Malizia weekend yako na Kibao Rangi ya Chungwa unakikumbuka?

May 31, 2009

Najua weekend ndio imekwisha tena na tunajiandaa kuingia maofisini kesho malawira, Naomba nikumburudishe na Kibao Rangi ya Chungwa toka kwao wana Kilimanjaro Connections Band. Kaka Beny Wisa upoo? Mukulu Kiiza, Le Suveree Maghambo, Mukubwa Baty na Six bila kumsahau Suveree Ling;ande, mnanini bwana. pateni burudani unilelee mwanangu Juma na Dula. hehehehe


Tyson afiwa na mwanaye!!

May 31, 2009

miketyson_wideweb__430x284 Mtoto wa bingwa wa zamani wa masumbwi Mike Tyson amefariki hospitalini baada ya kuanguka na kuburuzwa na mkanda wa mashine ya kufanyia mazoezi(Treadmill) iliyomo kwenye chumba chake cha kufanyia mazoezi nyumbani kwao Phoenix huko Marekani tarehe 26 May 2009.

mike-tysondaughter1

Awali mtoto Exodus alikutwa na kaka yake mwenye miaka 7 akiwa amebanwa shingo na mkanda kwenye mashine hiyo ndipo alipokimbizwa hospital lakini alifariki siku moja baadaye.


Feisal Ismail na Baby Madaha wazindua kwa shangwe!!

May 31, 2009

. Wanamuziki Feisal Ismail na mwenzake Baby Madaha majuzi wamezindua albamu zai chini ya Kampuni ya Pilipili Entertainments.

Katika uzinduzi huo ambao ulifanya kwa aina yake na kuhudhuriwa na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara mama Marry Nagu, pia Ritah Paulsen  alikuwepo Mkurugenzi wa kampuni ya Bench Mark Production waandaaji wa Bongo Star Search ambao  msanii Feisal aliibuliwa huko.

Baby Madaha akithibitisha ubora wake jukwaani wakati wa Uzinduzi wa Video yake, Picha na Full Shangwe.

 DSC02081 [800x600] Kutoka kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika, Mwanamuziki Feisal Ismail maadam Ritah Paulsen Mkurugenzi wa Benchimark Production kampuni, ambayo pia inaandaa Bongo Star Search na Waziri wa Viwanda na Biashara mama Marry Nagu wakiwa katika picha ya pamoja, Feisal aliibuliwa na Bongo Star Search mpaka hapo alipofikia katika mafanikio yake.


Illuminata aulamba u Miss Universal

May 31, 2009

064vv

iluminata james usiku wa kuamkia leo ametangazwa kuwa mshindi wa miss universe tz 2009, baada ya kuwabwaga wenzake kadhaa kwenye mtanange ambao ulikuwa na burudani lukuki.

Mashindano hayo ambayo yalifanyika katika ukumbi mpya wa Mlimani City Hall na kuhudhuria na mamia ya wapenzi wa burudani hasa sanaa ya urembo. Wanamuziki kadhaa walitumbuiza ikiwepo pamoja na AY, Wahuu toka nchini Kenya ambaye alibamba vilivyo, Diamond Musica ambao walimwaga Sebene la kufa mtu pamoja na kikundi machachari cha Ngoma cha Albino na kuufanya usiku huo kuwa wa aina yake.

Mbali na Illuminata mshindi wa pili ni evelyn almasi na hidaya maeda ambaye ni mshindi wa tatu.

SANY1716

Tano bora ya mtanange huo, Picha zote na Muhidini Issa Michuzi, habari na Robert William Mwafrica aka Mwafirombe.


Caouany nyota mpya kwenye ulimwengu wa Ubunifu

May 31, 2009

 G and Ritha [800x600] Mkurugenzi na Mbunifu wa mavazi kutoka kampuni ya Carpuany and Design Mamaa Grace Sinamwita kulia akipozi katika picha na Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Ritah Paulsen wakati wa uzinduzi wa kampuni ya Pilipili Entertainment uliofanyika jana sambamba na uzinduzi wa Video mbili za wanamuziki Baby Madaha na Faisal Ismail kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski. Capuany alikuwa Class mate wangu High School, hongera sana dadaa.


Queen Suzy avishwa pete ya Uchumba!!

May 29, 2009

DSC02238

Mnenguaji wa FM Academia Queen Suzy ambaye kwa sasa yuko Malaysia ziarani na Bendi ya The Kilimanjaro Connections amepata mchumba ambaye anatarajia kufunga naye ndoa baadaye mwaka huu. Suzy ambaye amevalishwa pete ya uchumba na Mchumba wake huyo raia wa Uingereza anayeishi na kufanya kazi nchini Malaysia.

DSC02239

Awali Queen Suzy alivalishwa pete hiyo kwenye sherehe ndogo iliyofanyika kwenye Jengo la KLCC na kuhudhuriwa na baadhi ya Wanamuziki na marafiki wa karibu wa pande zote.

Suzy anatarajia kurejea nyumbani baadaye mwezi ujao baada ya mkataba wao kumalizia na amesema mchumba wake pia anatarajia kwenda Tanzania mwezi July ambapo taratibu nyingine zitafuatwa.

Suzy ambaye yuko Malaysia tangu mwezi wa december mwaka jana akiambatana na wana mkorogo, pia amepiga mafanikio kwenye sekta nzima ya muziki kwani kwa sasa pamoja na kucheza pia ameanza kuimba chini ya gwiji muimbaji mkufunzi Delphinus Mununga (mdogo wa marehemu Kasheba), “kwakweli nafurahi mafanikio yangu kimuziki ningependelea kuimba zaidi kwani sasa nakiona kipaji changu cha muziki” alisema Suzy alipokuwa akiongea nami katika kiota chao cha Rum Jungle.

DSC02147

Queen Suzy akiwa na mpenzi wake kisiwani Lang’kawi-Malaysia.

DSC02139


Akamatwa na Polisi kwa kushinda Bahati nasibu ya Man U na Barcelona.

May 28, 2009

handcuff Mtu mmoja mwenye asili ya kimalay amekamatwa na polisi leo asubuhi baada ya kushinda bahati nasibu ya mpira kwa kutabiri matokeo kati ya Manchester United na Barcelona ambapo Barcelona waliibuka kidedea.

Mtu huyo ambaye jina lake halijatajwa amekamatwa leo asubuhi majira ya saa tatu kutokana na Kucheza bahati nasibu ambayo hairuhusiwi kwa Wamalay sheria ambayo imo kwenye dini ya Kiislamu ambayo Serikali ya Malaysia inaifata.

Kwa mujibu wa mashuhuda jamaa huyo alishinda gari aina ya Myvi yenye thamani ya Malysia Ringit 47,000 sawa na dola 13000 za kimarekani. Inasemekana mtu huyo alipinga na mwenzake katika klabu moja maarufu kwa kuangalia mpira maeneo ya kati ya jiji la Kuala Lumpur.

Kwa mujibu wa sheria ya Malaysia, jamii ya Wamalay waislamu (Bumi Putra) hawaruhusiwi kucheza aina yeyote ya michezo ya kubahatisha. Malaysia inajamii ya aina tatu, Wamalay walio wengi, Wachina na Wahindi.


%d bloggers like this: