Nawatakia Uzinduzi mwema Mashujaa Band lakini ninalo la kuwaambia.

November 28, 2012

Kwa mashabiki wa Muziki wa dansi watakubaliana na mimi kuwa Mashujaa Band ni moja ya bendi ambazo kwa kiasi kikubwa zimeleta ushindani mkubwa kwenye muziki wa dansi nchini ambao kwa muda mrefu ulikuwa umetawaliwa na bendi mbili za FM Academia na Twanga Pepeta.

Mashujaa wamekuwa wapinzani wakubwa wa Twanga bendi ambazo zinapiga muziki unaofanana, inawezekana ushindani huu unatokana na wamiliki wake kuwa maswahiba na kuchochewa na wanamuziki ambao wametoka bendi moja kwenda bendi nyingine hasa Twanga kwenda Mashujaa. Leo tunashuhudia Mashujaa wakizindua albamu yao ya Risasi kidole huku wakisindikizwa na nguli wa muziki barani Afrika Jean Bedel Tshituka Mpiana na bendi nzima ya Wenge BCBG. kwa wanaojua muziki wa Tanzania watakubaliana na mimi bendi hizi zimeleta mapinduzi na nafikiri MAshujaa wataweza kumfanya JB Mpiana aige kitu kutoka kwao na kesho na sisi tuseme JB Mpiana ametuiga.

Tulishuhudia Simba na YAnga zikitamba kwa muda mrefu leo hii hakuna aliyetegemea timu kama Azamu inaweza kuleta upinzani kwenye ligi ya Tanzania, mapinduzi haya katika sekta ya burudani ndiyo yaliyoibeba leo hii Mashujaa kuwa hapo ilipo, kwa nini mashabiki wawapende nyinyi na sio Twanga au bendi nyingine ni wazi kuwa wanataka kitu kipya na hakuna mwingine wa kuwapa hicho kipya zaidi yenu. Mashabiki ni wale wale ni lazima mjifunze ni nini kilipungua kwenye bendi nyingine ili nyie mkifanyie kazi kuwapa raha mashabiki, naurahi kuwaona kwenye mitandao jamii kwani mnasogea karibu na mashabiki ili waweze kuwapa mawazo yao, lakini kumbukeni ninachosema mimi hapa wapo wengi huko nyuma ambao hawana platform kama hii ya kuongelea, hatuandiki kwa nia mbaya ni kiroho safi tuu ili tuweze kujenga na kuendeleza muziki wetu wa dansi nchini.

Majuzi wanamuziki wa Mashujaa walikuwa kwenye kipindi cha Baragumu cha Channel Ten na wakinadi uzinduzi wao ambapo mashabiki wengi walipiga simu kuwapa usia na mawaidha mengi akiwemo rafiki yangu Mwaulanga. labda mi ningeongezea kidogo, Mara ya mwisho JB Mpiana anakuja nchini nilifanikiwa kuwepo kwenye kutano na waandishi wa habari na kati ya maswali aliyoulizwa ni jinsi gani anaweza kudumisha nidhamu ya wanamuziki wake ikizingatia wanawapenzi na mashabiki wengi, JB Mpiana alijibu kuwa hawaruhusu kunywa pombe kupita kiasi, kula vitu vya baridi, kunywa pombe siku ya show, huku akimtolea mfano Zulema ambaye alikuwa na tatizo la ulevi na kuwajibishwa. Ukiangalia jibu hili la JB Mpiana na jinsi ambavyo wanamuziki wa Bongo wanavyofanya utakubaliana na mimi kuwa bado tuna kazi ya kufanya.

Kwa wanamuziki wa Tanzania ulevi ni kitu cha kawaida, hawana muda wa kupumzika na ndio maana unakuta wengi wao wanakaaa kwenye chat kwa muda mfupi sana. huwezi kuwachukua wanamuziki wa bendi zetu na kuwakuta wanaimba masaa mawili mfululizo au play list ya nyimbo saba lazima unamkuta mtu amepotea jukwaani, mara nyingine hata verse yake inafikia ye hayupo jukwaani ama yuko na akina dada au kashikiria chupa ya lager akisogoa na mashabiki. mara ya mwisho JB Mpiana alipopiga pale Blue Pearl Ubungo Plaza alipiga non stop ya masaa kama matatu hivi yenye play list ya nyimbo za kutosha bila kupotea jukwaani na kila mtu aliridhika, sasa niachowaasa wenzangu MAshujaaa wakazanieni nidhamu wanamuziki wenu, wapigeni marufuku kulewa wakati wa kazi, kukaa na mashabiki wakati wa kazi, mazoea yawekwe kando na tufanye kazi muda wa kazi, Jana JB Mpiana akiongea na waandishi amewaasa esnsmuziki wa Tanzania kujituma na kuzipenda kazi zao na kuziheshimu ili waweze kufikia mafanikio, tunawatakia uzinduzi mwema.


JB Mpiana na Wenge BCBG wawasili usiku huu

November 27, 2012

https://i0.wp.com/2.bp.blogspot.com/-WlKkV-x5-jk/ULPT965OTFI/AAAAAAADsaQ/nCc_xh3tX4M/s1600/IMG_8970.jpg

Mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jean Bedel Mpiana aka JB Mpiana akitoka kwenye geti la kutokea abiria wanaowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere usiku wa kuamkia leo. Pichani JB anaongozwa na Ndanda Kosovo Kichaa mwanamuziki wa siku nyingi nchini kwetu.

Awali Spoti Starehe ilibahatika kuongea na Seguin Mignon na Genta Maccine ambaye ni atalaku baada ya kuunganishwa na Papaa Julie We Stone Ilunga Mbwebwe Presidaa Bana Congolee na Darisalama na kuthibitisha kuwa wako fit kwa ajili ya show hiyo.

 

https://i0.wp.com/2.bp.blogspot.com/-qf6id5Ht-YU/ULPT4pkvjGI/AAAAAAADsaA/I0Jy3iASIiA/s1600/IMG_8978.jpg

Suveree Mukulu Tshituka Papaa Cherie Dela Patrie Bin Adam Le Charismatique Jean Bedel Mukulu Mpiana akiwa na wenyeji wake pamoja na wanamuziki wa Wenge BCBG wakiongozwa kuelekea kupanda gari baada ya kuwasili jijini Dar usiku huu.

 

https://i0.wp.com/3.bp.blogspot.com/-ljFrakjt3gQ/ULPUAZY5TkI/AAAAAAADsaY/81oq8qemlVY/s1600/IMG_8983.jpg

JB Mpiana akiongea na waandishi wa habari kuhusu show yao hapa Tanzaia ambapo Alhamisi wiki hii watakuwa na onyesho jijini Arusha na ijumaa watakuwepo Leaders Club kwenye uzinduzi wa Risasi Kidole ya Mashujaa Band kabla ya kuelekea jijini Mwanza. (Picha zote na Blog ya Jamii)


Sharo Milionea updates; Kamanda Costantine Masawe athibitisha kifo chake

November 26, 2012

image

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Tanga Bw. Costantine Masawe amethibitisha kuwa msanii Sharo Milionea amefariki dunia baada YA kupata ajali huko Kijiji Lusanga Muheza Kilometa chache kabla hujafika Tanga mjini.

Sharo ambaye amezaliwa jijini Tanga na pia ni mwenyeji Wa Muheza alijizolea umaarufu kwa swaga zake Za kibrazamen katika uogizajI wake.

Awqli mitandao Habari zilithibitishwa na wadau kwenye mitandao YA kijamii ikimnukuu Tundaman kuwa alipigiwa simu na mtu toka Hospitali kupitia simu Ya Sharo Milionea akithibitisha Habari hizo na kunukuliwa kwenye Twiter na wadau.

Mwenyezi Mungu aiweke roho Ya Marehemu pema peponi Amen


Breaking News: Sharo Milionea apata ajali mbaya.

November 26, 2012
image

Sharo Milione na Swaga zake

Habari ambazo zimetufikia sasa zinasema muigizaji mchekeshaji na mwanamuziki Sharo Milionea amepata ajali. Aidha Habari ambazo Spoti na Starehe haijazithibitisha zinasema kuwa
msanii hiyo amefariki dunia.
Kwa mujibu Wa vyanzo vya Habari mjini Muheza Sharo alifariki Mara baada Ya kupaya ajali hiyo Majira Ya jioni Ya leo.
Bado tunazifatilia Habari hizo na tutafahamishana kilichojiri.


French Kiss Single ya Fally Ipupa inayomtambulisha kwa mashabiki “wapya”.

November 26, 2012

image

Fally Ikifanya kile akina dada wanakipenda, Kata Mauno

image

Fally Akimuomba mpenzi wake msamaha baada ya fumanizi akimpiga busu la mahaba shemejie.

Si kawaida kwa vijana wa sasa kupenda Bolingo wengi wanapenda Bongo Flava na nyimbo zao za kizazi kipya. Majuzi nilikuwa nimekaa na washkaji pale Kijiji Beach Kigamboni tukibadilishana mawazo huku tukigonga monde moja mbili na muziki wa hapa na pale. Ghafla ukapigwa French Kiss wa Fally Ipupa ikiwa ni Single yake mpya aliyoiingiza sokoni muda kidogo, baada ya kupigwa wimbo huu moja ya watu tuliokuwa tumekaa nao ni mwanadada Mary ni rafiki yetu  yeye anasema alikuwa hampendi kabisa Fally Ipupa wala muziki wa Bolingo lakini anasema wimbo huu umemfanya si tu aupende bali ampende Fally na ameshaanza kusikiliza nyimbo zake na kuzitafuta yeye pamoja na marafiki zake.

Inawezekana Marry na wenzake wameupenda wimbo huu kwa sababu ya ujumbe uliomo ambapo Fally anamuomba msamaha mpenzi wake kwa sababu alimfumania kimpiga busu la kimahaba (French Kiss) demu mwingine au kwa sababu wameuelewa ujumbe mzima kwenye wimbo husika au ni vile viuno vya Fally.

Alipohojiwa na mtandao maarufu wa Digital Congo baada ya kutoa hii Single yake mpya ya French Kiss Fally Ipupa alisema kuwa dhumuni lake ni kuwapata mashabikia ambao hawajawahi kuupenda muziki wa Congo kabisa na waanze kuupenda kupikia yeye. Fally anasema kuwa Jukumu kubwa walilonalo kizazi cha tano cha muziki wa Congo ni kuuvusha muziki huu kwenda Ulaya na America hata Asia sio kuwapigia waafrika walioko huko bali ni kwa ajili ya vijana walio kwenye nchi hizo, Fally alilirudia hili hata alipoulizwa baada ya kutoa Wimbo na Olivia ambaye walitumbukia kwenye mapenzi baadaye.

Katika kuitikia hilo hivi karibuni mwanamuziki mwingine ambaye alipanda kwenye chati na Fally Ipupa kwa pamoja Ferre Gola yeye anatoa Albamu yake mpya ambayo ndani yake anamshirikisha Celine Dion na Boss wa lebo ya Maybach Rick Ross albamu ambayo anasema anaitoa mkesha wa Chrismas, Ferre amesema sababu hizo hizo kama za Fally kuwa anataka kuweka ladha tofauti kwenye muziki wa Congo ili aweze kuwafikia na kuongeza mashabiki wapya toka kwenye miziki ya kizazi kipya.

Binafsi naweza kusema amefanikiwa, iwe ni ujumbe, lugha, rhythim au lolote Fally amefanikiwa kufikia lengo lake na kwa mtaji huu tutawaona akina Mary wengi wakiupenda muziki huu.


Women of Determination Award 2012 Kuhamasisha akina mama wa Kitanzania.

November 22, 2012

DSC_0567

Waratibu wa Kongamano la Woman of Determination Award and Conference 2012 toka kushoto Mama Benadeta Choma, Bi Fatma Kange na Dr. Ellen Otaro wakiongea na waandishi wa Habari asubuhi hii.

DSC_0579

Waaandaaji wakijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wao wa leo.

Tuzo za Women of Determination Award and Conference zinatazamiwa kufanyika tarehe 1 December 2012 katika hoteli ya Ubungo Blue Pearl jijini Dar Es Salaam.

Wakiongea na waandishi wa habari jijini leo, waratibu wa Tamasha hilo wamesema kuwa dhumuni kubwa la Tamasha hilo ni kujaribu kuwaweka pamoja wanawake waliothubutu ili kuchangia mawazo mwisho wa siku waweze kuwapa hamasa wanawake wa Tanzania ambao wengi wao hawana utayari wa kuthubutu. “…Wengi wa akina mama wamekuwa waoga kuthubutu tunataka kuwajengea uwezo ili waweze kuthubutu” alisema Dr. Ellen Otaro mmoja wa waandaaji wa Kongamano hilo.

Akiongea wakati wa mkutano huo na Waandishi wa Habari Bi Fatma Kange ambaye ni muasisi wa tuzo hizo amesema kuwa mwaka huu tuzo hizo zimeongezeka kwani wameongeza category ambapo wanawatambua na kuwapa tuzo wanawake ambao wamethubutu si tu kutoka jijini Dar Es Salaam bali Tanzania nzima kwa ujumla, aidha bi Kange amesema kuwa kuna haja ya kuwahamasisha mabinti zetu na kuwaweka karibu na hawa akina mama ambao wamefanikiwa ili kuwaonyesha njia kwamba wao wamefikaje fikaje.

Akichangia hoja hiyo Dr. Ellen Otaro ambaye ni mmoja wa wadau kwenye kongamano hilo amesema kuwa kauli mbiu ya wanawake wakiwezeshwa wanaweza inawafanya akina mama kusubiri kuwezeshwa jambo ambalo linafanya akina mama wengi kutofanikisha ndoto zao lakini “seeing is believing” wakiwaona wenzao wakiongea njia walizofikia kuwafanya wafike walipo, wanawake wanaweza kufanikisha ndoto zao. Aidha akijibu swali la waandishi wa habari Bi Benadeta Choma amesema kuwa Tuzo za mwaka huu zitawaleta pia wake wa viongozi na wanawake wa kawaida wakijumuika pamoja na wale kumi na moja ambao wameteuliwa na kamati kupata tuzo hizo, aidha Mama Choma amesema kuwa washindi wa tuzo hizo watapewa vyeti na ngao maalumu kwa ajili ya kumbukumbu za mchango wao kwa walichokifanya na huko mbeleni wanafikiria kuanza kutoa pesa kama hamasa kwa akina mama wengine waweze kuthubutu.

Awali akiongea na Spoti na Starehe Mama Choma alisema kuwa Kongamano hili linatofauti na mengine kimtazamo kwano pamoja na burudani na chakula cha usiku kwa siku hiyo, akina mama waweza kujifunza baada ya kusikia kutoka kwa washiriki mbali mbali, “fikiria binti akimuona Mwanamke mwenzake akiendesha ndege au basi au Daktari ambaye ametokea Kijijini akasomea kijijini lakini ni Daktari bingwa anaongea pale mbele ni wazi na yeye atajipa moyo kuwa akijitahidi na yeye anaweza” alisema Mama Choma.

Kongamano la Women of Determinations litafanyika jioni ya Tarehe 1 Desemba 2012 katika ukumbi wa Ubungo Blue Pearl ambapo Wanaopenda kushiriki wanatakiwa kulipa shilingi elfu thelathini kwa mtu mmoja na kama ni kikundi cha watu wa tano watalipa shilingi laki moja hii ikiwa ni Gharama ya chakula cha jioni, na kutakuwa na burudani ya muziki pia. aliongeza Mama Choma na kuongeza kuwa Si dhumuni lao kuwachangisha akina mama kwani wangependa akina mama wengi zaidi washiriki lakini bado hawana wadhamini wa kuzidhamini tuzo hizo na pesa hizo ni kuchangia gharama kidogo ambapo watapata na Elimu, chakula cha jioni na Muziki.

Akichangia hoja hiyo Bi. Kange amesema kuwa kikubwa ni ile elimu ambayo anakuja kuipata toka kwa akina mama wenyewe waliofanikiwa wakiongea toka kwenye vinywa vyao.

inakadiriwa zaidi ya wanawake mia tatu watashiriki kwenye kongamano hilo ambalo huu ni mwaka wa pili tangu liasisiwe. Kauli mbiu ya mwaka huu ya kongamano hilo ni Kuwajenga, Kuwatambua na Kuwaunganisha.


Ali Kiba na Saida Karoli kuiwakilisha Tanzania KORA 2012

November 19, 2012

AliKibaSaidaKAroli

Tuzo za Muziki za KORA zimewadia na kurejea kwa kasi kubwa huku Tanzania ikiwakilishwa na wanamuziki wawili Ali Kiba ambaye yuko kwenye kundi la Wanamuziki Bora wa Kiume toka Afrika Mashariki na Saida Karoli ambaye yuko kwenye kundi la Wanamuziki bora wa kike wa Afrika Mashariki.

Kundi la Ali kiba ambali lina wanamuziki sita wakigombania tuzo hizo nao ni Jimmie Gait Feat Dk – Furi Furi Dance, (Kenya), Kidum Feat Sana – Mulika Mwizi, (Burundi), Ali Kiba Feat Lady Jay Dee – Single Boy, (Tanzanie), Redsan – Ila Wewe, (Kenya) Chris D – Aisha, Burundi
Mulatu Astatke – (Ethiopie). Kundi hili ni gumu kwa kiba kwani lina wanamuziki kama Kidumu na Redsan ambao kila mmoja wana umaarufu hata nje ya nchi zao huku mwanamuziki kama Kidumu akiwa maarufu kwa kuimba Kiswahili, Kifaransa na Kiingereza ambapo anao uwezo na nafasi kubwa ya kupata kura kutoka kwa nchi zote zinazozungumza Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili pia.

Kundi jingine ni la Saida Karoli ambaye naye alitamba sana Afrika ya Mashariki lakini amekuwa kimya kwa muda mrefu, kundi hili ni gumu kwa kuwa Karoli anakutana na wanamuziki kama Juliana ambaye ana umaarufu sana katika Afrika ya Mashariki, Kwa wale wanaoangalia kipindi cha Tusker Project Fame, wanamkumbuka huyu ni mmoja wa ma jaji kwenye reality show hiyo, huku Hellen Berhe wa Ethiopia akiwa na shows nyingi na mashabiki wengi ndani na nje ya Ethiopia. Kundi la Karoli wapo Juliana Kanyomozi – I Am Ugandan, (Uganda), Marya – Shiki Simu, (Kenya), Helen Berhe – Lebe, (Ethiopie)
Asther Aweke – Lu Mili, (Ethiopie) Saida Karoli – Sakina, (Tanzanie) Ikraan Caraale – Gaarsiiya, (Somalie). Huku Best Director Tanzania inawakilishwa na Jessy Nottola

mwanzilishi na muandaaji  Ernest Adjovi akimtangaza mwanamuziki machachari toka America R & B singer, Chris Brown, ndiye atakuwa mburudishaji toka nje. Mashindano haya ambayo yaliasisiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1994 kwa muda mrefu yalikuwa yakifanyika nchini Africa ya Kusini na yalisimama kwa kama miaka miwili na ushehe kabla ya kuendelea tena mwaka huu.

Kwa wapenzi wa Lingala JB Mpiana atachuna na Ferre Gola kwenye kundi lao la wanamuziki bora wa Afrika ya kati huku kukiwa na wanamuziki kama Lokoua Kanza – Nakonzonga, (Rdc), JB M’piana – La Danse Du Cheval, (Rdc), Lord Ekomy Ndong – Bi Se Fe Nale, (Gabon), Freddy Massamba – Lobelanga, (Congo Brazza), Totoi Bolabote – Botaka, (Guinée Equatoriale), Ferre Gola – Tchekele Pete, Rdc, Kundi hili huwa linaingiza wanamuziki wengi na ndipo watu kama Koffi na Werasson walipata umaarufu baada ya kuchukua zawadi nyingi kwenye tuzo hizi za Kora.

 

Best Male West Africa
Fuse ODG Feat Itz Tiffany, Donae – Azonto, Ghana
Molare – Coupé Decalé, Côte D’ivoire
Dj Arafat – Kpankaka, Côte d’Ivoire
D Banj – Oliver Twist, Nigeria
Sekouba Bambino – Sinontena, Guinée
Flavour – Adamma, Nigeria

Best Female West Africa
Omawumi- If You Ask Me, Nigeria
Viviane Ndour – Kumu Nexxul, Senegal
Chindima – Kedike, Nigeria
Fafa Ruffino Feat Rockin Squat – Ilé, Benin
Claire Bahi Feat. Dj Arafat – Comme Ceci Comme Cela, Côte D’ivoire
Suzanna Lubrano – Pensa Na Mi, Cap Vert

Best Male East Africa
Jimmie Gait Feat Dk – Furi Furi Dance, Kenya
Kidum Feat Sana – Mulika Mwizi, Burundi
Ali Kiba Feat Lady Jay Dee – Single Boy, Tanzanie
Redsan – Ila Wewe, Kenya
Chris D – Aisha, Burundi
Mulatu Astatke – Ethiopie, Ethiopie

Best Female East Africa
Juliana Kanyomozi – I Am Ugandan, Ouganda
Marya – Shiki Simu, Kenya
Helen Berhe – Lebe, Ethiopie
Asther Aweke – Lu Mili, Ethiopie
Saida Karoli – Sakina, Tanzanie
Ikraan Caraale – Gaarsiiya, Somalie

Best Male Central Africa
Lokoua Kanza – Nakonzonga, Rdc
JB M’piana – La Danse Du Cheval, Rdc
Lord Ekomy Ndong – Bi Se Fe Nale, Gabon
Freddy Massamba – Lobelanga, Congo Brazza
Totoi Bolabote – Botaka, Guinée Equatoriale
Ferre Gola – Tchekele Pete, Rdc

Best Female Central Africa
Princess Leoni Kangala Feat Pili Pili Magale – Nzara, Centrafrique
Barbara Kanam – Djarabi, Rdc
Charlotte Dipanda – Coucou, Cameroun
Lady Ponce – Secouer Secouer, Cameroun
Meje 30 – Fimbu Ya Bakanda, Rdc
Mounira Mitchala – Independence, Tchad

Best Male Southern Africa
Madruga Yoyo – Vamos La, Angola
Maya Cool – Faz Um Milagre Em Mim, Angola
The Dogg – The Deception, Namibie
Alain Ramanisum – Sega Sexy, Ile Maurice
Richard – Vou Cuidar De Ti, Mozambique
Mbongeni Ngema – My Baby, Afrique Du Sud

Best Female Southern Africa
Zahara – Loliwe, Afrique Du Sud
Lizha James Feat. Perola – Leva Boy, Mozambique
Yola Araujo Feat. Jacob Desvarieux – E Hoje Ou Nunca, Angola
Toya Delazy – Pump It On, Afrique Du Sud
Titica Feat Ary – Olha O Boneco, Angola
Shelby – Damata, Angola

Best Male North Africa
Cheb Khaled – C’est La Vie, Algerie
Kader Japonais – Gachitili Ma Vie, Algerie
Yassine Rammi Feat. Hammid B – Ya, Maroc
Madou Mc – La Tête Haute, Tunisie
Hossam Habibi – Bafkar Feek, Egypte
Dizzy Dros – Casafonia, Maroc

Best Female North Africa
Kadidja Yama – Samhay, Maroc
Zina Daoudia – Saken Aisha, Maroc
Hasna El Becharia – Djazair Johara, Algerie
Nadia Laarousi – Lil Ya Lil, Algerie

Best African Group
Magic System – La Danse Des Magician, Cã´Te D’ivoire
Toofan – C Magik, Togo
X Maleya – Tchokolo, Cameroun
Malaika – Never Change My Mind, Afrique Du Sud
Camp Mulla – Party Don’t Stop, Kenya
Gal Level – Ohole, Namibie

Best Male Diaspora (USA)
Chris Brown Feat. Lil’wayne & Busta Rhymes – Look At Me Now, Usa
Jay-Z Feat Kanye West – Niggaz In Paris, USA
Chris Brown – Yeah, USA
P Diddy – I’m Coming Home, USA
Florida – I Got A Feeling, USA
Wiz Khalifa – Roll Up, USA

Best Female Diaspora (USA)
Rihanna – We Found Love, USA
Rammy – G For Gentlemen, Côte D’ivoire
Beyonce – Run The World, USA
Nikki Minaj – Superbass, USA
Keri Hilson Feat. Nelly – Lose Control, USA
Tolumide – For Me, USA

Best Male Diaspora (Europe and Carribean)
Sexion D’assaut – Avant Qu’elle Ne Parte, France
Stromae – Alors On Danse, Belgique
Logobi Gt Feat Sisi K Et Bb Model- Elle Danse Sexy, France
Victor O – Vini Dou, France
Jim Rama Feat Alan Cavé – Mon Seul Regret, France
Slaï – Ça Ne Te Convient Pas, France

Best Female Diaspora (Europe and Carribbean)
Njie – Marzouk Ethnie, France
Michelle Henderson – Pani Pawol, Dominique
Tanya St Val – N’oublie Pas, France
Stevy Mahi – Yenki Pou Vou, France
Jocelyne Labylle – Quelqu’un De Bien, France
Sega El – Jaloux, France

Best Male Gospel
Landry Foua Bi – La Clé De Ma Liberté, Côte D’ivoire
Yvan – Ton Amour Me Suffit, Benin
Thocco Katimba – Ambuye Ndiribe Nanu Mau, Malawi
Carlam – Prospérité, Gabon
Skuulfo – Adandesie, Ghana
Mesach Semakula Feat Dj Michael – Nina Omukwano, Ouganda

Best Female Gospel
Soeur Lydie Nseya – Bolamu, Rdc
Bernice Blackie – Crucifixion, Liberia
Tonzi – Shima Imana, Rwanda
Rebecca – I Need You More, Nigeria
N’lauretta – Hommage À Jésus, Cameroun
L’or Mbongo – Yeshua, Angola

Best Gospel Group
Joyous Celebration – Wangilwela, Afrique Du Sud
Seraphim Song’s – Impundu, Burundi
Infinity – Press On, Nigeria
Soweto Gospel Choir – Avulekile Amasango, Afrique Du Sud
Dmk – Don’t Worry, Zambia
Gael – Amour Eternel, Rdc

Best Male Traditional
Kiflay Issak – Mekseb, Erythrée
Stanlux – Africavio, Togo
Nasser – Moustapha, Mauritanie
King Ayisoba – Awudome, Ghana
Koo Nimo – Sounds From Ghana, Ghana

Best Female Traditional
Hamsou Garba – Magana Zoutchi, Niger
Aida Sam – Saraaba, Senegal
Myriam Fares – Tlah, Maroc
Queen Koumb – Sissa Na Bu Ngussu, Gabon
Affou Keita – Commandant, Côte D’ivoire

Best Group Traditional
Les Reines Mères – Tos, Côte D’ivoire
Ni Malagasy Orchestra – Salegy, Madagascar
Tinariwen – Tenere Taqqim Tossam, Mali
Les Frères Guedehoungue – Feu De Brousse, Benin
Sotheca – Goly, Côte D’ivoire
The Dizu Plaatjies Ibuyambo Ensemble – Izindiba, Afrique Du Sud

Best Male Newcomer
Aslay – Niwenawe, Kenya
Floby – Saanida, Burkina Faso
Loyiso – Wrong To You, Afrique Du Sud
Aziz Azion – My Oxygen, Ouganda
Davido – Dami Duro, Nigeria
John Chiti – Wapusuku, Zambie

Best Female Newcomer
Djelika Diawara – An Mi Woula, Mali
Amira Fathy – Ou’bal El Banat, Egypt
Keko Feat Madtraxxx- Make You Dance, Kenya
Nuella – Wakoulezi, Cote D’ivoire
Sessimã – Mayavio, Benin
Sacha Feat Bably- Nsobanurira, Rwanda

Best Director
Clarence Peters For Capital Dreams – Kedike Of Chindima, Nigeria
Dj Marcell- Leva Boy Of Lizha James, Mozambique
Ash Dibben – Loliwe Of Zahara, Afrique Du Sud
Gelongal – Kumu Nexxul Of Viviane Ndour, Senegal
Grand Poucet – Coupé-Décallé Of Molare, Côte D’ivoire
Jessy Nottola – Oh Amadou Of Amadou Et Maryam, Tanzanie.


Albamu ya Ferre aliowashirikisha Rick Ross na Celine Deon kutoka Dec 14

November 15, 2012

Mwanamuziki Ferre Gola ametangaza kuachia Albamu yake mpya ya Boîte Noire au “black box”  tarehe 14 December 2012. Hii itakuwa albamu ya tatu tokea nguli huyu atoke kivyake.

Ferre ambaye kwa sasa anasemwa kufanya kazi usiku na mchana anasema Albamu hiyo itakuwa ya kufungia Mwaka na kuanzia mwaka mpya wa 2013 huku akiwashirikisha wanamuziki nguli kama Rick Ross na Cellion Deon, hii imefanya albamu hii isubiriwe kwa hamu kwani inakuwa imekata kiu ya wapenzi wa Hip Hop, na Celine Deon ambaye anaimba mahadhi ya Slow Jams huku mzee mzima Ferre Gola akitoka Kicongo Congo kwetu sisi wapenzi wa bolingo, hii ni mara ya pili kwa mwanamuziki wa Congo kushirikisha wanamuziki wa Marekani.

Albamu hii ambayo inasemwa na wanastratejia wa uchumi na muziki kuwa imefanywa ili kuongeza uelewa na mashabiki wa muziki wa Lingala Ulaya na America ambapo wanamuziki hawa wanapendwa sana.

Kabla ya kwenda solo Ferre ambaye aliwahi kufanya kazi na kundi la Quartier Latin International na baadaye kuanzisha Marquis de Maison Mère ambapo alikuwa na watu kama Bill Clinton Kalonji ambaye aliwahi kutamba sana na WMMM kama atalaku. Tungoje tuone jinsi itakavyokuja hasa uwemo wa hawa ma nguli.


Historia ya Werasson ndani ya Kitabu

November 13, 2012

Hadji Le Jeebenique

Nadhani Werrason ni mmoja wa wanamuziki wa Congo wenye washabiki wengi sana hapa nchini na Africa kama sio duniani kiujumla.Lakini kwa muda mrefu mashabiki na wapenzi wake hao wamekua wakimfahamu Le Roi De La Forret Papaa na Exocee Mobali ya Mama Pastor Sylvie Mampata kijuu juu tu.Lakini safari hii mashabiki wake na wa muziki kiujumla hususan wanafamilia wa wenge wamepewa fursa maalum ya kumjua nguli huyu wa muziki wa congo kupitia kitabu maalau ambacho kimeshachapishwa kikielezea historia ya mwanamuziki huyo binafsi na katika harakati zake za kujiingiza kwenye muziki,kuwa star na mpaka sasa kumiliki bendi kubwa na yenye mafanikio makubwa pia.

Dondoo za yaliyomo kwenye kitabu hicho ni kwamba ndani ya kitabu hicho werrason anaelezea kwa mfano wenge musica ilivyozaliwa.Katika hilo Werrason anasema mwanzoni kabisa walikua yeye Werra,Aime Buanga,Jean Belix Luvutula,Didier Masela na Christian Zitu,ambapo Aime Buanga alichukuliwa kama muanzilishi wa kundi kutoka na yeye kujitolea nyumba ya wazazi wake alimokua akiishi itumike kama sehemu ya kufanyia mazoezi ya kundi lao hilo na pia Didier Masela nae kwa upande mwingine akichuliwa kama muanzilishi pia kutokana na kwamba wazo la kuanzisha bendi lilitoka kwake.Lakini wakati fulani kwenye siku hizo hizo za mwanzo mwanzo za kundi lao Aime Buanga alitaka kuachana na kundi hilo changa ili aendeleze kipaji chake kwenye sanaa za mapigano (martial arts) huku akimpa masharti rafiki yake werrason kwamba kama unataka nirudi kundini na wewe jiunge na mimi kwenye sanaa za mapigano(martial arts) sharti ambalo kwenye kitabu hiki werra anadai alilitekeleza kwa kujumuika na swahiba wake kwenye martial arts.

Wakati ya Werrason na Aime Buanga yakiendelea hivyo kwa upande mwingine Didier Masela alikua shule nje ya Kinshasa katika mji mdogo uitwao Mbanza Boma pamoja na Alain Makaba.Baadae huku nyuma Jb Mpiana akafika kuja kujiunga na bendi ambapo werra anasema katika kitabu hiki akamueleza “rafiki yangu nimesikia wewe ni muimbaji mzuri sana kama hitajali naomba uniimbie wimbo kidogo nikusikie na mimi” baada ya kauli hiyo ya werra jb inaelezwa akaimba wimbo uitwao “Abidjan” wa Viva la Musica uliotungwa na Debaba,ambapo Werrason mwenyewe na kila aliekuwepo pale wakavutiwa nae sana kiasi cha kumpigia makofi kwa wingi na watu wote,baada ya hapo werra akapendekeza Jb ajiunge na bendi ambapo Jb alikubali bila kusita.Siku hiyo miongoni mwa waliomshuhudia Jb akiimba pamoja na werrason ni Didier Masela na Jean Belix.Na aliyemleta na kumtambulisha Jb hapo kundini alikua ni Jean Belix Luvutula ambae walikua wakiishi jirani na alikua akimuona Jb akiimba mtaani.

Baadae Blaize Bula akaletwa na Makaba kujiunga na bendi kama mpiga drums kutokana na kwamba alikua mpiga drum wa bendi ya shule waliyokuwa wakisoma lengo likiwa aje achukue nafasi ya binamu yake werrason  aliyekwenda kwa jina la Ladins Montana ambae ndio alikua mpiga drums,lakini Sele Bula akaonekana hana muonekano wa bcbg lakini Makaba kwa kujua kipaji cha Sele kwenye uimbaji pia akasisitiza aingizwe kundini.Hivyo wakawa wamempata Blaize(sele)Bula kama muimbaji,na kwa upande mwingine Jb ambae alikua tayari kundini alikutana na Tata Mobitch Adolphe Dominguez ambae alikua ni mtoto wa tajiri mkubwa sana Congo lakini pia akiwa na dancer mzuri akicheza sana nyimbo za DEFAO.Jb na Adolphe baada ya kujuana kutokana na Jb kuvutiwa na uvaaji wa Adolphe wakatokea kuwa marafiki wakubwa huku Adolphe akimpigisha Jb pamba za ukweli kiasi cha kung’aa mbaya miongoni mwa wanabendi,ndipo baadae Jb akamtambulisha Adolphe kwa Werrason na wengine kundini ambapo wakaanza kumfundisha muziki Adolphe hapo hapo kundini huku yeye akilipa fadhila kwa kuwafadhili upande wa mavazi kupitia utajiri wa babake!

Kitabu kimeongelea mambo mengi hatuwei maliza ngoja nitoe dondoo za alichozungumzia werra kuhu su maisha yake binafsi.Katika maisha yake binafsi werra anasema alikutana na mkewe kipenzi Mama Pastor Silvie Mampata akiwa shule kupitia rafiki yake kipenzi wakati huo aitwae Wasenga Kipuni.Sylvie alikua ni binti wa mfanyabiashara tajiri na aliutumia utajiri wa babake kuisadia sana wenge huyu mama kupitia kwa werrason.

Kuhusu mgawanyiko kitabu kinaeleza kwamba ni uamuzi wa Jb kurekodi “Feux de l’amour” kwa kuwashirikisha wanamuziki wengine toka nje ya wenge kama alivyofanya Alain Makaba kwanza kwenye album yake solo iitwayo “Pile ou face” hapo ndipo mgogoro wa kiuongozi ulipoanza kuibuka,ambapo baada ya mafanikio ya Feux de l’amour Jb kwa kushirikiana na SIMON SIPE ambae ndie alikua meneja wao akisimamia kila kitu mpaka production zao wakanogewa na kutaka kutoa album nyingine solo ya pili ya Jb,hapo ndipo werra alipokasirika na kuitangaza album yake Kibuisa mpipa huku akiwa hana hata nyimbo moja wakati huo akiitangaza ila tu alitaka kumuonyesha Jb kwamba hawezi kutoa album solo ya pili wakimtazama tu.

Baada ya hapo bendi ikagawanyika na werra  ili kushindana na Jb akawa na mawazo ya kuanzisha tu bendi haraka haraka na kuanza kuperfom matokeo yake akachemsha sana mwanzoni kwenye concerts zake za awali zikawa “flop” mpaka ndugu zake wanaotoka kijiji kimoja kina Marie Paul wakamuonea huruma na kuamua kumsaidia ambapo Marie alimpa bure mwanamuziki wake JDT na yeye mwenyewe akawapata watu kama Didier Lacoste, Adjan n.k. ndipo mambo yakaanza kwenda vizuri sasa na kutoa FORCE INTERVENTION RAPIDE. Ambapo badae mwandishi wa kitabu hiki nae alimpa wazo werra la kutarget zaidi concerts za watu wa kawaida kuliko za VIP kama wafanyavyo Bcbg, pia werra akapata msaada mkubwa toka kwa mamaa Tshala muana, baadae wakapata kazi ya kwanza ulaya kwa kualikwa kwenda kupiga London ambapo muandishi wa kitabu hiki alifanya kazi ya ziada kwa ku organize umati wa watu kwenda kumpokea werra na bendi yake airport katika safari ambayo masela aliachwa kin na ikawa mwisho wako kundini.


Cindy Olomide alipomwaga chozi jukwaani kukumbuka alipotoka.

November 8, 2012


Wimbo unaitwa Lily Kanik uliimbwa na Koffi Olomide. Wimbo huu ndio uliompa Cindy maks alipoitwa kwenye interview ili awe mmoja wa waimbaji wa Koffi, Lily Kaniki ni mama yake na Claudia Sasou Ngueso mke wa Denis Sassou Ngueso.


Cindy alipokuwa akiimba wimbo huu alitoa machozi utaona anashindwa kuimba kabisa na Koffi anamwambia aendelee kuimba, kisa cha kutokwa na machozi ni fikra akikumbuka alikotoka na anasema wimbo huu kila akiuimba anakumbuka safari ya ndoto yake ya kuja kuwa mwanamuziki, kwa Sasa Cindy si tu mwanamuziki ndani ya Quartier Latini bali ni mpenzi wa Koffi Olomide ambaye wameshibana kwelikweli.
Katikati ya mwaka huu Koffi alimnunulia gari ainaya Jaguar kama zawdi kwa kumzalia “kindu chedi”.
Ndani ya video hii utamuona kwa mbali Zakarie Bababaswe ambaye alikuwa mshereheshaji kwenye Concert hii iliyofanyika Inter Continental Hotel huko Kinshasa. Kiukweli hii ni Cencert ya kuitazama jumapili ukiwa umepumzika na Glass ya wine pembeni.

Merci mingi Papaa Julie We Ston kwa kuniletee DVD hii direct from Congo Merci Papaa Cisco ndani ya Kwetu Saloon weeeee!! kitokoooo.


Tour Eifel ; Utunzi wa Titina Alcapolne unaoliza mashabiki

November 8, 2012

Moja kati ya wanamuziki wa Wenge ya JB Mpiana ambao waliondoka na bado nawalilia Allain Mpela, Huyu bwana alikuwa anauwezo mkubwa si tu wa kutunga bali alikuwa anakarabati Verse, yaani wimbo ukitungwa wakisikilizishana yeye huwa anazirekebisha na akirekebisha na kuzitengenezea mtiririko wa sauti hakuna anayepinga na moja ya albamu ambazo alishiriki kwa kiasi kikubwa kuiratibu ni hii ya Titanic (Titanike) ambayo waliitoa baada ya kuparaganyika na akina Werason na wao kuunda WMMM, Kila anayeipenda BCBG atakubaliana na mimi hili lilikuwa kundi bora kuwahi kutokea na labda mungu angejalia lingeendelea kubaki vile vile, kwa mashabiki wa Wenge kila wimbo huu ukipigwa leo huwa wanatoa machozi wakikumbuka jinsi jamaa walivyoshambulia Zenith na ziara walizozifanya baada ya Albamu hii.

Japokuwa wimbo huuu ulitungwa na mpiga drums maarufu Titina Alcapone ukisikiliza beti ya Allain Mpella Afande utakubaliana na mimi kuwa alikuwa jembe, msikilize kuanzia 3:20 kisha unipe maoni yako.

Mwingine ambaye kwa sasa mepotezwa kabisa na hajawahi kuwika tangu atoke kundini ni Aimelia Lyase Doming’ong’o ambaye kwa kiasi kikubwa JB Mwenyewe ameweza kuziba pengo lake kwa kuimba sauti yake ingawa ya Aimelia ni kali na nyembamba zaidi lakini pengo lake haijaonekana sana.

Wimbo huu ni kwenu Jay Single Suvereigh Mukullu, Papaa Mabamba Maregesi pamoko sana mkuu (Full Mzaire), Papaa Julie We Ston Presidaa Bana Kongolee na Darisalama, Papaa Sultan ndani ya jiji la Dar, Engineer Mboneka Mwana BCBG, Juma Mukulu nakati ya Airport, Hadji Le BeeCeeBeeGeeque Nambari wani, Mapenzi Club tuko pamoja, Muzee ya Tunduma sina haja ya kukutaja, Papaa na kati ya Muscat unajijua, Wenge BCBG Arusha Club pamoja sana.

Weekend njema.


Shandra ya Josky Kiambukuta; Story ya Mwanadada aliyeteswa kimapenzi.

November 8, 2012

Huwa napendelea kwenda Kemondo Sound sababu Richard Mangustine akiniona tu kwanza atasema Papaa Pius Bamalaa na wimbo utakao fuata ni huuu kisha atanigongea Tour Eifel, Liberation na No Comment Tshengen zote za BCBG.

Kaka yangu Edwin Mikongoti ambaye alinifundisha mimi kuupenda muziki wa Zaire anasema kuwa huu ndio ulikuwa mmoja wa Nyimbo bora kabisa kuwahi kuimbwa na Josky Kiambukuta na TP Ok Jazz, ingawa walikuwa na albamu nyingi lakini wimbo huuu uliwanyanya wawe maarufu zaidi si kwa Congo tu bali Africa nzima.

Nilikuwa najiuliza ni jinsi gani ma producer wa zamani walikuwa wakiumia kichwa kwa maana mpangilio wa vocals, Vyombo, Melody na Tempo ziende sawa. ama kwa hakika huu ulikuwa ni uwezo mkubwa sana. Wimbo huu Chandra uliimbwa na Josky Kiambukuta ni story ya ukweli inamhusu mwanadada ambaye alimpenda jamaa anaitwa Shandra ambaye alimpenda sana, ila inaonyesha Shandra kama hajali sasa bidada anamwambia kuwa Shandra nifanye nini ujue nakupenda, basi nitupe hata kwenye t akataka bado nitakupenda tu, sipendi mwanaume yeyote aninyooshee kidole wala anitongoze mi ni wako na roho yangu iko kwako.

Vilio vya hivi vichache sana maana siku hizi dada zetu ndio wanaongoza kwa kuliza. hahahaha enjoy the music.!!!!

Andika Email Yako hapo nitakutumia MP3 ya wimbo huu na Ringtone pia.


Justin Timberlake na Jessica Biel wapumzika Fungate lao Serengeti Tanzania

November 5, 2012

image

Maharusi Newlyweds Justin Timberlake (31)  na Jessica Biel (30) wakionekana walipokuwa wakishuka kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro International Airport kwa ajili ya safari ya siku tano ya fungate lao baada ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa mitandao Picha hii ni ya October 21 siku mbili baada ya harusi yao.

Maharusi hao ambao walitua Uwanjaa wa KIA kwa kutumia ndege yao binafsi walichukua Helcopta mpaka Singita Hotel, aidha habari zinasema kuwa maharusi hao walikaa kwa siku tano nchini Tanzania katika hotel ya Singita Grumet ambayo ni hotel namba moja duniani, chumba kwenye hotel hiyo ambavyo ma Super Stars wanafikia ni USD 7500 kwa usiku mmoja. Bieb ambaye ni mara yake ya pili kuja nchini baada ya kuja mara ya kwanza mwaka 2010 alipopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mpango wa maji safi duniani akiwa na Emile Hirsch, Isabel Lucas, Santigold, na Lupe Fiasco.

Wawili hao ambao suala la ndoa yao limekuwa gumzo na siri kubwa mpaka Picha hii ambayo imesambaa kwenye mitandao mbali mbali na kuzua mijadala imeonyesha kuvutia mamia ya mashabiki ndani na nje ya Tanzania kuvumbua walipo kwa ajili ya fungate. Wengi wa wachangiaji wametoa mchango wako huku wakishauri serikali kutumia nafasi hizi kuitangaza Tanzania kimataifa, “…I say let them enjoy our beautiful Tanzania! I just hope TTB can make the most of this exposure to attrack others!! and more tourists,” alisema Bw.  Jacob Selengia mchangiaji  kwenye mtandao wa Facebook. Mdau mwingine Maregesi Mabamba yeye anashauri wadau wa utalii kuzituma hizi habari na kuzichangia na wadau ili tuweze kuutangaza utalii wetu Kimataifa, “wanakuja watu wengi maarufu hatujui lakini hata tukijua hakuna tunalofanya ingekuwa wenzetu Kenya ungeona habari kila sehemu” alisema Mabamba.


Albamu mpya ya Ferre Gola akimshirikisha Celine Deon na Rick Ross kutoka Desemba.

November 2, 2012

ferre

Niliwahi kuandika jinsi kizazi cha nne kilivyoamua kuupeleka muziki wa Congo international, Mwanamuziki Ferre Gola baada ya Fally kuimba na Olivia yeyey ametoka na Mwanamuziki Mcanada mwenye asili ya Ufaransa Celine Dion na bingwa mwingine ambaye majuzi aliwakonga nyoyo mashabiki wa Tanzania kwenye tamasha la Fiesta Rick Ross.

Ferre ameipa albamu yake hiyo mpya jina la Boîte Noire ama Black Box itakuwa sokoni December ambapo amesema itakuwa ni zawadi ya Christmass kwa mashabiki wake, hayo yalithibitishwa na Meneja wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Jet Set bwana Vasco Mabiala, Bwana Mabiala pia alisema kuwa albamu hiyo imepewa jina hili kwa vile Black Box ni kisanduku ambacho kinatoa wingu la ni nini kimetokea hasa kwenye ndege zikipata ajali, anaeleza kuwa kwenye box la albamu hiyo yeye ndio atafungua milango endelevu kwenye sokola Ulaya na America kwa kuwashirikisha miamba hao wawili ambao wanakubalika na wana mashabiki sio Marekani tu bali duniani kote.

Ferre amesema kuwa Nyimbo zote ziko tayari, zimeshafanyiwa uchanganyaji na Video ziko kwenye hatua za umaliziaji ili zitoke kwa pamoja. 


%d bloggers like this: