9, 2014

Huwa nawatania marafiki zangu wa Congo laiti kama wangekuwa na Beach kama tu za kwetu sijui ingekuwaje maana hiyo Planet Sono Beach (Mayi ya Pembe) ni sehemu tu maji yametuama pembezoni mwa mto, ni eneo liko nje kidogo ya mji wa Kinshasa kama unaelekea Airport kwa wanaoijua Kinshasa, Ukiangalia haina chochote cha kuvutia ila vurugu zake ni balaa kila mwanamuziki mkubwa ameshapiga huko na sio mara moja. mara nyingi show zao huanza mchana watu wakila na kunywa na kuendelea mpaka lyamba.

Hii ni show ya JB Mpiana akiwa na Wenge BCBG huko Planet Sono Beach Mayi ya Pembe. matamasha mengi ya wanamuziki wa Congo hufanywa hapa yakiandaliwa na kudhaminiwa na makampuni makubwa ya vinywaji kama Primus ambao ni wadhamini wa JB Mpiana, Skol ambao ni wadhamini wa muda mrefu wa Koffi, Tigo na wengineo.

Ni show ambazo zinatia raha kuangalia kwani kuna kuwa na kila aina ya shamrashamra na watu wanajiachia sana kwani hakuna kiatu kirefu (mchuchumio) wala kuogopa kutoka jasho, wengi wa washabiki huwa wamevaa beach wear au smart casual tuu kwani wako beach.


Sultan De Bruneil Kaskinto wimbo wa JB Mpiana ulisababisha mtafaruku Brunei

November 23, 2011

Wimbo wake JB Mpiana- Sultan De Bruneil Kaskinto ilikuwa kwenye albamu ya Tojou Humble au TH, ikiwa ni majibu kwa mwanamuziki Werason alipotoa Albamu ya Solola Bien akimwambia JB Mpiana sema tena na JB akamjibu mi ni mnyenyekevu daima.

Katika Wimbo huu ambapo JB alitaka kujifananisha na Mfalme wa Brunei na kuwapa shavu baadhi ya washabiki wake huko Nchini Brunei hali haikuwa hivyo kwani ni mwaka jana tuu wananchi waliandamana na kutumia picha za wimbo huo kwa kile walichotafsiri wao ni muonekano wa familia ya kifalme kwani familia ya Kifalme inalaumiwa kwa kuponda starehe na kutumia mamilion ya dola za walipa kodi kwa ajili ya maisha yao binafsi, hasa mtoto wa kiume wa mfalme huyo ambaye anajulikana kwa kuponda maraha na mkali wa wanawake jambo ambalo ni kinyume kwa wananchi wa nchi hiyo ambao wengi wao ni wadini.

Awali akiongea nami kwa njia ya email mmoliki wa blog ya Papar Demokrasi (asubuhi ya Demokrasia) Saifudin Alhadawi alitaka nimwambie maana ya wimbo huu. “Ni mfalme wetu, hatujui mnasema nini juu yake, mbona kuna wanawake wanacheza nusu uchi? ilihoji sehemu ya email hiyo ndefu iliyoandikwa kwa Kiingereza na Bahasa Malayu ambayo ni lugha inatumika huko.

Baada ya kupitia Blog ile nikaona picha za maandamano ambazo nilizichapisha kwenye Blog yangu ya kwanza ambayo ilifungwa na Google pamoja na akaunti yangu ya Youtube.

Baada ya kutafuta maana ya wimbo ule na kuwasiliana na Saifudin akaniambia Blog yake haiko hewani ila tafsiri ile waliitumia kwenye gazeti la Borneo Bulletin.

Akijibu kupitia kwa webmaster wake Guy Guy Mpeye, JB alinijibu kuwa hakuwa na leo hilo kabisa kwani yeye alifananisha maisha ambayo mfalme wa Brunei anaishi na huku ikifahamika kuwa Brunei wananchi wake wanaishi kwa raha kwa sababu ya hazina ya mafuta iliyo nayo.

Leo nakuletea tafsiri ya Wimbo huo kama ilivyokokotolewa na Wenge BCBG die hard member Mwambungu nakati ya Tunduma.

Wimbo: Sultan De Bruneil

Mtunzi: JB M’piana

Album: TH

Bendi: Wenge BCBG

Yela no nga bolingo nayo

Oyo ezali lokola mbuma

Elengi Oyo ezanga mokuwa

Lokola mbinzo oyo etonda

Saveur Le sultan de Bruneil

Ooh Kas Kaskito mobali ya

Malonga.

Unipe mapenzi yako laini kama tunda

tamu lisilo na mfupa kama jongoo

aliyezidishwa ladha jina lake Sultan

wa Brunei Kas Kaskito mwanamume

mtanashati

Mokolo Kaskito abengaki ngai

il faut omona presence ya Kaskin

teint d’ ebene, sourire eclatant na

ba frime mobali ya solo jeune homme

a` louer Aaah jeune homme elegant

Siku kaskito aliniita mara ya kwanza

muonekano wake ulikua wa pekee

rangi ya ngozi yake mti wa mpingo

tabasamu inayovutia pia

mwanamume mwenye maringo

Ba proposition nyonso basalaki ngai

pe ya sango oo peau elegant na

carisme ya ba amoureux ee

Maombi mapenzi niliyopewa na

na Kaskin Kaskito mobali ya tembe

Kaskin Kaskito mwanaume

mwenye sifa nyingi na mvuto wa

mapenzi.

Po ba professeur bayebisaki

Ngai soki mokolo abengi yo il

Faut otelema

IL faut oyoka nano, tango

Mosusu okotinda yo, il se

Peut ako kabela yo

Po mwana etinda akufaka

nzala te eloba bakulutu uu

Maman.

Walimu walinifahamisha kama

ukiitwa na mtu mzima inabidi

kusimama inatakiwa kumsikiliza

kwanza wakati mwingine anaweza

akakutuma au akakupa zawadi

kwamba mtoto anayekubali

kutumwa hawezi kufa njaa

mababu walisema.

Eeeh aaah toi c’est moi, moi

c’est ton remede d’amour (2x)

Eeeh aaah wewe ndio mimi, mimi

ndio dawa yako ya mapenzi

Chorus:

Ba banda bolingo batika

Miso etondaka te nakolula

eluli ye, iya olele

Eluli kaskito iya olele

Bolingo kwitikwiti imaole

Iya olele

Bolingo kwitikwiti imaole

Iya olele (2x)

Kwitikwiti kwitikwiti

Walioanza kupenda hawajachoka

Kolinga teo, iya olele

kupenda, iya olele

Macho hayachoki kupenda

yamechagua, iya olele

Yamemchagua Kaskito, iya olele

Mapenzi ni ulevi imaole iya olele

Mapenzi ni ulevi imaole iya olele

ulevi ulevi

Shai Ngenge

Que je me pende Lisette

Menga pour te prouver

que je t’aime

Wawa Mbula, Lucien Katanga

Hugue Mazomba

Que je me plonge dans le feu

Pour te prouver que je t’aime

Sabena Wanani, Didi Ongwari

Kijokolo

Nijiue Lisette Menga ili uamini ya

kama nakupenda

Wawa Mbula, Lucien Katanga

Hugue Mazomba

Nijitupe motoni ili uamini ya kama

nakupenda

Sabena Wanani, Didi Ongwari

Kijokolo

JB M’piana

Non non non non moi je t’aime

Oh Mimi Kas, Papy Kas I love you

Pusana pembeni nga natala kitoko

nayo

Papa leki Carly moi je t’aime oh seka

moke nga natala nzela ya mino nayo

aa aa aa aa koloba na moto te

RPT Chorus

kweli kweli mimi nakupenda

mimi Kas, Papy Kas nawapendeni

sogea karibu nione uzuri wako

Baba mdogo Carly mimi nakupenda

cheka kidogo nione mwanya

wako aa aa aa usimwambie mtu yeyote


JB Mpiana na Werrason Ngiama ndani ya Congo Rhumba; Nani zaidi?

September 7, 2011

JB Mpiana na Werra

Werrason na JB katika Video zao mpya.

Na The Romantic

Hapa leo tuna video za nyimbo mbili za mafahali wawili, Ya kwanza ni video ya wimbo Bologna ambao Jb amemtungia rafiki yake aitwae Patric Bologna, wimbo huu upo kwenye album mpya ya Jb na Bcbg iitwayo Sayons Serieux ambayo imeingia sokoni na video ya pili ni wimbo Likambo wa werrason ambao unapatikana kwenye album yake mpya Malewa Part 2.

Kitu kizuri hapa ni kwamba wote wamezipiga nyimbo hizo katika mtindo wa taratibu wa  Congo rhumba ambazo mara nyingi ndio zimekua anga za Jb, Werra this time kasema hapana na mimi nitafanya Congo Rhumba ili wale wanaosema siwezi waone, Kama kawaida mdau kazi yako hapo ni rahisi tu, zitazame  hizo video na toa maoni yako. Mimi binafsi ni mpenzi wa sports cars, hayo magari waliyotumia hawa waungwana wawili sio siri nimeyakubali,vjapo siwezi kusema la nani ndio limenikuna zaidi lakini lipo moja nimelipenda zaidi, kwa sasa na reseve comments zangu kidogo.

Bologna ya JB Mpiana

 

Mzee mzima Igwe katika album yake mpya akaja na kitu hii hapa

Likambo ya Werrason in Congo Rhumba

SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE (Sehemu ya II)

August 31, 2011

Majuzi tuliona jinsi Wenge kuanzia Mwanzo ilivyoaanza mpaka ilipofikia kumeguka kwa JB Mpiana na Werason (Kama uliikosa bofya hapa), Leo hii tunaanza kuiangalai Wenge BCBG ya JB Mpiana. Endelea…

Shukrani za kipekee kwa Hadji Le Jbnique kwa kukokotoa na kutohoa habari hii mpaka leo unaisoma wewe, Respect Grand Rapids nakati ya USA.

image

Adolph Dominguez, Blaise Bulla, Werrason, Didie Masela na Allain Makaba

walikuja kushtuka na kugundua Kina werra hawako nao tena wenge ilipopata contract kwa jitihada za SIPE kwenda kutumbuiza Ulaya Katika ukumbi wa BATACLAN,Paris na wakati huo huo kuitumia nafasi hiyo kwenye kufanya album ya TITANIC huko huko Paris

Wenge BCBG ilizaliwa JB Mpiana akiwa kiongozi wa bendi,Blaize Bula akiwa Chef d’orchestre,Alain “Prince” Makaba akiwa artistic Director na SIMON SIPE akiwa producer. Waimbaji wakiwa JB mwenyewe, Alain Mpela, Aimelia Lyase Demingongo na Blaize Bula, wapiga guitar Alain Makaba,Burkinafaso Mbokalia na Japonais(solo & rhythm),Patient Kusangila(rhythm & Bass), Titina(Drums), Ali Mbonda, Seguin Mignon(Tumba), Theo Bidens (keyboard), na Powerful AtalakUs toka kwao Roberto Ekokota “Le Grand Chibuta na Tutu Caluggi.

image

Kundi la Wenge Musica BCBG 1987, Kwenye Mic ni Werrason na JB Mpiana, Picha na Wikipedia

Mwanzoni wanamuziki wengi wa kawaida kundini humo akiwemo Alain Mpela ambae amekiri walikua hawajui kinachoendelea walikua wakidhani bado ni wenge musica ileile moja kwa kuwa mpaka nyimbo za album ya TITANIC walizifanyia mazoezi pamoja (nadhani ndio maana hata tukisikiliza kwa makini TITANIC na FORCE INTERVENTION RAPIDE zinavyoanza ni kama zinafanana)na kwa wenge walivyokuwa wanafanya kazi,ilikua ni kawaida kwao wakati mwingine kupiga show hasa local wakiwa hawajakamilika wote,sometimes wanaweza kuwepo wote akamiss labda makaba na blaize bula au hao wakawepo akamiss werrason, au wote wakawepo akamiss JB,

Hivyo basi kitendo cha werra,adolphe na didier masela hakikuwashangaza na kuwafanya wahisi labda kuna mgawanyiko wa bendi tayari,wakajua ni utamaduni wa wenge wa kawaida si unajua mastaa wakiwa kundi moja tena,japo walikua wanajua mitafaruku imekuwa ikiendelea mara kwa mara katika maisha ya wenge lakini si yakufikia kuzigawa bendi.

Lakini walikuja kushtuka na kugundua Kina werra hawako nao tena wenge ilipopata contract kwa jitihada za SIPE kwenda kutumbuiza Ulaya Katika ukumbi wa BATACLAN,Paris na wakati huo huo kuitumia nafasi hiyo kwenye kufanya album ya TITANIC huko huko Paris.,ndipo katika hali isiyo ya kawaida wakiwa na katika maandalizi ya ziara hiyo ambayo hupewa kipaumbele sana na wanamuziki wa congo wakawa wanashangaa mbona jamaa hawaonekani hata mazoezini wakati kuna safari nzito kama hiyo!na ilikua ni katika kipandi hicho hicho pia ambapo Ali Mbonda akaingia kwenye historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza kuitosa bendi mpya ya WENGE BCBG kwenda kwa kina WERRASON baada ya jina lake kutokuwemo kwenye trip nyeti kama hiyo huku jina la msaidizi wake chipukizi wakati huo katika kupiga mbonda (tumba) Seguin Mignon likichukua nafasi yake(Seguin sasa hivi ndio mpiga drums namba moja wa BCBG).

Kwa hiyo hiyo ndio ikawa safari yao ya kwanza ulaya bila kina werrason,wakapiga show hiyo hapo chini kama wanavyoonekana huku wakihitajika kutoa maelezo ya kina kwa mashabiki kuwaeleza kilichotokea huko nyumbani Kinshasa na kupelekea kujiweka pembeni na wenzao(werra,adolphe na masela),Ekokota yupo kundini hapo anaonekana akifanya kazi na Tutu Caludji “no.1”.

na

Baada ya Ali Mbonda kujiondoa kundini baada ya kukerwa na kutojumuishwa kwenye safari ya ulaya jambo ambalo limekua la kawaida mno kwa Ali na wanamuziki wengi offcourse wa congo wanapokosa kuwemo kwenye tour za Ulaya,Mtu wa pili kujiondoa BCBG akawa ROBERTO EKOKOTA mara baada ya concert hiyo ya BATACLAN hapo juu aliamua kupumzika kutokana na matatizo ya kiafya hali iliyomfanya ashindwe hata kuweka Atalaku zake kwenye album ya TITANIC na kumuacha Tutu Caludji amalize kila kitu mwenyewe,ndio vile tunaisikia TITANIC mpaka leo,pale ni bila le Grand Chibuta Ekokota,angeshiriki sijui ingekuwaje,mi sijui tuwaachie wenyewe!.

Baada ya kumaliza recording ya TITANIC walirejea nyumbani congo wakimuacha Alain Makaba huko ulaya kwake ambako alishakua amehamia. Walipofika Congo wakawakuta kina werrason ndio wameshaitengeneza bendi yao wanajiandaa Force Intervention Rapide(Lakini walikua bado hawajaipa hilo jina, maana nalo lina hadithi yake halikuja tu kama mvua),Baada ya mapumziko mafupi ya safari ya ulaya kazi ikaanza kwa Chef d’Orchestre Blaize Bulla Kuanza kutafuta vijana wa kuwa recruit. Hapa walihitaji mpiga bass yani pure bassist atakaeziba pengo la Didier Masela badala ya kumtegemea Patien Kusangila ambae kiasili alikua ni mtu wa rhythm guitar,pia walihitaji atalaku ataeziba pengo la Ekokota,kwa upande wa bass Blaize Bulla akaanza kumchokonoa Koffi kwa kuvamia ngome yake na kufanikiwa kumshawishi Sunda Bass ambae hata hivyo hakua na nafasi huko Quartier latin, alikua ni under ground bassist nyuma ya Fally Tyson na mwingine pia.

image

Engineer Blaise Bula, Alishiriki kwa Kiasi kikubwa kuiunda Wenge BCBG ya sasa.

Hivyo Sunda Bass akawa mtu wa kwanza kuwa recruited,baada ya hapo chini wenge bcbg chini ya Blaize Bulla ambae alipania kuisuka bendi upya ikawaita ma-atalaku wa tatu kuwafanyia majaribio ili wampate mmoja atakaemsaidia Tutu Caludji,miongoni mwa walioitwa ni Bidjana ambae baadae alienda zaiko huyu Genta Lisimo “Anti biotique” ambae wakati huo alikua akitokea Anti Choc kwa mzee Bozi Boziana,Tutu Caludji akamkubali zaidi Genta ambae nafasi yake kule kwa Bozi ikazibwa na Theo Mbala toka Big Stars ya Defao.

Engeneer Blaize Bula hakuishia hapo katika harakati zake za kuijenga BCBG, akaona kuna haja pia ya kuimarisha safu ya uimbaji kwa kuongeza waimbaji wachache,ndipo akawasiliana na rafiki yake na muandishi wa nyimbo zake wa siku nyingi toka enzi za wenge musica original ambae pia alikua muandishi wa nyimbo wa CHOC STARS na si mwingine bali ni JULES KIBENGA MAKIESE a.k.a. Jules Kibens(najua wengi mtashangaa lakini ndio ukweli),pia akamtafuta RIO KAZADI “rIO de janeiro” ambae alikua Chef D’ Orchestre katika bendi iitwayo JOLINO akiwa na akina KABOSE, CHAI NGENGE na baadae BILL CLINTON Pia alikua chini yake hapo JOLINO.

image

Hata Rais Kabila pichani amejaribu kwa uwezo wake kuwapatanisha wanamuziki wa Congo, kama ilivyo kwa picha hii.

Rio nae akamwambia Blaize Bulla kwamba kama anamtaka yeye basi pia amchukue na rafiki yake Chai Ngenge,Blaize akakubali hivyo wote wakajiunga BCBG,Pia kutokana na kutomuamini Burkinafaso kutokana na tabia yake ya kuhamahama Bulla aliamua pia kumchukua ALBA ACCOMPA aje asaidiane nae na kwa kuwa wote kundini walimjua ALBA kutokana na kwamba alishajaribiwa kundini wenge oariginal na kuonekana anafaa lakini akawa amechelewa wakati anajiandaa kujiunga na bendi ndio ikawa inavunjika.Baada ya hapo ikawa ni mazoezi tu na show za ndani,then wakapata contract nyingine kubwa ya kupiga kusafiri kwenda ulaya kupiga ZENITH na OLYMPIA,Safari ambayo ilizua mtafaruku mkubwa ulioitingisha sana BCBG Katika historia ya maisha yake,mtafaruku uliosababisha JB awe kama alivyo hivi tunavyomuona sasa na BCBG yake.

Je nini kilitokea….twende pamoja siku ya Ijumaa tutakapo kuwa tunakamilisha makala hii ya Historia ya kuvunjika kwa Wenge Musica na miaka mitatu ya mwanzo ya JB Mpiana na Werrason.

Kama una maoni usisite kuniandikia kwa piusmicky@yahoo.co.uk au SMS ONLY 0713 666616.


Salamu za FALLY IPUPA na FERRE GOLA toka WENGE BCBG.

April 20, 2011

Tuitazame video hiyo hapo chini kwa makini,hizo mimi binafsi naziita ni salamu kwa Ferre na Fally pamoja na Ma Ipupanaises na Ma Ferrettes wote mliopo humu ndani, JB anamtoa kijana huyu anaitwa ERIC MENTHE aje kushughulika na vijana wenzake Fally na Ferre wakati yeye mzee mzima JB Mukubwa akishughulika na LE ROI DE LA FORRET WERRASON, kijana hapa anaonekana akifunika vilivyo na kitu chake cha congo rhumba kinachokwenda kwa jina la MY LOVE, Kibao hiki kipo kwenye album mpya ya wenge Bcbg inayokwenda kwa jina la SAYONS SERIEUX, Sikia sauti ya dogo Eric Menthe Hapo halafu utaelewa kwa nini nilisema hizi ni salamu za Fally na Ferre,wakae chonjo dogo anakuja vibaya………na Kwa ambao wamekua wakisema JB hajamtoa mtu wamsikilize kijana huyu pamoja na sakoko kwenye Kitu LIBEREE….

Pata mzigo huu…kama kawaida tunacheza taratibu eeeeeh!


Wenge wametoka mbali jamani!

March 30, 2011

Wenge musica the university of music ilianza huku street mpaka kufikia anga za kimataifa,mnawakumbuka hawa? kina nani ,wako wapi  na wanafanya nini kwa sasa? itakua si vibaya kwa wanaojua tukikumbushana majina ya vijana hawa marafiki sana enzi hizo wakiwasha moto wa burudani na kulichemsha jiji la KIN na vitongoji vyake, tizameni video hii vizuri jamani…..watu wanatoka mbali…tumshukuru sana mungu leo tupo hapa ni kwa mapenzi yake,kesho hatujui tutakua wapi,hawa watu naamini wao wenyewe binafsi wanapoitizama video hii wanakua na furaha na pia huzuni.Pata Picha mwenyewe then toa comment yako.

Ukiangalia kwenye Video hii utamuona JB Mpiana, Allain Prince Makaba, Utamuona Engineer Blaise Bulla utamuona Patient Kusangira na wengineo wakongwe. ama kweli watu wanatoka mbali.


Wimbo(Nzembo)-Champion Kapangala

March 23, 2011

Wimbo(Nzembo)-Champion Kapangala , 

Mtunzi (composer)- JB Mpiana ,

Albam- Titanic

Bendi- Wengi BCBG    

 

Kama kawaida wiki hii nawaletea kibao Champion Kapangala ambacho kinapatikana kwenye Albam ya Titanic, Albam hii ilitungwa baada ya kundi la Wenge Musica kumeguka na walipohojiwa kipindi wamekuja nchini JB Mpiana alisema analifananisha kundi lake na wale walionusurika kwenye janga la kuzama kwa meli ya Titanic miaka kadhaa iliyopita. Kwani kumeguka kwa kundi hilo lilikuwa tukio la ghafla na ni janga kama Titanic.

Albam ilikuwa nzuri sana ukiisikiliza hii albamu utawasikia vyema miamba kama Allain Mpela, Aimelia, Tutu Caludji walivyotamba bila kumsahau mzee mzima JB Mpiana.

nisikunyime uhondo anza kudadavua yaliyomo ndani ya mashairi haya mwanana.

 

Yaka Champion po tobima lelo yo ee tolakisa na ba-banda aa ee tosi tolingani yee yango nasengi nayo yozala pene na ngai  tosimba bolingo ya seko na seko kapangala yoka aa nakoloba lisusu trop te po nayebi, e osi okola ozali na mayele ya bomoto kolula lula mabe bilula lula kolo.                                                                                    

Njoo Champion tutoke leo  na kwaonesha  mahasimu wetu namna tunavyopendana  ndio maana nakuomba uwe pembeni yangu  tupendane mpaka milele , Sikiliza kapangala siwezi kuongea sana tena sababu nafafahamu ya kuwa umeshakua na akili ya kiutu uzima (Kibinadamu) kupenda penda ni vibaya                 

Chorus x 2                                                                                                                                                             
Champion Kapangala , Azali kitoko belomme Teint Rose  Pale nga naluli ye se ye ooh se ye ooh                       

Champion Kapangala,  ni mvulana mzuri mwenye weupe  uliochanganywa na rangi ya pinki  nimemchagua yeye tu yeye tu.

 

JB: 

Pasi ya bolingo nakomona nani akozala ata temoin se motema na ngai moko mishonga yoka Denis Mutombo  Michel Osako…….

 Shida ya mapenzi nayoiona nani atakua shaidi najua ni roho yangu nzuri yenye Mishonga sikia Denis Mutombo   

 

Chorus:

Champion Kapangala , Azali kitoko belomme Teint Rose  Pale nga naluli ye se ye ooh se ye ooh                       

Champion Kapangala,  ni mvulana mzuri mwenye weupe  uliochanganywa na rangi ya pinki  nimemchagua yeye tu yeye tu.

                                                                                                                                               

Alain Mpela: 

Namituni na motema  na nga lulu Iyolo  tata wani tata wani Raymond Muludiki Shalai pamba Claude Pirens Gourverneur zindo Juju Mwanga Henry Magie                                                                                                        

Najiuliza moyoni mwangu  Ilulu Iyolo ,Baba yangu, Baba Yangu  Raymond muludiki, Shalai pamba,  Claude Pirens,   Gouverneur Zindo,Juju Mwanga, Henry Magie.                                                                                  

Aimelia;  Eloko Nzambe  apamboli na Mokili nani aboya nani abongola moyi ekoma butu nani achanger mungwa ekoma sucre ezali se yo tata nzambe moto okela Didier Ikoko , Ali Jabir , Annie Dembo,Jules Guyslain nga nalela Gina leleee.

 Nani atabadilisha kitu mwenyezi mungu alibariki hapa duniani nani atabadilisha mchana iwe usiku , nani atabadili chumvi iwe sukari  ni wewe mwenyezi mungu uliyeumba Didier Ikoko, Ali Jabir, Annie Dembo, Jules Guyslain mimi nampenda Gina Lele                                                                                                     

 

Chorus:

Champion Kapangala , Azali kitoko belomme Teint Rose  Pale nga naluli ye se ye ooh se ye ooh                       

Champion Kapangala,  ni mvulana mzuri mwenye weupe  uliochanganywa na rangi ya pinki  nimemchagua yeye tu yeye tu.

 

Wimbo huu umedadavuliwa na Msomaji wetu maarufu Shaibu Mwambungu. Ingawa kuna baadhi ya maneno yameachwa tunaomba anayeweza kutia nyama afanye hivyo. Ila hii ilikuwa Wenge.


Ngiama analeta mambo!!

March 16, 2011

Majuzi nilipokea Copy ya DVD ya Live ya Werasson huko Bukavu DRC show ambayo ilipigwa tarehe 15/10/2010. Ilikuwa shoiw ya kufa mtu ikizingatiwa Werasson alikuwa hajafanya show maeneo haya kwa muda mrefu.

Eneo la Bukavu linawazungumzaji wengi wa kiswahili na ili kuwabamba basi Werason alitumbukizia ghani ndani yake ana sema “Ngiama analeta mambo…” huku mashabiki kwa mamia wakiitiakia.

Bofya upate mambo, Asante sana Julie Ellystone we ni kiboko na tutapanda Punda tu hata kama mtaleta mambo. Hakuna malewa wala nini hata mkilewa tutawapandisha Punda mtakwenda tuu. Salaamu kwa Werasonique wote.


JB Mpiana alipofanya kweli Ufaransa

June 26, 2008

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

Kama kawaida Ziara ya JB Mpiana ilihitimishwa Ndani ya Bataclan Paris, Ufaransa tarehe 22 mwezi huu na mambo yalikuwa moto, JB Mpiana anayetamba na Albamu yake Mpya Ya Quel Est Ton Probleme? Aliwaburudisha mashabiki walijaza ukumbi kwa nyimbo za zamani na zikichanganyika na mpya, Kama Zadio Congolo, Mtindo wa Lopele pia mashabiki walilipuka nao kinoma, Kali ni pale kibao matata cha Liberez kilipoanza kuimbwa, Wimbo huu umo kwenye Albamm yake mpya na umetokea kupendwa sana. Liberez ni utunzi wa mwanamuziki mpiga Bass gitaa wa Wenge BCBG Sunda Bass. Onyesho limesifiwa kwa kuwa na Sound System nzuri na Jb alitumia muda vizuri na muda wote mashabiki walifurahi.


%d bloggers like this: