Tuzo ya Sembene katika ZIFF 2010

March 31, 2010


Tuzo ya Ousmane Sembene katika ZIFF 2010.

Mshindi kupata kitita cha Dola 5,000/=

Shirika la GTZ likishirikiana na Tamasha la nchi za Jahazi (ZIFF) kwa mara ya tatu tena mwaka huu 2010 watatoa tuzo ya Filamu ya Ousmane Sembene, tuzo hii italenga hasa katika filamu fupi ambazo hazijazidi dakika 20 na ambazo zitakua zimezungumzia au kugusia masuala yanayoikabili jamii ya kitanzania hasa katika mambo ya Ukimwi, Jinsia, Elimu na umasikini.

Mshindi atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani 5,000 taslimu papo hapo kwaajili ya kumsaidia katika kutengeneza filamu nyingine ama kuboresha kazi zake.

Wale wote watakaotaka kushiriki katika tuzo hii wawasilishe filamu zao kabla ya tarehe 30/04/2010 kwa kujaza fomu za kawaida zinazopatikana katika tovuti yetu

www.ziff.or.tz

Daniel Nyalusi

Events and Film Program Coordinator

Zanzibar International Film Festival


Albamu ya Wagosi hatimaye yaingia sokoni

March 31, 2010

image

Baada ya kukwaruzana na Serikali na kulazimishwa kusimamishwa kuingia sokoni kwa Albamu ya Wagosi wa Kaya inayojulikana kama
“miaka 10 ya maumivu” hatimaye albamu hiyo imeruhusiwa na serikali.

Akiongea na mtandao huu kitaa mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo Mkoloni amesema kuwa “tuliambiwa tubadilishe baadhi ya maneno kwenye baadhi ya nyimbo ambayo kimsingi serikali iliona kuwa na uchochezi na tumefanya hivyo” alisema Mkoloni. Sasa mambo ni shwari na Mpango mzima uko sokoni.

Vijana wa Muziki wa kizazi kipya wamekuwa wakiimba mara nyingi kuhusu mapenzi ni mara chache kwa vikundi au mtu mmoja mmoja anaamua kushikia bango matatizo ya kijamii jambo ambalo lingekuwa jukwaa zuri la kufikisha ujumbe wa machungu ya wananchi huku chini. Kila la heri wagosi.


Rangi ya Chungwa waikumbuka?

March 31, 2010

Hii ilikuwa Rum Jungle Club, Kuala Lumpur MAlaysia mapema mwaka jana ambapo Kilimanjaro Connection chini ya Mkubwa Kanku Kelly walikuwa wakifanya vitu vyao hapo.

Huwa nafikiria kuwa kuna uwezekano kuwa wanamuziki wa zamani walikuwa na vipaji sana hasa kupanga sauti na vyombo kwani ukiangalia Technolojia ya zawani na jinsi muziki ulivyokuwa ukipangiliwa na kusikika vizuri basi utakubaliana na mimi kuwa wanamuziki walikuwa na vipaji sana kwani siku hizi muziki wote unatumbukizwa kwenye Computer na kuchujwa na vyombo vingine viko Computerized hali inayopelekea wapiga vyombo wasipate taabu sana hata waimbaji kwa ajili ya kuetengeneza na ku balance sauti.

Kwa heshima na taadhima naomba wimbo huu wa Rangi ya Chungwa uwaburudishe wapenzi wa muziki wa nyumbani… Kakam Benny Wissa upoo? yako hii kaka. Wimbo huu ulipigwa miaka hiyo sijui mpigani naomba nikumbushwe lakini hapa umepigwa tena na The Kilimanjaro Connections Band.


Mayi ya Sika ya Werrason

March 31, 2010

Binafsi ukiniuliza napenda nini kwa Werrason nitakwambia Sebene ila Kuna watu wanaitwa Werrasonique hawa ni wapenzi damu wa mwanamuziki Ngiama Makanda Werrason, ni kazi kuwabadili mawazo kuhusu jamaa huyu kama ilivyo Pius na JB Mpiana, hawa bwana nakupeni burudani wote Pdg Le Big Prodyuza Maghambo Philipo popote ulipo tuko pamoja sana tuu, Boss Chizenga, Ally Tandika, Bob Rashy, Boss Chizenga na wengine wote wapenzi wa Werrason.


Manchester Utd Mbendembende kwa Bayern Munich, Rooney ajeruhiwa

March 31, 2010

image

Bayern Munich walinyakuwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester United katika dakika za mwisho mwisho za raundi ya kwanza ya robo fainali za michuano ya kilabu bingwa Ulaya.

Manchester United walikuwa wamebahatika angalau kujinyakulia pointi moja wakati walikuwa wamefungana 1-1 mnamo dakika 90 za mchezo.

Lakini katika dakika za nyongeza, Ivica Olic alimpokonya Evra mpira, akapiga chenga moja, mbili, tatu na kusukuma mkwaju pembeni mwa goli.

Man U walianza kwa matumaini makubwa wakati mshambulizi matata Wayne Rooney alipopachika bao la kwanza mnamo dakika mbili za kwanza.

Ili kujiondolea aibu ya kushindwa nyumbani, Bayern Munich ambao walikuwa wamepoteza nafasi nyingi murua katika kipindi cha kwanza walirejea na mikikimikiki.

Franck Ribery alipiga mzinga ambao uligonga guu la Rooney na kumwacha kipa Van der Sar kuusindikiza na macho tu.

Kuna wasiwasi kwamba Rooney amepata jeraha la mguu na alionekana akitembea kwa uchungu.

Hili ni tukio ambalo litawakera mashabiki wa Man U wakati wakijiandaa kuonana na Chelsea katika mechi kali ya ligi kuu hapo Jumamosi.

Katika mechi nyingine kwenye kundi hilo, Lyon waliitandika Bordeaux 3-1.


March 30, 2010

Nahodha wa Arsenal Cesc Fabregas haijafahamika kama ataweza kucheza siku ya Jumatano mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya Ubingwa wa Ulaya dhidi ya Barcelona baada ya kuumia mguu.

Fabregas anatibiwa kutokana na kuchubuka vibaya mguu wake na goti wakati wa walipotoka sare na Birmingham siku ya Jumamosi na siku ya Jumanne hakufanya mazoezi.

Naye kiungo wa Barcelona Andres Iniesta imefahamika hatacheza mchezo huo wa siku ya Jumatano.

Iniesta alitolewa wakati wa mapumziko siku ya Jumamosi walipoifunga ba0 1-0 Real Mallorca.


Wamtambua nani hapa?

March 29, 2010

image

Hawa ni ma dancer wa Twanga Pepeta Internationally, Je wamtambua nani hapa?


%d bloggers like this: