B’AMBI FASHION HOUSE PRESENTS THE GOLDEN MIND FASHION SHOW

April 30, 2010

image

B’AMBI FASHION HOUSE PRESENTS THE GOLDEN MIND FASHION SHOW

On May 8th Brenda Nambi, the designer and owner of Bambi Fashion House will unveil her latest collection called the "Golden Mind Collection". In line with the global fashion trends, Brenda Nambi has created a fashion theme based around the color gold. This elegant and stylish collection is targeted towards hard working, independent women who have achieved their respect without losing their femininity & hence the fashion & style in them.. The Golden Mind Collection will be displayed in a classy fashion show that will take place at the Garden City Rooftop.

Be part of this elegant affair that will attract Kampala’s corporate class, entertainment and fashion personalities, business leaders, and the elite of Kampala’s social scene.  Bambi Fashion House promises an exciting evening of stunning fashion and entertainment.

For tickets or info please call 0782 506 684

Proudly sponsored by Redd’s, Talent 256, The Red Pepper and D Mark


Origin Africa Designer Showcase

April 30, 2010

image

Inaugural “Origin Africa Designer Showcase” was held on 28 April 2010 in Nairobi at the Laico Regency which saw two Tanzanian Swahili Fashion Week designers Robi Morro and Jamilla Vera Swai Launch their new collection.

Tanzania Cotton Board’s (TCB) Textile Sector Development Unit (TSDU) – through the
Organisers’ of the Swahili Fashion Week – had facilitated the participation of Robi Morro and Jamilla Vera Swai.

The work of the Textile Sector Development Unit has been made possible by support from the Gatsby Charitable Foundation and its associated Tanzania Gatsby Trust (TGT). Tanzania Cotton Board wants to ensure that more Tanzanian grown cotton is transformed into higher value added products in Tanzania

**********************

Robi Morro of Mapozi Designs collection is named Garden of Style, which is inspired by the woman.” A woman is like a flower, she blossom well if taken good care of” said Robi. “The pieces are very feminine, flirty, sassy colourful and fun aimed at bringing out the woman’s beauty with the use of bold colourful floral prints.” added Ms Morro.

a Robi Morro Of Mapozi Designs Collection 2010

image 

image

image

 

Jamila’s Collection is named “Say and Color Zero” Inspired by her daughter of two first school homework “Say and Color Zero”. This became her constant routine for every evening. “Her favourite colors being red and black, I decided working with that by layering them by individual colors, with the print zero” said Jamilla.

A Jamilla Vera Swai Collection 2010

image image

 

image

image

image image image

A Jamilla Vera Swai Collection 2010


The Sporah Show kuanza kuonyeshwa Star TV

April 30, 2010

image

Kipindi cha Talk Show cha The Sporah Show kinachoonyeshwa na BET TV kitaanza kurushwa hewani wiki hii kupitia  Star TV.

Nilipofanya mahojiano naye kwa mara ya kwanza takribani miezi minne iliyopita alisema hiyo ilikuwa ni moja ya malengo yake kufanikisha kipindi chake kuonwa na Watanzania hapa nyumbani. Bofya hapa kusoma mahojiano hayo.


Mduariko wa ki beachi beach Chadibwa.

April 29, 2010

PICT0044

Mambo ya mduara haya ndani ya fukwe ya Chadibwa. ni kila Jumamosi.


Hiki ndio kipindi cha kutafuta Nyumba Dasilamu.

April 29, 2010


Ze Comedy bwana… We acha tuu.

April 29, 2010

Sina haja ya kuandika kuhusu kipaji walichonacho jamaa cha kuigiza. Kuna mvua Dar Es Salaam nzima nadhani unahitaji kupanua mbavu kwa kucheka kidogo. Basi anza siku yako na hii.


Interyaichapa Barcelona, yatinga fainali

April 29, 2010

Inter Milan chini ya Jose Mourinho, ilicheza mechi ya kujihami kuizuia Barcelona isifunge zaidi ya goli moja na kufuzu kucheza fainali ya kombe la ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya kwenye mechi iliyochezwa Nou Camp, himaya ya Barcelona.

Jose Mourinho akimpa pole mlinda mlango wa Barcelona, Victor 
Valdes, baada ya Inter kufuzu.

Mourinho ameiwezesha Inter kufika fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1972.

Wakicheza ugenini na faida ya ushindi wa 3-1 walioupata nyumbani, Inter walilazimika kucheza kwa zaidi ya saa moja wakiwa na wachezaji 10 baada ya Thiago Motta kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumfanyia madhambi Sergio Busquets.

Lakini Barca walishindwa kufungua milango ya Inter mpaka mkwaju wa Gerard Pique ulipohitimisha mpambano huo mkali.

Baada ya hapo shambulio la Bojan Krkic lilikataliwa na mwamuzi, na Inter walifanikiwa kulinda idadi yao ya magoli kuweza kucheza fainali ya ligi ya vilabu bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu 1972.

Miamba hiyo ya Italia, sasa itachuana na Bayern Munich katika fainali itakayopigwa uwanja wa Bernabeu tarehe 22 Mei wakati Mourinho atakapoongoza timu yake kuwania taji hilo kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 40.

Jitihada za Barcelona kuwa timu ya kwanza kutetea kombe hilo, ziliisha kwa uchungu kutokana na Inter Milan kucheza kwa kujilinda na kuikatisha tamaa Barcelona iliyoichapa Arsenal jumla ya magoli 6-2 katika hatua iliyopita.


Kama: Utunzi wake Werasson enzi za Wenge Musica.

April 29, 2010

Kuna nyimbo ambazo Werason aliwahi kutunga basi ni huu wa KAMA, enzi hizo bado wakiwa Wenge Musica BCBG.

Kwa wapenzi wa Wenge watakubaliana na mimi kuwa Werasson ni mmoja wa waandishi wazuri sana wa mashairi. ingawa beti zake nyingine alikuwa anawapa watu wengine waimbe. Ukiongelea Wenge ya wakati huo kila mtu alikuwa na jukumu lake, Pengo la mtu kama Blaise Bulla aka Engineer lilikuwa kubwa kwani yeye kazi yake kubwa ilikuwa kuwapanga waimbaji na hata ikibidi kumnyang’anya mtu beti yake kama atahisi beti hii hawezi kuiimba vizuri na kumpanga sauti ya nani iingie baada ya mmoja kumaliza. Si hivyo tu ushirikiano waliokuwa nao ulileta mabadiliko na mageuzi kwenye kizazi cha tatu cha muziki wa Congo.

wakumbukwe daima waliokuwemo enzi hizo Kama JB Mpiana, Werrason, Adolf Dominguez, Patient Kusangira, Sunda Bass, Allain Makaba, Roberto Wunda Ikokota na wengineo ambao walipaisha vilivyo bendera ya Wenge Musica BCBG.


Man City yaomba isajili kipa wa muda

April 29, 2010

image

Manchester City imeiandikia Bodi ya Ligi Kuu ya England ikiomba iruhusiwe isajili mlinda mlango kwa mkopo wa dharura hadi msimu huu utakapomalizika.

BBC imegundua kuwa Bodi ya Ligi Kuu ya England huenda ikatoa idhini kwa City kusajili mlinda mlango wa muda kuziba pengo la mlinda mlango wao Shay Given aliyeumia.

Shay Given hataweza kucheza katika michezo mitatu iliyosalia kabla ligi haijamalizika baada ya bega lake kuchomoka siku ya Jumamosi walipotoka sare ya kutofungana na Arsenal.

Stuart Taylor ambaye ni mlinda mlango wa akiba naye hali yake si nzuri, Joe Hart anachezea Birmingham kwa mkopo, hali inayowafanya kuwa na mlinda mlango mmoja tu Gunnar Nielsen.


Dafu na Samaki wa kuchoma … Duh!

April 29, 2010

IMG_1463

Samaki wa Kuchona.

 IMG_1453

Mambo ay Kimalay, Menu hii ni dafu na Samaki wa Kuchoma kwenye jani la mgomba, hii kali kwelikweli.


KFF yapinga kutengwa katika soka Kenya

April 29, 2010

Katika mgogoro unaoendelea, shirikisho la soka la Kenya, KFF, baada ya kupoteza rufaa katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo, kutaka litambuliwe kusimamia soka ya Kenya, limesema halikubaliani na uamuzi unaonufaisha wapinzani wao, FKL.

Mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo, The Court of Arbitration for Sport (CAS), iliamua kuwa Football Kenya Limited (FKL) ndiyo itasimamia shughuli za soka nchini Kenya.

Lakini Kenya Football Federation (KFF) imesema haikubali na inapinga uamuzi huo. "Hatubaliani kabisa na uamuzi huu, tumeshangazwa sana," mwenyekiti wa KFF , Sam Nyamweya alieleza.

Shirikisho la soka la duniani Fifa linaitambua FKL kama mamlaka halali ya kusimamia soka ndani ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Mgogoro baina ya pande hizo mbili umekuwa ukiunguruma kwa zaidi ya miaka sita.

"Endapo CAS inasema sisi siyo wanachama wa Fifa na hatukutakiwa kwenda CAS, basi walitakiwa kukataa kesi yetu tangu mwanzo," Bw Nwamweya alisema.

"Tunasubiri wanasheria wetu watushauri kuhusu hatua tunazoweza kuchukua na ninakuhakikishia kuwa tutachukua hatua."


Rooney mchezaji bora wa mwaka wa PFA

April 28, 2010

image

Wayne Rooney amechaguliwa mchezaji bora wa mwaka wa Chama cha Wacheza soka wa Kulipwa ama Professional Footballers Association(PFA).

Mshambuliaji huyo wa Manchester United aliyekwishafunga mabao 34 msimu huu, amewashinda wachezaji wengine walioteuliwa akiwemo Didier Drogba, Carlos Tevez na Cesc Fabregas.

Rooney, mwenye umri wa miaka 24, amesema: "Najisikia vizuri kushinda tuzo hii kwa sababu kura zimepigwa na wachezaji wenyewe. Kwa hiyo ni heshima kubwa na nasikia raha."

Tuzo ya mchezaji bora kijana imekwenda kwa James Milner wa Aston Villa.


“Tanzanians are supporting homegrown brands more than ever before”

April 28, 2010

image

The unchallenged popularity of hip hop culture in Tanzania would suggest that after a decade-plus of local creativity there should now be a lively local urban fashion industry, supported by today’s popular artists and media.

Indeed, there have been a few local initiatives, from hip hop artists releasing their own gear (remember Gangwe Gear, sported by Gangwe Mobb around 2001?) to businessmen attaching their name to locally produced jeans. But the transition from ‘localized’ international fashion to truly innovative signature products is a slow one, and successful local fashion brands have been few.

One of the shining stars in the urban clothing industry in Tanzania is Kina Clothing. Started by recently remigrated Tanzanian Mkuki Bgoya and his business partner Susan Mosi, within a few months Kina managed to create a buzz and a rising demand; they even got the attention of some copycats.

Africanhiphop.com spoke to Mkuki about the philosophy behind the brand, the cultural landscape of East Africa in 2009, the much heralded resurgence in international interest in the African continent and how this benefits young people in Africa, and the existence of a uniquely Tanzanian fashion identity.

Click here to read more!


Snoop Dogg; “Nataka kumfundisha Beckam ku-rap”

April 28, 2010

image

Rapper maarufu Snoop Dogg ametangaza dhamira yake ya kutaka kumfundisha mchezaji maarufu wa mpira wa Miguu David Beckham kufoka (rap) akisema kuwa Beckham atangara sana kama akiamua kuingia kwenye Muziki huo.

Beckham alikutana na Snoop wakati wakifanya shooting ya tangazo la Adidas ambalo linatarajiwa kutoka karibuni.

“Beckham and I go way back. He’s like a brother. I’m gonna show him to rap, for shizzle. He’s my boy. He was terrific with my kids and they had a great time as he taught them how to shoot and score the perfect goal,”  alisema Snoop akikaririwa na mtandao wa female.co.uk

Nataka kumsaidia Beckham maana kwenye soka anaumizwa kila siku, hivyo najitolea kumfundisha ku rap. aliongeza Dogg.

Pata picha mzee mzima kashika mic itakuwa si ya kitoto.


Wimbo wa Kombe la Dunia Africa Ya Kusini 2010; Chameleon Feat Kelly Rowland, 2face, Samini, Krotal, Awadi, Rola, Jozi – Everywhere You Go

April 28, 2010

siku 43 kabla ya kufikiwa kwa michuano ya kombe la dunia 2010 kuanza huko South Africa , tayari wanamuziki na ma kampuni mbali mbali wamesha toa ikiwemo nyimbo na matangazo kama chachu ya kutangaza Michuano hiyo mikubwa ulimwenguni kupigwa huko Africa kusini

  MTN wameachia wimbo ambao ni wa World unaoitwa “Everywhere You Go” alioimba mwanmuziki kutoka Uganda Dr. Chameleon akishirikiana na wanamuziki master mbali mbali kutoka Africa pamoja na US. Walioshirikishw katika wimbo huo ni pamoja na Kelly Rowland US, Nigeria’s 2face Idibia, Ghana’s Samini, Cameroon’s Krotal, Senegal’s Awadi, Rola, South Africa’s Jozi, Zuluboy, pamoja na Kwesta, Slikour. Nyimbo hiyo ya mahadhi ya mirindimo ya ki sasa zaidi ni kama R & B mwanzoni wimbo na sehemu ya pili ya wimbo huo ipo katika mahadhi ya kitamaduni na mchanganyiko wa reggae. Hongera chamilion twangoja kuona utakacho kifanya huko Africa kusini lakini pia kutuburudhisha zaidi.

Na Malkia wa Bambataa


Gloson; Blogger mtoto ashinda tena!

April 28, 2010

image

niliwahi kuandika kuhusu huyu mtoto Gloson, Blogger mdogo toka Malaysia ambaye kwa kiasi kikubwa amejizolea umaarufu duniani kote kwani pamoja na umri mdogo ameshatunga vitabu viwili vya mashairi akiwa amenyakua zawadi kadhaa kwenye category yake upande ya poetry.

hivi karibuni mtoto huyu alijishindia zawadi kemkem baada ya kuibuka mshindi kwenye shindano la ku Blog kuhusu  Territory ya Malaysia (Blog4FT (Federal Territories) contest!).

Yeye aliandika kuhusu likizo yake kwenye jiji la Kuala Lumpur ikiwa ni hadithi kwa njia ya Picha zaidi(Gonga hapa).

Mara ya kwanza nilipomuona kwa macho yangu ilikuwa wakati wa maadhimisho ya kampeni ya kitalii ya Visit Malaysia katika jengo la KLCC nchini Malaysia, na kipindi hicho alikuwa na miaka 10 tu. nilivutiwa sana naye kwani aliandika poetry nzuri sana kuhusu theme hiyo. Tangu hapo nikawa mfuasi wa Blog yake.

Gloson ameandikwa kwenye vyombo vingi sana vya habari ndani na nje ya Malaysia, Hii yote ni kutambua mchango wake na kipaji chake.

Huu ulikuwa utambulisho wangu miaka miwili iliyopita niliandika kuhusu mtoto huyo kipindi hicho akiwa na miaka 10 tu.

Gloson, 10 Years Old

Gloson, 10 Years Old

Jina Gloson kwa Malaysia limekuwa si geni kwenye vyombo vya habari hasa baada ya kuandikwa sana kw mwaka jana namaanisha nusu ya mwisho ya mwaka jana.

Gloson ni mtoto wa miak 10 lakini ni Blogger anayekuja kwa kasi akiwa na miezi si zaidi ya saba kwenye ulimwengu huu wa magazeti tando, Kipaji chake si tu kwa kublog bali ni uwezo mkubwa alionao wa kujieleza, mara ya kwanza nilisoma kwenye gazeti la The Star haikuniingia hadi nilipoona akihojiwa kwenye Chanel kubwa ya Tv3 na kumuona kwa macho yangu.

Dogo anakipaji kweli kweli na ye anasema ana blog kila kitu anachoona kina manufaa kwa jamii na katika blog yake pia amefundisha jinsi ya kuandika Post yenye mvuto na jinsi ya kuchangia topic bila kwenda nje ya mada, akiwa ni wanafunzi wa shule ya msingi Gloson anasema alipata wazo la Ku blog toka kwa mama yake ambaye alimshauri ablog naye akaanza.

Mbali na kipaji hicho pia Gloson anakipaji cha kuandika mashairi akiwa meshaandika zaidi ya mashairi 100 ambayo yamechapishwa http://www.poetrytalents.com

Ikiwa na miezi 6 tu tangu ianzishwe blog ya Gloson ambayo inakwenda kwa anuani ya http://www.glosonblog.com/

Nafurahi ninapo share nilichojifunza na wenzangu

"Nafurahi ninapo share nilichojifunza na wenzangu"

“naamini nina mchango kwa jamii mengi waweza kujifunza toka kwangu na kuelimika, kuna mengi yakujifunza kwenye mtandao, napenda Internet naweza kufanya kila kitu kuanzia Homework, games, kununua vitu na kuwasiliana na vitu, alisema Gloson alipohojiwa kwenye Tv3. “kuna vitu siwezi kuwaeleza wazazi wangu moja kwa moja lakini huwa natuma email na naenda kulala nikiamka baba atanijibu ama kwa email au hata akikaa kimya najua anatafakari na amepata ujumbe wangu” aliongeza mtoto huyu anayejua kujieleza kwa lugha ya ufasaha na kufanya wtangazaji wote kucheka.

Pamoja na vipaji hivyo pia Gloson anakipaji cha kutumia Photoshop kwa ajili ya kucheza na picha, na ni mtundu wa mambo ya mtandao pia.

Si mbaya mtembelee hapa utakuta mengi sana ya kujifunza toka kwake. Wana Blog wenzangu mpooo!!!!?


Habari njema kwa wenye watoto wenye matatizo yanayohitaji matibabu nje.

April 28, 2010

image

Kwa Kushirikiana na SickKids Hospital ya Toronto, natafuta watoto wagonjwa, chini ya miaka 14 ambao wanahitaji operation moja ili wapone na kwamba matibabu hayo hayapatikani Tanzania. Matibabu yote ni bure hospitali; na gharama za kuishi huku kwa mtoto na baba au mama najitolea mimi. Tunaweza kuanza maongezi sasa na tukaonana nikija March. Pia napenda kuwajulisha kwamba Serikali ya Canada, kupitia CIDA, "imetangaza" kutoa "misaada" zaidi kwa Tanzania na Ghana kwa mambo ya afya. Nina imani serikali ya Tanzania imejulishwa tayari.

Kama una ndugu yako, jirani yako au mtoto unamjua, tafadhali wasilisha report ya Daktari pamoja na maombi kwa anuani hapo chini:-

Mabula Sabula
Executive Vice President
Dillon-Kaijuka Associates, Inc.

108 S. Joliet St., Joliet, IL. 60436 USA
Investment & Development Services   
Tel:   +1312-376-8106  E- Fax: +1206-337-1688 Skypename:mabsab

Website: www.dillonkaijukaassociates.com 

Email:  contact@dillonkaijukaassociates.com
Canada: Tel:    +1416-546-6542  Cell:    +1647-281-6474 

Email:  mabsab@hotmail.com  or mabsab@rogers.com

Au wasilisha kwangu najua jinsi ya kumfikishia Ndugu Mabula.

piusmicky@yahoo.co.uk, Tel: +255 713 666616 au Zilete Chuo Cha Diploamasia, Kurasini – Dar Es Salaam,

ulizia Ndugu Pius Mikongoti.

NB: Ndugu Mabula ni Mtanzania na alikuwa hapa nchini siku chache zilizopita, Naomba tutumie nafasi hii kwa wale wanaowajua watoto wote wenye matatizo ilimradi wako chini ya miaka 14. Asanteni.


Inaugural “Origin Africa Designer Showcase”

April 28, 2010

image

Collection Made from Local Fabrics Made in Tanzania
Inaugural “Origin Africa Designer Showcase” will be held on 28 April 2010 in Nairobi at the Laico Regency. It is hoped that this will promote opportunities for local talent and local manufacturers to work together to develop a strong African fashion industry.

It is aimed to raise awareness about Africa as a preferred sourcing destination and to give up and coming designers the chance to work alongside industry leaders in designing apparel with commercial appeal and African flair. Its also to provide an opportunity for designers to present their latest designs and talents as well as providing a platform to create new networks, to promote and profile to the world at large, African fashion; where Origin Africa celebrates innovation, resourcefulness and design, that is uniquely African.

The Designer Showcase shall bring along designers from Kenya, Uganda, Ethiopia and Tanzania at this industry event only. Tanzanian Designers showcasing the Ready to wear Collection are Jamilla Vera Swai and Robi Morro of Mapozi Designs.

Jamila’s Collection is named “Say and Color Zero” Inspired by her daughter of two first school homework “Say and Color Zero”. This became her constant routine for every evening. “Her favourite colors being red and black, I decided working with that by layering them by individual colors, with the print zero” said Jamilla.

Tanzania Cotton Board’s (TCB) Textile Sector Development Unit (TSDU) – through the Organisers’ of the Swahili Fashion Week – has facilitated the participation of Robi Morro and Jamilla Vera Swai.
The work of the Textile Sector Development Unit has been made possible by support from the Gatsby Charitable Foundation and its associated Tanzania Gatsby Trust (TGT). Tanzania Cotton Board wants to ensure that more Tanzanian grown cotton is transformed into higher value added products in Tanzania

“If more Tanzania fashion designers showcase their designs regionally and internationally that this will have a positive impact upon Tanzania’s textile industry – especially that part of the industry that makes kanga and Kitenge cloths.” said Mark Bennett, Textile and Apparel & Trade Specialist for the Textile Sector Development Unit.
“We would hope that stylish Tanzania made clothes – made from kanga and Kitenge cloths become essential fashion items in the West” concluded Mr. Bennett.

Robi Morro of Mapozi Designs collection is named Garden of Style, which is inspired by the woman.” A woman is like a flower, she blossom well if taken good care of” said Robi. “The pieces are very feminine, flirty, sassy colourful and fun aimed at bringing out the woman’s beauty with the use of bold colourful floral prints.” added Ms Morro


UNDER TEHE SAME SUN WAKUTANA NA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA!!

April 28, 2010

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Rais na muasisi wa Under The Same Sun, Peter Ash (kushoto) kutoka Canada ambaye ni albino na na Mkurugezi wa Utawala wa Under The Same Sun, Paul Ash kabla ya mazungumzo yao kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 26, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Message Sent….!

April 27, 2010

image


%d bloggers like this: