Ronaldo bado anakula tuzo!

August 31, 2008

Manchester United's Cristiano Ronaldo holds the best forward award at the draw for the 2008/2009 Champions League in Monaco, August 28. Ronaldo believes he could be back playing for Manchester United by the end of September after completing his recovery from ankle surgery.
Mchezaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo akiwa ameshika zawadi yake ya “best forward award 2008/2009” kwenye shindano lililofanyika huko Monaco majuzi, August 28. Ronaldo alisema anaamini atarejea uwanjani karibuni na kukabiliana na changamoto ya kuendeleza kipaji chake kwenye mchezo wa kandanda hasa baada ya kufanyiwa upasuaji wa ankle.


Arsenal yainyoa Newcastle 3-0

August 31, 2008

Arsenal's Togolese Striker Emmanuel Adebayor (right) vies with Newcastle's Argentinian Defender Fabricio Coloccini during their Premier League match against Newcastle at the Emirates Stadium, London, England, on August 30. Arsenal won 3-0.
Mchezaji wa Arsenal toka Togo Striker Emmanuel Adebayor (right) akigombea mpira na mchezaji wa Newcastle Mu-Argentinian Fabricio Coloccini wakati wa mchezo kati yao wa Premier League hapo jana katika uwanja wa Emirates Stadium, London, England, August 30. Arsenal won 3-0.

Mwaisa kama nakuona full shangwe!!


Mheshimiwa Kikwete katikati ya Game ya Kikapu.

August 30, 2008
Mheshimiwa Jakaya Kikwete wa tatu kulia akifuatilia game kwa makini.

Mheshimiwa Jakaya Kikwete wa tatu kulia akifuatilia game kwa makini.

Game inaendelea

Game inaendelea

Mh. JK akiingia uwanjani
Mh. JK akiingia uwanjani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipata kuhudhuria game ya wanawake WNBA kati ya Washington Mystics (75)vs Chicago Sky(79), game ambayo ilimalizika kwa Chicago Sky kushinda kwa vikapu 79 kwa 75. Game hii iliyofanyika jana hapa washington, d.c katika uwanja wa verizon center na kuhudhuliwa na mh JKPicha zote na Dan Machimu


P.Diddy alalamika kuhusu Bei ya wese!

August 30, 2008

Mwanamuziki P Diddy alalamika kuhusu upandaji wa bei ya mafuta nchini marekani. Mwanamuziki huyo amesema kuwa kwa sasa anatumia ndege za wananchi kwenda safari zake kwasababu ya upandaji huo wa mafuta. Kwasasa hivi ameweka kando privet jet yake kwakuwa imekuwa ni gharama sana kuitumia. Akitumia ndege yake Inamgarimu dola za kimarekani 250,00 kwenda L.A na kurudi NY.

P Diddy karibu katika maisha yetu!


Kutoka umiss paka mgombea mwenza

August 29, 2008
Sarah Palin

Sarah Palin

Governor wa Alaska ambaye amechaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Mccain katika kinyanganyiro cha uraisi Marekani. Mnamo waka 1984 Sarah Palin alifanikiwa kuwa mshindi wa pili katika mashindano ya umiss huko Alaska. Huu ni mfano mzuri kwa mamiss wakitanzania….

Wengi wanasema kuwa uteuzi wa McCain kumchagua mama huyu ili awe vice president ni njia mojawapo ya kumkata miguu bwana Obama…. Wanategemea watu wengi kuunga mkono kuwa na mwanamke katika uongozi wa juu Marekani.


Chumba Cha joker chapanda dau

August 29, 2008
Heath Ledger

Heath Ledger

Chumba cha kwenye hoteli aliyokuwa anakaa Muhigizaki wa filamu kimepanda dau kwa $4000 zahidi ya bei ya mwanzo. Health Ledger ameigiza katika filamu ya batman darknight kama joker. Alikutwa kwenye chumba hicho alichokuwa anakaa amefariki.


KIPANYA jijini BERLIN

August 29, 2008
Dying! Katuni ya Kipanya

Dying! Katuni ya Kipanya

Katuni ya kipanya imeshiriki maonyesho wa uchoraji huko berlin yalioenda kwa jina la Underground Exhibition. Katuni ya dying imependwa sana na watu… kwakutoa ujumbe mkubwa na utaalamu uliotumika kuchora katuni hiyo. Kipanya ni Katuni zinazochorwa na Mtanzania Ali Masoud. Kijana aliyevuka hatua kubwa sana katika usani  wa uchoraji na pamoja na kujiingiza katika Mitindo na lebo yake ya KP. Hongera sana Kaka Masoud.


Upigaji picha ni sanaa bwana..!!

August 29, 2008
Wanne Star

Wanne Star

Wane akiwa hewani kwenye moja ya shoo zake hivi karibuni,Wane kwa sasa anataka kufungua bendi yake atakayoiita Tanzania tradional african dance,je atamudu kupenya kwenye soko la muziki wa sasa,hasa ukizingatia muziki wa asili haupewi kipao mbele sana kama muziki mwingine,je mnaushari gani kwake,kwamba ni vema akabaki kama alivyo kuliko kuanzisha bendi ama ?

Hivi ni baadhi tu ya vitu adimu ndani ya Foto Baraza


Wanaitwa Umoja Group

August 29, 2008
Kundi la Umoja

Kundi la Umoja

Pichani ni wanamuziki wa Kundi la Umoja walipokuwa nchini hivi karibuni, Picha hii imepigwa na Michuzi Jr,, pamoja na nyingine nyingi zinapatikana kijiji cha Foto Baraza, Mdau Mkwaya anasema “…Mi nawakubali katika ubunifu wa nguo na mipangilio ya rangi, zaidi nawapenda kwa mipangilio ya ala na sauti, Tanzania sijui sie letu ni lipi jamani.”

Je we wasemaje?


Houston kaeni mkao wa kula….!!

August 28, 2008
Ally Kiba

Ally Kiba


Blogger ashikiliwa na FBI kwa kosa la kusambaza muziki bila idhini

August 28, 2008
Cover

Cover

Mwandishi wa gazeti tando (Blogger) huko Los Angeles Marekani Kevin Cogill  (miaka 27) ameshikiliwa na makachero wa FBI kwa kutuhumiwa kunakili na kuusambaza nyimbo kutoka kwenye Albamu ya “Chinese Democracy” iliyoimbwa na kundi la  Guns N’ Roses  na kuisambaza kwenye mtandao wake bila idhini ya kundi husika.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyowakilishwa mahakamani kundi la muziki kupitia kwa wakili wao wanasema kuwa kundi lao halitapata mauzo ya kuridhisha na hivyo kuingia hasara kutokana na nyimbo zao kusambazwa ilihali bado hawajausambaza kwenye soko, maredio au hata kumbi za burudani.

Kufatana na habari tulizo zipokea hapo jana, mwandishi huyo alifikishwa mahakamani juma tano na kupigwa faini la dola elfu kumi kwa kosa hilo. Isome hapa


Spika Sitta afagilia Bongo Fleva

August 28, 2008
Samuel Sitta

Samuel Sitta

SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, Samuel Sitta, amesema anawazimia sana wasanii wa kizazi kipya (Bongo Fleva), akiwemo wanamuziki Jackline Ntuyabaliwe ‘Kyline’, Bushoke na Ali Kiba.

Sitta alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati alipokuwa akiongezea kwenye jibu la aliyewahi kuwa Waziri wa Michezo ambaye sasa ni Wazari wa Nchi Ofisi za Makamu wa Rais (Muungano), Seif Khatib aliyesema vijana wa Bongo Fleva waachwe wajimwage kwa sababu kila enzi ina vitabu vyake na vijana hao wanatoa burudani kwa Watanzania. Awali, Mbunge wa Nyang’wale, James Msalika (CCM), alitaka kujua serikali inasema nini juu ya mitindo ya mavazi kwa vijana wa sasa na muziki wa kizazi kipya, Bongo Fleva, ambao unaonekana kumomonyoa utamaduni wa Tanzania.


John Legend- If you are out there!

August 28, 2008

Mwimbo alioimba kwa chama cha democratic wakati Obama akitangazwa kuwa mgombea wa chama hicho pamoja na mgombea mwenza wake


Je wamtambua nani hapa?

August 28, 2008
Picha ilipigwa kwenye msiba wa marehemu Rukia Bruno na mpiga picha wa GP

Picha ilipigwa kwenye msiba wa marehemu Rukia Bruno na mpiga picha wa GP


ASET kuwasherehesha wanahabari Jumamosi

August 28, 2008
Aisha madinda wa Twanga Pepeta

Aisha madinda wa Twanga Pepeta

KAMPUNI ya burudani ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) imeandaa bonanza jumamosi kwa ajili ya vyombo vyote vya habari ambalo linatarajia kufanyika keshokutwa katika viwanja vya Leaders klabu.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Asha Baraka alisema Dar es Salaam jana kuwa bonanza hilo la ASET Media Bonanza linatarajia kuanza saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana, ambapo kutakuwa na michezo mbalimbali.

Aliitaja baadhi ya michezo itakayochezwa katika bonanza hilo ni mbio za magunia, kuvuta kamba, kufukuza kuku, riadha mita 100, netiboli pamoja na mpira wa miguu. Alisema katika tamasha hilo timu mpira wa miguu ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari itapambana na timu mchanganyiko za veterani kutoka klabu mbalimbali, ambazo hucheza mechi kila Jumapili katika viwanja hivyo.

Asha alisema baada ya michezo kufanyika ambayo itamalizika saa 7 mchana, saa 8 itaanza burudani ya muziki wa dansi itakayoporomoshwa na bendi ya Msondo Ngoma Music pamoja na African Stars ‘Twanga Pepeta’. Alisema kampuni yake imeamua kuandaa bonanza hilo la waandishi wa habari kutokana na kushirikiana katika kuendeleza michezo, burudani na kuandika habari za jamii.

Nakuacha na kibao Aminata kilichotungwa na Mwanamuziki Amigolas ambaye kwa sasa ameamua kustaafu kazi hiyo. (Gonga hapa usome sababu zake)


Stars kuivaa Mauritius kwao!

August 28, 2008
Wachezaji wa Taifa Stars walipocheza na Ghana majuzi

Wachezaji wa Taifa Stars walipocheza na Ghana majuzi

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inatarajia kuondoka nchini Septemba 5 kuelekea Mauritius kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya timu hiyo kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela, timu hiyo itaingia kambini kesho na itaondoka na kikosi cha wachezaji 22.

Naye Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbrazili, Marcio Maximo alisema kikosi kitakachoingia kambini ni kile kilichochoteuliwa wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Ghana wiki moja iliyopita.

Alisema baada ya mchezo huo atakipangua kikosi ambacho kitavaana na Cape Verde, kabla ya kutaja kitakachocheza na Sudanu katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka la ndani.

Alisema mchezo dhidi ya Mauritius ni mgumu kwa kuwa timu hiyo itacheza nyumbani huku ikiwa na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa na kwamba ingawa Taifa Stars haina nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia bado itacheza kwa nguvu kusaka ushindi.

Source: Majira


Mtoto wa Dr. Dre Afariki

August 27, 2008
Mwanamziki na Producer Dr.Dre

Mwanamziki na Producer Dr.Dre

Mtoto wa mwanamziki wa miondoka ya Hip-hop afariki dunia. Andre mwenyemiaka 20 amekutwa akiwa amefariki nyumbani kwake baada ya kuparty usiku na marafiki. Chanzo cha kifo cha Mtoto huyo bado akijajulikana.


R.Kelly Akana soo la South Afica

August 27, 2008

Mwanamziki wa Miondoko ya R&B, amekanusha kuwa atamboi chochote kuhusu madai yaliotolewa na mwanamke kutoka South Africa. Mwanake huyo anadai kuwa Aliweka $130,000 katika account ya R.kelly ili mwanamziki huyo aende akafanye shoo mwaka 2005!

Police wamefuatilia na kukuta deposit slip katika office ya mwanamama huyo offisini kwake inayoonesha kuwa hela hizo zilienda kwa mwanamziki huyo. Na pia wamefanya utafiti na kugundua account ni halali ya R.Kelly.


BBA3! Layota Afichua siri

August 27, 2008
Layota Akimfahamisha morris kuwa anampenda

Layota Akimfahamisha morris kuwa anampenda

Mwanadada wa kitanzania Layota atoboa siri kwa Hazel na Tokondwa ni nani anayempenda kati ya Morris na ricco. Mwanadada huyo amesema kuwa yeye amevutiwa na kijana wa kiuganda (morris). Wakati washiriki wenigine wakiwa wanajadiliana mambo Layota alimfuata morris chumbani na kumueleza hisia zake. Morris alimbusu shavuni na kuelekea alipoitwa.

Layota tangia aingie katika jumba hilo la Big Brother amekuwa akilala kitanda kimoja na ricco. Je leo usiku Layota atalala na nani? Pia ricco atafanyaje akigundua kuwa Layota anamfagilia morris na sio yeye?

Haya yote Utayapata Katika Blog yako ya Spotina Starehe.

Layota akielezea jinsi anavyofurahia wakati wa kuoga

Layota akielezea jinsi anavyofurahia wakati wa kuoga


BBA3! Mjue Layota

August 27, 2008

Layota ni mwanadada mwenye umri wa miaka 2. Anafanya kazi ya usecretary Tanzania. Katika profile yake kwenye show ya BBA3 anaonesha kuwa nyumbani kwao ni Mombasa….. Je ni kweli Mdada huyu ni Mtanzania? Tungependa kupata Ufafanuzi zahidi kutoka kwenye vyombo usika.

Layota
Watazamaji wengi wa BBA3 wamekuwa wakijiuliza kweli Tanzania akuna Madaktari wa meno? Watazamaji wao wametoa fikira zao tofauti kutokana na mshiriki Layota Kuwa na meno yenye rangi (yakichagga). Wakiulizana kuwa wameshindwa kungarisha meno ya mshiriki wao! Watazamaji hao wakaendelea kuulizana kuwa yawezekana elimu ya Afya ya mdomo ni ndogo Nchini Tanzania kwakuwa richard naye alikuwa anakwepaga kupiga mswaki na wakati mwingine hata kuoga na alikuwa havai nguo ya ndani….. Hayo yalikuwa ni Mitazamo ya Watazamaji mbali mbali wa BBA3.
Layota Alivyoingia katika jumba la BBA. Aliweza kuzoeana na washiriki wenzake kwa muda mfupi sana. Na kuonesha kuwa amelizoea jumba hilo kwa kuwa huru kufanya kile alichokuwa anataka kufanya.
Layota akiwa Diary Room

Layota akiwa Diary Room

Layota anapenda sana kwenda shopping na kucheza muziki. Anamfagilia Chris Tucker and Owen Wilson.
Layora Akisoma maelezo ya kazi

Layora Akisoma maelezo ya kazi

Layota Akijivinjari na rico

Layota Akijivinjari na rico


%d bloggers like this: