Diamond aichomolea buku 10 ya Wema Jukwaani!!

March 31, 2012

Diamond alikuwa na onyesho usiku huu katika ukumbi wa Mlimani City, mashabiki wengi walihudhuria show hii ambayo kwa hakima imefana kwa kukusanya watu “classy” kwa kuwa kiingilio chake kilikuwa 50,000/-. Moja ya matukio ambayo kila mmoja lilimshangaza ni kitendo cha Diamond kukataa kupokea tuzo ambazo mashabiki walikuwa wakimtunza na alipokwenda Wema Sepetu kumtunza Diamond alikataa kupokea hata pale Weema alipoongeza pesa bado Diamond alikataa kupokea na kuendelea kuimba, ndipo Meree Wema alipoamua kuzitupia jukwaani na kuondoka huku mashabiki makumi kwa mamia wakipiga mayowe.

image

Pichani Diamond akifanya vitu vyake na mashabiki wakifuatilia.


Vinara wa Muziki Afrika

March 30, 2012

image

Inawezekana Akon akawa ni msanii wa Afrika mwenye mafanikio makubwa sana na anayekubalika duniani. Hapa apichani akiwa na mwanamuziki Fally Ipupa walipokutana huko USA.


Halafu we unajiita mshabiki ….!!!

March 30, 2012

image


FALLY IPUPA FT. MEJE 30 , FANNY , MOKOBE , KRYS – CONCERT VIP LIVE PISCINE GHK 2009

March 30, 2012

Kwa muda mrefu Congo ilikuwa haina mwanamuziki mpya wa kike ambaye angeweza kuitangaza na kung’aa nje na ndani kama walivyio akina Tshala Muana, Mbilia Bell na wengineo miaka yao ambao kwa kiasi fulani mpaka sasa wako kwenye muziki.

Huyu mwanadada anaitwa Meje 30 ambaye alianikwa na mwanamama Tshala Muana, wataalamu wa muziki wanawashindanisha huyu na Cindy Olomide mke wa sasa wa Koffi Olomide.

Kiukweli wote wanaimba sana na tuliwahi kuweka post zao humu. Leo nakuacha na kibao hiki ambacho Fally Ipupa aliwashirikisha Meje 30, Fanny, Makobe, KRYS ilikuwa ni VIP Concert mwaka 2009.


CHAZ BABA ACHAGULIWA KUWA RAIS WA MASHUJAA BAND.

March 29, 2012

image

Juzi Tarehe 27 march 2012 Wanamuziki wa Mashujaa Musica walimchagua kwa kishindo Chaz Baba kuwa Rais wao ktk uchaguzi uliokuwa wa uwazi na haki. Baada ya wasimamizi wawili ambao ni wadau wa Mashujaa,na waliopendekezwa na Wanamuziki wenyewe wakisaidiwa na Mnenguaji mmoja Swty Beby walihesabu kura kwa uwazi na hatimae kutangaza matokeo.Chaz Baba alishinda kwa kupata kura 19 kati ya 26 zilizopigwa.

Ratiba yao ya kila siku.

image


TOUR EIFFEL WENGE BCBG BY TITINA ALCAPONE

March 29, 2012

na Shaibu Mwambungu
-Mbinga Ruvuma

   

                                                      
Naye epai nayo oyambanga Anne                                          
Ba reve nanga nakokomisa botoli nanga Mwana ya beaute byome 
Oyambanga naesengo mama na Diana.
                                      

*Nimekuja kwako Anne nipokee nijitahidi kufanikisha ndoto zangu, mpenzi Anna, Msichana mwenye urembo, Nipokee kwa furaha mama na Diana.        

Eeh bolingo ya bomoi bwa lobiko, Otiaka nga malasi,Tobalana lelo yo na kati ya ndako ya Nzambe, Banguna bayoki nkele lokola basambwe, Anne Maria mwana mama Sophia, Bolingo ekokola, libala ya mamelo molongani nanga kitoko nayo ya si Sirene                                         
 

*Eeh mpenzi  wa moyoni nipake marashi ili leo tuoane katika nyumba ya
mwenye enzi mungu (Kanisa) maadui wachukie na kusumbuka. Anne maria mama sophia Penzi litaendelea kukua, ndoa ya Amani(Baraka) Mpenzi wangu  urembo wako ni Nguva.
 

                                                 
Anne Maria Anne ya Monzele Nameleyo lokola mayi ya minuit sambo,
Yosilisanga masumu maso malongwa fiance nanga nakomi nasuka na we      

*Anne maria rafiki wa Monzele nikukunywa kama maji ya usiku saa Saba ili uniondolee dhambi zote mambo yamezidi mpenzi wangu nimefika kikomo.   

Ya leo mama, Cherie nanga kanga motema na baye bainaka Yaka lelo yo pembeni nanga Nazua yo lokola Sirene nanga.               

*Leo mama, mpenzi wangu kaza moyo zidi ya mahasidi, Njoo leo pembeni/
karibu yangu , Nikubebe kama Nguva wangu.
  

         
Chorus:Bolingo nanga okomi konyokolo nga Motema nanga na pinzoli
nganakokufa, Na epai nayo nazali lokola fololo, Vraiment mwana mama
kitoko nayo bijou ya talo x2
                                          

*Mpenzi wangu waanza kuninyanyasa, Moyo wangu nitakufa kwa kudondosha machozi,  Nimekuja kwako kama ua,Hakika mpenzi urembo wako ni kama kito cha thamani.                                

Afande: Hata tokotikala biso mibale na Mokili, Tikala Adam  ngai Eva
tobota bana.
                                                           
*Hata tukibaki sisi  wawili hapa duniani acha uwe Adamu na mimi Eva
tuzae watoto.
 

                                                        
Afande: Lamentation eloba boye , Rien ne peutse paire surcette tere,
Rien ne peutse faire souverain Mukulu,Rien ne peutse faire  Manu
Luvaka,Rien ne peutse faire na mokili, Sans que Nzambe azala Mokolo.   
*Biblia yasema kuwa hakuna kitachoweza fanyika.., Hakuna kitachowezekana Souverain Mukulu (JB) Hakuna kitachofanyika Malu Luvaka,Hakuna
kitochofanyika duniani,Bila maamuzi ya Mwenye enzi Mungu.
              

Afande: Toyaka na Mokili oyo Mama mama mamaaa,Basusu Babenz basusu na Makolo.                                                                                                                                                             & nbsp;                           

Tumekuja hapa duniani wengine wanatembea na Mabenzi(magari) wengine huenda kwa
miguu.

RPT CHORUS

Papa Pius Mtohoo huo kiasi wadau wafurahie kidogo mambo japo si tafsiri
sahihi na baadhi ya maneno huenda yakakosekana ivumiliwe sio lugha yetu kama kuna mdau anazo nyamanyama aongezee- Shaibu Mwambungu
-Mbinga Ruvuma


Samata aumia bega, kukaa nje kwa siku 10.

March 26, 2012

SAMATA out pour une dizaine de jours !

Mbwana Samata akitolewa uwanjani baada ya kuumia bega lake la kushoto, Habari zinasema kuwa Samatta itabidi akae nje ya uwanja kwa siku 10 akiendelea na matibabu. TP Mazembe walicheza walicheza na Power Dynamo katika mchezo ambao walitoka 1-1.

Bwana ambaye alitoka nje akiwa shujaa wa mchezo kwani goli pekee la Mazembe lilifungwa naye katika dakika ya 16.


%d bloggers like this: