King Blaise si huyu!

August 25, 2008
FM Academia

FM Academia

Mwanamuziki wa FM Academia King Blaise wa kwanza kushoto anaonekana walipokuwa kwenye onyesho kwa ajili ya vunja jungu huko Tabata, onyesho ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo. King Blaise alisemekana kutimlia Uholanzi (gonga hapa uisome) na baadaye habari toka kwa mshabiki nambari One wa FM Academia Big Producer Maghambo aliniahakikishia kuwa King Blaise atarudi na ataonekana jukwaani muda si mrefu na anakuja na Albamu yake (solo) inakwend kwa jina la Tumpokee Mfalme. (Picha na Muhidini Issa Michuzi).


Yu wapi King Blaise??

August 11, 2008
King Blaise

King Blaise

Mtunzi na mwimbajiwa Bendi ya Muziki wa Dansi nchini FM Academia King Blaize inadaiwa ameikacha Bendi hiyo na kutimkia Majuu, chanzo chetu cha habari kinasema Blaize kwasasa yupo nchini Uholanzi kwa kile kinachodaiwa kwenda kutafuta Maisha.

Ni karibia muda wa mwezi mmoja washabiki wa FM wamekuwa hawamuoni jukwaani walipotaka kujuwa ni wapi yupo Mkali huyo wa sauti ya kulalamika msemaji mmoja kutoka katika bendi hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema Blaise kwasasa yupo Uholanzi akisaka maisha baada ya kuona mambo hayamuendei sawa hapa Tanzania. Read the rest of this entry »


%d bloggers like this: