John Terry ahojiwa na polisi

November 30, 2011

John Terry siku alipokwaruzana na Anton Ferdinand

John Terry siku alipokwaruzana na Anton Ferdinand

Nahodha wa England John Terry amehojiwa na polisi kuhusiana na tuhuma alimtolea maneno ya ubaguzi Anton Ferdinand.

Terry, mwenye umri wa miaka 30, ambaye pia ni nahodha wa Chelsea, anakanusha kumtolea maneno ya kibaguzi mchezaji huyo wa QPR wakati wa mchezo wa tarehe 23 mwezi wa Oktoba.

Polisi wamethibitisha “mtu mwenye umri wa miaka 30 amehojiwa tarehe 25 mwezi wa Novemba. Hajakamatwa.”

Chama cha Kandanda cha England -FA- kwa upande wake kinachunguza suala hilo.

Baadhi ya watu wamedai mkanda wa video uliorudiwa baada ya mechi iliyochezwa uwanja wa Loftus Road Terry alionekana akitumia lugha ya kibaguzi, wakati FA ilisema ilipokea malalamiko hayo.

Ferdinand awali alitoa taarifa kwa FA, akisema “analitilia maanani sana” suala hilo, lakini hatafafanua hadi uchunguzi wa FA utakapokamilika.

Uchunguzi wa FA kuhusiana na suala hilo hautatolewa hadi polisi watakapokamilisha uchunguzi wao.

Katika taarifa baada ya mechi ya Loftus Road, Terry alielezea tukio hilo kama ni “kutoeleweka” na akadai anayemtuhumu “alifika hatua ya mwisho ya suala hilo kwa makosa juu ya muktadha wa kile ambacho nimeonekana nikikisema”.

Aliongeza: “Kamwe siwezi kusema kitu kama kama hicho – Nimeshangaa watu kufikiria kama naweza kutamka hayo.”


Breaking News: Werasson apata ajali,avunjika mkono

November 28, 2011

image

 

Na Mabrook, Montreal Canada
Habari zilizotufikia punde zinasema wanamuziki wa WMMM wamepata ajali na inaripotiwa kuwa kiongozi wake Igwe Ngiama Makanda alias Werasson amevunjika mkono.

Kwa sasa habari hazijaeleza chanzo cha ajali ila habari zinasemakuwa Werrasson alikuwa akitokea mji alikozaliwa Wa Bandundu.

Aidha habari zaidi zinasema kuwa kiongozi wa Wenge BCBG JB Mpiana na Adolph Domibguez walikuwa kati ya watu wa kwanza kwenda kumfariji, habari zinasema JB Mpiana alikuwa wa kwanza kufika na alikwenda hospitali huku akibubujikwa na machozi kwani aliyempa taarifa alimwambia Werasson amefariki, “…Kwanza tulishangaa JB alipataje taarifa mapema vile… na alipofika alikuwa akitokwa machozi kwani aliyempatia taarifa alimueleza kuwa Werrason amefariki dunia” alisema Yanki Mpuyi ambaye alikuwepo wakati wa ajali.

Kisha waliwaacha wao wawili tu (JB na Werrason) humo chumbani hospitali kwa zaidi ya nusu saa wakiongea na kisha JB alitoka nje huku bado akibubujikwa machozi aliendelea kueleza Yanki na Heritier pamoja na Kakol ambao walikuwepo Hospitali muda wote, kisha waliingia Frere Patrice pamoja na mama yake mzazi ambaye alikuwa amehamaki na kumbusu mwanaye aliyekuwa akigugumia kwa maumivu makali.

Inasemekana kuwa mashabiki walifurika hospitalini na katishia kuichoma hospitali kama kipenzi chao atafariki ndipo Local Authority walipokaa na kuamua kuwa Werrason apelekwe nje ili kulinda usalama kwani ni kipindi cha uchaguzi hivyo mashabiki wangeweza kutumia nafasi hiyo kuleta fujo.

Kwa sasa Werrason amepelekwa India kupitia Afrika ya Kusini kwa matibsbu zaidi kwa ndege ya kukodi ya Ethiopian Air Line ambayo imelipiwa na Rais Joseph Kabila. Wengine walikwenda kumfariji ni pamoja na Didier Lacoste na Koffi Olomide. Kisha Werrasson ataenda USA ambako atakwenda kumsalimia mwanae Exocee ambaye yuko huko na mkewe na mwanaye mwingine Glady.

Ikumbukwe kuwa Werrason ni mmoja wa wanamuziki waliokuwa wakimkimkampenia Rais wa sasa Joseph Kabila.

Wananchi wa Congo jana walipiga kura kuchagua Rais na Wabunge ambapo wanamuziki kadhaa wameripotiwa kuomba baadhi ya nafasi.


Ni Kweli Makaba alifiwa na Babaake mzazi

November 28, 2011

 

imageBaada ya baba mzazi wa JB Mpiana kufariki yapata miongo miwili sasa, na baadaye baba yake Aadolphe Dominguez, Kisha Blaise bula na baadaye tena Vieux cyprien na hivi karibuni Papa Kifaya toka WMMM sasa baba yake mzazi Alain Prince Makaba Papa Clément makaba amefariki dunia.

Mzee makaba alifariki dunia zaidi ya wiki sasa na habari zinasema maziko yalisha fanyika huko Congo.

Makaba aliwahi kuwa mmoja wa waanzilishi wa Wenge Musica BCBG na kwa sasa yuko Ufaransa akiendesha shughuli zake za maisha amesema kuwa Baba yake mzazi alikuwa na matatizo ya kiafya bila kutoa maelezo zaidi.

Kwa mujibu wa habari za awali Mzee Makaba amefia Kinshasa na wanamuziki wengine waliowahi kufanya kazi na Makaba wakiwemo Didie Massela, Adolphe Dominguez, JB Mpiana , Igwe Werrason Ngiama Makanda, Alain Mpela Afande, Titina, Theo Bidens, Blaise Bula wamekuwa walishiriki katika kuandaa mazishi.

Habari zinasema kuwa Aimelia na Kusangila waliwasili wakiongozana na Makaba mwenyewe kwa ajili ya kuhudhuria mazishi.


Jasiri haachi Asili…..

November 28, 2011

Na Jennifer Livigha wa Chinga One Blog.

Full Mzuka

Full kupagawisha!

Full Support!


Ya Mheshimiwa Mr II na Ruge yanaongeleka

November 28, 2011

rugesugu

Mwaka jana June 30, 2010 niliandika makala yangu nikisema Sugu na Ruge malizeni tofauti zenu kimya kimya.  Mpaka leo ni takribani mwaka mmoja na miezi miwili na siku kama mbili tangu makala yangu. Makala ile niliandika ikiwa ni baada ya kutokea sintofahamu ambayo ilipelekea Mheshimiwa Mbilinyi kuwekwa ndani kwa kile kilichodaiwa kusambaza CD ambayo ilikuwa ikimkshifu Bwana Ruge.

“Hakuna wa kumhukumu mwengine hapa ila mi nasisitiza tu tofauti hizi zisiwagawe wadau wa burudani, zisiwagawe wasanii kwani sekta ya burudani ndio pekee inayoweza kuondoa tofauti za kisiasa baina ya makundi ya vijana na zinawakutanisha vijana wengi zaidi wenye utashi na mtaguso tofauti tofauti, Waziri Mheshimiwa John Nchimbi chukua hatua kulimaliza hili na naimani kwako linawezekana na kufikiwa muafaka.”

Katika makala ile nilijaribu kuwakumbusha wote wawili wajibu wao kwa jamii ikiwa Mheshimiwa Mbilinyi Kama msanii ambaye jamii inamuangalia yeye kwa ulimwengu wa sasa vijana wengi wanakuwa wakiwafatilisha wasanii na kwa upande mwingine kwa Ruge ama yeye binafsi au kama taasisi ana mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya vijana kutokana na ukweli kwamba yupo kwenye chombo ambacho anawagusa vijana wengi sana na kirahisi zaidi.

Kwa sasa Mheshimiwa Mbilinyi si msanii tu bali ni sehemu ya chombo muhimu ambacho kinatunga sheria kwa nchi, Bunge ni taasisi nyeti na kubwa yenye heshima kubwa, kwa safari ya Mheshimiwa Mbilinyi hakika haya ni mafanikio makubwa si tu kwake bali inaonyesha nguvu ya Sanaa nzima ya muziki kwa mara ya kwanza imetoa Mbunge.

Sitaki kuongelea chanzo cha mgogoro wao hapa kama unataka kujua basi bofya hapa

Katika makala yangu ile nilijaribu kuelezea ikiwa tofauti hizi zikiachiwa nini kinaweza kuwa madhara si tu kwa wahusika bali hata kwa sekta nzima ya burudani. majuzi tulishuhudia tamko naweza sema zito toka kwa Mheshimiwa Mbilinyi akisema kwa msisitizo kuwa Mkoa wa Mbeya hawataki tamasha la FIESTA ambalo linaandaliwa na kuratibiwa na Prime Time promotion na Clouds Media Group. Bado ukiangalia hapo chanzo ni zile zile tofauti ambazo wadau wa burudani tunazijua. Tofauti ambazo zinahitaji kuongelewa ili kuzimaliza nachelea kusema hilo linawezekana kwani hata biff zao zikiendelea hakuna kinachoweza kubadilisha kilichoshatokea.

Tofauti hizi ni hatari hasa kwa sekta ya burudani na wasanii kiujumla kwani kunakuwa na mgawanyiko na kuwatia uwoga wasanii wale ambao wanahisi wangetaka kumshirikisha Sugu kwa namna yeyote iwe kikazi au kimawazo kwani kufanya hivyo ni hatari kwa kazi zao kisanii ama kwa kuogopa kuingia kwenye malumbano au kwa nyimbo zao kutopigwa redioni au kwenye TV Stesheni kabisa. Ni wazi kuwa hakuna kituo cha redio kinachomilikiwa na Clouds Media Group kinaweza kucheza wimbo wowote wa Mheshimiwa Mbilinyi kwa sasa, hapo ndipo tulipofikia na huo ni ukweli usiopingika.

Kwenye makala yangu nilionyesha wasiwasi mkubwa nilisema hizi tofauti zenu hazitoishia hapo tuu mtazipeleka au zitawapeleka mbali, Majuzi tumeshuhudia malumbano mengine na kwa wakati huu ikiwa katika chombo cha juu kabisa cha kutunga sheria pale Mheshimiwa Mbilinyi ambaye ni waziri kivuli wa Vijana na Michezo alipokuwa akichangia hotuba ya Mheshimiwa waziri Nchimbi kwa kile kilichotafsiriwa kuwa ilikuwa ni muendelezo wa tofauti zile zile ambazo niliziandika hapo awali.

Ingawa mchango wa Bwana Mbilinyi ulilenga kuwatetea maslahi ya wanamuziki lakini kwa upande mwingine ilikuwa ni shutuma za moja kwa moja kwa Bwana Ruge na Taasisi ambazo zinahusiana na yeye ama moja kwa moja au kikazi.

Pamoja na kuwa Mheshimiwa Mbilinyi alikuwa anatetea maslahi ya wanamuziki serikalini, mwisho wa siku Serikali inatengeneza platform kwa taasisi binafsi kama hizo za Prime time Promotion na ukiangalia ndio zinazotoa ajira kwa wasanii hawa. Tangu tamko la juzi la Sugu Bungeni hakuna msanii yeyote aliyediriki kumuunga mkono hadhani, kwenye gazeti, radio au hata mitandao jamii !! JE unadhani hakuna ambao wanakubaliana na Sugu kwenye hili? Jibu ni kuwa wapo lakini wanajua madhara ya kuonyesha kumuunga mkono Mbilinyi. Na ndio hasa kiini cha makala yangu hii najaribu kuangalia athari za mgogoro wa mafahari hawa wawili kwa sekta nzima ya burudani ikigusa vijana zaidi.

Kwani kwa sasa Muziki unaajiri vijana wengi zaidi jambo linalopelekea kupunguza tatizo kubwa la ajira kwa vijana.

Sasa kwanini tufikie hapo? ni bora kuwakalisha hawa wawili na naamini kabisa Waziri husika anaouwezo wa kufanya hili kwani Waziri mwenyewe ni kijana na jambo hili linagusa wadau wake kwa kiasi kikubwa. kwani wengi wa waathirika kwa namna yeyote ile ama iwe upande wa Mheshimiwa Mbilinyi au upande wa Taasisi ambazo zinamhusu Ruge kibinafsi au kikazi waathirika bado ni vijana.

Baada ya pale Bwana Ruge alitoa Tamko ambalo kwa walipata kumsikiliza utakubaliana na mimi alionyesha kukerwa sana na kilichotokea na binafsi yake alivunja ukimya kwa kujibu shutuma zile moja baada ya nyingine.

Katika waraha huu wa Bwana Ruge aliongelea kukashifiwa kwa Clouds Media, THT na yeye binafsi na alitoa maelezo marefu ambayo mwisho wa siku si mimi na wala wewe msomaji unaweza kubadilisha mtazamo wa wawili hawa.

Mheshimiwa Waziri alipokuwa akijibu hoja za Bwana Mbilinyi alisema kwa utani Mheshimiwa Mr Sugu ni Sugu Kweli kweli kwani hoja hizi tulishazijibu zaidi ya mara moja na bado amezileta Bungeni. Kama alijibiwa na bado amezileta Bungeni basi ujue kuwa kuna ambacho haridhiki nacho ila ni kipi inawezekana kuna anachokijua zaidi.

Hakuna wa kumhukumu mwengine hapa ila mi nasisitiza tu tofauti hizi zisiwagawe wadau wa burudani, zisiwagawe wasanii kwani sekta ya burudani ndio pekee inayoweza kuondoa tofauti za kisiasa baina ya makundi ya vijana na zinawakutanisha vijana wengi zaidi we utashi na mtaguso mbalimbali, Waziri Mheshimiwa John Nchimbi chukua hatua kulimaliza hili na naimani linawezekana na kufikiwa muafaka.

Ni mtazamo tuu.

  


Mgaagaa na upwa…

November 24, 2011

Photo0546

Kigamboni hivi karibuni…


Wenge Musica vs Koffi Olomide "@ Mzalendo Pub

November 24, 2011

image

Dakika 120 za Extended Non Stop Mayenu kati ya Koffi Olomide na Wenge Musica.

Dakika 60 za Koffi na Dakika 60 Za Wenge Musica huku Ma DJ MacKay na Dj Too Short wakisababisha pale kati, ni siku ya ijumaa tarehe 25 November 2011.

Hii ni Party ya Msisimko wa mwisho wa mwezi. Jamani wadau hapo chacha… Chezea Wenge wewe!!!!


%d bloggers like this: