The Kilimanjaro Connections Band yaendelea kutesa Kuala Lumpur Malaysia

January 26, 2013
251929_4163633330638_486942009_n

MBELE WAIMBAJI ALLY SAMA, DOTO RAMADHANI, NYUMA KANKU KELLY, SIJALI MORIS ( Drums), FARIALA MBUTU ( Bass), BEN OMAR ( Guitarist), DONALD ( Keyboard)

Unapokuwa nje ya nchi kila kitu cha nyumbani una kimiss hasa kwa wapenda Burudani inakuwa ni mtihani maana unakutana na burudani lakini katika utamaduni mwingine kabisa. Tangu kukua kwa uchumi wa nchi za Mashariki ya mbali kumefanya vijana wengi wa Kiafrika hasa kutoka Afrika ya Magharibi, kukimbilia nchi za Asia ambazo uchumi wake umekua kwa kiasi kikubwa,  moja ya nchi ambazo zinakimbiliwa ni Malaysia bila kusahau, Singapore, Vietnam, Hongkong na hata China.  Nchi hizi zinakimbiliwa sana na vijana hawa na kwa sasa kumekuwa pia na lindi la wanafunzi waotoka nchini Tanzania, kenya, Botswana, Zimbabwe na hata Sudani ambayo kwa watanzania wao hawako katika kutafuta maisha bali kutafuta elimu ambapo wengi wa wanafunzi wamekuwa wakikimbilia Malaysia kwa ajili ya elimu ya juu,

Iinakadiriwa kuwa Malaysia ina wanafunzi zaidi ya elfu hamsini wanatokea Afrika ambapo Tanzania pekeeina wanafunzi zaidi ya elfu kumi.  Chachu ya kuwepo kwa jumuiya hii ya Waafrika imepelekea wafanyabisahara wa Kimalay kuangalia ni jinsi gani wanaweza kujichanganya na kuangalia kuweza kuitumia jumuiya hii kibiashara, mmoja ya wafanyabiashara hao ni Mkurugenzi wa Club ya Rum Jungle ambayo ipo jijini Kuala Lumpur. Katika Club hii ndipo unaikuta bendi pekee iliyojizolea umaarufu si Malaysia pekee bali South East Asia bendi ya The Kilimanjaro Connection chini ya uongozi wake Le Gendary Kanku Kelly.

Bendi hii ambayo kwa takribani miaka zaidi ya kumi sasa imekuwa ikitoa burudani South East Asia huku miaka zaidi ya sita ikijikita jijini Kuala Lumpur imeweza kupeperusha vizuri bendera yetu na ni mahali si tu vijana wanakutana bali hata mabalozi wa kutoka nchi za Kiafrika na wanafamilia wao wamekuwa wakijumuika katika klabu hii ya Rum Jungle kupata vionjo na burudani ya nyumbani.

The Kilimanjaro Connections wamejikita kupiga muziki wa dunia nzima huku wakipiga nyimbo zote maarufu duniani na hata zile za Asia, za Kimalay na Kichina jambo linalowaongezea umaarufu na kugonjwa vichwa vya habari kula uchao. Miaka kama miwili iliyopita bendi hii nilipokutana nayo walikuwepo watu mahiri kama Maneno Uvuruge ambaye ni mcharaza gitaa maarufu ambaye binafsi nilianza kumsikia akivuma na vijana Jazz miaka hiyo nikiwa mdogo, pia kuna mtu kama Faliyala Mbutu ambaye ni mume wa ndoa wa Luiza Mbutu huyu jamaa anapiga gitaa la Bass na kiukweli namkubali sana, kuna Sijali Moris kwenye chants na Drums na kwenye Tumba, Pakacheni mzee mwenyewe Kanku Kelly.

kwa sasa Bendi hii imeongeza wanamuziki wengine wapya na line up nzima ni kama ifuatavyo, FALIJALA MBUTU (bass guitor), BEN OMARI ( guitar), SIJALI MORISI ( drums), DONALD ( keyboads) , DOTTO RAMADHANI ( Female singer), ALI SAMA ( male singer) na KANKU KELLY ( percussions& trumpet), ni timu ya watu saba ambao wanafanya kazi ya bendi ya watu 25 kwani wakiimba wimbo wa Wenge BCBG ambayo ni bendi ya watu 25 unapata kila kionjo!!

Kiukweli bendi hii inaburudisha sana na nawakubali sana binafsi, ni huku ndipo nilipomuona Queen Suzy kwa mara ya kwanza mwka 2006 ambapo Kilimanjaro Connections walikuwa wakitumbuiza Kuala Lumpur. Bendi hii imezidi kujizolea umaruufu kwani kwa sasa inapiga siku sita za wiki na kupumzika jumapili tuu hii ni kutokana na matakwa ya wadau na mashabiki wa bendi hii ambayo ina mkataba wa miezi sita kupiga katika Club hiyo kila mwaka, “Kiukweli tunashukuru jinsi tunavyopendwa hapa KL, mashabiki wanafanya mpaka tunakosa muda wa kupumzika sasa” alisema Kanku alipoongea na Spoti na Starehe.

Tunawatakia kila la heri katika shughuli zenu.


Na hawa ni wadada wa Koffi Jukwaani Zenith

January 22, 2013

Tofauti na JB Mpiana ambaye wadada wake wanaonyesha umri umeenda na wamenenepa, Wanadada wa Mwanamuziki Koffi Olomide wao bado wako fit na wanaonyesha wanaweza kuhimili mikiki kwa muongo mwingine, angalia video hii ya Koffi Zenith na hawa nai wadada wa Koffi.


Satellite Plus 2: Zawadi ya Christmass toka kwa Werasson kwa Mashabiki wake

January 22, 2013

image

Kama Video haichezi bofya picha hiyo.

Mwanamuziki Werasson Ngiama usiku wa tarehe 26 alizindua Single yake mpya ijulikanayo kama Satellite Plus 2 ambayo ime kwenye albamu yake mpya ijayo.

Uzinduzi huo ulifanyika huko Matongee kwa mashabiki wake na mbele ya meya ya mji huo Mheshimiwa Meya Jean-Claude Kadima na pia rais wa muungano wa wanamuziki wa Congo Kiamuangana Mateta Verckys ambao kwa pamoja walinunua CD na DVD ya single hiyo. Ikumbukwe kuwa Werasson alikuwa pia akisherehekea siku yake ya Kuzaliwa kwani yeye amezaliwa Tarehe 25 December na ndio asili ya jina lake la Noel.

Werasson na kundi zima la Wenge Musica Maisson Mere waliufunga mwaka jana kwa kupiga concert mbili kubwa moja siku ya tarehe 29 katika mji wa N’Djili na nyingine tarehe 30 katika viwanja vya Assossa Kasavubu.

Show zote mbili zilifana sana na Werason na kundi lake la Wenge Musica Maison Mère walitambulisha singo yake mpya ijulikanayo kama Satellite Plus 2 ambayo ni moja ya nyimbo zilizomo kwenye albamu yake hii mpya ijayo ya Flèche Ingeta ezui ezui. Wimbo huo ulilipua mashabiki waliokuwa wamefurika kwenye viwanja hivyo na kuonyesha kuufurahia pale Roi de la Forêt Werrason Ngiama Makanda alipoimba na mashabiki kutaka kuurudia mara kwa mara.


Dizoizo ya Allain Prince Makaba

January 10, 2013

 

Dizoizo ni mmoja ya nyimbo zilizokuwa kwenye Albamu ya Pentagone, moja ya albamu bora kabisa zilizowafikisha Wenge walipo kabla ya kuparanganyika.

Huu wimbo huu ni utunzi wake Allain Prince Makaba , Napenda sana walivyoimba kwenye wimbo huu hasa verse ya Mpela na Werrason kiukweli wameimba vizuri mnooo nitauchambua wimbo huu na kukuelezea kila kitu ndani yake, stay tuned, hii ndio Spoti na Starehe.


Orijino Komedy: Vengu anaendelea vizuri

January 10, 2013

VENGU LIST

Kundi la Orijino Komedy wakiwa na mwenzao Vengu ambaye kwa sasa anasumbuliwa na maradhi, na kwa mujibu wa Masanja Vengu anaendelea vyema.

Baada ya minongono mingi kuhusiana na hali ya msanii mwenzao Vengu, hatimaye memba wa kundi ya Ze Orijino Komedy Masanja mkandamizaji amefunguka na kueleza kuwa msanii mwenzao Joseph Shamba aka Vengu anaendelea vizuri baada ya kurejea kutoka India alikokuwa akitibiwa.

akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook leo Masanja amesema kuwa Vengu bado anaendelea kupata matibabu akiwa nyumbani “Ukweli ni kwamba Ndugu yetu Joseph Shamba (Vengu) yuko nyumbani akiendelea na matibabu yake na uangalizi wa mara kwa mara kwa madaktari baada ya kurejea kutoka India.” alisema masanja na kuongeza “…Muda mwingi tuko naye na tunazidi kumuombea apone na arejee kutoa burudani. Na mnaomuombea mabaya na kumzushia habari za kila aina tunawakabidhi kwa Mungu awajalie busara.”

Habari hizi zimekuja wakati mzuri kwani habari za kuugua na ugonjwa wa Vengu upatikanaji wake si wa wazi licha ya mashabiki na jamii kufahamu kuwa Vengu anaumwa basi.

Tunamuombea mwenyezi Mungu amjalie mja wake aweze kupona na kurejea kazini kulitumikia taifa na jamii kwa ujumla.


Koffi Olomide amzawadia Cindy zawadi ya mwaka mpya.

January 9, 2013

88982-0

Mwanamuziki Koffi Olomide ametangaza kutoa Single CD mpya ya mwaka 2013 ambayo amesema itakuwa ni zawadi kwa mpenzi wake Cindy.

Naahidi Single hii itakuwa moto wa kuotea mbali na nawaahidi wapenzi wangu wataifurahia, Koffi aliyasema hayo alipokuwa akisherehekea sherehe ya mwaka mpya na kuukaribisha mwaka 2013, aidha Koffi amesema kuwa Single “Karibu Varieties”, alikuwa akiongea na kipindi cha TRNC kinachotangazwa na Mamie Ilela na itakuwa sokoni mwanzoni mwa mwaka huu.

Single Cindy “hii ni zawadi ambayo nimechagua kumpa Cindy, nafikiri ni zawadi ambayo anastahili mwanamke mrembo kama yeye, mngoje na mtaisikiliza” aliongeza Koffi. Koffi anatazamiwa kuanza ziara ya Africa Magharibi ambayo itaanzia Togo hivi karibuni.


Breaking News: Sajuki Afariki dunia

January 2, 2013

Habari zilizotufikia asubuhi hii zinasema kuwa muigizaji toka familia ya Bongo Movie Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki Amefariki Dunia alfajiri ya leo.

Sajuki amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kukaukiwa na damu mara kwa mara maradhi yaliyomsumbua kwa muda mrefu mara ya mwisho alitibiwa nchini India ambako alikaa kwa muda kidogo.

Sajuki alikuwa amelazwa hospitali ya taifa ya Muhimbili kabla mauti kumkuta alfajiri ya leo. Hivi karibuni kundi la wasanii walifanya Tamasha kuchangia muendelezo wa matibabu ya msanii huyo ambapo ghafla alianguka jukwaani alipoombwa awasalimie mashabiki katika uwanja wa Sheikh Amri Beid huko Arusha.

Buriani Sajuki, mashabiki wako wataendelea kukukumbuka daima. Bwana alitoa na bw


%d bloggers like this: