Kura zitamponya Latoya jumapili hii?

September 19, 2008
Latoya

Latoya

WATAZAMAJI wa shindano la Big Brother 3 linalofanyika nchini Afrika Kusini, jana walianza kupiga kura ya kuchagua mshiriki atakayerudishwa katika jumba hilo, kutoka katika ‘shimo la taka’.

Washiriki walioko katika shimo hilo ni pamoja na Mtanzania, Tawana na Latoya ambako mmoja kati yao, anaweza kubaki katika jumba hilo kwa mara nyingine, lakini ukweli wa hilo utajulikana Jumapili ijayo, Juzi usiku wakati wa shoo ya moja kwa moja, mtangazji wa jumba hilo, KB aliwatangazia watazamaji kuanza kupiga kura, kwani sasa wameanza rasmi shindano hilo, na kuanzia wakati huo mshiriki mmoja kila wiki atatakiwa kutoka katika jumba hilo.

Latoya na Tawana ambao wametenganishwa katika shimo hilo, ambako watakuwa wakiangalia mambo yote yanayoendelea katika jumba hilo, wakiwa katika makazi ya muda, washiriki wenzao wanafikiria kuwa, wataondoka pamoja huku wengine wakisubiri kuona nani atarejea.

Mshiriki mmoja aliyepo katika shimo la taka, ndiye anayetakiwa kurudi katika jumba na mwingine kuwa ndiye amehamishwa moja kwa moja.

Watazamaji watatakiwa kupiga kura kumchagua yule, ambaye wanataka arudi katika jumba hilo.


Latoya ndiye mrithi wa Richard kwenye BBA3

August 25, 2008

Layota

Anaitwa Latoya ndiye muwakilishi wa Tanzania Kwenye “mashindano” ya Big Brother Afrika 3.

Je ataweza kuweka rekodi waliyoweka kaka zake Mwisho mwampamba kwenye BBA1 alipoibuka wa pili na Richard kwenye BBA2 alipoibuka kidedea?

Bonyeza hapa upate uhondo mambo yameshaanza!!


%d bloggers like this: