Watu wametoka mbali jamani

August 3, 2008
.

.

Wa Kwanza Kushoto ni Shagie Sharufa, Modogo Gian Franco Fere, Marehemu Mama Mere Malou (Maddame ya Porto) na Papa Wemba. Kwa faida ya wasomaji wangu, Mama Mere Malou alikuwa Mkongo anayeishi Paris Ufaransa, alishiriki kwa kiasi kikubwa kuukuza na kuutangaza muziki wa Kongo bara Ulaya, alikuwa ndio mdhamini na mpokezi wa wanamuziki wa Kongo kila wakifanya ziara Ufaransa.
Hii ndio “starehe” ya burudani, Big Producer Maghambo umesomeka.


Msiba wa Mama Mere Malou na Zadio Kongolo

July 8, 2008

Msiba wa Mama Mere Malou na Zadio Kongolo

Titina ambaye ambaye alimuwakilisha Koffi na Quartier Latin na Mpiga Gitaa la Rhythm wa Wenge BCBG Alba ambaye alimuwakilisha JB Mpiana na Wenge BCBG wakiwasili msibani.
Papa Wemba (wa pili) akiongoza waombolezaji kubeba jeneza la mama Mere Malou, Inasemwa kuwa Marehemu Mere Malou alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mzee Papa Wemba.
Fallu Ipupa Di Cap akiwa na Producer maarufu Manuru vaka kwenye msiba wa Mere Malou. Fally alitoa rambi rambi ya Euro € 1,500 kwenye msiba huo.
Kuna Post inayosema Zadio Kongolo shabiki namba mojawa Wenge BCBG,

Kwenye maoniya post hiyo Kuna mdau analalamika kuwa huyu bwana si maarufu kama tunavyomkuza na kusema hakwenda Bruxelles kwa ajili ya Onyesho la BCBG, ila alikwenda kwa ajili ya msiba wa Mama Mere Malou “madame ya poto“, ukweli ni kwamba kuna tofauti kubwa tangu mama Mere Malou afariki alizikwa siku ya Jumamosi tarehe 29 ya Mwezi March kwenye Makaburi ya jumping Jack na Onyesho la JB Mpiana lilikuwa tarehe 3 May 2008 huko huko Bruxelles. Si nia ya safu hii kubishana bali ni katika hali ya kuwekana sawa. Kwa faida ya wasomaji wangu, Mama Mere Malou alikuwa Mkongo anayeishi Paris Ufaransa, alishiriki kwa kiasi kikubwa kuukuza na kuutangaza muziki wa Kongo bara Ulaya, alikuwa ndio mdhamini na mpokezi wa wanamuziki wa Kongo kila wakifanya ziara Ufaransa.
Hii ndio “starehe” ya burudani, Big Producer Maghambo umesomeka.

%d bloggers like this: