PACHA WA P-SQUARE APORWA NA MAJAMBAZI..!

May 31, 2011

Na G5 Click

Mmoja wa pacha wanaounda kundi la P-Square,Paul Okoye alionja joto ya jiwe baada ya kuvamiwa na majambazi alipokuwa njiani kuelekea Victoria Island kucheki washikaji zake Paul alikuwa akiendesha mkoko wake mpya aina ya BMW X6 lenye plate number za “RUDE BOY”na kwa moyo wa utu aliokua nao ndio uliomponza,coz alisimama njiani kutoa msaada kwa waliopata ajali na watu wawili kutokea pasipojulikana na kumtolea bastola na kumpora simu,fedha na vito vya thamani na vinginevyo

GARI YA PAUL OKOYE….BMW X6-RUDE BOY….

Paul alifunguka kuwa baada ya watu hao kuchukua walichotaka,walitaka pia kuchukua funguo ya gari ndipo alipopata msaada wa mama mmoja kupiga kelele na kusababisha waporaji hao kusepa na kushindwa kupora gari lake.


Tony Nyadundo, Mfalme wa Ohangla

May 31, 2011

The Benga Maestro, Tony Nyadundo katika moja ya maonyesho yakeNaanza kwa kumpongeza Obama!! Tony Nyadundo ni mzaliwa wa Kanda ya Ziwa huko Kenya. Anatokea katika kabila la Wajaluo (Luo), Tony Nyadundo amejipatia umaarufu kwa aina ya mziki wake na ni jambo la kawaida kupita mitaani na kusikia nyimbo zake zikichezwa. Aina ya muziki wake inajulikana kama Ohangla (Muziki toka kanda ya Ziwa) na sasa yeye anajulikana kama Mfalme wa Ohangla. Tony ni mmoja wa wanamuziki walifaidika na muziki wake na kuufanya muziki huo kukubalika na rika lote. Tony pamoja na kaka yake anayejulikana kwa jina la Jack Nyadundo naye anapiga aina ya muziki kama wa Tony kama mdogo wake naye anakubalika sana kwenye Muziki na umaarufu wao ni mkubwa hasa Sehemu ambazo Wajaluo wanatoka.

Tony ambaye anatamba na nyimbo kama Dawa ya Mapenzi,Isanda Gi hera, Obama na nyinginezo nyingi ameshafanya matamasha ya muziki nchi mbali mbali ikiwemo Ujerumany na USA pia achilia mbali hizi za Afrika. Umaarufu huu unafuatia aina ya muziki wake ambao unajumuisha ala za asili, uchezaji pamoja na uimbaji ambao huvutia kwa taratiibu na kuupandisha toka Mziki wa Vilabu vya Pombe, Bar mpaka sasa zimbo zake zinapigwa hata kwenye Kumbi za Burudani zikichanganywa na Genge, muziki maarufu wa Kenya.

Mwaka 2006 alitoa albamu yake iliyoitwa Obama. Ikiwa ni kumuenzi Seneta Barak Obama wakati huo ambaye Baba yake ni Mzaliwa wa Kenya kama Nyadundo.

Wakati wa tamasha la Kisima Music Award mwaka 2007 alishinda kwenye kundi la Muziki wa kiasili. Tony ambaye binafsi anaweza kutumia ala zote za kiasili, muziki wake anatumia ala za kiasili tupu isipokuwa kinanda cha kupuliza tuu amefanikiwa kuweka utamaduni na muziki huo katika chati ya Muziki kitaifa na kimataifa.

Bonyeza Player upate Uhondo wa mwanamuziki Tony Nyadundo, Ukiangalia kwenye hii Video Utamuona Waziri Mkuu Raila Odinga, Prof Anyang Nyong, na wajaluo wengine ambao wapo kwenye nafsi za juu kichama(ODM) au kiserikali.


Sakata la Rushwa FIFA, Ushahidi wa Mlungula watolewa.

May 31, 2011

image

Hii ni picha ya Mlungula ambao Afisa wa Caribbean football walipewa kama “Takrima” na mgombea wa Uraisi wa FIFA Mohamed bin Hammam.

Pesa hizo kwenye picha zinaonyeshwa kwa uzuri zikiwa ndani ya Bahasha ambapo zilikuwa jumla ya Dola za Kimarekani 40,000 zikiwa zimepangwa kwenye mafungu ya Dola elfu 10 kila moja. Bahasha hii ilikuwa na jina la Mjumbe toka Bahamas.

Kwa mujibu wa ushahidi huu, hii ilikuwa May 10, na hapa ni Hyatt Regency hotel huko Trinidad ambapo wajumbe wa Caribbean Football Union (CFU) walialikwa kwenye mkutano maalumu kumsikiliza mgombea kiti cha Urais wa FIFA Mohamed Bin Hammam alipokuwa akiwakilisha sera zake Soma Zaidi Hapa.


Nafasi za Masomo 2011/12 Centre for Foreign Relations

May 31, 2011

Namna Mbwana Ali Samata alivyopokelewa TP Mazembe.

May 31, 2011


TAJIRI WA TP MAZEMBE MOISE KATUMBI CHAPWE AKIMUITA MBWANA SAMATTA KUMTAMBULISHA RASMI KWA VIONGOZI NA MASHABIKI WA TIMU HIYO.

MBWANA ALI SAMATTA AKIMWAGA SPECH KWA MASHABIKI WA TP MAZEMBE.

MBWANA ALI SAMATTA AKIWASILI UWANJANI KWA ULINZI MKALI.

RAISI WA TIMU YA TP MAZEMBE MOISE KATUMBI CHAPWE AKIWASILI UWANJANI KUMTAMBULISHA SAMATTA KWA MASHABIKI WA TIMU HIYO.

Picha na Habari na Shafii Blog.


Werrason kwa Jukwaa balaaa

May 27, 2011

THE BEAT FESTIVAL

May 27, 2011

THE_BEAT_FESTIVAL_1

THE BEAT FESTIVAL

27.05.11 – 20.00 -00.00

venue: Triniti – Msasani rd. 26, Oysterbay DSM

JHIKOMAN – Roots Reggae

www.jhikoman.com

MZUNGU KICHAA – Reggae/World

www.myspace.com/mzungukich

aa

FID Q – conscious HIPHOP

www.facebook.com/fidhop

BONGO BEAT – festival backing band

The Beat is a monthly festival (usually on the last friday of the month) showcasing the best live music from Tanzania and abroad. The festival is hosted by Mzungu Kichaa and features some of the best local and international talent passing through Tanzania.

Triniti (www.triniti.co.tz) provides a relaxed ambience to enjoy good music taking you far away from the cities hustle and bustle, and yet it is still very central. Entrance is only 5k at the door.

Please join this page and hit the like button. 

www.facebook.com/TheBeatFestival

powered by CARAVAN RECORDS

www.myspace.com/caravanrec


Kind Regards,
Caravan Records
MANAGEMENT
Tel: +255 763 822 022
E-mail: kichaamusic@gmail.com

www.myspace.com/caravanrec

www.myspace.com/mzungukichaa
www.facebook.com/mzungukichaa


%d bloggers like this: