Maswali…

March 31, 2011

Wananchi wakiwa wamepanga foleni kuulizwa maswali kwa Mh. Waziri wa Ardhi Prof Anna Tibaijuka.

Posted with WordPress for BlackBerry.


Mkutano unaendelea…

March 31, 2011

Posted with WordPress for BlackBerry.


Mamia ya wana Kigamboni wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Prof. Anna Tibaijuka

March 31, 2011

Wananchi wakimsikiliza Pro. Anna Tibaijuka kuhusu mradi wa Mji wa Kisasa, Mvutano ni mkubwa kati ya wananchi ambao wanataka kujua hatma yao.

Posted with WordPress for BlackBerry.


Waliko Blaise Bula, Didier Masela Mpela na wote walianza wenge pamoja

March 31, 2011

Kwenye Video hii utamuona Didie Masela ambaye alikuwa akipiga Gitaa la Bass, Hapa alialikwa na JB kuonyesha cheche kwenye moja ya show za Mukulu.

Msomaji wangi Simon Peter alitaka kujua walipo baadhi ya wanamuziki wa Wenge BCBG, ningependa kujua walioko wakina Blaise Bula, Didier Masela Mpela na wote walianza wenge pamoja na the all time best one and only lady dancer, Pia kuna aliyetaka kujua aliko Cele Bulla.

Ni kweli kabisa kwa sasa Ingenieur Cele Bulla a.k.a. Blaize Bulla AZONGI na KIN,amerudi kinshasa congo baada ya kukaa Ulaya muda mrefu,anasema ukitaka kupiga hatua kimasoko na kipato katika muziki mahali salama ni congo kuliko ulaya,kama mtakumbuka baada ya wenge musica bcbg 4*4 kugawanyika 1997,

...

Cele alibaki na JB wenge bcbg wakafanya album moja TITANIC then Blaize akajiondoa kwa J.B.Mukubwa na kuamua kutoka solo,akatoa album yake ya kwanza ikiitwa PONDERATION, Ikafanya vizuri tu ndani ya Congo nadhani hata nje pia,baadae akaja na Bana balia Ngando.Sasa hivi amekuja na album mpya na bendi yake.

Alain Mpela “Afande”

...

Mpela yeye yuko kivyake sanasana amekua akishirikiana na yule mdogo wake aliekuwa kwa Le Rambow du zaire papaa na didi stone koffii charles Antoine Olomide mopao le shake spear de Kinshasaa aitwae Bouro Mpela,tayari wanayo album ya pamoja ambayo ni mikono ya Producer ALAIN PRINCE MAKABA a.k.a.”INTERNET” inaitwa MORTEL COMBAT,

Alain makaba Prince

...

Makaba kama ulivyoona hapo yeye kwa sasa ni producer anamiliki studio yake mwenyewe huko Brussels,Belgium.Le foundee Didier masela KUNA Kipindi baada ya kujitoa kwa werrason alijiunga na jeshi la congo lakini akaacha baadae,kwa sasa yupo Kinshasa na mara moja moja amekua akishiriki shows za J.B.Mpiana kama mwanamuziki mualikwa,unaweza kucheck moja ya shows angalia video hapo juu alipoalikwa utamuona gitaa lake la bass kama kawaida yake full kuchangamka stejini.

 

Big Tata Adolphe Dominguez

...

Dominguez  yeye yupo na bendi yake ya wengee tonytonya.


Wanachotamani wachorwaji kama wangekutana na wachoraji!

March 30, 2011

...

Picha hii ni ya kuchora na imechorwa na Cartoonist ambaye anajaribu kuyaweka kwenye mchoro mawazo ya wachorwaji kama wakikutana ana kwa ana na wachoraji.


Yanga 2-1 Azam jioni hii

March 30, 2011

...

Azam walamba ice cream zao wenyewe!


Gongolamboto tuko pamoja na Japani tuko nanyi pia.

March 30, 2011

...

FAIR PLAY; Mshabiki akionyesha bango la kuwafariji Gombo la Mboto na Japan pia, Hii ilikuwa kwenye mechi uwanja wa Taifa baina ya Taifa Stars na Jamhuri ya Kati. Sehemu ya mapato ya mechi hiyo ambayo ni asilimia moja (1%) yalitolewa kwa ajili ya waathirika wa mabomu wa Gongo la Mboto, na jana wametangaza kuwa takribani Tsh Milioni moja na ushehe ikiwa ni asilimia moja ya Milioni mia imetolewa kwa ajili hiyo.


%d bloggers like this: