Anaconda na Fally Ipupa

September 25, 2013

1235327

Ukitaka kujua ugumu ama urahisi wa kumiliki bendi muulize Muumin Mwinyijuma atakwambia na Tamtam yake, Muulize Asha Baraka na Twanga yake, Muulize Engineer Martin Kasyanju na Ngwasuma yake ama Muulize Ally Choki na Extra Bongo yake.

Lady Jaydee aka Binti Machozi ni mwanamuziki ambaye kama ni kuchora chati ya mafanikio utaona inaanzia chini kabisa na ikienda ikiongezeka kila uchao, tangu amemiliki bendi kuna mara kadhaa amejaribu kuhujumiwa bila mafanikio na anazidi kusonga tuu. Pichani akiwa jijini Nairobi na Mwanamuziki Mahiri Fally Ipupa De Caprio ambaye naye anapasua anga si tu la Africa bali duniani, hii ilikuwa jijini Nairobi, ilikuwa kitu gani? Je wana program pamoja? tega sikio hapa hapa utapata jibu lako. 


Video ya Natamani kuwa Malaika ya Jay Dee iko jikoni

July 16, 2009

Wimbo wa Natamani Kuwa Malaika wakwake LAdy Jay Dee unatamba na Video yake ndio iko mbioni inapikwa sasa na kikosi cha Ogopa Dee Jays toka kwa Baba Moi, kazi ya shooting ya Video hiyo ilifanyika hivi majuzi na inatazamiwa kukamilika na kuanza kuonekana mwishoni mwa mwezi huu wa July au mwanzoni mwa mwezi ujao. Vazi la Jay Dee limebuniwa na Ali Remtullah

Jay Dee akiwa na baadhi ya watoto kwenye shooting ya wimbo huo pale Gymkhana Club

 

Marcell na Lucas wa Ogopa Dee Jays kwenye moja ya location Kwa habari na Picha zaidi mtembelee Binti Machozi kwenye Blog yake.


Lady Jay Dee ni zaidi ya mwanamuziki

April 30, 2009

n590146649_2170467_667435

Ukinitajia mwanamuziki Lady Jay Dee kwangu ninayojinsi  ninavyomuangalia mwanadada huyu. Napenda sana ubunifu alionao na jinsi anavyoimba kwa kutumia sauti asilia ambayo inaandikika kimuziki, nikiwa namaana kuwa muziki wake uko kwenye Note za kimuziki hasa na hivyo kutompa kazi prodyuza yeyote au wapiga vyombo wake.

Nilipopata nafasi ya kuongea na Maneno Uvuruge (Gonga hapa usome mahojiano naye)ambaye kwa wakati fulani aliwahi kufanya kazi na Machozi Band yake Lady Jay Dee anasema kuwa kati ya watu alifanya kazi nao basi hatomsahau Lady Jay Dee kwani walikuwa wakiongea lugha moja “unajua kama mtu anayeimba anaimba kwenye note hupati taabu mpiga ala, ila kama muimbaji anatoka nje ya note anakupa taabu wewe kumfunika ili washabiki wasielewe, alisema Uvuruge ambaye anapiga Solo kwenye Band ya Kilimanjaro Connection inayopiga muziki nchini Malaysia kwa sasa.

Kwangu mimi Lady Jay Dee ni zaidi ya Mwanamuziki.

Hivi karibuni mwanamuziki huyu alitembelea huko mikoa ya kusini na kugawa Vyandarua kwa ajili ya kampeni ya kutokomeza Malaria na huko alikutana na Mwanamuziki maarufu Barani Africa Balozi wa Malaria Afrika Princess Vyone Chaka Chaka.

11

Lady Jay Dee akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda huko Ntwara.

12

Akichangia jambo pamoja na Waziri Mkuu na Yvone Chaka Chaka Kulia.

n590146649_2161315_1150291

akiwa Hospitali na kugawa Vyandarau kwa akina mama wajawazito

Sikiliza kibao cha Siwema toka kwake Lady Jay Dee anayepiga gitaa mwanzo kulia ni Maneno Uvuruge.


Mambo ya Sweet Eazy Jumamosi hii

February 4, 2009

Sweet Eazy, this Saturday, 7 February. See below flyer for details.

Reservations: 0755 75 40 74.

Karibu.

.
.

Lady Jay Dee kuwania tuzo KORA 2008

July 26, 2008
Judith Wambura AKA Lady Jay Dee

Judith Wambura AKA Lady Jay Dee

Mwanamuziki nyota wa Tanzania, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ameteuliwa kuwania tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Afrika Mshariki katika Tuzo za Kora 2008. Kwa mujibu wa gazeti la New Vision la Uganda, Jaydee ni mwanamuziki pekee kutoka Tanzania kuchangulia kwenye kinyang’anyiro cha mwaka huu.

Jaydee ambaye anawania tuzo hiyo pamoja na Susan Kerunen, Klear Kut, Michael Ross na Blu3 kutoka Uganda na nyota wa Kenya, Nameless, Valerie Kimani na Wahu. Mwanamuziki huyo pekee wa bongo fleva kutoka Tanzania anawania kunyakua tuzo hiyo ambayo fainali zake zitafanyika Desemba 6, Tinapa, Nigeria.

Kwa mara ya kwanza msanii bora wa Afrika ataondoka na kitita cha dola za Marekani milioni moja kutoka First Bank of Nigeria. Tuzo za Muziki za Kora ni kubwa Afrika zinazojumuisha wakali kutoka nchi mbalimbali.

Jaydee ambaye amewahi kutwaa tuzo kadhaa za kitaifa na kimataifa aliwahi kuchaguliwa kuwania tuzo za Kora mwaka 2003 (Mwanamuziki wa kike anayechipukia Afrika) na mwaka 2005 (Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika). Katika tuzo za mwaka jana Ambwene Yesaya ‘AY’ alikuwa ni msanii wa Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo hizo. (Na Habari Leo)


%d bloggers like this: