Maximo alia Yanga wamemnyima wachezaji kujiunga na Taifa Stars

February 9, 2009

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Marcio Maximo amesema kuwa analia na timu ya Yanga ambayo imekatalia wachezaji wake 10 kujiunga na timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo wa majaribio na Zimbabwe.

Akionge na BBC Maximo amesema kuwa Yanga ambao wamempa sababu ya kujiandaa kwao na mechi ya Marudiano na Mauritius ambayo wiki iliyopita waliwachapa bao 8-1.

Maximo amesema kuwa YAnga imesema haiwezi kumpa wachezaji hao wote ambao yeye binafsi anasema anawahitaji sana.

Aidha kocha MAximo alisema timu yake haiigopi michuano ya kimataifa ambayo Taifa Stars itashiriki ikiwa ni michuano ya Afrioca kwa wachezaji wanaocheza ligi ya nyumbani.

Tanzania ambayo imepangwa kundi la kifo linalozishirikisha Zambia na Senegal na Ivory Coast inahitaji mazezi na mechi nyingi za majaribio kwa ajili ya kuzikabili timu hizo, akiongelea juu ya hilo Maximo amesema kuwa uzoefu ndio kilio chake kwa Timu ya Taifa kwani haina mechi nyingi za kimataifa na wachezaji wengi si wazoefu wa ichezo ya kimataifa.

Hali kadhalika MAximo amesema kuwa anafuraha kwa sasa ngalao timu kubwa zimeanza hata kutupia macho Tanzania na anasema hii ni nafasi pekee kwa wachezaji hao kujiuza kimataifa kwa kupitia michuano hii.


We acha tuu kufungwa kunauma bwana…!

February 6, 2009

Kipa wa Etoile d’Or Mirontsy ya Comoro alipoamua kukaa chini baada ya Yanga kupachika bao la nane katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa kwenye uwanja wa Taifa wikiendi iliyopita. Yanga ilishinda 8-1 huku mshambuliaji wake Mkenya, Boniface Ambani akipachika mabao manne peke yake. Picha na Mwanaspoti


Yanga yafanya mauaji, yamchapa mtu 8-1

February 1, 2009

Mashabiki wa YAnga jana uwanjani, Picha kwa hisani ya Michuzi

Mashabiki wa YAnga jana uwanjani, Picha kwa hisani ya Michuzi

TIMU pekee yenye kipa mzungu Afrika Mashariki na kikosi ghali zaidi nchini na makocha watatu wa kigeni, leo imeicharaza bila huruma timu ya  Etoile d’or ya Comorro katika msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 8-1.

Katika mchezo huo ambao Yanga walionyesha ufundi wa hali ya juu na kushangilia mwanzo mwisho na mashabiki wao wakisaidiwa na mashabiki wa Simba. HAbari toka uwanjani zinasema mashabiki wa Simba walishindwa kujizuia na kuonyesha uzalendo wao kwa vijana wa Yanga ambao walionyesha kandanda safi.

Aidha Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega alisema kuwa sakata la kipa Mserbia, Cirkovic Obrem aliyekuwa na utata katika leseni yake limeshatatuliwa na kwamba kazi moja tu uwanjani.

Timu hiyo inayoongoza Ligi Kuu ya Bara kwa pointi 39, iliwatumia vizuri zaidi washambuliaji wake Ben Mwalala, Shamte Ally, Mrisho Ngassa na Mike Baraza huku kwenye ulinzi akisimama Nurdin Bakar, Shadrack Nsajigwa, George Owino na Nadir Cannavaro.


Pole Cannavaro

September 1, 2008

Beki mahiri wa Yanga na timu ya Taifa Nadir Haroub “Cannavaro” amepatwa na pigo kubwa baada ya kufiwa na mchumba wake akiwa katika harakati za kujifungua hivi karibuni.

Cannavaro amekumbwa na balaa hilo saa chache baada ya kuiwakilisha Yanga katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Prisons ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa 4-0 jana jioni.

Blogu hii inampa pole Nadir Haroub kwa matatizo yaliyompata. Bwana ametoa, na bwana ametwaa, jina la bwana libarikiwe.

Je wajua?…. Yanga wanatisha!!

September 1, 2008
Golikipa namba moja wa Yanga Juma Kaseja akipongezwa na wenzake.

Golikipa namba moja wa Yanga Juma Kaseja akipongezwa na wenzake.

Mlindamlango namba moja wa mabingwa wa soka wa Bara Yanga Juma Kaseja ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kati ya wanasoka 334 waliopitishwa na shirikisho la soka, TFF, kucheza ligi kuu ya Bara msimu huu, imefahamika.

Habari za uhakika zilizopatikana jijini kutoka ndani ya TFF zinasema baada ya mikataba yote ya wachezaji kuwasilishwa kwenye shirikisho hilo, Kaseja ameongoza kwa kulipwa mshahara wa shilingi milioni moja kwa mwezi.

Aidha, Kaseja pia ndiye mchezaji aliyeweka rekodi ya dau kubwa zaidi la usajili la dola za Marekani 35,000 (sawa na sh. milioni 40.6).

Chanzo hicho cha habari kutoka ndani ya TFF ambacho hakikupenda kutajwa gazetini kinasema mshahara wa Kaseja upo wazi katika mkataba wake wa mwaka mmoja wa kuichezea Yanga akitokea kwa mahasimu wa timu hiyo Simba na kwamba kiasi hicho ni kikubwa kuliko wachezaji wote wa kigeni.

Mikataba ya wachezaji wengine inaonyesha anayelipwa kima cha chini kabisa anapokea shilingi 100,000 kwa mwezi.

Yanga ndiyo timu inayodaiwa kulipa mishahara minono zaidi wachezaji wake ikifuatiwa na Simba, baada ya kupata udhamini wa pamoja wa kampuni ya bia, TBL.

Timu zinazofuatia kwa kulipa mishahara mizuri, kwa mujibu wa habari kutoka TFF, ni Kagera Sugar na Mtibwa Sugar.

Baada ya hapo, kilisema chanzo hicho, timu za taasisi za majeshi ya ulinzi na usalama za Polisi Morogoro, Polisi Dodoma, JKT Ruvu na Prisons zinafuatia kwa maslahi bora kwa wachezaji.

Toto African inayodhaminiwa na Serengeti, SBL, na Moro United na Azzam zinazomilikiwa na wafanyabiashara zinafuatia zikiwa mbele ya Villa Squad iliyo chini ya Chama cha soka cha wilaya ya Kinondoni, KIFA.


Yanga mambo swafiiii!

August 26, 2008
  • Yalipa Faini na kumalizana na  TFF

Kikosi cha Yanga.... Moto

Kikosi cha Yanga.... Moto

Yanga iliagizwa kulipa faini hiyo baada ya kushinda rufaa yake ya kupinga kufungiwa miaka miwili na TFF kushiriki michuano ya kimataifa kutokana na kitendo cha kutotokea uwanjani katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu michuano ya Kombe la Kagame dhidi ya Simba Julai 27 mwaka huu.

Hata hivyo TFF baada ya uamuzi huo wa Kamati ya Nidhamu, ilisema suala hilo ingelipeleka kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo kitakachofanyika mwezi ujao kwa ajili ya mwongozo zaidi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Iman Madega alisema kwa sasa wapo huru kushiriki michuano hiyo, baada ya kukamilisha taratibu kama walivyoelekezwa na Kamati ya Nidhamu na kuwa walilipa faini hiyo Jumamosi na zimepokewa .


Yanga yapanga kwenda CAS

August 9, 2008

Yanga Uwanjani

Yanga Uwanjani

Uongozi wa klabu ya Yanga, unatarajia kwenda katika Mahakama ya Usuluhishi wa masuala ya michezo ya Kimataifa (CAS), kwa ajili ya kulishtaki Baraza la soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ili kupinga kufungiwa miaka mitatu kwenye Kombe la Kagame.

Yanga, imefungiwa na CECAFA kushiriki michuano hiyo inayoshirikisha klabu bingwa za Afrika Mashariki na Kati kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na viongozi wa klabu hiyo kukataa kupeleka timu uwanjani kucheza mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo dhidi ya Simba.

Yanga, ilishindwa kufika uwanjani kwenye mchezo huo kwa madai kuwa Shirikisho la soka nchini (TFF), limeshindwa kutekeleza makubaliano waliyokubalina ya kupatiwa kiasi cha Sh. milioni 50 kabla ya mchezo huo. Read the rest of this entry »


Yanga wahisi mchezaji wao katorokea Ubelgiji

August 9, 2008
Kabanda

Kabanda

UONGOZI wa timu ya Yanga umesema unahisi kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Laurent Kabanda yupo nchini Ubeligiji.

Kabanda alitoweka kambi ya timu hiyo katika mazingira ya kutatanisha Julai 26 ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika hivi karibuni dhidi ya Simba, mchezo ambao Yanga hawakufika uwanjani.

Katibu mkuu wa Yanga, Lucas Kisasa alisema hadi sasa bado hawajampata mchezaji huyo, lakini hisia zake zinaonyesha kuwa yupo nchini Ubeligiji.

“Bado mpaka sasa hatujampata ingawa kutokana na uelewa wangu nahisi yupo nchini Ubelgiji kwa kuwa mara kwa mara alikuwa anasema kuwa amepata timu huko.

“Tutaendelea kumtafuta kwa nguvu zote kwa kuwa sheria za mpira zipo wazi. Tunaamini tutampata kwa kuwa hawezi kucheza mpira sehemu nyingine bila ridhaa yetu,” alisema Kisasa.

Kabanda alianza kuwa na mgogoro na kocha mkuu wa timu hiyo, Dusan Kondic baada ya kumuweka benchi kwenye mchezo kati ya timu hiyo na APR katika michuano ya Kagame.


Ama kweli Ngoma ya kitoto haikeshi

July 25, 2008

Habari zilizotufikia  muda mfupi uliopita toka kwa mdau na shabiki mmoja wa Simba zinasema kuwa timu ya Yanga ya Tanzania leo “imefungwa kwa taabu” na Tusker ya Kenya katika mchezo wa Nusu fainali ya Kombe la Kagame, Ama kweli Mbuzi yake kamba.

Habari kamili inakuja


Yanga yatia fora kwa mapato mechi ya Ufunguzi

July 17, 2008
Picha hii ilopigwa na Majig Mjegwa ikiwaonyesha Mashabiki wa Yanga kwenye mechi ya Ufunguzi

Picha hii ilopigwa na Majig Mjegwa ikiwaonyesha Mashabiki wa Yanga kwenye mechi ya Ufunguzi

TFF jana ilitangaza mapato ambayo yalipatikana kwenye ufunguzi wa michuano ya Tasker kati ya mechi za timu za Simba na Tusker ya Kenya na ile ya mahasimu wao Yanga na APR ya Rwanda.

Akitangaza mapato ya mechi ya ufunguzi, Dar es Salaam, jana ambayo ilizikutanisha Simba na Tusker ya Kenya, Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, alisema zilipatikana sh. milioni 79.6, ambapo watu 18,420 walilipa kiingilio.

Alisema mechi kati ya Yanga na APR ya Rwanda iliyochezwa Jumapili katika uwanja huo zilipatikana sh. milioni 95 kutokana na watu 23, 719 kulipa viingilio, ambavyo vilikuwa sh. 25,000, sh.20,000, sh. 15,000, sh.10,000, sh.7,000, sh.5,000 na sh.3,000.

Wachunguzi wa mambo ya kispoti wanasema kuwa hii inaonyesha umaarufu wa timu ya Yanga umeongezeka kulinganisha na Simba, na huenda ikatokana na usajili wa Timu ya Yanga ambapo Kusajiliwa kwa kipa Juma Kaseja kumefanya mashabiki wa Mpira kutaka kumuona awapo uwanjani.

Katika mtanange huo wa Yanga na APR mashabiki walilipuka pale KAseja alipokuwa akiingia n wachezaji wenzie uwanjani na kuwa akishangiliwa kila awapo na mpira na mashabiki wa Simba walisikika wakimzomea na kumtupia maneno ya kejeli ingawa hayakufua dafu kutokana na mashabiki wa Yanga kuwa wengi na wenye nguvu zaidi.

Aidha Mwakalebela alisema kuwa kutokana na mwamko uliooneshwa na mashabiki wa mpira wa miguu, mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza ambazo zilipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Taifa zamani sasa zitachezwa Uwanja Mkuu wa Taifa.


%d bloggers like this: