MCD na Atalaku Ferguson wajiunga na Mashujaa Musica

April 23, 2012

image

Anaitwa Saulo John ‘Ferguson’ RAPPER na MUIMBAJI mahiri nchini; LEO AMESAINI MKATABA WA MIAKA MINNE na MASHUJAA BAND:

Show ya utambulisho yeye na MCD itafanyika ijumaa tarehe 27 april pale pale BUSINESS PARK-victoria kijitonyama

image

Naye Mpiga tumba maarufu kwa jina la MCD ametwangazwa kuhamia kundi la Mashujaa Musica leo kwa mkataba wa miaka miwili ambapo atatambulishwa tarehe 27 April ndani ya ukumbi wa Business PARK-VICTORIA KIJITONYAMA

Mashujaa Musica wamekuwa wakijiimarisha safu yao ya uimbaji na sasa wameanza kuimarisha safu ya vyombo, ama kwa hakika kwa sasa upinzani wa Muziki wa dansi umerejea baada ya muda mrefu bendi kama Twanga na FM Academia kushika jahazi jambo lililosabababisha ufinyu wa mageuzi ya burudani.

Tunatumai huu hautakuwa upinzani wa nje ya jukwaa la muziki na  burudani na kuwa chachu ya mageuzi katika sekta nzima ya muziki wa Dansi.


%d bloggers like this: