Yanga yaingia mitini…”Pa panga hapaingii kisu”

July 27, 2008
Wachezaji na Viongozi wa Simba, Picha na Muhidini Issa Muchuzi

Wachezaji na Viongozi wa Simba, Picha na Muhidini Issa Muchuzi

Ama kweli “pa panga hapaingii kisu”, Timu ya Simba ya Dar Es Salaam leo imetangazwa mshindi wa tatu wa mashindano ya Kagame Cup baada ya timu pinzani ya Yanga kuingia mitini kwenye mchezo wao wa kugombea nafasi ya tatu, Yanga ambayo hadi sasa haijajulikana sababu ya kuikacha mechihii inasemekana kuwa ilitaka ilipwe 35,000,000 kabla ya kuchezwa kwa mechi hii, Hizi ni habari toka kwa wadau wa soka ambazo mpaka sasa hazijathibitishwa ila tutawaletea habari zaidi kadri tukizipata, KWa habari na Picha zaidi mtembelee Michuzi.


Pashoka hapaingii kisu, Ni Simba na Yanga Leo

July 27, 2008
Yanga na Simba Leo

Yanga na Simba Leo

Leo ndio leo Uwanja mpya wa Taifa nyasi za bandia zitakapowaka moto wakati timu za Simba na Yanga zitakapokutana katika kugombea nafasi ya Tatu ya Kombe la Kagame. Mchezo huu utachezwa Uwanja mpya wa Taifa na utaanza saa nane juu ya alama mchana. Yanga wanasema walijifungisha ili wakutane na Simba kwao ndio muhimu kuliko Kombe teh teh teh teh.


%d bloggers like this: