Liberez live ndani ya Boat

April 11, 2012

Baada yauwanja wa burudani kugubikwa na wingu zito la kifo cha ndugu yetu Kanumba ambaye amehitimisha siku zake 10321 jana pale Kinondoni Makaburini leo tugeuke kwenye burudani yetu kama kawa kama dawa.

Huwa na jaribu kuwaza je ingekuwaje Congo wangekuwa na bahari maana jamaa wanapenda starehe ajabu, pichani ni JB Mpiana na kundi ake la Wenge BCBG wakitumbuiza ndani ya tamasha la Avec Inon nadhani ndivyo linavyoitwa. Mukubwa Hadji muzee wa Mapezi Club sikiliza kuanzia 1:06 Sikia jinsi jamaa anavyoimba ni balaa.

Advertisements

Mamia wamzika Kanumba

April 11, 2012

image

Nyumba ya mwisho ya Marehemu Kanumba alipozikwa, Raha ya Milele umpe eeeh bwana na mwanga wa milele umuangazie.

image

Mwili wa Marehe Steven Kanumba ukiwa umelala ndani ya Jeneza na wananchi wakipita kutoa heshima za mwisho pale viwanja vya leaders kabla ya kuelekea makaburini Kinondoni hapa hapa Dar Es Salaam.

image

Mamia ya wananchi wakiwa viwanja vya Leaders mchana wa leo

image

Mamia ya wananchi wakiwa viwanja vya Leaders mchana wa leo

image

Mheshimiwa Mbunge na mwanaharakati wa muziki wa kizazi kipya Mheshimiwa sana Joseph Mbilinyi aka Sugu akitoa heshima zake za mwisho mbele ya mwili wa Marehemu Kanumba.

image

Kamanda wa Polisi wa Kanda Kuu ya Dar Es Salaam Kamanda Kova akitoa heshima zake za mwisho.

Kwa miaka yangu 37 ya uhai sijawahi kuhudhuria msiba wa mtu ambaye si kiongozi na akazikwa kama alivyozikwa Steven Kanumba, ama hakika Steven Kanumba amemaliza siku zake 10321 leo hii kwa maziko ambayo kila mmoja yamemgusa.


%d bloggers like this: