Michael Jackson ‘hakufanyiwa hila’

June 29, 2009

 

Na Mwandishi wa BBC

Waombolezaji wa Michael Jackson

Madaktari waliochunguza kifo cha mwanamuziki maarufu wa mtindo wa Pop, Michael Jackson, aliyefariki dunia Alhamisi, wamesema matokeo ya awali hayajaonyesha hila yoyote.

Lakini vipimo vingine vikiwemo vya sumu vimechukuliwa ambapo uchunguzi wake unaweza kuchukua majuma kadhaa, ofisi ya mchunguzi wa vifo vya Los Angeles ilieleza.

Maafisa wamesharuhusu ndugu kuuchukua mwili wa Jackson, lakini bado hakujawa na taarifa zozote kuhusu mazishi yake.

Waombolezaji wakiwemo wasanii wenzake, viongozi wa mataifa mbali mbali na mashabiki wamekuwa wakitoa rambi rambi zao kwa mwanamuziki huyo.

Jackson aliyekufa akiwa na umri wa miaka 50, siku ya kifo chake alikimbizwa hospitalini huko Los Angeles, Marekani, baada ya kupata matatizo yanayodhaniwa kuwa ya moyo.

Picha za maisha ya Michael Jackson

Taarifa za awali zilieleza kuwa mwanamuziki huyo alikuwa hapumui wakati madaktari wa huduma ya kwanza walipofika kumsaidia nyumbani kwake maeneo ya Bel Air yapata saa sita na nusu majira ya huko. Lakini mwishowe maafisa wakathibitisha kifo chake.

Utata mkubwa uligubika hali ya afya ya mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na albamu mbali mbali kama Thriller.

Maoni ya kifo cha Michael Jackson

Wavuti ya TMZ ambayo huandika taarifa za watu mashuhuri katika maswala ya burudani ilikuwa ya kwanza kuandika kuwa Michael Jackson mwenye umri wa miaka 50 alikuwa ameaga dunia.

Vile vile, gazeti maarufu la Los Angeles Times liliandika katika wavuti yake kuwa Michael Jackson amefariki. Lakini vyombo vingine vya habari vilikuwa vikisema alikuwa bado yu hai, ingawa alikuwa mahututi.

Picha za maisha ya Michael Jackson

Madaktari wa huduma ya kwanza walijaribu kuuzindua moyo wa Jackson wakati gari ya wagonjwa ilipokuwa ikimkimbiza katika hospitali ya UCLA, maafisa wameeleza.

Jackson alikuwa akitarajiwa kuanza matamasha mbali mbali ya kufufua kipaji chake kwenye ukumbi wa O2 jijini London ifikapo tarehe 13 Julai.

Imeelezwa alikuwa na historia ya matatizo ya kiafya na hajawahi kukamilisha ziara ya matamasha kwa kipindi cha miaka 12 iliyopita.

Maoni
Utakumbuka kitu gani kuhusu maisha ya mwanamuziki Michael Jackson? Tuandikie nasi tutayachapisha maoni yako katika wavuti hii.


Wakenya walamba nafasi za mwanzo Standard Chartered KL Marathon-Malaysia

June 29, 2009

image

Washiriki wa Standard Chartered KL Marathon 2009 toka Kenya  Julius Karinga (centre) akiwa amekula pozi na washindi wenzie, mshindi wa pili Nelson Kirwa Rotich (right) na mshindi wa tatu  Armon Kipchichir Kemei (left). Mashindano hayo yalifanyika siku ya Jumapili jana hapa Kuala Lumpur na kushirikisha washiriki zaidi ya 12,500 toka kila pembe duniani na kushuhudia wakenya wakishika nafasi zote tatu za mwanzo. Gonga hapa Kwa habari zaidi, Mshindi wa kwanza aliondoka na Cash USD 20,ooo pamoja na zawadi nyingine toka kwa wadhamini mbalimbali.


Kilimanjaro Connection waiaga Malaysia kwa show ya kufa mtu!!

June 28, 2009

DSC01185

Faijala Mbutu mpiga gitaa mahiri wa The Kilimanjaro Connection Band akiwajibika jukwaani wakati wa shoo yao ya mwisho jijini Kuala Lumpur jana, huyu ni mume wa Luiza Mbutu wa Twanga Pepeta.

Kundi la Muziki wa Dansi la The Kilimanjaro Conections Band jana walifanya shoo yao ya mwisho kuwaaga mashabiki wao wa Malaysia kabla ya kuondoka kurejea nyumbani kwa mapumziko mafupi. Shoo ya jana ilikuwa ya kufa mtu na kuhudhuriwa na mamia kwa mamia ya mashabiki na kufanya ukumbi wa Rum Jungle kuwa mdogo.

Kundi hili ambalo lilikuwa nchini Malaysia kwa takribani miezi sita limejizolea umaarufu na kuitangaza Tanzania kwa kiasi kikubwa baada ya kuwa gumzo na story na picha zao kutawala kurasa za burudani kwenye magazeti yote ya Malaysia.

Siku ya jumatatu wana morogo walitumbuiza kwenye ukumbi wao wa Rum Jungle na mara baada ya kumaliza kiongozi wa bendi Kanku Kelly alitangaza kuwa wiki hii ni ya mwisho kwao na kuibua kelele za simanzi toka kwa mashabiki na akina dada walishindwa kuvumilia na kububujikwa na machozi kwani Rum Jungle palikuwa kiota mwanana kwa wale wapenzi wa Live Band.

The Kilimanjaro Connections Band wako pia kwenye mazungumzo ya awali kwa ajili ya mikataba zaidi ya maonyesho huku Mashariki ya Mbali.

Bendi hii inaongozwa na wanamuziki hodari Kanku Kelly mwenyewe anayeimba na kupiga Konga, Trampet na ala nyingine, pia yumo Faijala Mbutu huyu ni mume wa Luiza Mbutu wa Twanga Pepeta, hali kadhalika kuna Maneno Uvuruge anayepiga gitaa la solo, huyu bwana hupagawisha watu kwa umahiri wake wa upigani solo na jinsi anavyomchezesha mwanadada Queen Suzy, Wengine ni Geofrey Kumburu anayecheza Keyboard, Sijali Moris ambaye anapiga Drums kama Papito Mbala bila kuwasahau wataalamu wa sauti Delphine Mununga na Modester Nyoni mdogo wake Luiza Ntoni au Luiza Mbutu wa Twanga.

DSC01189

Mcharaza gitaa la solo Maneno Uvuruge kulia huku Queen Suzy akiwajibika kwenye kipaza sauti, Queen Suzy amebadili style na kwa sasa anaimba na kucheza awali alikuja kama mcheza show wa kundi hili, Hongera mama.

DSC01188

wakipanda wanamkorogo panakuwa hapatoshi.

DSC01186

Mbutu kushoto, Kanku Kelly katikati na Queen Suzy wakiwa kazini.

DSC01181

Kutoka kulia ni Delphinus Mununga, Modesta Nyoni (mdogo wake Luiza Nyoni au Luiza Mbutu), Kanku Kelly and Farijala Mbutu.

image

We acha tuu

image

Bango la wanamkorogo kwenye klabu ya Rum Jungle.


Michael Jackson afariki dunia.

June 26, 2009

image

Mwanamuziki wa mkali wa Pop Duniani Michael Jackson amefariki dunia. Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la CNN Michael Jacksom amefariki dunia na alikutwa katika jumbalake la kifahari huko Bel-Air akiwa mahututi, habari za awali zinasema alipata Stroke.

Kwa mujibu wa Polisi na msemaji wa kikosi cha Fire Cap. Steve Ruda alisema kuwa walipokea simu ya 911 toka kwenye jumba la Michael walipokwenda walimkuta akiwa katika hali mbaya na kumpa huduma ya kwanza kabla ya kumshamishia UCLA Medical Centre. Mamia kwa maelfu ya waandishi walikuwa wamekusanyika nje ya Hospital hiyo ambapo habari za ugonjwa na uvumi wa kufariki Michael Jackson ambaye amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi ulimwenguni zilikuwa zimeenea kote kwa kasi ya ajabu.

Michael amefariki akiwa na miaka 50. Mwezi huu unaokuja Michael alitazamiwa kutangaza kustaafu muziki rasmi kwa show kubwa ambayo ilipangwa kufanyika nchini Uingereza

Mungu aiweke roho ya marehemy mahala pema peponi-Amen.

Nakuacha na kubao They Don Care about us toka kwake marehemu Michael Jackson


Michael Jackson afariki dunia.

June 26, 2009

image

Mwanamuziki wa mkali wa Pop Duniani Michael Jackson amefariki dunia. Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la CNN Michael Jacksom amefariki dunia na alikutwa katika jumbalake la kifahari huko Bel-Air akiwa mahututi.

Kwa mujibu wa Polisi na msemaji wa kikosi cha Fire Cap. Steve Ruda alisema kuwa walipokea simu ya 911 toka kwenye jumba la Michael walipokwenda walimkuta akiwa katika hali mbaya na kumpa huduma ya kwanza kabla ya kumshamishia UCLA Medical Centre. Mamia kwa maelfu ya waandishi walikuwa wamekusanyika nje ya Hospital hiyo ambapo habari za ugonjwa na uvumi wa kufariki Michael Jackson ambaye amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi ulimwenguni zilikuwa zimeenea kote kwa kasi ya ajabu.

Michael amefariki akiwa na miaka 50. Mwezi huu unaokuja Michael alitazamiwa kutangaza kustaafu muziki rasmi kwa show kubwa ambayo ilipangwa kufanyika nchini Uingereza

Mungu aiweke roho ya marehemy mahala pema peponi-Amen.

Nakuacha na kubao They Don Care about us toka kwake marehemu Michael Jackson


We Can….!

June 25, 2009

image

Shabiki wa timu ya Taifa ya USA akiwa ameshika picha ya Rais wa USA Mh. Obama wakati wa mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Confederation huko Afrika ya Kusini kati ya USA na Spain ambapo USA iliushangaza ulimwengu kwa kuwabwaga Spain 2-0.


Wengi wamzika Nasma

June 24, 2009

image

Mume wa marehemu  Bw. Omary Kilongole (Pili kulia) akiwa na waombolezaji wakisoma dua katika maziko ya mkewe NAsma Hamisi Kidogo makaburi ya Kisutu jana. Picha na GPL

Waombolezaji wengi walijitokeza katika kuaga safari ya mwisho ya mwanamuziki Nasma Hamis Kidogo ambaye alifariki dunia ijumaa jijini Dar Es Salaam.

Nasma Hamis ambaye ameacha watoto sita alifariki dunia baada ya kupatwa shinikizo la damu. wanamuziki wakutoka makundi mbalimbali ikiwa ni Taarabu, muziki wa kizazi kipya, kwaya, bendi za dansi, waigizaji na watangazaji wa Luninga na Radiao walikuwepo nyumbani kwa baba mdogo wa marehemu na makaburini kwa ajili ya kumsindikiza mpendwa wao Nasma, mazishi yalifanyika katika makaburi ya kisutu huku waombolezaji wakiongozwa na mume wa marehemu Omary Kilongole.

Baadhi ya nyimbo alizotamba nazo msanii huyo ni Mwanamke mazingira,Subira Heri,Mpenzi na sanamu la michelin,pia enzi za uhai wake aliimbia vikundi kadhaa kikiwemo Egyptian,Babloom,Tanzania One Theatre na Muungano Cultural Troup. marehemu ameacha watoto sita wawili wa kiume na wanne wakike, na wajukuu wawili.


%d bloggers like this: