Unaikumbuka Loketo Group?

 Wakati huo Loketo Group ikiwa na mkali wa kupiga solo barani Afrika Diblo Dibala na wakongwe wengine kama Aurlus Mabere, Jean Baron, Lucien Bokilo, Mack Mackaire ambaye alikuwa anapiga Drums huyu jamaa alikuwa balaa na wengineo waling’ara sana na kufanikiwa kuziteka nyoyo za wapenda midundo ya Afrika si tu kwa Congo bali kwa Bara zima la Afrika.

Namkumbuka Ronald Rubinel ambaye alikuwa anapiga kinanda enzi hizo wapiga vinanda mashuhuri walikuwa yeye na Jamaa wa Pepe Kalle kama sikosei anaitwa Butamu. Huku wakiwa na wacheza show wao wawili “Wana Wandere” wazungu ambao walikuwa wakicheza vilivyo.

Kwa kilingala Loketo inamaana chezeza hips zako “move your hips” na ndivyo Aurlus Mabere ilikuwa style yake ya kuchezesha.

Mwaka 1987 wakiwa wametiamia Loketo waliwasha moto kwenye klabu moja ijulikanayo kama Kennel Club huko San Francisco Amerika na inasemekana ile ilikuwa ni Concert kubwa na iliyobamba sana. Baadaye walianza kutoa kila mmoja na solo albam yake. Jamaa walitisha sana.

Kaka yangu Mungu Marehemu Nhangale Nkandi Mungu amlaze peponi alikuwa analipenda sana hili kundi enzi hizo tunakunywa Texco Club pale Sea View Upanga kabla ya kuingia Pink Coconut nilikuwa mdogo lakini burudani nilikuwa naipenda sana.

Wimbo nimeweka Malou kwa heshima ya mdau Le Grand Paa Sentuke, Sikiliza huu wimbo pale Lucien Bokilo alipompa nafasi Diblo Dibala ambaye kwa kiasi kikubwa aliutendea haki.

Nimefarijika kupata simu kutoka kwa mdau na shabiki mwenzetu Neema Jua akiwa Dodoma Mwangaza Fm anasema anapenda sana tunavyowachambua na kuuchambua huu muziki wa Africa Congo. Na kwa leo alitaka kujua kuhusu Aurlus Mabere na loketo Group yake.

19 Responses to Unaikumbuka Loketo Group?

 1. Predator says:

  Nakuambia ndugu yangu enzi hizo ndio miziki ilikuwa miziku. Diblo Dibala akawa mchawi mwenyewe, wana Soukous akina Lokassa, Ngouma na Geo Bilongo hawangemfikia. Kwa wale wapenzi wa Loketo hebu Pius wawekee video ya wimbo ‘Malou’ ili waburudikie kuwaona talanta chipukizi wakati huo wakiwemo Awilo Longomba na Lucien Bokilo.

 2. Stivin says:

  Huu wimbo ulitungwa na Marehemu Jean Baron RIP

  • Anonymous says:

   Mimi n Cliffe Omboto kutoka sehemu za kisumu nauliza je naweza zipata vipi hizi CDs za loketo za kitambo za video nawapenda sana hawa majamaa..

 3. chembera says:

  …ni kweli kabisa LOKETO walikuwa wanatisha,kundi lilivunjika…wanadai sababu kubwa ilikuwa Aurlus mabele alikuwa kistarehe mno badala ya kazi na kutafuta pesa…hii ilifanya kutofautiana na Diblo dibala…ambapo diblo alijitoa na kuanzisha MAtchatcha Group akiwa na kina Fede Lawu,Otis Mbuta,na kutoa vibao ka OK madame,hata hivyo mabelee nae hakubaki nyuma…alikuja na album ya Generation wachiwa akiwa amemuibua KAYERN madoka kwenye solo gitaa…swali wako wapi hawa wmanguli wa muziki wa kongo?

 4. Predator says:

  Mwenzangu Chembera umenichangamsha kwelikweli hapo namna ulivyodadisi mpangilio wa wenye bendi hadi walipotengana. Je, baada ya Diblo kuunda Matchatcha, mbona Fede Lawu alitumia jina hilohilo (album ya Soucis) tu baada ya kutengana na Diblo?

 5. Akaro says:

  Ngouma Loketo ni kiboko yao kwa kuchezea nyuzi bila kusahau Saladine.

 6. Vincent says:

  Hawa jamaa walikuwa wanatisha,album ya Extra Ball,Embargo ndio zilikuwa za kwanza kuwafahamu hawa jamaa mwaka 1993 nakumbuka nilikuwa darasa la kwanza,lakini sijajua kwa nini katika album ya ‘Extra Ball’ ya video nyimbo kama ‘Cindy’,’Pardon’ hazipo lakin katika audio ipo!

 7. Abeid says:

  Jean Baron amefariki mwaka 2005. RIP. Ndiye aliyetoka na albam yenye wimbo maarufu mamilolo

 8. Silas John says:

  Ki ukweli kundi hili la Loketo nililipenda sana hasa ktk nyimbo walizoshirikiana wote kama Liste rouge utawasikia vizuri Aurlus Mabele,Jean Baron na Lucien Bokilo wakizikonga roho za wapenzi wao.Yaani ilikuwa burudani tupu haitatokea tena.

 9. BENARD J. NTAMBALA says:

  NAKUMBUKA KIKOSI CHA LOKETO GOUP ARIKUWA
  1-MAK MAKAIRE
  2-AWIRO
  3-AURUS MABELE
  4-DIBLO DIBARA
  5-RUSIAN BOKILO
  6-ROKASA

 10. Anold Audax says:

  nakumbuka mbali sana baba yangu kipindi hicho alikuwa anarekodi radio casseti.Nilikukuwa mdogo lakini ilikuwa raha sana

 11. SIMON MTAHA says:

  ASANTE KWA KUTUKUMBUSHA. NAOMBA UWATAFUTE LOKETO UTUJUZE HILI KUNDI LIKO WAPI.WAMEKUFA AU WAKO HAI

 12. tony kombe says:

  asante sana kwa uchambuz mzur kaka..
  mimi nilitaka kuja historia ya ali koko ..nazani umenielewa kama jna nimekosea lakin ushajua namzunguzia nan asante kaka

 13. Things i have constantly told people is that while looking for a good on-line electronics shop, there are a few issues that you have to factor in. First and foremost, you want to make sure to find a reputable plus reliable shop that has enjoyed great evaluations and ratings from other buyers and marketplace analysts. This will make sure that you are getting through with a well-known store to provide good support and aid to its patrons. Thank you for sharing your notions on this blog site.

 14. We absolutely love your blog and find the majority of your post’s to be exactly I’m looking for. Do you offer guest writers to write content to suit your needs? I wouldn’t mind producing a post or elaborating on a lot of the subjects you write regarding here. Again, awesome web log!

 15. Right now it sounds like BlogEngine is the best blogging platform out there right now. (from what I’ve read) Is that what you’re using on your blog?

 16. Admiring the dedication you put into your site and detailed information you offer. It’s good to come across a blog every once in a while that isn’t the same outdated rehashed information. Great read! I’ve saved your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

 17. I’m really enjoying the theme/design of your website. Do you ever run into any web browser compatibility issues? A couple of my blog visitors have complained about my website not working correctly in Explorer but looks great in Safari. Do you have any advice to help fix this issue?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: