Flaviana Matata; Mrembo mwenye style yake ya nywele

January 12, 2008

.

Mlimbwende Flaviana Matata

Unapoongelea sekta ya ulimbwende kwa walimbwende wetu wa ndani na nje ya Tanzania, basi hutoacha kumtaja Flaviana Matata, tofauti ya mlimbwende huyu na wenzake wanaofanya shughuli za ulimbwende ndani na nje ya nchi yetu ni uzuri wa asili na staili yake ya nywele ,tangu ang’are kwenye ulimwengu huu wa Ulimbwende Flaviana amekuwa na stayle ya ya kukata nywele ndogo na hajabadilisha style ambayo imekuwa ni alama yake, Mrembo huyo ni matunda ya Bibiye Mariah Sarungi wa Compass Direction ambaye amekuwa na mafanikio katika shughuli hizi za Urembo, ni hivi karibuni tuu Mariah Sarungi alimuandaa mlimbwende mwingine Miriam Odemba alifanya vizuri kwenye shindano la Miss Earth lililofanyika huko Phillipines. Hongereni walimbwende.


%d bloggers like this: