Ronaldinho huyoo AC Milan

July 16, 2008
.

.

Picha hii iliyotolewa leo na AC Milan ikimuonyesha Ronaldinho, akiwa na Mkurugenzi wa michezo wa AC Milan Adriano Galliani mara baada ya kumalizika kwa kikao chao leo hii July 16, 2008. Ronaldinho kuhusu uhamisho wake (soma post ya chini kwa habari zaidi), Leo hii Ronaldinho atakwenda Italy kupima Afya na kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya Serie A, Hii ni kuhitimisha jitihada za klabu nyingine ya Manchester City ambayo ilitoa donge la Dola Milioni 50 kumnyakua Ronaldinho, lakini habari za ndani zinasema Ronaldinho alipenda zaidi kwenda AC Milan kuliko kucheza Uingereza. (AP Photo/Manu Fernandez)


AC Milan yamnyakua Ronaldinho

July 16, 2008
Ronaldino Gaucho

Ronaldino Gaucho

Serie Siku moja baada ya klabu ya Rais wa Barcelona kutangaza ofa waliopewa na klabu ya Man City, Klabu ya AC Milan ya Italy imetanaza kushinda kinang’anyiro cha kumsajili mchezaji huyo machachari toka Brazil jana jumanne katika mkataba wa miaka mitatu.

Ingawa habari za fngu lililotumika kumnyakua mchezaji huyo hazijawekwa bayana na AC Milan akini mazungumzo baina yao yalikwenda vizuri.

Gazeti moja la Uitaliano la Gazzetta dello Sport limesema kuwa Milan wametoa ada ya uhamisho kati ya Dola milioni 30 na itamlipa Ronaldinho Dola milioni 10.4 kwa kila msimu kwa muda wa miaka yote mitatu.

Milan walitangaza kwenye tovuti yao jana baada ya siku nzima ya majadiliano kati ya Raisi wa Barcelona Joan Adriano Galliani mazungumzo yaliyofanyika mjini Catalan.

Ronaldinh atakwenda leo jumatano kwa ajili ya kuangalia afya (medical checkup) na wanategemea atajiunga na Timu hiyo mara baada ya kumalizika kuwakilisha Nchi yake kwenye michezo ya Olympic mwaka huu lakini atakwenda kwenye mazoezi ya AC Milani mara baada ya kumalizika kwa vipimo ilisema taarifa hiyo.


Ronaldinho: Bye bye Barcelona

July 15, 2008

Mchezaji wa Barcelona Ronaldinho akiingia kwenye gari yake mara baada ya kikao na viongozi wa Klabu yake ya Barcelona hapo jana 14 July, 2008, Rais wa klaby ya Barcelona Joan Laporta amesema wamepokea ofa ya Euro 32 million (sawa na Dola 51 million) toka klabu ya Manchester City kwa ajili ya kumuachia mchezaji huyu ambaye alipata kuwa mchezaji bora wa Dunia kwa miaka miwili said. AFP PHOTO / JOSEP LAGO (Photo credit should read JOSEP LAGO/AFP/Getty Images)


%d bloggers like this: