Stars, Brazil kuonyeshwa mataifa 160

May 31, 2010

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Leodegar Tenga akifafanua kuhusu ujio wa timu ya Brazil, kulia ni mratibu wa ujio wa timu hiyo, Philpe Huber kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam .Picha na Fidelis Felix.

PAMBANO la soka la kimataifa kati ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Brazil litaonyeshwa katika mataifa 160 duniani kupitia Global TV ya Brazil.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa habari jana kwenye Hoteli ya Movenpick Dar es Salaam kuwa hiyo itasaidia wachezaji wa Tanzania kutangaza soka yao kimataifa.
“Ni nafasi ya wachezaji wa Tanzania kujitangaza katika mataifa hayo 160 duniani na wahusika wa utalii watakuwa na nafasi ya kuutangaza utalii wa Tanzania,” alisema.
Brazil itawasili nchini Jumapili Juni 6, saa 4:00 usiku ikitokea Afrika Kusini ikiwa na kundi la wachezaji 23 na wajumbe wengine 37 na Jumatatu watacheza mechi yao hiyo itakayoanza saa 12:00 jioni na wataondoka baada ya mchezo huo.

gonga hapa kusoma zaidi


Mourinho sasa ni meneja wa Real Madrid

May 31, 2010

Klabu ya Real Madrid ya Uhispania imetangaza kwamba itamjulisha Jose Mourinho rasmi kwa mashabiki wao, Jumatatu ijayo.

Jose Mourinho

Mourinho atajulishwa kwa mashabiki wa Real siku ya Jumatatu

Klabu kilitoa taarifa kuthibitisha hayo.

Marais wa vilabu vya Inter Milan ya Italia, na Real Madrid, walikutana Ijumaa mjini Milan, Italia, kutatua masuala yote, hasa ya kifedha, kuhusiana na Jose Mourinho kuhama kutoka Inter, na kuelekea Uhispania.

Real Madrid wameshawahi kunyakua ubingwa wa Ulaya mara tisa.

Jose Mourinho anaondoka Inter baada ya msimu uliokuwa wa fanaka mno, kupata ushindi katika mashindano matatu muhimu Italia, ikiwa ni pamoja na kuwa klabu bingwa barani Ulaya.

Hata hivyo klabu ya Inter haikutoa maelezo kamili katika taarifa hiyo, kuhusu mapatano hayo kati ya rais wa klabu Massimo Moratti na mwenzake wa Real, Florentino Perez.

Lakini vyombo vya habari nchini Uhispania vimekuwa vikielezea kwamba Inter watapata euro milioni nane, ambazo ni sawa na dola milioni 9.80.

Mourinho aliiongoza Inter kupata vikombe vitatu muhimu, na alimalizia kwa ushindi katika fainali ya klabu bingwa Ulaya, dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani katika uwanja wa Bernabeu, mjini Madrid.


Kili Ripkin na Not You

May 31, 2010

Peace and Love Family Finally I Present to you the long awaited video by Kil Ripkin titled "Not You" Directed by Science Projects and Produced by Eric G, The Balancing Act out Soon.

Kili Ripkin


mpigie kura ay ashinde tunzo za MUSEKE AWARDS

May 28, 2010

Chaguo la Teenz na Kili Awards tumekamata n’ I believe niko na support kubwa nyuma yangu that’s y tunashinda. Now ni tym ya Museke Awards. u can vote kwenye website yao for free na mara nyingi utavyoweza ili AY ashinde.
Niko kwa 5 Categories:
Artist of the year / Best Male / Best Collaboration (feat. Avril n’ Wahu) / East African Song (Leo; original version) / Hip Hop Song (Leo:Original version).
ingia www.awards.museke.com kisha vote kwa AY.. Awards zitafanyika tarehe 1 June
ONE!


Elton John asababisha utata Morocco

May 28, 2010

Na BBC

Mwanamuziki wa Uingereza Elton John anatarajiwa kuwepo katika tamasha nchini Morocco licha ya kuwepo wito wa kuzuiwa.

Wapiganaji wa kiislamu wamejaribu kuzuia mwaliko wake huo, wakidai kuwa mwanamuziki huyo aliyeweka wazi kuwa anafanya mapenzi ya jinsia moja anaenda kinyume na maadili ya umma.

Lakini waratibu wa tamasha la Mawazine huko Rabat wametetea uamuzi wa kumwalika John, kwa madai ya "kustahamiliana kimaadili".

Elton John

Elton John

Wiki iliyopita, tamasha lililopangwa kufanywa huko Misri liliahirishwa baada ya John kusema katika mahojiano ya jarida moja kuwa Yesu alikuwa anafuata mapenzi ya jinsia moja.

Mkurugenzi wa sanaa wa tamasaha la Mawazine Azizi Daki ameiambia BBC kuwa wanatarajia umati mkubwa kujitokeza kwenye oneysho lake.

Amesema, " Kawaida umati mkubwa ni takriban watu 40,000."

" Usiku wa leo tunatarajia takriban watu 60,000 kuja kumwona Elton John."

Bw Daki amesema hii ni mara ya kwanza kwa John kufanya onyesho Morocco na ana umaarufu sana nchini humo.

Amesema, " Kipaji chake kimekuwa cha kuridhisha sana, anawafanya raia wa Morocco wawe na matumaini na kila mmoja anajua nyimbo zake."

Wasanii maarufu

Lakini mapema mwezi huu, chama cha Islamist Justice and Development (PJD) lilipinga onyesho hilo la John.

Read the rest of this entry »


Mayaula Mayoni Afariki Dunia

May 28, 2010

image

Mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mayaula Mayoni amefariki dunia huko Ubelgiji. Kwa mujibu wa habari tulizozipata Mayaula alikuwa akisumbuliwa na kansa ya Ubongo.

Mayaula (64) aliwahi kuishi Tanzania wakati baba yake akiwa ni afisa muandamizi wa Ubalozi wa Zaire ya wakati huo na katika kipindi chake MAyaula aliwahi kuchezea klabu ya Yanga ya Jijini Dar Es Salaam.

Pata kibao cha Doudou A Mwen toka kwake Marehemu MAyaula Mayoni.


50 Cent: Get Skinny Or Die Tryin’

May 28, 2010

Die-hard 50 Cent fans won’t recognize the rap superstar in a new photo that has surfaced in US Weekly

The normally buff and chiseled G-Unit head lost 54 pounds for a role in Things Fall Apart, a movie he wrote and stars in, about a promising college football player who gets cancer.

"I was starving," the 6-foot artist, who reduced his weight from 214 pounds to 160, told the magazine. To lose the weight, 50 walked three hours a day on a treadmill for nine weeks and lived on a liquid diet.

When the shocking photo hit the web, some speculated that he was sick, but a longtime spokesperson said that was not the case.

"I can confirm that he is indeed okay," the spokesperson told Yahoo! Music.

Clearly, the rapper born Curtis Jackson takes his acting just as seriously as his music. He recently discussed having some of his tattoos surgically removed because it affected his film career, requiring him to be on set for several additional hours each day for extra makeup.

He has multiple films in preproduction, and previously appeared in Get Rich Or Die Tryin’, Home Of The Brave, and Call Of Duty: Modern Warfare 2.

Things Fall Apart costars Ray Liotta, Lynn Whitfield, and Mario Van Peebles, who also served as director.

Follow Me on Twitter.


%d bloggers like this: