LEO NIMEWARUDISHA KWENYE ENZI ZILE NA KOFFI OLOMIDE, WIMBO ” PAPA BONHEUR “

September 30, 2014

 

BOFYA KICHWA CHA HABARI NA UBURUDIKE

PAPA BONHEUR NI WIMBO ULIO MLETEA SIFA NYINGI SAANA KOFFI OLOMIDE LE GRAND MOPAO, wakati Album hii ilipotolewa, CD zote zilinunuliwa kwa Wingi, Ilibidi zichapishwe nyingine.

Sifa kutokana na Wimbo huo ” PAPA BONHEUR ” Ulipelekea KOFFI OLOMIDE apate mialiko kutoka kwa RAIS WA GABON Marehemu OMAR BONGO ODIMBA, kadhalika kwa RAIS DENIS SASSOU NGWUESSO .

” PAPA BONHEUR ” NI WIMBO UNAOPATIKANA KWENYE ALBUM  ” Haute De Gamme/Koweit Rive Gauche ” ILIOTOLEWA MWAKA 1992 MWEZI WA PILI, PRODUCER AKIWA ” SONODISC “.

MTAWAONA WANAVYO NENGUA AKINA DADA : ROSETTE KAMONO Yuko Jijini Paris Keshakua Mlokole, JACQUIE DE KANAM’S ambae kwa sasa ni Marehemu, FLORIANNE MANGENDA Maskani yake JIJINI BRUSSELS, na FIFI MISS YOLO Pia yuko PARIS.

Kwenye Album hii, KOFFI OLOMIDE kapata ushirikiano wa Wataalam wa Muziki :

  • Nyboma Canta (Mwimbaji)
  • Jeffard Lukombo (Mwimbaji)
  • Luciana Demingongo (Mwimbaji)
  • Deésse Mukangi (Mwimbaji)
  • Beniko Popolipo (Guitarist)
  • Dally Kimoko (Guitarist)
  • Nguma Lokito (Bassist)
  • Djoudjou Music (Ngoma)
  • Code Niawu (Percussions )

Bila kusahau Mchango wa SUZY KASEYA na MAIKA MUNAN.

 

L.W.L

 

 


WIMBO MPYA MZURI WA KIJANA MICHEL SYNTHE ALIE JIONDOA KWA FERRE GOLA

September 30, 2014

 

BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI USIKILIZE WIMBO ( AUDIO )

MICHEL SYNTHÉ NI MPIGA KINANDA, YEYE NIKATI YA VIJANA WA MWANZONI KUJIUNGA NA FERRE GOLA TOKEA MWAKA 2007.

ILIPOFIKIA MWAKA 2011 KUTOKANA NA SABABU ZAKE BINAFSI KAAMUA KUJIONDOA.

NAONA KAFANYA KAZI NZURI KABISA ANAHITAJI PONGEZI.

 

L.W.L

 

 


MPYA HIYO YA CHIKITO MAKINU ( AUDIO )

September 29, 2014

BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI USIKILIZE UIMBAJI MARIDADI WA CHIKITO

JUMATATU NJEMA NA WIMBO AUDIO WA KIJANA CHIKITO MANIKU ” BOLINGO OKANGA ”

CHIKITO NI MWIMBAJI MZURI TENA MWENYE KIPAJI, TUKIWA BADO TUNASUBIRIA AZIMIO LAKE, SWALI JE? UPO UWEZEKANO KWAKE YEYE KURUDI  KWA FERRE GOLA AMBAE BADO MAWASILIANO HAIJAKATIKA, AU NDO YUKO NJIANI KWENDA KUJIUNGA NA WENGE MUSICA MAISON MERE YA NGIAMA MAKANDA WERRASON ? MWENYEWE KASEMA ANAPENDELEA KUANZA CAREER SOLO NA YUKO KWENYE MATAYARISHO YA ALBUM YAKE YA KWANZA ” HIROSHIMA “. KWENYE MUZIKI WA CONGO LOLOTE LAWEZA KUTOKEA !!!

 

L.W.L


ALBUM MPYA YA MKONGWE ” SESKAIN LAMBERT DIEUDONNE MOLENGA “

September 29, 2014

 

 

10636036_10202699632960392_1675838316836135725_nseskain-molenga

 

 

UKIHITAJI KUSIKIA RUMBA LA UKWELI, BASI BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI

Mzee SESKAIN MOLENGA kwakweli katoa Rumba kali kabisa ambayo hua Bidhaa hadimu kabisa siku hizi kwenye Muziki wa Congo.

Kwaukumbusho, SESKAIN MOLENGA ni mmoja kati ya Waanzilishi wa Orchestra EMPIRE BAKUBA ya akina PEPE KALE

Kwenye Album ” EMPIRE BAKUBA LÉGENDE “,SESKAIN MOLENGA kaweka Nyimbo 17 ambazo zote ni Nzuri.

Album hii Ilipata Ushirikiano Mkubwa wa wataalam wa Muziki, Timu ya Waimbaji ikiongozwa na NYBOMA, Kwenye GITA mtawakuta DALLY KIMOKO na DIBLO DIBALA, Kwenye BETTRY Wapo THEO BLAISE akisaidiwa na SOLO SITA.

Album ” EMPIRE BAKUBA LÉGENDE ” yaja kwa wakati Mzuri ilikuleta Marekebisho kwenye Muziki wa Rumba uliojipoteza siku hizi kwa kujaa na Majina ya Watu, kwakua Humu Hamuna ” LIBANGA “.

Haya Burudikeni na Wimbo ” BAKOLUKA TO KABUANA ”

 

L.W.L

 

 

 

 

 


JAMANI HUYU KOFFI OLOMIDE MWISHO KABISA, TIZAMENI TANGAZO AKIJISIFU YEYE NI VIEUX ” EBOLA “

September 28, 2014

 

BOFYA KICHWA CHA HABARI UTIZAME TANGAZO LA KOFFI ” EBOLA ” ETI KAWAZIBA MIDOMO WOTE WALIOKUA WAKICHUKULIA JINA HILO KAMA ” TUSI ” .

Katika mahojiano yake na Mtangazaji MAMI ILELA, KOFFI OLOMIDE kasema kwanza analipenda saana jina la ” VIEUX EBOLA ” MZEE EBOLA, JINA LENYE NGUVU LAPELEKEA WATU WAMKIMBIE NAKUMUOGOPA .Kamtaka yeyote yule ambae kajihisi anayo matatizo naye, basi ajitokeze na azungumzie nini kiini cha ugonvi wao, Mwenyewe kashangaa kuona watu Wanamsakama, Kapokea Msg nyingi sana zikitokea Pande zote za Dunia wakimtaka Ugonvi kati yake na JB MPIANA uishe!!! Kwake yeye kaona Wengi wamionea Wivu. Kwenye Video Nyingine, KOFFI OLOMIDE kasema : ” LAITI ASINGEKUA YEYE NI KOFFI OLOMIDE, BASI NAYE ANGEMCHUKIA KOFFI OLOMIDE, KWAKUA JAMAA YUKO JUU SAAANA…

 

L.W.L


REPA ” KIRIKOU ” KAJIONDOA WENGE MUSICA MAISON MERE YA WERRASON, KARUDI KWA FERRE GOLA

September 28, 2014

 

BOFYA KICHWA CHA HABARI UPATE KUTIZAMA VIDEO.

REPA ” KIRIKOU ” AMBAE MWANZONI ALIKUA KWA FERRE GOLA, NAHAPO BAADAE  KAHAMIA WENGE MUSICA MAISON MERE YA WERRASON, KAAMUA KURUDI ZAKE NYUMBANI KWAO KWA FERRE GOLA.

KASEMA KWENYE MOJA YA RAPU ZAKE ” MTU HUJISIKIA RAHA UKIWA NYUMBANI KWENU,HUKO KWA WANANDUGU WA FAMILIA, KUNA WAKATI MWENGINE MTU HUKOSA RAHA ” WALIKUA WAKINILAZA NJAA, NILIKUA SIPEWI NAFASI NZURI YAKUJIELEZA,NI KWAMAANA HIYO NAAMUA KURUDI ZANGU NYUMBANI KWETU. NAKUTAKA RADHI ” KAKA YANGU FERRE GOLA NAOMBA MSAMAHA ” .

NDIPO FERRE GOLA KASEMA : KIRIKOU UMEKARIBISHWA, HAPA NI NYUMBANI KWENU,KAWAAMBIA MASHABIKI WALIOKUA HAPO KWENYE UKUMBI WA  MAZOEZI KWAMBA : ” KIRIKOU NI KIJANA ALIE NA KIPAJI CHA HALI YAJUU KWENYE  RAPU,BAADHI YA RAPU MLIZOZISIKIA KWENYE ALBUM ” BOITE NOIRE ” NI YEYE KAZIWEKA.

KIRIKOU KAIMBA RAPU ZENYE UTATA : (chez koko na biso ba liaka ba kabela nga , ba lataka na defisanga ) / HUKO KWA BABU YETU WATU WANATUMIA CHAKULA KWA WINGI ILA MIMI WANANIMEGEA CHAKULA WENGINE HUNUNULIWA NGUO HUKU MIMI NAENDELEA KULAZIMA .

TUNAENDELEA KUZIFWATILIA HABARI KWA UMAKINI

 

L.W.L

 

 


WEEKEND NJEMA NA MSANII ” KUKUSON ” KUTOKA CONGO DRC NAWIMBO WAKE ” EBEBA “

September 27, 2014

 

INCHI YA CONGO INAYO VIPAJI VINGI MNOO VYA MUZIKI, MBALI KABISA NA HAO WANAO FAHAMIKA,

MZIKILIZENI KIJANA  ” KUKUSON ” AKIIMBA WIMBO WA KIZALENDO ILIKULAANI KITENDO CHA VITA KUENDELEA MASHARIKI MWA INCHI HIYO.

 

L.W.L


%d bloggers like this: