HISTORIA YA MWANAMUZIKI FERRÉ GOLA. SEHEMU YA TATU

January 30, 2014

Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza jinsi Ferre Gola alivyoingia Wenge Musica akiwa ni mwanamuziki wa mwisho kuwa recruited kabla ya bendi hiyo kuvunjika na pia sehemu ya pili kuangalia maisha yake ndani ya BCBG mpaka alipoamua kutoka kivyake na kuanzisha bendi yake…. Leo ni sehemu ya Tatu kama inavyoletwa kweu na msimulizi wako mahiri Lubonji wa Lubonji.

Mwanamuziki Ferre Gola akiteta jambo na mke wa mfanyabiashara maarufu Macheni hii ilikuwa alipokuja nchini kutoa burudani.

FERRE GOLA na Group Les Marquis de maison Mère, wakafaanikiwa kutoa Album yao MIRACLE, Utazikuta nyimbo Amour ya Intérêt na 100 kilos utunzi wa FERRE GOLA,
Ecole utunzi wa JUS D’ÉTÉ MULOPWE, TRAHISON wa BILL CLINTON KALONDJI.
ALBUM MIRACLE ilipokelewa vizuri sana, mashabiki, wapenzi wa muziki pia wajuzi wa maswala ya muziki wakawaweka kwenye nafasi ya kwanza kabisa kwa wanamuziki wa kizazi kipya huko CONGO (5th generation).
Ingawa mambo yao yawaendea vizuri kutokana na SHOO zao kujaa watu wengi, kushangiliwa kwa nguvu, na pia kupata mashabiki wengi, kadhalika Album yao kupokelewa vilivyo, Baadhi ya wandishi wa Habari wakasema:” VIJANA HAWA WANAVIPAJI VYA HALI YA JUU, WANAWEZA KUSONGA MBELE KABISA, ILA WANATATIZO MMOJA KUBWA SANA, NALO NIKUTOKUWA NA LEADER KATI YAO. NA NDILO LILILO WAPONZA.”

MGAWANYIKO WA GROUP LES MARQUIS DE MAISON MÈRE

Hali yakutoelewana ikazidi kukua,mikokotano huku na huku, kila Mmoja kajidai ndie yu LEADER, wengine wajidai ndio wakali kuzidi wengine ,mizozo ya hapa na pale ikazidi kujitokeza.
Hali hiyo ya Utata ikaleta chuki na dharau, ndipo mgawanyiko ukatokea.
FERRE GOLA na BILL CLINTON wakawa pande mmoja, huku JUS D’ÉTÉ MULOPWE na salio la Group pande zao.
FERRE GOLA na BILL CLINTON wakachukua uamuzi wa kurudi mjini KINSHASA kujifiriria na kupata ushauri ili wajiendeleze kimuziki, Kwa upande wake JUS D’ÉTÉ kaamua kubaki PARIS na kujichukulia kama kiongozi pekee wa Group LES MARQUIS DE MAISON MÈRE.

MJINI KINSHASA MAELEWANO KATI YA BILL CLINTON NA FERRE GOLA YAKATOWEKA.
Wa kwanza kuchukua ndege na kurudi KINSHASA alika BILL CLINTON, katua kwenye uwanja wa ndege wa NDJILI tarehe 15 February 2005, siku nne baadae yaani tarehe 19 February 2005 FERRE GOLA naye katua MJINI KINSHASA. Huku Mashabiki wakisubiria kuwaona pamoja kwenye Press conference, FERRE GOLA kapata tetesi ya kwamba BILL CLINTON hatokuja kushirikiana naye kwenye Press conference ,na tayari ameshakua na kundi lake na kalipa jina la ” LES MARQUIS SAMOURAÏS”. FERRE GOLA kwa upande wake, kalizimika kuunda kwa haraka kundi lake kalipa jina la “ MARQUIS DES BEAUX – GARÇONS “.

MKONGWE KOFFI OLOMIDE KAINGIA UWANJANI :
KOFFI OLOMIDE LE GRAND MOPAO kamtaka kwa hali na mali FERRE GOLA ili ajiunge na Group lake la QUARTIER LATIN. Kafanya juu chini kwa kuwarubuni ndugu wa karibu wa FERRE GOLA ili wamshawishi ajiunge naye,na hajafaanikiwa. Basi ikabidi amtafute Jamaa wa karibu sana na FERRE GOLA ambae FERRE GOLA hua kampa heshima zote, Jamaa anaishi barani Ulaya, Jina lake JÉRÔME MONTIGIA, huyu ndie kafaanikisha ujio au uhamisho wa FERRE GOLA kujiunga na Group QUARTIER LATIN ya MOPAO MOKONZI. Ndipo FERRE GOLA kafanyiwa mkataba maalum, na baadhi ya vipengele vya mkataba huo ni kwamba FERRE GOLA atapeya DOLA elfu 15000, na mkataba ni waku renew kila baada ya mwaka mmoja, kwa makubaliano ya pande zote mbili.

KOFFI AMKABIDHI FERRE 15,000 USD

Kitendo cha KOFFI OLOMIDE kumkabidhi FERRE GOLA kitita cha DOLA elfu 15000, kilileta gumzo kubwa hasa kwenye vyombo vya habari, kwa sababu ni jambo ambalo halijawahi kutokea. Ndipo walivyo weka kwenye vichwa vya habari (LE TRANSFERT LE PLUS CHER (THE MOST EXPENSIVE TRANSFER ).

WAPAMBE WA WERRASON WAJA JUU :
Kitendo alicho kifanya KOFFI OLOMIDE kumchukua FERRE GOLA,kiliwaudhi saana wapambe,wapenzi na watu wa karibu wa WERRASON. Kwa madai yao, wanasema ya kwamba, KOFFI OLOMIDE ndie aliye washawishi kina FERRE GOLA, BILL CLINTON, JUS D’ÉTÉ, SERGE MABIALA, JAPONAIS na kadhalika watoroke na waunde Group LES MARQUIS DE MAISON MÈRE. Nia yake halisi ni kumdhuru na kumuathiri WERRASON aumie na aanguke kimuziki, kwa hali hiyo hatokua na mpinzani.

MJINI PARIS, Waliandamana hadi kwenda kwenye nyumba ya KOFFI OLOMIDE huku wakitoa matusi makali dhidi yake. kwa bahati nzuri hapaja tokea madhara yeyote.
Kwa upande wake KOFFI OLOMIDE kajitetea kwa kusema hana jambo lolote na WERRASON ambae kamchukulia kama Ndugu, na wala hajamchukua FERRE GOLA kutoka kwa WERRASON bali kwenye Group LES MARQUIS DE MAISON MÈRE.

AJIRA YA FERRE GOLA KWA KOFFI OLOMIDE MOPAO MOKONZI
mwishoni mwa mwaka 2005, FERRE GOLA kajumuika na KOFFI OLOMIDE na kundi lake kwenye SHOO nyingi Mjini KINSHASA, ULAYA, na sehemu mbalimbali ulimwenguni. FERRE GOLA akiungana na Group QUARTIER LATIN, wakaingia STUDIO na kutoa SINGLE ” BOMA NGAI NA ELENGI ” (BONA NGA N’ELENGI). Uhondo na utamu utaupata utakapo sikiliza marudio ya wimbo “SISI SILIVI” usikilize hapo chini.
Baada ya hapo, FERRE GOLA katia kwenye ALBUM DANGER DE MORT wimbo wake maarufu INSECTICIDE.

 

MZOZO WAJITOKEZA KATI YA FERRE GOLA NA KOFFI OLOMIDE
Tukiwa tayari Mwaka 2006, maelewano kati ya FERRE GOLA na tajiri wake KOFFI OLOMIDE yakawa sio mazuri. FERRE GOLA akawa anagoma kufika mazoezini, hadi kufikia kutotokea kabisa kwenye SHOO zilizo fanywa kwenye ukumbi wa BATACLAN na ELYSÉE MONTMARTRE MJINI PARIS.
Kitendo hicho hakijamfurahisha KOFFI OLOMIDE, akawatuma wajumbe wamshauri kijana ili apate kujirekebesha na aendelee na muziki.
Tarehe 07 AUGUST 2006, KOFFI OLOMIDE na kundi lake walikua MJINI BRUSSELS (BRUXELLES) kwa ajili ya SHOO kwenye ukumbi wa MARIGNAN, huko pia FERRE GOLA hajaonekana huku akitoa sababu ya kwamba anaumwa. Sawa sababu inaeleweka, ila kwa mshangao Mkubwa kesho yake kaonekana kwenye sehemu maarufu MJINI BRUSSELS inayoitwa ATOMIUM akiimba kwenye KERMESSE iliyo andaliwa na wa KONGOMANI waishio hapo.

Subira za KOFFI OLOMIDE ziliisha, ndipo kamtafuta jamaa JÉRÔME MUTINGIA, alie faanikisha ujio wa FERRE GOLA QUARTIER LANTIN ili aingilie kati kwa kumshawishi FERRE GOLA atekeleze mkataba walio saini kati yao.
KWA NINI FERRE GOLA KASUSA KUFANYA MAZOEZI ? ITAENDELEA…

 


Koffi akanusha kumhujumu Mpiana onyesho la Zenith

January 28, 2014

Mwanamuziki Koffi Olomide ambaye kwa siku za karibuni urafiki wake na JB Mpiana uliwashangaza watu kadri ulivyokolea, amekanusha kuhusika na hujuma ya kufutwa kwa onyesho la JB Mpiana ambalo lilipangwa kufanyika Zenith mwaka jana.

Koffi aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba wa kufanya show mboli mjini Brazavile mwisho wa mwezi huu na mwanzoni mwa mwezi ujao. Koffi amesema anasikitishwa na habari zinazovumishwa kuwa ameshiriki katika kuwachochea “wanazi” wa JB wafanye fujo kupinga show hiyo isifanyike “Hizo ni habari za uvumi na zinafaa kupuuzwa na wapenzi wa muziki wetu, sina sababu ya kufanya hivyo kwa sababu sifaidiki na chochote kwani mimi nina mashabiki wangu na yeye ana wakwake” alisema Koffi akionyeshwa kukerwa na swali hilo. Koffi aliripotiwa na vyombo vya habari kuwa amekuwa na ukaribu na JB Mpiana siku za karibuni jambo ambalo liliwashangaza watu.

Koffi atafanya onyesho lakwanza la VIP January 31 katika ukumbi wa Olympic Palace huko Brazaville ya Congo na siku ya tarehe 1 Feb atafanya onyesho jingine la wazi akiwa na Honorable Cindy le Cœur na bendi nzima ya Quartier Latin International pia atamtambulisha muimbaji mpya ambaye ameshiriki pia kwenye albamu mpya ya kundi hilo ya 13 ème apôtre


Ziara ya Celeo Scram North Kivu yaonyesha ukali wake.

January 15, 2014

Kwa Tanzania hueda jina Celeo Scram ni geni ila kwa wanaofatilia muziki wa Congo hasa historia ya WMMM jina hili si geni kabisa kwani huyu dogo ambaye aliwahi kuwa atalaku wa WMMM kwa sasa anafanya kazi kivyake na anafanya vizuri sana.

Celeo yuko kwenye ziara ya kutembelea jimbo la Kivu huko Kaskazini mwa DRC na ilianzia mji wa Kasindi ambao unapakana na Uganda, Siku ya Jumamosi mwanamuziki huyo anayependwa zaidi na vijana aliwapa burudani mashabiki lukuki ambao walifurika kumuona, kulikuwa na shamrashamra nyingi ambapo shabiki mmoja Papa Vambé aliwaalika mashabiki wa mwanamuziki huyu kujumuika naye kwenye nyama choma iliyoambatana na vileo katika himaya yake, ziara hii itampelekea kwenye miji kadhaa jimboni humo na itamalizika weekend hii, Celeo kwa sasa anatamba na albamu yake mpya inayojulikana kama Ici c’est Paris


Fally; “Ilikuwa hofu zaidi ya maumivu”

January 15, 2014

Mwanamuziki Fally De Cap amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki tangu alipopata ajali na kusema kuwa kimwili hakupata madhara makubwa sana ila hofu na msongo wa mawazo wa ajali ile ndio uliomsumbua zaidi ya maumivu kidogo aliyoyapata. “Nawashukuru kwa meseji zenu na kuniombea nipone haraka, ni mapenzi makubwa ambayo yamenifanya nipone haraka” alisema Fally kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Fally alipata ajali akitokea kwenye matembezi huko Kinshasa DRC katika barabara ya uhuru, ajali iliyohusisha magari mawili na gari la pili ndio lilikuwa na majeruhi zaidi ukilinganisha na la mwanamuziki huyo. “…Kwa sasa naendelea vizuri na Daktari wangu amenipa mapumziko mafupi ila nitarejea kwa kishindo” alosema Fally.


HISTORIA YA MWANAMUZIKI FERRE GOLA SEHEMU YA PILI

January 15, 2014

Na Lubonji wa Lubonji

Baada ya Wiki iliyopita kuona ni jinsi gani Ferre aliingia Wenge na kwa taarifa tu nikukumbushe kuwa Ferre ndio alikuwa kijana wa mwisho kuwa recruited ndani ya Wenge Musica kabla haijapanguka, kisha tukaona alivyokwenda kwa WMMM ya Werasson ambako aliondoka baada ya miaka saba na kuanzisha ya kwake….. Je nini kinaendelea?? Ungana na Lubonji kujua zaidi….!!

Ujuzi wake wa Muziki, ukuaji wa kipaji chake ulistajabisha wengi, Jina la FERRE GOLA sio la kutambulishwa tena, Ndipo yalipoaanza majungu ili wampokonye kijana huyu kwa WERRASON,kwa kutumia mbinu mbalimbali.
Wakaanza kumtumia wajumbe kwa madhumuni ya kumshawishi aungane nao huku wakimpa ahadi kemkem… watafaanikiwa kweli? Jibu tutaliona hapo baadae.
Tunapata fursa hii kwa kukumbusha ya kwamba FERRE GOLA ndie Mtunzi wa wimbo maarufu Victime D’Amour unao patikana kwenye Album ya WENGE MUSICA MAISON MÈRE inayoitwa A LA QUEUE LEU LEU iliotolewa mwaka 2002, kadhalika na wimbo Chetani (Shetani) kwenye Album hiyohiyo na nikutokana na wimbo huo wa Chetani (Shetani) ndipo walipoanza kumpachika jina la Chetani (Shetani), Sikilizeni huo wimbo Mmusikie FERRE GOLA CHAIR DE POULE (SHETANI) anavyo onyesha umahiri wake wa uuimbaji.

KUUNDWA KWA GROUP LES MARQUIS DE MAISON MÈRE
Baada ya kupata sifa nyingi na tunzo nyingi ikiwa ya mwimbaji bora akiwa pamoja na WERRASON, Bila kusahau kuzungumzia kujiondoa kwa DIDIER MASELA (LE FONDATEUR) ambae huchukuliwa kuwa muanzilishi wa WENGE MUSICA BCBG,Pia kujiondoa kwa ADOLPH DOMINGUEZ ambae kaenda kuunda kundi lake la WENGE TONYA TONYA,FERRE GOLA kachukua naye uamuzi wa kujiondoa WENGE MUSICA MAISON MÈRE mwaka 2004.

Mwaka huo 2004 wakiwa dhiarani barani Ulaya (Mjini London),FERRE GOLA CHAIR DE POULE kawahamasisha wenzie kina DIDIER KALONDJI (BILL CLITON), JUS D’ÉTÉ MULOPWE, SERGE MABIALA, JAPONAIS MALADI,PICASS MBAYO, na MIMICHE BASS watoroke na kujiondoa kwenye Group WENGE MUSICA MM,kwa madai kwamba wanavyo vipaji vyakujiendeleza wenyewe kimuziki,pia kuna wadhamini ambao wako tayari kuwasaidia. na ndivyo walivyo unda Group LES MARQUIS DE MAISON MÈRE.

Kitendo cha FERRE GOLA kujiondoa WENGE MUSICA MAISON MÈRE,kilileta Gumzo kubwa kwenye Miji ya Kinshasa, Brazzaville, Brussels na hasa PARIS sehemu ambayo FERRE GOLA na Wenzie waliweka maskani yao. Kwakweli WERRASON alitokea kumpenda saana kijana FERRE GOLA,na kuondoka kwake kulimfanya WERRA asikitike Mnoo,na Group nzima iliathirika kwa kiwango flan,kwa kuwa FERRE GOLA ndiye kwa wakati huo kiongozi wa Group, ukizingatia pia NI MWANAMUZIKI NYOTA. Kwa upande wa wapenzi wa WENGE MUSICA MAISON MÈRE walikua wenye hasira sana dhidi ya FERRE GOLA kujiondoa,wanasema kamkashifu na kukosa fadhila kwa yule aliemtoa ushamba (WERRASON)

Wakiongonzwa na Mpambe N°1 wa WERRASON, SANKARA DENKUTA ambe kamtukana FERRE GOLA matusi ya nguoni, katoa maneno makali na ya khebehi ilhali yamuumize na kumdhalilisha FERRE GOLA.
Hali hii ya Udhalilishaji adharani ulifanya Mama Mzazi wa FERRE GOLA atoe machozi na kulia, alipokua akihojiwa na mwandishi wa habari ambae kwa sasa ni Mbunge huko CONGO, Mheshimiwa ZACHARIE BABABASWE, Mama huyo kasema namnukuu :(Namshukuru WERRASON kwa sababu kuwepo kwa mwanagu pembeni yake kumemfanya ajiendeleze kisanaa na kimapato pia, Mbona hajaniita ili tuliongelee swala la FERRE GOLA kujitoa kifamilia? namuomba WERRASON kwa mara nyingine aingilie kati na kuwakataza akina SANKARA DENKUTA waache kumkashifu na kumtukana FERRE, laa sivyo kitakacho wafikia watakiona wenyewe…)

UZINDUZI WA GROUP LES MARQUIS DE MAISON MÈRE
Nakumbuka SHOO yao ya kwanza ilikua Jumamosi tarehe 07-08-2004 kwenye Ukumbi wa LSC de PARIS,unao patikana sehemu inaitwa SAINT DENIS. Shoo ilianza rasmi Saa 02H45′ Hadi Saa 07H00′ Asbuhi…
FERRE GOLA CHAIR DE POULE, DIDIER KALONDJI BILL CLINTON, JUS D’ÉTÉ MULOPWE, JAPONAIS, SERGE MABILA, DJO LAKIS… WALIWASHA MOTO!!! SHOO ILIKUA NZURI SANA. Palikua hakuna sehemu pakushikilia kwakuona Ukumbi ulivyo Jaa watu. Vijana walishangaza wengi kwa ginsi walivyo kaa imara jukwaani,Ingawa watu wengi walienda kwenye SHOO kwa hali ya Udadisi kushuhudia kama hawa Jamaa wanao uwezo wa kufanya Kweli au Laa!!! Ukumbe wote ulisimama na watu kushangilia kwa shangwe alipo tokea FERRE GOLA CHAIR DE POULE na kuimba wimbo VITA IMANA kwa sauti nyororo ambayo yaweza kumtoa Nyoka ukingoni…
WAKONGOMANI wenyewe wanasema SHOO EZALAKI TRÈS BIEN MPE MUSIQUE EVANDA!!! maana yake (SHOO ILIKUA NZURI SANA NA MUZIKI WA UHAKIKA NA WENYE KUTULIA)… Itaendelea..


Fally Ipupa apata ajali

January 9, 2014

Habari zilizotufikia asubuhi hii zinasema kuwa Mwanamuziki Fally Ipupa amenusurika kifo baada ya gari lake aliyokuwa akiendesha aina ya  Bentley kupata ajali kwa kugongana na gari jingine huko Boulevard Barabara ya uhuru almaarufu kama 30 Juin huko Congo DRC.

Habari zinasema kuwa hakuna aliyepoteza maisha kwenye ajali hiyo iliyohusisha magari mawili ila abiria wamejeruhiwa akiwamo mwanadada aliyekuwa ndani ya gari ya Fally na kukimbizwa hospitali ya Ngaliema Falvien. Awali habari zilitapaa kuwa Fally amekimbizwa hospitalini hapo na kufanya watu kadhaa kufurika lakini ikathibitishwa na mashuhuda kuwa Mwanamuziki huyo kipenzi cha wengi yu buheri wa afya isipokuwa majeraha aliyopata mkononi mwake ambao awali ulisadikiwa kuwa umevunjika.

Spoti Starehe inawatakia wapone haraka na kurejea kwenye burudani.

jyk9bW1389213892

Wasamaria wema wakiwa eneo la ajali na kuwasaidia majeruhi.

JzyJhm1389213849

Sehemu ya gari ambayo Fally aligongana nalo usiku wa kuamkia leo.

kzCLPV1389213782

Mwanamama ambaye alikuwa kwenye gari iliyogongana na gari ya Fally akiwa kwenye gari ya wasamalia wema kukimbizwa Hospitalini.

GqQFFb1389212400

Gari ya Fally Ipupa aina ya Bentley ambayo ilipata ajali usiku wa leo huko Congo.

ciPbjw1389212507

Gari ya Fally aliyokuwa akiendesha mwenyewe ikiwa imefunguka Airbags baada ya ajali ya usiku wa leo.


HISTORIA YA MWANAMUZIKI FERRÉ GOLA.

January 6, 2014

Na Lubonji wa Lubonji.

SEHEMU YA KWANZA.

https://i2.wp.com/www.baziks.net/news/FERRE-GOLA-LES-TRAVAUX.jpg

FERRÉ GOLA kwa jina lake kamili HERVÉ GOLA BATARINGE,ni MTUNZI,MUIMBAJI,DANCER yaani MWANAMUZIKI kamili kutoka CONGO.

FERRÉ GOLA,kazaliwa mjini KINSHASA, tarehe 03-03-1976.

Akiwa passionate wa nguvu kwa fani ya muziki tokea bado mdogo, FERRÉ GOLA, pindi atokapo Shule, alikua akienda kujishughulisha na mazoezi ya Muziki, kwa kua madhumuni yake nikua mwanamuziki mkubwa na mwenye jina.

Ndoto yake ya kuwa Mwanamuziki yaanza kukamilika mwaka 1995 wakati wa sherehe za kermesse huko KINSHASA sehemu inayoitwa BANDALUNGWA ama BANDAL.

FERRÉ GOLA kaletwa na kutambulishwa ndani ya Group WENGÉ MUSICA BCBG na WERRASON NGIAMA,ikumbukwe ya kwamba ni WERRASON ndie kamleta pia ALAIN MPELASI (MPELA).

FERRÉ GOLA,alikua kijana mdogo na wa mwisho kutokana na Umri wake kukubaliwa ajiunge na WENGÉ MUSICA BCBG kabla ya mgawanyiko, pamoja na kijana mwengine SEGUIN MANIATA ambae yeye alikua Drumeur-Percussionist.

Baada ya Mgawanyiko wa WENGÉ MUSICA BCBG, HERVÉ GOLA ambae kwa sasa hujulikana kwa jina la “FERRÉ CHAIR DE POULE” Jina alilopachikwa na ADOLPH DOMINGUEZ kwa mujibu wake mwenyewe, FERRÉ GOLA CHAIR DE POULE yeye kaamua kuambatana na WERRASON kwenye Group WENGÉ MUSICA MAISON MÈRE huku JB MPIANA MUKULU akawa na Group lake la WENGÉ MUSICA LES ANGES ADORABLES.

FERRÉ GOLA, kakaa pamoja na WERRASON kwa kipindi takribani miaka 7 (1997-2004) Hadi kapewa cheo cha kiongozi wa Group WENGÉ MUSICA MAISON MÈRE kwenye miaka ya 2000, ikiwa baada ya kujiudhulu kwa Mpiga GITA machachari CHRISTIAN MWEPU ambae kachangia kwa kiasi kikubwa kwenye ALBUM yao ya SOLOLA BIEN.

Kwenye Album hiyo SOLOLA BIEN, Mtaukuta Wimbo mzuri sana wa VITA IMANA (hapo chini) ukiwa utunzi na uimbaji wa FERRÉ GOLA mwenyewe.

FERRÉ GOLA kajiondoa kwenye Group WENGÉ MUSICA MAISON MÈRE mwaka 2004, na kuunda group nyingine LES MARQUIS DE MAISON MÈRE,akiwa pamoja na BILL CLITON KALONDJI, JUS D’ÉTÉ MULOPWE, SERGE MABIALA, JAPONAIS, PICASS MBAYO na MIMICHE BASS.

Itaendelea.


%d bloggers like this: