Kali ya Zecomedy

August 30, 2009

Unajua kipaji cha kuchekesha mtu kwenye  nchi kama Tanzania ambayo theluthi ya wakazi wake hawana uhakika wa kula yao ya kesho si jambo dogo kama unavyofikiria. anyway naweza sema jamaa wanafikiria sana hawa.


hata kama mpende jirani yako ndio hivi kweli!!! lol

August 28, 2009

image


Werrason in the Taj Pamodzi Hotel Zambia.

August 27, 2009

image

[image]
[image]
[image]
[image]

Werason Makanda na kundi zima la Wenge Musica Maison Merre WMMM hivi karibuni alifanya onyesho la kufa mtu huko Zambia ikiwa ni muda mfupi angu onyesho la mwanamuziki mwinine Nguli Koffi Olomide nchini humo ambapo Wanamuziki wa Condo wanatamba.

Werason alikonga nyoyo za mashabki kwa sebene zake na alicheza nyimboo mchanganyiko mpya na za zamani. Wacheza shoo wa werason waliweza kuchengua mashabiki vilivyo kwa mujibu wa Huy guy Mpeye ambaye anasema mashabiki hawakuweza kukaa kwenye viti muda wote. hata hivyo kwa mashabiki wa Werason wanaliona pengo la wanamuziki walotoka hasa mcheza shoo Bibiciya Mfwengi ambaye hivi karibuni alirejea kwa koffi kwa mbwembwe.


Montana Kamenga atoka kivyake!

August 27, 2009

image

Montana Kamenga ambaye aliwahi kutamba sana na ndugu yake General Defao na baadaye kuhama, kwa sasa anatamba na albamu yake ambayo iko sokoni inayokwenda kwa jina la Conclusho Renverso Albamu hii inasemwa kuwa ina nyimbo nzuri na kwa mujibu wa Digitaoll Congo inasemwa kuwa Albamu imepokelewa vizuri na mashabiki.

Nakukumbusha enzi za Montana akiwa na Big Stars


Lini wataitwa timu ya Taifa hawa?

August 27, 2009

nizar akinyanyasa

 

Pichani juu ni Mchezaji Nizar Khalfan ambaye aliwika na Taifa stars kwa sasa yuo ughaibuni alicheza soko huko.

Nizar ni mmoja ya wachezaji wachache wa Tanzania ambao wanacheza soka la kulipwa huko nje ya Tanzania lakini tunafaidikaje na wachezaji hawa bado hatujaona.

Miaka ya nyuma soka letu lililega lega sana na watu walitupia lawama kwa serikali kuitekeleza timu ya Taifa lakini kwa sasa hakuna sababu hiyo kwani wadhamini wengi wamemwaga pesa nyingi kwenye timu ya Tafa jambo ambalo watu wanahoji ni nini kinatukwambisha?

Binafsi huwa najiuliza kwa nini wachezaji hawa walioko nje ya nchi ambao wanatamba kwa namna fulani kwenye timu zao hawaitwi kwenye timu ya taifa kuna mchezaji kama Kali Ongala, Deo Njohore, Nizar Khalfan na wengine wengi ambao wanacheza nje, naimani uzoefu wao unahitajika katika kuchanganya akili ya mpira na vipaji. Vipaji tunavyo lakini je vipaji vinaendelezwaje?

Picha kwa hisani ya Michuzi Blog


Mwanamitindo aliyehukumiwa viboko ahairishiwa hukumu kwenye Mwezi mtukufu.

August 25, 2009

image

Mwanamitindo Sari Dewi akilakiwa na Baba yake mzazi mara baada ya kurejeshwa nyumbani na maofisa wa Mahakama ya Kadhi hapo jana.

Mwanamitindo Kartika Sari Dewi Shukarno jana aliachiwa huru na mahakama ya kadhi ya jimbo la Pahang hapa Malaysia.

Kartika ameachiwa huru kwa sababu ya mfungo wa mwezi mtukufu. Awali ilifahamika kuwa Kartika alichukuliwa nyumbani kwa baba yake alipokuwa tangu aliposomewa hukumu yake kwa ajili kwenda Gereza la Kajang ambapo alitakiwa kwenda kutumikia adhabu yake ya kuchapwa viboko sita kwa kosa la kunywa pombe hadharani. Hata hivyo hukumu hiyo siyo kuwa imefutwa bali imehairishwa hadi mwezi mtukufu utakapokwisha.(Gonga hapa kwa habari zaidi)

image

Mfano wa jinsi adhabu ya viboko kwa akina mama inavyotekelezwa hii ni Indonesia.


Century man: Rooney afunga goli lake la 100 Man U walipomchapa mtu 5-0!!

August 23, 2009

image

Wayne Rooney amefunga goli lake la 100 akiwa na Man U kwenye mechi iliyowapa nguvu mpya, ari mpya na kelele mpwa mashabiki wa timu hiyo baada ya mwanzo mbaya na kufungwa na wiki iliyopita. Manchester United jana aliwafunga Wigan bila huruma bao 5-0 mabao ambayo yalifungwa kipindi cha pili.

Katika mchezo wa jana mabao wawili ya Rooney yalimuwezesha kuwa na magoli 101 katika timu ya Man U.

Owen ndiye aliyefungua karamu ya magoli kwa kupachka bao la kwanza kitokea benchi.

image

Dimitar Berbatov alifunga bao la pili na la mwisho lilifungwa na Nani.


%d bloggers like this: