
Kocha Arsene Wenger
Kocha wa Arsenal kibabu Arsene Wenger amesema kuwa kama kuna mtu anayepaswa kulaumiwa kwa matokeo mabaya ya klabu yake kwa msimu huu basi ni yeye.
Wenger amekaririwa akisema hayo na BBC kufuatia kipigo kingine hapo jana walipocheza na Bolton na kufungwa bao 2-1.
Arsenal wamebakiza michezo minne mkononi huku wakiwa nyuma ya vinara Manchester United ambayo itakutana na Arsenal jumapili ijayo, Kama wakishinda Man U basi huu utakuwa msimu wa sita kwa Arsenal kumaliza bila kikombe.