Robinho akanusha kubaka!!

January 29, 2009

.

.

Mchezaji anayeongoza kwa kusajiliwa kwa gharama kubwa Mbrazir Robinho amekanusha shutuma ambazo zime failiwa police dhidi yake kwamba amemnyanyasa kijinsia binti wa miaka 18 ambaye kisheria inasomeka kama ubakaji.

Ingawa haijasemwa wazi alichokifanya hasa Robinho hanbari zinasema alimshika maungo kwa kumdhalilisha binti huyo bila idhini yake.

Habari kutoka kwa msemaji wa mchezaji huyo Chris Nathaniel zinasema kwamba Robinho alihojiwa na police na si kwenli kwamba alikamatwa bali alikutana na Polisi kwa utaratibu ambao pande zote mbili zilikubaliana. Pia aliongeza kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi wa shutuma hizo na Robinho mwenyewe amesema yuko tayari kushirikiana na Polisi.


Chelsea yaibuka kidedea kwa Man City kwenye “Mchezo wa Kitajiri”

September 14, 2008
Wachezaji wa Man City wakimpongeza Robinho baada ya kupachika bao la kwanza dhidi ya mchezo wao na Chelsea leo

Wachezaji wa Man City wakimpongeza Robinho baada ya kupachika bao la kwanza dhidi ya mchezo wao na Chelsea leo

Klabu ya Chelsea usiku huu imeibuka mbabe wa mchezo kati yake na Man City kwa kuitungua mabao matatu kwa moja (3-1) katika mchezo “wa kitajiri” uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa.

Huku akilipa limbikizo la ada ya uhamisho ilovunja rekodi ya Paund £32.5million, Robinho aliweza kuwafanya Man City waongoze dakika ya 13 ya mchezo kwa kupachika bao safi la free kick na kufanya Man City iongoze, bao lao lilidumu kwa dakika tatu tu kwani Chelsea kupitia kwa Ricardo Carvalho iliweza kuasawazisha bao lile na kufanya ngoma kuwa droo mpaka mapumziko, Dakika ya Frank Lampard alipachika ao safi la pili kwa Chelsea na kufanya mayowe ya Man City kuanza kuzizima, Chelsea walizidi kulisakama langoo la Man City na kufanikiwa kuongeza kimoja kupitia kwa mchezaji mkongwe Nicolas Anelka na kufanya mabao kuwa 3-1. Hata hivyo nahodha John Terry alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kucheza madhambi.


Brazil yaitungua Chile 3-0

September 8, 2008
Robinho

Robinho

Mchezaji wa Brazil Robinho akishangilia bao lake kwenye mchezo wa kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia Afrika Kusini 2o1o dhidi ya Chile. Kwenye mchezo huo Brazil ilishinda 3-0. Robinho amesajiliwa na Man City ambao kwa sasa wanataka kumsajili Ronaldino pia.


Man City wamnyakua Robinho

September 2, 2008
Roginho

Robinho

Manchester City wamefanikiwa kuwazidi kete Chelsea kwa kumchukua Mbrazili forward Robinho toka klabu ya Real Madrid kwa rekodi ya uhamisho ya kwa UK ya £32.5m.

Chelsea wamekuwa wakimfukuzia mchezaji huyo mwenye iaka 24 lakini Man City wamefanikiwa kumnyakuwa kwa mkataba wa miaka minne.

“Binafsi nafurahi kufanya kazi na kijana mdogo mwenye uwezo na akli ya mpira awapo uwanjani, tunafarijika kuwa ataleta changamoto ya ushindi kwenye timu yetu alisema Boss wa Man City  Mark Hughes  kwa mujibu wa Mtandao wa BBC.

Baada ya kusikia habari za Man City klabu ya Chelsea imekiri kumkosa Robinho ni pigo kwenye mikakati yao lakini pia imehakikisha kikosi ilichonacho kinatosha kufanya mambo kwa vikombe.


Brazil yamtema Robinho kikosi cha Olympic

July 22, 2008
Robinho

Robinho

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Brasil na Real Madrid ya Hispania Robinho jana ametemwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kitakachokwenda kwenye ngija ngija za kuwania medali ya dhahabuu kwenye michezo ya Olympic huko China imefahamika leo.

Sababu za kumtema Robinho zimesemwa kuwa ni kutokana na machezaji huyo kuwa majeruhi kwa mujibu wa daktari wa timu ya Real Madrid.

Hata hivyo Shirikisho la soka la nchini Brazili limelaani uamuzi wa Real Madrid na kuuita wa dharau kwa nchi yao na wabrazili kwa ujumla kwa kusema hizi ni njama za kutaka kumtumia mchezaji huyo. akizungumzia sakata hilo, daktari wa timu ya Brazili Luiz Alberto Rosan alisema kuwa alijua kuwa Robinho ni majeruhi lakini bado alikuwa na nafasi ya kupona kwani aliumia kidogo sio vya kumfanya ashindwe kucheza kwa muda mrefu. Aidha akiongea juu ya sakata hilo Robinho mwenye miaka 24 anayecheza nafasi ya forward alisema kuwa amesikitishwa na kuikosa nafasi ya kuichezea timu yake kwenye mashindano muhimu ya Olympic huko Beijing.

Akizungumzia suala hili agent wa Robinho Wagner Ribeiro alisema sijawahi kumuona Robinho aliwa na huzuni kiasi a hiki, mara ya mwisho ni kipindi mama yake mzazi alipotekwa nyara na maharamia mwaka 2004. ingawa baadaye aliachiwa bila kudhuriwa.


%d bloggers like this: