Zadio Kongolo Shabiki nambari wani wa JB Mpiana na Wenge BCBG

December 23, 2008
Anaitwa Zadio Kongolo ukipenda muite ZK wengine humuita Sir Joe Kongolo, ni mfanyabiashara wa Kongo anayeishi Uingereza, Huyu ni mpenzi mkubwa wa JB Mpiana na Wenge BCBG kwa ujumla, ni maarufu kwa kutunza pesa, kwenye onyesho moja la JB alimtunza mwanzo hadi mwisho wa nyimbo (kwa nini asiimbwe!!!) kwenye kila onyesho la JB Mpiana Ulaya humkosi huyu bwana, kama anavyoonekana pichani alisafiri kwenda Belgium hii ilikuwa kwenye onyesho la JB Mpiana mwezi uliopita tarehe 3 May Bruxelles.
JB Mpiana humuimba karibia katika kila wimbo lazima atamtaja ni kama vile unavyosikia PDG Ndama, Abdul Tall Omary Tall, Andrew Traders wanavyotajwa kwenye nyimbo za nyumbani, lakini Zadio amekwenda mbali zaidi kwani kwenye Albamu ya JB Mpiana ambayo inatamba sasa ya “Quel est ton probleme” akimaanisha Nini Tatizo lako?. Jb amemtungia wimbo kabisa Zadio unaoitwa Zadio Kongolo – ZK.
Angalia na usikilize hapo chini, pia wimbo huu uwaburudishe wadau wangu PDG Mukubwa Ling’ande, Big Producer Magambo, Papaa Masabo, Mukulu Biloko Zadio wa Darisalama, Papaa Kasapila, Mukubwa Shabani, Ally Tandika – Tajiri mtoto, Batty William Mwafrica na wengine wengi, Mna nini bwanaaa.
Post hii ilikuwepo kwenye Spoti na Starehe ya awali na nimeiweka kwa maombi ya mdau Mwemtsi baada ya ubishi kati yao. hehehehe

Msiba wa Mama Mere Malou na Zadio Kongolo

July 8, 2008

Msiba wa Mama Mere Malou na Zadio Kongolo

Titina ambaye ambaye alimuwakilisha Koffi na Quartier Latin na Mpiga Gitaa la Rhythm wa Wenge BCBG Alba ambaye alimuwakilisha JB Mpiana na Wenge BCBG wakiwasili msibani.
Papa Wemba (wa pili) akiongoza waombolezaji kubeba jeneza la mama Mere Malou, Inasemwa kuwa Marehemu Mere Malou alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mzee Papa Wemba.
Fallu Ipupa Di Cap akiwa na Producer maarufu Manuru vaka kwenye msiba wa Mere Malou. Fally alitoa rambi rambi ya Euro € 1,500 kwenye msiba huo.
Kuna Post inayosema Zadio Kongolo shabiki namba mojawa Wenge BCBG,

Kwenye maoniya post hiyo Kuna mdau analalamika kuwa huyu bwana si maarufu kama tunavyomkuza na kusema hakwenda Bruxelles kwa ajili ya Onyesho la BCBG, ila alikwenda kwa ajili ya msiba wa Mama Mere Malou “madame ya poto“, ukweli ni kwamba kuna tofauti kubwa tangu mama Mere Malou afariki alizikwa siku ya Jumamosi tarehe 29 ya Mwezi March kwenye Makaburi ya jumping Jack na Onyesho la JB Mpiana lilikuwa tarehe 3 May 2008 huko huko Bruxelles. Si nia ya safu hii kubishana bali ni katika hali ya kuwekana sawa. Kwa faida ya wasomaji wangu, Mama Mere Malou alikuwa Mkongo anayeishi Paris Ufaransa, alishiriki kwa kiasi kikubwa kuukuza na kuutangaza muziki wa Kongo bara Ulaya, alikuwa ndio mdhamini na mpokezi wa wanamuziki wa Kongo kila wakifanya ziara Ufaransa.
Hii ndio “starehe” ya burudani, Big Producer Maghambo umesomeka.

%d bloggers like this: