Ya Mheshimiwa Mr II na Ruge yanaongeleka

November 28, 2011

rugesugu

Mwaka jana June 30, 2010 niliandika makala yangu nikisema Sugu na Ruge malizeni tofauti zenu kimya kimya.  Mpaka leo ni takribani mwaka mmoja na miezi miwili na siku kama mbili tangu makala yangu. Makala ile niliandika ikiwa ni baada ya kutokea sintofahamu ambayo ilipelekea Mheshimiwa Mbilinyi kuwekwa ndani kwa kile kilichodaiwa kusambaza CD ambayo ilikuwa ikimkshifu Bwana Ruge.

“Hakuna wa kumhukumu mwengine hapa ila mi nasisitiza tu tofauti hizi zisiwagawe wadau wa burudani, zisiwagawe wasanii kwani sekta ya burudani ndio pekee inayoweza kuondoa tofauti za kisiasa baina ya makundi ya vijana na zinawakutanisha vijana wengi zaidi wenye utashi na mtaguso tofauti tofauti, Waziri Mheshimiwa John Nchimbi chukua hatua kulimaliza hili na naimani kwako linawezekana na kufikiwa muafaka.”

Katika makala ile nilijaribu kuwakumbusha wote wawili wajibu wao kwa jamii ikiwa Mheshimiwa Mbilinyi Kama msanii ambaye jamii inamuangalia yeye kwa ulimwengu wa sasa vijana wengi wanakuwa wakiwafatilisha wasanii na kwa upande mwingine kwa Ruge ama yeye binafsi au kama taasisi ana mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya vijana kutokana na ukweli kwamba yupo kwenye chombo ambacho anawagusa vijana wengi sana na kirahisi zaidi.

Kwa sasa Mheshimiwa Mbilinyi si msanii tu bali ni sehemu ya chombo muhimu ambacho kinatunga sheria kwa nchi, Bunge ni taasisi nyeti na kubwa yenye heshima kubwa, kwa safari ya Mheshimiwa Mbilinyi hakika haya ni mafanikio makubwa si tu kwake bali inaonyesha nguvu ya Sanaa nzima ya muziki kwa mara ya kwanza imetoa Mbunge.

Sitaki kuongelea chanzo cha mgogoro wao hapa kama unataka kujua basi bofya hapa

Katika makala yangu ile nilijaribu kuelezea ikiwa tofauti hizi zikiachiwa nini kinaweza kuwa madhara si tu kwa wahusika bali hata kwa sekta nzima ya burudani. majuzi tulishuhudia tamko naweza sema zito toka kwa Mheshimiwa Mbilinyi akisema kwa msisitizo kuwa Mkoa wa Mbeya hawataki tamasha la FIESTA ambalo linaandaliwa na kuratibiwa na Prime Time promotion na Clouds Media Group. Bado ukiangalia hapo chanzo ni zile zile tofauti ambazo wadau wa burudani tunazijua. Tofauti ambazo zinahitaji kuongelewa ili kuzimaliza nachelea kusema hilo linawezekana kwani hata biff zao zikiendelea hakuna kinachoweza kubadilisha kilichoshatokea.

Tofauti hizi ni hatari hasa kwa sekta ya burudani na wasanii kiujumla kwani kunakuwa na mgawanyiko na kuwatia uwoga wasanii wale ambao wanahisi wangetaka kumshirikisha Sugu kwa namna yeyote iwe kikazi au kimawazo kwani kufanya hivyo ni hatari kwa kazi zao kisanii ama kwa kuogopa kuingia kwenye malumbano au kwa nyimbo zao kutopigwa redioni au kwenye TV Stesheni kabisa. Ni wazi kuwa hakuna kituo cha redio kinachomilikiwa na Clouds Media Group kinaweza kucheza wimbo wowote wa Mheshimiwa Mbilinyi kwa sasa, hapo ndipo tulipofikia na huo ni ukweli usiopingika.

Kwenye makala yangu nilionyesha wasiwasi mkubwa nilisema hizi tofauti zenu hazitoishia hapo tuu mtazipeleka au zitawapeleka mbali, Majuzi tumeshuhudia malumbano mengine na kwa wakati huu ikiwa katika chombo cha juu kabisa cha kutunga sheria pale Mheshimiwa Mbilinyi ambaye ni waziri kivuli wa Vijana na Michezo alipokuwa akichangia hotuba ya Mheshimiwa waziri Nchimbi kwa kile kilichotafsiriwa kuwa ilikuwa ni muendelezo wa tofauti zile zile ambazo niliziandika hapo awali.

Ingawa mchango wa Bwana Mbilinyi ulilenga kuwatetea maslahi ya wanamuziki lakini kwa upande mwingine ilikuwa ni shutuma za moja kwa moja kwa Bwana Ruge na Taasisi ambazo zinahusiana na yeye ama moja kwa moja au kikazi.

Pamoja na kuwa Mheshimiwa Mbilinyi alikuwa anatetea maslahi ya wanamuziki serikalini, mwisho wa siku Serikali inatengeneza platform kwa taasisi binafsi kama hizo za Prime time Promotion na ukiangalia ndio zinazotoa ajira kwa wasanii hawa. Tangu tamko la juzi la Sugu Bungeni hakuna msanii yeyote aliyediriki kumuunga mkono hadhani, kwenye gazeti, radio au hata mitandao jamii !! JE unadhani hakuna ambao wanakubaliana na Sugu kwenye hili? Jibu ni kuwa wapo lakini wanajua madhara ya kuonyesha kumuunga mkono Mbilinyi. Na ndio hasa kiini cha makala yangu hii najaribu kuangalia athari za mgogoro wa mafahari hawa wawili kwa sekta nzima ya burudani ikigusa vijana zaidi.

Kwani kwa sasa Muziki unaajiri vijana wengi zaidi jambo linalopelekea kupunguza tatizo kubwa la ajira kwa vijana.

Sasa kwanini tufikie hapo? ni bora kuwakalisha hawa wawili na naamini kabisa Waziri husika anaouwezo wa kufanya hili kwani Waziri mwenyewe ni kijana na jambo hili linagusa wadau wake kwa kiasi kikubwa. kwani wengi wa waathirika kwa namna yeyote ile ama iwe upande wa Mheshimiwa Mbilinyi au upande wa Taasisi ambazo zinamhusu Ruge kibinafsi au kikazi waathirika bado ni vijana.

Baada ya pale Bwana Ruge alitoa Tamko ambalo kwa walipata kumsikiliza utakubaliana na mimi alionyesha kukerwa sana na kilichotokea na binafsi yake alivunja ukimya kwa kujibu shutuma zile moja baada ya nyingine.

Katika waraha huu wa Bwana Ruge aliongelea kukashifiwa kwa Clouds Media, THT na yeye binafsi na alitoa maelezo marefu ambayo mwisho wa siku si mimi na wala wewe msomaji unaweza kubadilisha mtazamo wa wawili hawa.

Mheshimiwa Waziri alipokuwa akijibu hoja za Bwana Mbilinyi alisema kwa utani Mheshimiwa Mr Sugu ni Sugu Kweli kweli kwani hoja hizi tulishazijibu zaidi ya mara moja na bado amezileta Bungeni. Kama alijibiwa na bado amezileta Bungeni basi ujue kuwa kuna ambacho haridhiki nacho ila ni kipi inawezekana kuna anachokijua zaidi.

Hakuna wa kumhukumu mwengine hapa ila mi nasisitiza tu tofauti hizi zisiwagawe wadau wa burudani, zisiwagawe wasanii kwani sekta ya burudani ndio pekee inayoweza kuondoa tofauti za kisiasa baina ya makundi ya vijana na zinawakutanisha vijana wengi zaidi we utashi na mtaguso mbalimbali, Waziri Mheshimiwa John Nchimbi chukua hatua kulimaliza hili na naimani linawezekana na kufikiwa muafaka.

Ni mtazamo tuu.

  


Shaggy kutumbuiza Nane Nane Leaders

July 25, 2008
Shaggy akikamua

Shaggy akikamua

MWANAMUZIKI wa miondoko ya Ragga kutoka nchini Marekani, Shaggy atawasili nchini Agosti 7 kwa ajili ya kutumbuza katika siku kuu ya Wakulima, maarufu kama Nane Nane, kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.

Shaggy, ambaye jina lake halisi ni Orville Richard Burrell na ambaye kwa sasa anatamba na vibao cha ”Bonafide Girl”, ”Sexy Lady” pamoja na ”Why Me”, atakuwa akifanya ziara ya pili nchini baada ya kuja mwaka 2006 kuja na kukonga nyoyo za mashabiki.

Mkurugenzi wa Prime Time Promotions, Godfrey Kusaga alisema mwanamuziki huyo ataongozana na wasanii mbalimbali maarufu kama Fabian Smith,Robert Livingstone, Maro Gordon na wengine wengi.

”Shaggy ataambatana na wasanii na wanamuziki 15 na watatumbuiza ‘laivu’ ili wasanii wa hapa nyumbani waweze kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwake,” alisema.

Kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa ni Sh 7000 na Kusaga alisema wameweka kiwango cha chini ili kila shabiki aweze kushuhudia onyesho hilo la mwanamuziki anayetamba duniani.

Alisema wanatarajia kuwa onyesho hilo litafungua sura mpya katika utamaduni wa matamasha nchini.


%d bloggers like this: