Bla Bla Bla ya Koffi

January 31, 2012

Kiukweli sijawahi kumakataa Koffi hata mara moja, jamaa ananifurahisha sana kutokana na njinsi anavyowapanga vijana wake na team work aliyonayo.


Heritier Watanabe kijana aliyeeibeba WMMM

January 31, 2012

Kwa wanamjua Werrasson hata kama hasemi hadharani ila Heritier Watanabe ni kijana ambaye kwa ukweli aliibeba sana WMMM.

Mi namkubali sana watanabe yeye kama yeye kwani jamaa anaimba sana na anaweza kunata na beat na hiki ndio ninachozipendea nyimnbo zake. Msikilize hapa Watanabe. kisha na we useme.


Abdallah Herry…!!

January 26, 2012

Anaitwa Abdallah Herry ni mtanzania ambaye anafanya shughuli zake huko Falme za Kiarabu. Abdallah aka Dullah alikuwa baunsa kwenye baadhi ya kumbi za starehe na mimi nilisoma naye Kinondoni High School na kipindi hicho alikuwa akifanya kazi na Clouds.

Kwa sasa Dulla ni Trainer kwenye Gym kubwa ambayo naye ana share na pia ana mikataba ya kufundisha mazoezi ya viungo kwa timu mbalimbali pia huko huko Falme za Kiarabu.

 


Wafanyabiashara waaswa kutumia Barcodes kuongeza wigo wa soko.

January 26, 2012

Wafanyakazi wa GS1 (TZ) National Limited wakiwapungua wadau mikono wakati wa Mkutano mkuu wa Wadau, L to R Fatma Kange (CEO), Andrew Karumuna (BArcode Executive), Pius Mikongoti (Barcode Executive) Clementine (Membership Office), Mabamba Maregesi (Barcode Executive), Judith (Accountant).

Wafanyabiashara na wajasiliamali waTanzaniawametakiwa kutumia Barcodes za Tanzaniakwa ajili ya kutanua wigo wa biashara zao kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kujiongezea masoko na faida zaidi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo alisema kuwa watanzania tumeachwa nyuma sana ukilinganisha na wenzetu wan chi jirani kama Kenya ambao wamechangamkia sana masoko ya kimataifa ukilinganisha na makampuni ya Tanzania, moja ya vigezo vya kufanya biashara kimataifa ni kuwa na Barcodes ambazo zinaweza kukutambulisha kitaifa na kimataifa.

Mpaka sasa jumla ya makampuni 98 yamepatiwa nambari za mistari yaani Barcodes kwa ajili ya kutumia kwenye bidhaa zao. Makampuni hayo ambayo yanafanya idadi ya bidhaa 1450 ambazo ziko sokoni mpaka sasa zinazotumia huduma za Barcodes za kampuni ya GS1 (TZ) National Limited.

Akizungumza wakati wa mkutano mkuuu wa mwaka wa wadau uliofanyika katika hotel ya Blue Pearl Ubungo jijini Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Bw. Elibarik Mmari alisema japokuwa GS1 inamuda mfupi tangu imeanza shughuli zake nchini Tanzania ikiwa na miezi mitano tu tangu ianze shughuli zake bado changamoto ni nyingi wanakutana nazo ikiwa ni pamoja na watanzania kutotambua umuhimu wa Barcode, “Bado teknolojia ya Barcode ni ngeni kwetu, watanzania wengi hawajatambua umuhimu wake kwenye biashara, hii ni changamoto kubwa kwetu kutoa elimu zaidi kwa umma” alisema Bw. Mmari.

Pia Bw. Mmari aliyataka makampuni makubwa ambayo yanatumia Barcodes za nje kubadilika na kujivunia utanzania kwani kwa kufanya hivyo wanakuza ya takwimu za kibiashara za mataifa hayo na Tanzania kuonekana haifanyi vizuri kwenye sekta ya Biashara kimataifa kwani mengi ya makampuni ambayo yana export bidhaa nje yanatumia Barcodes ama za Kenya au Afrika ya Kusini.

Aidha akitoa salamu zake mgeni rasmi katika mkutano huo Mh. Joyce Mapunjo Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara alisema kuwa, Serikali imefarijika sana kuona GS1 imefikia hapo ilipo ingawa inafanya kazi zake katika mazingira magumu Serikali kupitia wizara yake itaisaidia kwa kadiri inavyoweza, vile vile Bi Mapunjo alisema kuwa kuna umuhimu wa taasisi hizi zinazotoa huduma kwa wafanyabiashara ikiwemo TBS, SIDO, GS1, BRELA na TFDA wakawa na mkakati wa kufanya kazi pamoja ili kwa pamoja kuhakikisha kuwa wanarahisisha mazingira ya wafanyabiashara kufanya biashara na kuongeza soko si tu kwa faida ya wafanyabiashara bali kwa nchi kwa ujumla.

Wakati huo huo GS1 wamezindua tovuti yao inayopatikana kwa anuani hii www.gs1tz.org, akiongea kabla ya uzinduzi huo mtaalamu wa mifumo ya habari na mawasiliano na mifumo ya Barcode Bw. Pius Mikongoti alisema tovuti ya GS1 imezingatia kuwaarahisishia mawasiliano na upatikanaji wa fomu kwa ajili ya wanachama wao, kwani mfanyabiashara anaweza akaingia kwenye tovuti hiyo na kuongea moja kwa moja na ofisi aliyeko zamu kama anaswali lolote, vile vile tovuti hiyo inaweza kubadilishwa katika lugha mbali mbali kama Kiingereza, Kispaniola, Kifaransa, Kiarabu, Kihindi nk, kutegemea na mtu na matakwa yake.

MC wa Mkutano huo Bw. Kibonde kiongea na wadau.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo akiongea na jumuiya ya Wafanya Biashara na wadau wa GS1 *TZ( National Ltd katika mkuwano wa wadau jana.

Mgeni wa Heshima Bi. Joyce Mpunjo akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Bw. Yakub Hasham.

Meza kuu ikiwa imeongozwa na Mgeni rasmi Bi Mapunjo Katibu Mkuu wizara ya Viwanda na Biashara.

Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Bw Mmari akiongea na wadau wakati wa Semina hiyo. Katikati ni Mr Nanyaro wa TIRDO akifuat

CEO wa GS1 Bi Fatma Kange akiongea kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mkutano huo.

Mfanya biashara Dr. Mghimba wa BK Tea ya Bukoba akitoa ushuhuda jinsi Barcode zilivyoweza kumsaidia kwenye masoko.

Mmoja wa wafanyabiashara ambaye alikuwa akitumia Barcode za Kenyana sasa anatumia Barcode za Tanzania Ndugu Mlako, yeye anazalisha Ice Cubes.

Mama Ndula wa Ndula Products akipokea cheti maalumu toka kwa mgeni rasmi.

Wadau wa GS1 Wakiwa Mkutanoni.

Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF Mama Esther Mkwizu akizungumza katika mkutano huo.

Toka Kushoto Mwenyekiti wa Bodi wa GS1 Bw. Mmari, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo, Mwenyekiti Bodi ya TPSF Bi, Esther Mkwizu na Mkurugenzi mkuu wa Tirdo Bw. Nanyaro

Wadau wakiwa katika picha ya pamoja.

Bi Esther Mkwizu akizindua Tovuti ya GS1 http://www.gs1tz.org


FALLY IPUPA "CADENAS"

January 20, 2012

 

Walipooondoka akina Suzuki enzi hizo ile timu ya Koffi ilitabiriwa kuwa ingekuwa ni muda wa Koffi kutamba kwenye anga za muziki wa Kongo.

Alipohojiwa na Canal France International (CFI) – Koffi alisema kuwa Quartier Latin ni Dream Team (akiifananisha na timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya Marekani) kwani pale vinapikwa vipaji na kuvipa nafasi ila alisisitiza kuwa wale watakao jifunza kwa nidhamu na nidhamu ya Quartier Latin  ni kujali wapenzi zaidi kujua wanataka nini na ukawapa wanachokitaka basi utadumu kwenye soko, hiki ndicho alichotoka nacho Fally Ipupa kwa Koffi, kwa kweli kwenye hichi kizazi cha tano cha wanamuziki wa Congo jamaa yuko juu na anajitahidi sana kuwakamata mashabiki huku akittengeneza video zake kimataifa zaidi tofauti na zile Video za Ki Congo tulizozoea.

Papaa Julie We Eston, Papaa Sisco na Kati ya Kwetu Saloon Bana Congolee wa Kigamboni. tuko pamoja na jumapili kama kawa Bonanza la Diamond Musica ndani ya Chadibwa Beach- Kigamboni.

Sikiliza hili Rhumba kisha nipe maoni yako unamtabiria nini kwa mwaka huu kijana Fally Ipupa.

Ijumaa Kareem.


Wana “njenje” wa Indonesia

January 17, 2012

Kilimanjaro Band ni bendi moja maarufu sana ambayo inapiga nyimbo za ku copy za kimataifa, Inawezekana hawa jamaa wakawa wameiga jina la The Kilimanjaro Connection ya Kanku Kelly ambayo ilijizolea umaarufu sana Malaysia, Singapore, Indonesia na nchi za jirani kwani takribani kwa miaka kumi sasa wamekuwa wakipiga muziki hasa nchini Malaysia kwa mkataba wa miezi sita kila mwaka.

Sijui jina hili kama walikubaliana ila si mbaya wanatutangaza au wadau mnasemaje?


Best Group of the Decade-Extra Musica

January 17, 2012

Extra Musica ya ROGA ROGA yapata tuzo ya bendi bora kwa kipindi cha miaka 10 (Best Group of the decade) kutoka KUNDE MUSIC AWARD ya Burkinafaso!ubora huo Extra wameuonyesha kuanzia mwaka 2001-2011..pata mahojiano kati ya Roga roga na mwanahabari akielezea anajisikiaje bendi yake kupata heshima hiyo.

 

Moja ya kazi zilizoipatia extra tuzo hiyo,kitu kinaitwa- Plus Tard ,sikiliza masauti hapa vijana wanalia..


Roga le Special one..

January 17, 2012

Nani Kama wewe Roga roga le liberateur de la Extra Musica,

Kitu Racines utunzi wake Roga roga..sikiliza sebene la ukweli hapa..i luv this song


Siku Werra de la forret alipofunika kora!

January 17, 2012

Hii ni siku ambayo haitokaa isahaulike na mawerasonique na wapenzi wa muziki wa congo duniani kote.Ilikua ni mbele ya mzee Madiba Nelson Mandela,pata picha ujikumbushe ilivyokuwa….


Nani mchafu humu?

January 14, 2012

Bonchic Bon Genre na hawa ndio BCBG wenyewe, angalia mashabiki nani mchafu humu?


48 Heures Gecoco, Muendelezo wa Nyimbo zenye mtaguso wa mapenzi toka kwa JB Mpiana.

January 12, 2012

Huwa nina sababu ya kusema kwa nini nampenda JB Mpiana hasa ninapokutana na vitu kama hivi masikioni mwangu.

Kibao hiki kinaitwa 48 Hrs Gecoco kikiwa ni moja ya nyimbo mwanana ndani ya albamu ya JB Mpiana na Wenge BCBG ya TH – Toujours Humble chini ya wakongwe Sipe/Simon Muisic.

Humu utaona maujuzi ya JB kucheza na sauti kwani mashabiki wanakwambia JB anaweza kuimba sauti tofauti sita kama unabisha nakuwekea nyimbo sita zilizochambuliwa usikilize. najua Werasonike hii hamuipendi.

Ila sikiliza humu jamaa kaimba mwanzo hadi mwisho, kiukweli huu ni mmoja wa nyimbo ninazozipenda sana kwenye collection ya JB Mpiana niliyonayo kwenye Library yangu.

Wimbo huu kiufupi unaelezea mapenzi ya wawili ambao jamaa kaenda kutafuta ng’ambo na mwanamke baada ya kusubiri kwa muda mrefu anaamua kupasua jibu kumwambia jamaa arudi, utaona mwanamke anakimbizwa hospitali baada ya vipimo daktari anampina na inaonyesha ana masaa kadhaa tu ya kuishi ila hawaoni ugonjwa, ndo anampigia jamaa simu kumuhabarisha.

anyway wenye tafsiri rasmi hebu tupeni mauhondo. Pia samahani mashabiki wangu nilikuwa kimya kidogo nilikuwa kijijini.


Filamu ya I hate my Birthday kuwaweka pamoja Ray na Aunt Ezekiel.

January 11, 2012

MSANII nyota wa filamu bongo, Aunty Ezekiel, amesema kuwa baada ya kufunga mwaka sasa anatarajia kufungua na kazi mpya inayokwenda kwa jina la ‘I hate my birthday’, ambayo amecheza na Vicent Kigosi ‘Ray‘, huku itarajia kuwa sokoni muda wowote.
Msanii huyo kuzugumzia ujio wake mpya, alisema kuwa mbali na filamu hiyo ya kufungua mwaka pia atakuwa katika mchakato wa kazi nyingine aliyoipa jina la ‘House girl and House boy’.
Msanii hiyo alisema mwaka huu anataka kutoka kivingine kwani mashabiki wake wanahitaji kuona utofauti, ingawa watu wengi wamezoea kumuona akicheza filamu za mapenzi pekee.
Alisema kuwa yeye ni msanii hivyo anauwezo wa kucheza aina yoyote ya filamu kwani, anaweza kuuva uhusika hata wa msichana wa ndani ambapo ndiyo kazi ambayo itaonesha uwezo wake.
‘I hate my birthday’, ‘Naichukia siku yangu ya kuzaliwa’ hiyo ni filamu ambayo itakuwa na matukio mengi kwani hata Ray pia anaichukia siku hiyo hivyo watu watarajie kunaona ubunifu mkubwa ndani ya filamu hiyo kwani mwaka jana umepita na huu ni mwaka mwingine,” alisema.
Ray naye alisema ujio wa filamu hiyo ni mwanzo wa kazi nyingine kwani wanataka kutoa kitu ambacho kitawafanya mashabiki wao waone ni kweli wameingia mwaka mpya huku wakiwa na mambo mpya.


Tangazo

January 11, 2012

Tangazo


JB Mpiana Chante Kabila.

January 11, 2012

Mwaka juzi Mheshimiwa Rais Kabila alikataza Mabanga kwenye nyimbo za Congo kwa wanasiasa akasema zinapunguza credibility ya wafanyakazi wake kwa jamii.

Mwaka jana kulikuwa na uchaguzo Congo wanamuziki walitumika kwa kiasi kikubwa sana katika kampeni mmoja wapo wa wanamuziki hao ni JB Mpiana ambaye alitoa wimbo maalumu kumpigia debe Rais Joseph Kabila, Hii ni mara ya pili kwa JB Mpiana kumpigia debe Rais Kabila kwani kwenye uchaguzi kwa kwanza alifanya hivyo hivyo.


Usiyoyajua kuhusu Goli la Thiery Henry juzi…

January 11, 2012

Thiery Henry ambaye amejiunga kwa mkataba wa miezi miwili na Klabu yake ya zamani ya Arsenal anatawaliwa na namba 12 kwenye goli lake la jana….

  • Alianza mjadala wa kurejea Arsena kwa mkopo mwezi wa 12
  • Akafunga goli lake la 12 dhidi ya Leads
  • Alikuwa amevaa jezi namba 12
  • na Goli lilifungwa dakika 12 kabla ya mpira kumalizika.
  • Kumbuka hili ni goli lake la kwanza kwenye ligi hii kwa mwaka huu 2012

Na hii ndio Starehe ya Spoti bwana.


Chandra ya Bana Ok

January 11, 2012

Wakati huo bado sijaanza kupenda miziki ya Kizaire wimbo huu ulianza kunibadilisha mawazo hasa nilipokuwa nikimsikiliza Kaka yangu mkubwa Mr. Edwin Mikongoti akiimba wimbo huu kila jamaa akiwa mchupa lazima aweze hii kanda (wakati huo ni kanda na santuri) basi nikatokea kuupenda sana.

Wimbo unaitwa Chandra uliimbwa na Ok Jaz (Bana Ok) enzi hizo wakiwa na akina MAdillu System pamoja na Josky Kiambukuta na wengineo ambao kwa pamoja walitengeneza kundi zima la OK Jaz ambalo kwa kiasi kikubwa lilizalisha magwiji wa muziki wa Congo tunaowaona leo hii.

Kaka Hadji Le Geebeeneeque na Papaa Julie We Stone Ilunga Presidaa Bana Congolee na Darisalama hebu tupeni kidogo kuhusi hawa jamaa.


Sebene la Ngwasuma balaa

January 11, 2012

Mdau anauliza, Papy Kakol na Titina Alcapone nani zaidi?

January 11, 2012
Kaka kati ya Papy Kakol na Titina Alcapone nani mkali maana mimi naona kma kakol akifanya recording anakuwa hatishi sana kama live na Titina katika live hajamfikia kakol na tofauti nyingine ni kwamba titina anatumia all pieces za drumset wakati Kakol mostly anapiga snare zaidi hebu nisaidieni jamani.
Othuman Rolenza

Pride Fm

January 10, 2012

Pride Fm


Werrason – Techno Malewa Generique Suite et Fin

January 6, 2012

Habari za mwaka mupwa bandugu bapendwa, nimekuwa kimya kidogo kwa sababu ya mapumziko ya mwaka mupya nilikuwa nje ya mji huko kijijini Mlimba.

Naomba tuukaribishe mwaka kwa kumtendea haki King of the Jungle Werasson Ngiama Makanda jaribu kuangalia quality ya hii Video kisha unipe mchango wako.


%d bloggers like this: