Harusi za Kimalay, Sehemu ya Pili.

May 17, 2010

n618528368_1348020_2812

Nimeirudia hii baada ya kupata ombi toka kwa Bi. Harusi mtarajiwa Dada Mayasa, sijui labda anataka kuiga vindu humu.

Mara ya mwisho niliandika kuhusu harusi za kimalay (gonga hapa) na huu ni muendelezo wa mfululizo ma tukio zima la siku hiyo ambayo kila mmoja huwa anaiwazia maishani.

Wamalay tumefanana nao kwa Mila na Desturi kwa kiasi fulani, ama kwa hakika ukibahatika kuhudhuria harusi za kimalay utafurahi mbwembwe na shamrashamra za harusi. Kwa kawaida wao hawachangishani kama tunavyofanya sisi, ni jukumu la familia kufanikisha shughuli hii, na kwa taarifa yako sherehe ya kawaida ya mtu wa kawaida hugharimu kuanzia Ringit 100,000 hadi laki tatu kutegemeana na familia. Ringit 100,000 ni sawa na Tsh 30,000,000/- , Milioni 30.

Gonga hapo chini upate kuona mtirirko wa matukio kwenye harusi hii ya rafiki yangu Nazmi ambaye alimuoa bibiye Aimi.

Read the rest of this entry »


Harusi za Kimalay! We acha tuu!

January 21, 2009
Katika mambo ambayo hugharimu pesa na muda basi ni harusi na si kwa nyumbani tu bali utamaduni huu nimeuona hapo nyumbani na Asia pia lakini Malaysia kwa maoni yangu imezidi, Wamalay hutumia pesa nyingi sana kuandaa harusi, Kwa hulka ya Kimalay harusi yaweza kuchukua hadi wiki mbili ikisherehekewa kwa matukio mbali mbali, Harusi iliyovunja rekodi ni kati ya mwanamuziki Mawi na mwanamuziki mwenzie Ekin ambao wanatamba kwenye nyanja ya muziki hapa Malaysia na Asia kwa ujumla.
Harusi ya Mawi inasemekana imegharimu si chini ya Malaysia Ringit 300,000 karibu sawa na dola za kimarekani 100,000.
Hii ikiwa ni pamoja na zawadi za bwana harusi kwa bi harusi ikiwa ni pamoja na Vidani na vito vya thamani.

Maharusi Mawi na Ekin wakiwa Meza kuu mara baada ya kuwasili ukumbini kamla ya kubadili nguo kwa ajili ya kukata keki, Maharusi hawa walibadilisha nguo zaidi ya mara mbili kwa kila tendo muhimu, Ukumbi ulikuwa umepambwa na nakshi na taa za thamani na kuufanya uonekane madhari tofauti ikiwa na theme ya Mashariki ya Kati.

Unique: Hapa maharusi Mawi na Ekin wakikata keki maalum ambayo imetengenezwa kwa mandhari ya vijimito.
Proud moment: Mawi’s compatriots from Akademi Fantasis 3 (from left) Ekin, Akma, Elizza, Amelia, Marsha and Idayu.


Mmoja auawa, wawili wajeruhiwa kwa risasi Malaysia

August 6, 2008

Pichani kushoto, Askari kanzu akiwa amemsikilia mtuhumiwa mwanadada toka Liberia huku wengine wawili wakiwa wamelala chini mmoja amefariki na mwingine anayeonekana hapo alipigwa risasi ya tako.

Tukio hili lilitokea jana hapa malaysia baada ya polisi kufuatilia nyenendo za watuhumiwa hawa watatu ambao wote ni raia wa Liberia kulalamikiwa na baadhi ya watu kujihusisha na biashara ya dola fake “Black Money” ambapo walikuwa wakibadilisha dola 50,000 kwa 16,000 Malaysian Ringit (kwa kawaida 1USD=3.2 Malaysia Ringit0 na inasemekana wako hapa tangu january na polisi wanakesi zaidi ya 20 kuhusiana Black Money. Kwa mujibu wa ripoti ya kipolisi, Kumekuwa na wimbi kubwa la kesi za uhalifu kutoka kwa jumuiya ya Waafrika hasa Waafrika Magharibi ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakijihusisha na biashara haramu za madawa ya kulevya, Fedha bandia na hata utapeli wa kudanganya wafanya biashara kwa kutumia mitandao ya kompyuta ya bandia na hivyo kujipatia pesa nyingi kutoka kwa raia wa huku ambao wanapendelea kufanya biashara kwa kutumia mtandao wa internet (e-commerce and e-business).


“Fungasheni mrudi kwenu”, Malaysia yawaambia wachezaji wa kigeni

August 4, 2008
Mykie Opur wa Kenya na Rashid wa Tanzania, Wanasoma na pia wanacheza soccer nchini Malaysia

Mykie Opur wa Kenya na Rashid wa Tanzania, Wanasoma na pia wanacheza soccer nchini Malaysia

“Its Offical, The foreign players may pack and go back to their home country…” ndivyo lilivyoanza gazeti la tThe Star toleo la jana, Chama cha mpira wa miguu cha Malaysia (FAM | Football Association of Malaysia) kimetangaza rasmi kuwa kuanzia msimu ujao wa Ligi wachezaji wageni wote hawataruhusiwa kucheza ligi hiyo, Kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na vyombo vya habari jana,  uamuzi huo umechukuliwa ikiwa ni kulinda hadhi na wachezaji wa ndani ambapo inasemekana hakuna mageuzi yeyote yaliyoletwa na wachezaji walitoka nje ya Malaysia katika kuendeleza mchezo wa Soka.

Aidha ripoti hiyo inasema kuwa wachezaji hao wamekuwa wakilipwa tofauti na wachezaji wa ndani ambapo wao kwa kiasi kikubwa wanakatishwa tamaa na kudumaza soka. Wakiongea wadau wa soka wamekuwa na mtazamo tofauti kulingana na suala hili ambapo wengine wameonyesha kufurahishwa na wengine wamekuwa wakilipinga kwa kusema kuwa michezo nia yake ni kukutanisha watu na kuwapa burudani, ili kufanikisha hilo mchezo wa mpira nao haujitengi na michezo mingine bila kusema nani anayetoa burudani hiyo alisema Kim Ng alipokuwa akiongelea suala hili.

“Ligi yetu bado ni changa hatujafikia kiwango cha ligi ya Uingereza hawa watu wanalipwa pesa nyingi na hakuna mabadiliko kwenye soka letu matokeo yake Timu yetu ya Taifa haifanyi vizuri” alisema Makamu wa Rais wa shirikisho hilo Ndugu Khairy Jamaluddin.

Hivi karibuni chama cha mpira wa miguu nchini Uingereza kimekumbwa na kigugumizi juu ya kuamua ama kuwafukuza ama kuwapunguza ama kutowaruhusu kabisa wachezaji wageni katika vilabu, Vilabu vya Uingereza ndivyo vinaongoza kwa kuchukua wachezaji wengi toka mataifa mbali mbali na hivyo kuchangia kuipa umaarufu ligi ya mchezo huu duniani kote.


Uraia wa Avram Grant almanusura ungeikatisha ziara ya Chelsea Malaysia

July 15, 2008

Kuondoka kwa kocha wa Chelsea Avram Grant na ujio wa Kocha mpya F. Scolari kumeokoa Ziara ya klabu ya Chelsea hapa Malaysia ambayo awali ilitishia kuifuta kutokana na Kocha huyo wa Zamani kutoruhusiwa kuingia Malaysia kwa sababu ya uraia wa Israel, Malaysia haina mahusiano yeyote ya kibalozi au kibiashara na Israel kwa vile Malaysia inatambua Taifa la Palestina ambalo ni mahasimu wakubwa wa Islael. Marufuku hiyo isingeishia kwa Kocha Grant pekee bali hata mchezaji Tal Ben Haim ambao kwa pamoja walihitaji kuomba vibali maalum ili kutembelea baadhi ya nchi za Kusini Mashariki mwa Asia. (Habari hii kwa Mujibu wa Aljazeera)


%d bloggers like this: