Grab your copy!!

September 30, 2009

Agosti 1


Wamtambua nani hapa?

September 30, 2009

image

Wallah hakuna kitu kigumu kama kumchekesha au kumfurahisha mtu mwenye njaa!! Pichani ni vijana wa Clouds FM kila mmoja wao akiwakilisha kipindi chake kwa wakati wake, Je wamtambua nani hapa na swali la pili kipindi cha nani unakifurahia kama utatupa na sababu si haba….!


Miss Singapore 2009 avuliwa taji Sababu ya “Wizi”

September 30, 2009

image

Mshindi wa Miss Singapore Ris Low (19), Ameachia ngazi baada ya kuandamwa na vyombo vya habari kwa kashfa ya wizi wa kadi ya malipo ya bank (Credit Card Fraud).

Miss Low ambaye aling’ara mno kwenye mashindano ya Miss Singapore 2009 toka vitongoji hadi kunyakua taji la Miss Singapore na Miss Photogenic 2009 pamoja na mataji mengine 6, kinyakuwa jumla ya mataji 8, anatuhumiwa kutenda kosa hilo alipokuwa akifanya kazi kama receptionist na kwa mujibu wa record za kipolisi Miss Low alitenda kosa hilo zaidi ya mara moja kwa kadi za wateja tofauti akizitumia kwa kununua Vito vya thamani, Shopping, Manukato na matumizi mengine yake binafsi.

Kwa mujibu wa waandaaji wa Miss Singapore ERM World Marketing pamoja na habari za Kipolisi Ris Low alihukumiwa kifungo cha nje cha uangalizi kwa miaka miwili kwa vile ana umri chini ya miaka 21 ambayo kwa sheria za Singapore miaka 21 ni mtu mzima.

Mapema wiki iliyopita Ris alikanusha vikali wakati habari hizo zilipoanza kuvuja dhidi yake, hadi baadaye magazeti yalipotoka na ushahidi dhidi ya tuhuma dhidi yake.

Katika ushindi wake Ris Low ulikumbwa na kebehi ambapo kuna wakati alinangwa kuwa hajui ung’eng’e kama vile ilivyomtokea Kanumba majuzi, Katika kashfa hiyo ambayo iliwagawa mashabiki wengi walimbeza kutokana na Interview yake ya kwanza na sesheni ya Luninga angalia chini hapo.

Hata hvyo kwa mujibu wa waandaaji na Online Community ya wana Singapore, wanasema Miss Low alijieleza kwa ufasaha wakati wa Fainali zilizofanyika Shangrila Hotel hapo July 31.


TEVEZ afanya mambo, Afunga magoli 2 kati ya 3

September 29, 2009

image

Mchezaji wa Manchester City Carlos Tevez jana alionyesha makali yake alipopachika mabao mawili kati ya matatu kwenye mechi ya jana walipocheza na West Ham United.

Mpaka mwisho Man City walikuwa wanaongoza 3-1. Carlos Tevez alifunga bao la kwanza dakika 5 baada ya mchezo kuanza, lakini dakika ya 24 Carlton Cole alisawazisha bao hilo ambalo lilidumu kwa takriban dakika sita tu kwani Man Coty walifunga bao la pili lililowekwa kimiani na Martin Petrov dakika ya 31 kabla ya Tevez kufunga bao la tatu dakika ya 61 ya mchezo ikiwa ni dakika 16 tangu kipindi cha pili kianze.

Mpaka mwisho Man City 3 na West Ham 1


Msimamo wa ligi ya uingereza mpaka sasa!!

September 29, 2009

msimamo


AY Funga kazi Malaysia

September 28, 2009

Katika kuandika historia ya Bongo Flava kipande hii ya dunia mwanamuziki AY alifanya onyesho lake la kwanza kwa Asia hapa Kuala Lumpur Malaysia siku ya Jumanne tarehe 24 Sep katika ukumbi wa Titanium.

AY Ambaye aliingia kwa mbwe,bwe za wanadada wawili wa Asia kuonyesha ni jinsi gani anakubalika na kuanza na wimbo wake wa Habar ndio hiyo!! Ama kweli ilikuwa burudani ya kukata a shoka \. Spoti staehe inaungana na wana East Africa wote kukupongeza kwa kuwashangwesha hapa MAlaysia.


Hamilton Kidume Formula 1 Street Qualifying – Marina Bay Singapore

September 27, 2009

image

Williams Formula One driver Nico Rosberg, McLaren Formula One driver Lewis Hamilton and Red Bull Formula One driver Sebastian Vettel (L-R) pose for a photograph after the qualifying session of the Singapore F1 Grand Prix. The race will be held on Sunday night.


%d bloggers like this: