Duh mchizi sijui alikuwa anamwambia nini jamaa?

December 29, 2008

.

.

Mwanamuziki wa kizazi kipya Chid Benzino akiteta jambo na Shaggy alipokuwa nchini sijui alikuwa akiteta nini lakini mchizi namkubali sana kama unaweza tafuta wimbo wa Hapo Vipi Remix wa Prof J usikie alivyonata na beat!!  Gonga hapa usikilize


Scolari: Bado milango ya ubingwa iko wazi

December 29, 2008
.

.

Chelsea midfielder Frank Lampard (L) akishangilia bao lake pamoja na mchezaji mwenzie toka Nigerian John Mikel Obi (R) baada ya kufunga bao la pili kwenye mchezo wa jana baina ya Chelsea na Fulham ambao ulimalizika kwa 2-2.

Kocha wa Chelsea Luiz Felipe Scolari anasema kuwa bado milango ya ubngwa iko wazi pamoja na Liverpool kukwamia uongozi kwa kuichapa New Castle bao 5.


Liverpool bwana… we acha tuu!!

December 29, 2008

.

.

Steven Gerrard (R) Liverpool sent a message to the rest of the Premier League with an emphatic 5-1 win over Newcastle at St James’s Park to keep them top of the table. Steven Gerrard netted twice, while Sami Hyypia and Ryan Babel also got themselves on the scoresheet, before Xabi Alonso added the gloss with a 76th minute penalty.

Habari nyingine za michezo ligi ya uingereza


Vijana waaswa kutohudhuria “New Year Mega Sex Party”-Malaysia

December 29, 2008
Kamanda wa Policewa mji wa Joho Baru Malaysia akionyesha silaha zilizokamatwa toka kwenye operesheni maalumu kipindi hiki cha sikukuu.

Kamanda wa Policewa mji wa Joho Baru Malaysia akionyesha silaha zilizokamatwa toka kwenye operesheni maalumu kipindi hiki cha sikukuu.

Katika kile kinachoonekana kuwa upotofu wa maadili Serikali kupitia jeshi la Polisi nchini Malaysia limewaasa vijana kutoshiriki kwenye “Sex Party” ambayo iliandaliwa kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya. Sherehe hiyo ambayo inasemekana imekuwa ikiandaliwa mara kadhaa kipindi kama hiki mafichoni inasadikiwa kuhudhuriwa zaidi ya watu 500 kwa mujibu wa waandaaji waliozungumza na muandishi wa gazeti maarufu la The Star bila kujua.

Kwa mujibu wa gazeti hilo toleo la leo, mualikwa hutumiwa kadi ya  Xmas na Mwakampya na kupatiwa maelezo jinsi ya kushiriki, mwandaaji alisema “…kuna akina dada zaidi ya 200 wameshathibitisha kushiriki ikiwa wengine toka nchi jirani tunahitaji wanaume zaidi, kuna upungufu wa wanaume alisesitiza Ida”.

Malaysia ni nchi inayofuata sheria na dini maalumu ni ya Kiislam hivyo vitendo hivi ni utovu wa nidhani na upotoshaji wa maadili na havitavumiliwa alisema kiongozi mmoja wa dini kwenye Television ya Taifa. Isome habari kamili hapa


Thailand yaachia wafungwa wa Nigeria wakamalizie kifungo kwao!

December 29, 2008

.

.

Baadhi ya wafungwa wa Kinegeria wakitoka Gereza kuu la Bangkok Thailand kwa kile kinachoitwa mkataba wa makubaliano baina ya serikali mbili kubadilishana wafungwa. Wafungwa hawa wa Nigeria walikuwa magerezani Thailand kwa makosa mbali mbali ikiwamo mengi ya kuishi bila vibali maalum na udanganyifu wa njia ya mtandao. Serikali za Malaysia, Singapore, Thailand na Philipines zimekubaliana kufanya jitihada za pamoja kuthibiti uhalifu wa mtandao ambao kwa siliia kubwa umewatia hasara ya mamilioni ya shilingi wananchi wao.


Heri ya Christmas na Mwaka Mpya 2009

December 25, 2008

xmas“Nachukua nafasi hii kuwatakia wasomaji wapenzi Heri na Fanaka ya Christmas na Mwaka Mpya wenye amani. Wito wangu kwa kila mmoja wetu hiki ni kipindi cha kufikiriria mwaka umepita na kuyachambua malengo yako ya mwaka huu 2008 na ni kipindi cha kuweka malengo mapya ya mwaka 2009 na kukazania kuyafikia malengo hayo kwa njia iliyo halali”.

Pius Pius-Kuala Lumpur

Malaysia


Congolese Fashion Designer Gabriel Ba’s Christmas Eve In Harlem

December 23, 2008

Designer maarufu wa Congo Gabriel Ba’s ataonyesha mambo yake kwa nguo mpya alizonazo huko Windows Over Harlem, 163 W125th Street 3rd Floor, Harlem NY. usiku wa kuamkia Christmas (Christmas eve).

Katoka tamasha hilo ambalo pia litasindikizwa na onyesho la Muziki la Mkongwe Papa Wemba, Kwa mujibu wa waandaaji wa onyesho hilo wanasema litakuwa maalum wa ajili ya kuchangia wananchi wa Goma huko Congo ambao wanataabika baada ya Vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Bonyeza player upate uhondo


%d bloggers like this: