Blandine ya werrason, Wimbo usiopitwa na wakati.

April 16, 2012

Anaitwa LE ROI DE LA FORRET” NOEL NGIAMA WA MAKANDA a.k.a.WERRASON hii ilikuwa kipindi chake cha mwanzo cha kujitawala alipotoka na album yake ya Kibuisa Mpipa kama sijakosea maana hii ilikuwa ni Bonus Truck. Wakati huo bado akiwa na wataalamu wake kama akina Ferre na bado hajakimbiwa na wanamuziki wengi ambao kwa sasa wanatamba sana.

Wimbo huu aliuimba kwa mahadhi ya Congo Rhumba, mdau wangu Hadj le Jbnique (Mnazi mkubwa sana wa JB Mpiana)  ye alinikumbusha mbali sana kuwa album hii ilipikwa na mtaalamu wa Congo Rhumba ajulikanaye kama L.NZIMBI ikumbukwe kuwa huyu ndiye mpishi wa albamu ambayo mpaka leo inauza ya FEUX DE L’AMOUR” yakwake Jemedari SOUVERAIN LEADEUR YA BA WENGEE JB Mpiana ambayo aliitoa kama solo enzi kundi la Wenge Musica BCBG halijaparanganyika.

Huu ni moja ya nyimbo ambazo mimi binafsi Werasson amenifurahisha na kama ningepata nafasi ya kukutana naye na kumshauri ningemshauri a stick kwenye nyimbo hizi za taratibu.

Kitu inaitwa Blandine wakati huo wa Kibuisa Mpipa, Ni wimbo ambao huku kwetu hauku heat lakini ni moja ya nyimbo ambazo nazipenda sana kwa Werrason, Pia kuna vitu kama Koffi Ayiana ambacho niliwahi kukiandikia pia siku za nyuma. Kwa ufupi angalia nyimbo zinazombeba zaidi Werasson ni nyimbo hizi za taratibu zenye mahadhi ya Congo Rhumba ambayo Mkongwe JB Mpiana ni champion kwenye hizo najua ma werasonique mtabisha kwa hili lakini ni wazi na halipingiki.

Truck hii nilimsikilizisha Papaa Mabamba Abiud Maregesi weekend hii na akaniomba niiweke tena, Nimefanikiwa kumbadilisha huyu jamaa imani na mapenzi ya muziki pia ni maalum kwa Werasonique wooote Sadiq Tiger, Papaa Maendeka, Boss Chizenga, Moto Mkubwa Halid Mmanzi, Mdau wangu Steven na wapenzi wote wa Blog hii, Mukubwa Hadji Heshima kwako kiongozi na mnazi wa Wenge


Ma Designer wa Bongo wangarisha Kili Music Award

April 16, 2012

156170

Dayna Nyange dressed by FRANKOO DESIGNS at Kilimanjaro MUsic AWards. Franckoo designs ni Lebo ya mwanadada mwanamitindo Francisca Shirima ambaye kiukweli yuko juu sana kwa sasa na ukimuangalia huyu Bi Dada utakubaliana na mimi.

image

Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe(Left) Dressed in Sheria Ngowi Designs Ndani Ya Kilimanjaro Music Award 2012


JB Mpiana na BCBG waihama Crystal Club

April 16, 2012

Mashabiki wanadai kamkimbia Werasson.

 [http://www.congobilili.com/5385#]

Baada ya kuwa wakipiga shows zao kila jumapili katika kiota cha maraha cha CRYSTAL CLUB  ndani ya KIN kwa takriban miaka miwili,hatimae bendi wa wenge bcbg chini yake Salvatora De La Patria Papaa na Daida Mobali ya Amida Shatur JB MPIANA imeuhama ukumbi huo na sasa itakua ikitumbuiza katika ukumbi wa VENUS HOTEL(Ambiance),hivyo kwa mtakaotembelea Kinshasa kuanzia sasa basi msisumbuke tene kwenda CLUB CRYSTAL siku ya jumapili,kwa sasa mambo yote ya concerts za bcbg za kila jumapili yapo VENUS

Hii hapo juu  ni sehemu ya video iliyopigwa kwa simu ya mkononi siku ya kwanza bcbg kutumbuiza kwenye hicho kiwanja chao kipya kwa kila siku ya jumapili,show hii ilihudhuriwa na mastaa kibao katika tasnia ya muziki wa congo akiwemo Bill Clinton,baby ndombe,alain mpela na baadhi ya wanamuziki kutoka katika bendi ya Fally Ipupa

Hivi karibuni ilitangazwa kuwa Werrason na kundi zima Wenge Musica Maison Merre nao wameanza kupiga ukumbi jirani na hapo Crystal Club.

Kitendo cha mahasimu wawili kupiga kwenye eneo moja kinafanya wote kuwa na wakati mgumu kwani kila mmoja anatakiwa awaelimishe hasa mashabiki wao kuvumiliana na si kuleteana fujo kutokana na kuwa na ukweli kwamba mashabiki wa Werra na JB ni kama Simba na Yanga.

Werrason ametangaza kuachia Single yake inayojulikana kama « Honorable député ».

Kwa upande wake Werrason alitangaza ukumbi wa La salle Carlos ulioko Kinshasa kuwa ndio utakuwa ukumbi wake wa kujidai na kila jumapili atakuwa akipiga kwenye ukumbi huu ulioko complex Mwana Nteba

Mashabiki wa Wenge BCBG walikuwa wameshazoea kupata burudani kila jumapili kutoka kwa kipenzi chao JB Mpiana na bendi nzima ambapo wanafanya sho zao kila jumapili katika ukumbi wa “The Crystal Club” ambayo iko barabara ya 30Juin ambayo ni eneo moja na ambako Werrason atakuwa anapiga.

Inasemekana JB Mpiana amenunua ardhi jirani na hapo na ameanza ujenzi ambapo inasemekana anajenga studio pamoja na ukumbi wa kufanyia mazoezi na pia club. habari zinasema kuwa ujenzi umeshaanza kwa hiyo mashabiki watakuwa wameongezewa burudani zaidi.


Koffi azindua aina yake ya Perfume

April 16, 2012

BB Gout perfume by Koffi Olomide

Na Hadji BCBgeeque

image

Baada ya BB GOUT song  sasa anakuja kivingine na kisasa zaidi na BB Gout perfume by Koffi Olomide

KOFFI OLOMIDE sasa ameintroduce perfume line yake kama wafanyavyo mastaa wa marekani na ulaya kiujumla kujiingiza katika ujasiriamali kwa kuwa na clothing line,perfume line n.k.

BB Gout maana yake msichana mrembo mwenye mvuto ambae koffi aliwahi kumuimbia katika kibao kilichoitwa hivyo hivyo BB GOUT ambacho binafsi hukipenda sana kukisikiliza kutokana na mpangilio wake wa sauti pamoja na mashairi mazuri.

Pamoja na perfume hiyo mpya kwa kina dada toka kwa koffi olomide ili twende sawa tazama video ya kibao BB GOUT hapo chini na ukisikilize kwa makini.

Kina dada kazi kwenu BB Gout perfume by Koffi Olomide ndio hiyo sokoni…kiufupi hili ni bonge la move kwa muziki na wanamuziki wa congo ambalo naona kama limechelewa kutokana na umaarufu wa wanamuziki na muziki wa congo walitakiwa kuwa na product zao kama nguo, perfume, saa n.k. sokoni siku nyingi sana but its a good start, thanx koffi


Kanumba alitabiri kifo chake kwa Wimbo kama Bavon Marie.

April 16, 2012

Bado tuko kwenye Siku 40 za maombolezo ya kipenzi cha watanzania Steven Kanumba, Majuzi nilisikiliza TBC Radio nikamsikia Thimanga Kalala Asosa akiongelea jinsi Kanumba alivyotabiri kifo chake na kumfananisha na mwanamuziki aliyewika na kupendwa sana huko Congo miaka hiyo aliyejulikana kama Bavon Marie.

Wimbo huu ulitungwa na bwana Bavon Marie –Marie kama kutabiri kifo chake, nakuletea huo Wimbo baada ya kumsikia Papa Tshimanga Kalala Asossa katika kipindi cha TBC Radio akifananisha tukio la Marehemu Steven Charles Kanumba na kifo cha Bavon Kwa wingi wa watu waliohudhuria mazishi ambayo watu Wengi walikosa fursa ya kumuaga na tofauti ni hali ya hewa Bavon Kulikua na mawingu mazito Kule Kinshasa lakini Dar kulikuwa jua kali. Kwa waliofatilia mahojiano yale na kuombaniutafute wimbo huu nimeupata na shukrani za kipekee kwako Le Fimitive Didie Kinuani ya Tunduma Thabit Mwambungu kwa ukokotoo huu.

MASEKE YA MEME- PEMBE ZA KONDOO

BAVON MARIE MARIE

NEGRO- SUCCESS

Famille oyo motema mabe bondoki ekoma mosala,

Mwana moke lokola ngai bakundeli ngai maseke ya meme liboso ya lopango o batii ngai motema motomoto mpo nabala Te,

Familia hii ina roho mbaya uchawi umekua kazi,

Mvulana Kama Mimi wamenizikia pembe za kondoo mbele ya nyumba wamenitia hofu nisiolewe,

Kanda ya nini o bandeko mpo baliaka mbongo na ngaite balongola ngai motema e batia ngai motema ya soso mpo nakoma lokoso nasilisa mibali e ndoki mpe akufaka e nkisi mpe epolaka,

Hasira ya nini ndugu zangu sababu hawatumii pesa yangu wamenitoa roho wameniweka roho ya kuku ili niwe na tamaa nimalize wanaume mchawi huwa anakufa dawa nayo inaoza,

Malamu koboma ngai nakufa e nalembi ngai mwana moto.

Bora/vizuri mniue nife nimechoka Mimi mtoto wa mtu.

Bomengo nini na ngai o nazali na mbongo te o tokowela nini?

Utajiri gani nilionao sina pesa tunagombea nini?

Bondoki eloko mabe o banganga mpe bakufaka e Mokili oyo ya batu

Uchawi kitu kibaya waganga pia hufa dunia hii ya watu

Nalela na vie na ngai o nalembi Mokili te o balingi ngai nakufa e

Nalia maisha yangu sijaichoka Dunia kuishi wanataka nife

Naloba lisusu te o nazela kaka liwa ee

Sitasema tena nangojea mpaka kifo.


%d bloggers like this: