Mr Paul na The Okapi Guitars

June 30, 2012

Mr Paul akiwa na wanamuziki wa The Okapi Guitars hivi karibuni, Story zaidi inakuja….!!!


JB Mpiana na Werasson “macho kwa uso” kwenye msiba wa Mcheza show wa Wenge BCBG Monica Celes

June 27, 2012

IMG-20120627-WA000

Werasson Ngiama Makanda wa Wenge Musica Maison Merre akiwa na Papaa JB Mpiana wakijadili na kufatilia jambo kwenye msiba wa Mcheza Show mahiri wa Wenge Musica Monica Celes aliyefariki wiki iliyopita. Monica atakumbukwa kama mcheza show na kiongozi wa wanadada ambaye JB Mpiana alimpa kazi ya kumlea Mwana Nchuka, kale katoto kalikojiunga na Wenge kakiwa kadogo sana mpaka sasa amekuwa mdada.

Habari zinasema watu walilipuka kwa mayowe alipoingia Werasson msibani na wapambe wake na alijumuika na waombolezaji na kushiriki mpaka mwisho.

JB alimlilia sana Monica kwani ni mmoja ya wakongwe katika bendi ya Wenge Musica.

Shukrani za kipekee kwako Papaa Julie Weston Le Carismatique Le Presidaa Bana Congolee na Darisalaaam.

Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya marehemu – Amen.


Ferre, King Kester,Jb Mpiana

June 25, 2012

Ferre Gola live on stage akiwaenzi kaka zake kwa kuimba nyimbo zao. Hebu tumtazame na kumsikiliza akimpa shavu rais Jb Mpiana ambae yeye mwenyewe mpaka kesho anamtambua kama ndio alikua rais na kiongozi halali wa wenge musica bcbg 4×4 tout terrain.


Koffi na Mkewe Aliyah walipoonyesha jumba lao la kifahari

June 22, 2012

image

Mwanamuziki Koffi Olomide alitambulisha jumba lake kwenye sherehe ya ufunguzi wa jumba hilo ambalo limegharimu mamilioni ya shilingi na kunakshiwa kwa samani za bei ghali.

Mashabiki walipokea kwa hisia tofauti kitendo cha Mwanamuziki Koffi Olomide kuweka wazi Jumba lake la kifahari huku wengine wakimpongeza na wengine wakimwambia kitendo hicho ni kama dhihaka kwa wacongoman ambao wengi wao wanaishi kwenye dhiki kali huku weingine wakiwa wanataabika kupata mlo wao lakini wanajitolea kuchanga kununua kazi zake au kuingia kwa show zake.

Kiukweli ni jumba la kifahari sana na alialika watu mashahuri kwenye sherehe hii ambayo ilitumia pesa nyingi.

Jumba hili limejengwa kwenye vilima vya Fleury almaarufu kama a mont-fleury eneo maarufu kama Msaki ambapo watu wenye pesa ndio wanaishi huko. Koffi ni mmoja wa wanamuziki wakubwa si tu kwa Congo bali Afrika nzima ambaye kiukweli amekuwa na mafanikio makubwa tangu aanze muziki na amejizolea mashabiki wengi kote Ulimwenguni kutokana na muziki wake.

Kila la heri Mopao Mokonzi.


Werrason kwa Sebene Balaaa

June 22, 2012

Kiukweli nimesema na nitasema kila siku amkubali sana Werrason kwa sebene yuko makini na hasa baada ya kurejea kijana wake wa Solo Japonaise ambaye binafsi namkubali sana najua atakuwa balaa, hebu angalia hii show ya mwezi MArchi mwaka huu kisha nipe maoni yako.


Superstar Premier

June 20, 2012


Buriani Baba Kruvet.

June 18, 2012

Willy Edward 1974 – 2012

Nilipokea taarifa za msiba wa Willy Edward kwa masikitiko makubwa toka kwa Michuzi akiwa ameandika kwenye status yake ya facebook. Nilishtuka kwa vile Willy ni mtu si tu ninayefahamiana naye bali niliwahi kufanya naye kazi ofisi moja pale Business Times – Majira. Enzi hizo mi nikiwa head wa Production Department ya Matangazo ya Business Times, Majira, Maisha, Dar Leo, Sanifu na Spoti Starehe.

Willy Edward alifariki dunia Ghafla usiku wa kuamkia Jumamosi huko Morogoro, Hadi sasa hatujapata taarifa rasmi za kidaktari kuhusu kifo chake, lakini taarifa zilizopatikana kutoka kwa ndugu wa marehemu zinasema alikuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo.

Wakati huo nikiwa nikiwa Business Times, Willy tulikuwa wote tunasimamamia production ya Gazeti kuhakikisha kila kitu kiko sawa nakisha tunapeleka kurasa za gazeti wote kiwandani kwenye Printing wakati ofisi zikiwa Mtaa wa Bibi Titi na Kiwanda kikiwa Lugoda, yeye ndiye alikuwa akipeleka na kusimamia kurasa za editorial na mimi nikisimamia kurasa za matangazo, ni mtu ammbaye nilikuwa nafanya naye kazi kwa karibu kwani sisi pekee ndio tulikuwa watu wa mwisho baada ya maandalizi yote lazima tupeleke Pages kiwandani ndipo tunarejeshwa makwetu, na bila page zake basi za kwangu haziendi pia bila zangu za kwake haziendi na gazeti halitoki pia. Mzunguko huu ulinifanya kuwa karibu naye sana kwani baada ya hapo tunapanda gari na yeye anaanza kushuka kisha sie wengine humo njiani mnacheka na kupiga soga sana.

Willy alikuwa mshabiki sana wa michezo hasa mpira wa miguu, kiasi mtoto wake alimuita Kruvert jina la mchezaji wa Uholanzi Patric Kruvert na mi kila mara nilikuwa nikimuona namuita Baba Kruvert na ye kuniita Papaa kwa sababu napenda sana Lingala na muziki wake.

Willy Alifanikiwa kuaminika na kutokana na uwezo wake kazini alipanda daraja na kuwa Mhariri wa gazeti la Dar Leo kuanzia mwaka 2002 hadi 2005.

Kipindi cha mwaka 2006 hadi 2007 alikuwa akitumikia nafasi ya Mhariri wa Msaidizi wa Michezo gazeti la Majira na baadaye 2006 hadi 2007 akawa Mhariri wa Michezo wa gazeti hilo. Kisha alipanda na kuhamia vyombo mbalimbali kabla ya 2010 kujiunga na Jambo Leo.

Baada ya pilikapilika za Busniness Times mi nilitoka kwenye magazeti lakini nikiwa bado na mahusiano ya karibu sana na Willy huku akiniandikia makala mbali mbali za huku ninakofanyia kazi na pia Willy alikuwa mshabiki mkubwa wa Bolingo hasa JB Mpiana na alikuwa shabiki mkubwa wa blogu hii ya Spoti na Starehe na hivi karibuni tulikuwa na mpango wa kunipa Half Page ambayo ningekuwa naandika kuhusu muziki wa Congo kwenye gazeti la Jambo Leo ambalo marehemu alikuwa akifanyia kazi, tumekuwa tukiliongea hili mara kwa mara mpaka layout ya page tumeishaijadili na tulichokuwa tunajadili cha mwisho kabla ya kuanza ni heading ya page yangu.

Hili kwangu ni pigo kwani napenda sana kuandika na yeye tulikuwa tunaelewana sana na kuna wakati tulikuwa tukiandika makala hizi za Muziki wa Kongo pamoja na yeye na Frank Sanga.

Mara ya mwisho nilikutana na Willy tukiwa Airport mi nikielekea Malaysia na yeye akielekea Uturuki, tuliongea sana mpaka tulipoaachana na kuendelea kuwasiliana pia. Willy ameondoka huku akianza kufikia ndoto ambayo waandishi wengi wanaitaka, akiwa Mhariri wa Gazeti ambalo lilikuwa linakuja juu kwa kasi na kujiimarisha sokoni na kwa wasomaji, Gazeti la Jambo Leo ambalo linaongozwa na timu ya waandishi wachapakazi vijana.

Ni dhahiri jumuiya ya waandishi wa Habari imempoteza kijana mchapakazi ambaye uweledi wake katika fani ungekuwa darasa tosha kwa yoso wanaokuja na kuchipukia kwenye tasnia hii ya Habari.

Habari zinasema Willy atasafirishwa kwenda kuzikwa kwao huko Musoma

mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya
Habari Afrika na Uturuki


Sultan De Brunei Kastiko ya Wenge BCBG

June 15, 2012

Wimbo: Sultan De Bruneil

Mtunzi: JB M’piana

Album: TH

Bendi: Wenge BCBG

Yela no nga bolingo nayo

Oyo ezali lokola mbuma

Elengi Oyo ezanga mokuwa

Lokola mbinzo oyo etonda

Saveur Le sultan de Bruneil

Ooh Kas Kaskito mobali ya

Malonga.

Unipe mapenzi yako laini kama tunda

tamu lisilo na mfupa kama jongoo

aliyezidishwa ladha jina lake Sultan

wa Brunei Kas Kaskito mwanamume

mtanashati

Mokolo Kaskito abengaki ngai

il faut omona presence ya Kaskin

teint d’ ebene, sourire eclatant na

ba frime mobali ya solo jeune homme

a` louer Aaah jeune homme elegant

Siku kaskito aliniita mara ya kwanza

muonekano wake ulikua wa pekee

rangi ya ngozi yake mti wa mpingo

tabasamu inayovutia pia

mwanamume mwenye maringo

Ba proposition nyonso basalaki ngai

pe ya sango oo peau elegant na

carisme ya ba amoureux ee

Maombi mapenzi niliyopewa na

na Kaskin Kaskito mobali ya tembe

Kaskin Kaskito mwanaume

mwenye sifa nyingi na mvuto wa

mapenzi.

Po ba professeur bayebisaki

Ngai soki mokolo abengi yo il

Faut otelema

IL faut oyoka nano, tango

Mosusu okotinda yo, il se

Peut ako kabela yo

Po mwana etinda akufaka

nzala te eloba bakulutu uu

Maman.

Walimu walinifahamisha kama

ukiitwa na mtu mzima inabidi

kusimama inatakiwa kumsikiliza

kwanza wakati mwingine anaweza

akakutuma au akakupa zawadi

kwamba mtoto anayekubali

kutumwa hawezi kufa njaa

mababu walisema.

Eeeh aaah toi c’est moi, moi

c’est ton remede d’amour (2x)

Eeeh aaah wewe ndio mimi, mimi

ndio dawa yako ya mapenzi

Chorus:

Ba banda bolingo batika

Miso etondaka te nakolula

eluli ye, iya olele

Eluli kaskito iya olele

Bolingo kwitikwiti imaole

Iya olele

Bolingo kwitikwiti imaole

Iya olele (2x)

Kwitikwiti kwitikwiti

Walioanza kupenda hawajachoka

Kolinga teo, iya olele

kupenda, iya olele

Macho hayachoki kupenda

yamechagua, iya olele

Yamemchagua Kaskito, iya olele

Mapenzi ni ulevi imaole iya olele

Mapenzi ni ulevi imaole iya olele

ulevi ulevi

Shai Ngenge

Que je me pende Lisette

Menga pour te prouver

que je t’aime

Wawa Mbula, Lucien Katanga

Hugue Mazomba

Que je me plonge dans le feu

Pour te prouver que je t’aime

Sabena Wanani, Didi Ongwari

Kijokolo

Nijiue Lisette Menga ili uamini ya

kama nakupenda

Wawa Mbula, Lucien Katanga

Hugue Mazomba

Nijitupe motoni ili uamini ya kama

nakupenda

Sabena Wanani, Didi Ongwari

Kijokolo

JB M’piana

Non non non non moi je t’aime

Oh Mimi Kas, Papy Kas I love you

Pusana pembeni nga natala kitoko

nayo

Papa leki Carly moi je t’aime oh seka

moke nga natala nzela ya mino nayo

aa aa aa aa koloba na moto te

RPT Chorus

kweli kweli mimi nakupenda

mimi Kas, Papy Kas nawapendeni

sogea karibu nione uzuri wako

Baba mdogo Carly mimi nakupenda

cheka kidogo nione mwanya

wako aa aa aa usimwambie mtu yeyote


Umaarufu unalevya wasanii.

June 14, 2012

“Its easy to be number one but its hard to maintain to be number one” nimeanza na msemo huu kwa vile wengi wa wasanii wakipata umaarufu wana tabia ya kujisahau. hili mara nyingi limekuwa likileta manung’uniko kwa si tu mashabiki bali hata watu wengineo ambao si washabiki wa sanaa zao.

Nachelea kusema kuwa wanakuwa wanalewa ama sifa ama vijisenti ambavyo wanakuwa wamevipata na kusau mashabiki ndio wamewafanya wawe na umaarufu walionao na si tu mashabiki bali vyombo vya habari ndio vimewafikisha hapo walipo.

Binafsi nimekerwa sana na kitendo cha mwanamuziki Dully Sykes kukosa adabu akiwa si tu studio bali akiwa Live kwenye kipindi ambacho mashabiki wake wengi wanamsikiliza. Ndani ya wiki moja msanii huyu ameweza mara mbili kukosa adabu tena kwenye radio moja hiyo hiyo.

Wiki iliyopita akiwa live kwenye kipindi cha XXL Dully Sykes alimjibu fyongo mtangazaji Adam Mchomvu wa kipindi hicho mwanzo nilidhani ilikuwa utani lakini Dully alisisitiza kuwa hawezi kuongea na mtu mchafu kama Adam Mchomvu, “siwezi kuongea na mtu mchafu kama wewe angalia mi nywele yako…. mi naongea na Boss wako biashara si mtu mchafu kama wewe” alisema Dully. Baada ya kuangalia kipindi kile kesho yake kupitia Nyuma ya Lensi kupitia Clouds TV nikaona jinsi ile ilivyomuumiza Adam Mchomvu na alivyokuwa akitulizwa asiendelee kujibishana na Dully kiasi alivua headphones na kukaa pembeni.

Kumbuka Dully alikuwa akifanya mahojiano juu ya wimbo wake mpya ambao ameutoa kwa kumshirikisha Mwana FA. Baaada ya Single hiyo inayokwenda kwa jina la Ameen kupigwa hewani watu wakaanza kusema kuwa Single hiyo imefanyiwa sampling kutoka kwenye wimbo mmoja wa huko Jamaica. Hii ilimpelekea Gossip Cop wa Clouds fm kuruka hewani na kumuuliza kwanza Mwana FA juu ya hiyo ambaye alikiri kwa kiasi fulani midundo imefanana lakini alisema ailizwe Dully Sykes ambaye naye baada ya kupigiwa badala ya kujibu alionyesha kukerwa na swali hilo inawezekana style ya kuulizia ya Gossip Cop lakini Dully alimjibu kuwa haongei na mashoga na kumuonya asipige tena. (Gonga hapa kusikiliza zaidi)

Kiuungwana kitendo kile si kizuri  na si cha kiungwana na si kwa Dully tu lazima ujue ngaz unayopandia ndio utakayoshukia, waliokupandisha ni pamoja na vyombo vya habari ukifanya mchezo ndio watakaokushusha.

Nimeandika haya kiroho safi, wala isieleweke vibaya. Pamoja sana.


Mjengo wa Wema

June 14, 2012

Wiki hii habari za mjengo wa Wema zimekuwa zikigonga vichwa vya magazeti maarufu ya kuandika vituko vya ma Star, hasa baada ya Wema kuonekana kwenye kipindi cha Take One cha Zamaradi Mketema kinachorushwa na Clouds Television. Kama ulimiss kipindi kile basi si mbaya ukajikumbusha hapa.


Watoto waangukiwa na nyaya za Umeme na kuujeruhiwa vibaya Asubuhi hii.

June 13, 2012

IMG-20120613-WA002

Watoto watatu ambao hawajatambuliwa majina yao wakiwa wamelala nyuma ya Pickup kwa ajili ya kupelekwa Hospitali baada ya kujeruhiwa na nyaya za umeme.

IMG-20120613-WA001

Watoto watatu ambao walikuwa wakitembea pembezoni mwa barabara wameangukiwa na nyaya za umeme baada ya gari dogo aina ya Escudo kugonga nguzo asubuhi hii maeneo ya Mbagala Zakheem.

Watoto hawa watatu waambao walikuwa wakitembea pembeni wamejeruhiwa vibaya na kuunguzwa sehemu mbalimbali kwenye miili yao, ambapo wasamalia wema waliwasaidia na kuwapakia kwenye gari kukimbizwa Hospitali.


JB Mpiana kutoa Albamu mbili Mpya

June 12, 2012

Mwanamuziki JB Mpiana “Salvatore de la Patria” na kundi zima la Wenge BCBG wako Studio akimalizia Albamu yake mpya ambayo itakuwa maalumu kwa ajili ya kutoa shukrani kwa mfadhili na mmiliki wa studio Ndiaye ambayo amekuwa akifanaya nayo kazi takribani miaka 10 sasa.

JB amesema kuwa albamu hiyo kwa sasa inakaribia kukamilika, habari zinasema kuwa Albamu ya pili ya kundi hilo ni Albamu yao ya kawaida ambayo inakuja baada ya Albamu ya Soyons sérieux. JB ambaye albamu yake ya sasa ya Soyons Serieux inafanya vizuri bado anatazamiwa kuachia albamu hiyo baada ya katikati ya mwaka huu ina maana kuanzia mwezi wa nane.


Maisha Park Agreement; Mapatano yaliyolenga kuondoa tofauti za Wanamuziki wa Congo.

June 12, 2012

Tujikumbushe siku MAISHA PARK agreement ilivyosaidia kuandoa migogoro miongoni mwa wanamuziki nguli wa Congo,japo wengine mkutano na mazungumzo hayo yaliayoandaliwa na mzee Tabu Ley pamoja na Simaro Lutumba na kufanyika kwenye hiyo park iitwayo maisha ndani ya kinshasa haukuwasaidia sana kwani bado wameendelea kuwa mahahsimu mpaka leo,migogoro mikubwa iliyoweza kuzikwa na maisha park agreement kwa kiasi kikubwa ni ule wa Jb na Koffi na pia wa Werra na Jb na pia kwa kiasi fulani wa Koffi na mzee Papa Wemba…hebu tizama kwa uchache sehemu tu ya video hiyo ya maisha park agreement,hapo utaona kwanza mbwembwe za baadhi ya wanamuziki wakati wa kuingia kwenye ukumbi wa mkutano huo wa manguli wa muziki kinshasa, tazama kuanzia dk ya 09:15 uwasikie koffi, Jb na Papa Wemba wanasema nini kwa pamoja na kisha wanaimba wimbo mulolo kwa pamoja………..baada ya hapo utamuona na kumsikia Le Roi Pelee Marie Paul, Bozi Boziana, mama Tshala Muana nae atakua na yake na baadae mtawaona wote kwa pamoja wakipata chakula kwa pamoja huku utani wa hapa na pale ukiendelea koffi akiongoza kwa masihara mezani, hii ilikua 2005 mwishoni, kuna mahali utamuona madilu anamwita koffi wee Antony…wee Rambo mdogo wangu, Koffi ataitika na kufanya masihara kidogo ambapo kila mtu atacheka..


JB Mpiana kutoa Albamu mbili Mpya

June 12, 2012

Mwanamuziki JB Mpiana “Salvatore de la Patria” na kundi zima la Wenge BCBG wako Studio akimalizia Albamu yake mpya ambayo itakuwa maalumu kwa ajili ya kutoa shukrani kwa mfadhili na mmiliki wa studio Ndiaye ambayo amekuwa akifanaya nayo kazi takribani miaka 10 sasa.

JB amesema kuwa albamu hiyo kwa sasa inakaribia kukamilika, habari zinasema kuwa Albamu ya pili ya kundi hilo ni Albamu yao ya kawaida ambayo inakuja baada ya Albamu ya Soyons sérieux. JB ambaye albamu yake ya sasa ya Soyons Serieux inafanya vizuri bado anatazamiwa kuachia albamu hiyo baada ya katikati ya mwaka huu ina maana kuanzia mwezi wa nane.


Japonais Arejea WMMM kwa Mbwembwe

June 12, 2012

Mwanamuziki mkongwe aliyewahi kutamba wa Bendi ya WMMM yake Werason Ngiama Makanda amerejea kwenye kundi hilo baada ya kuihasi bendi hiyo kwa takribani miaka 10.

Japonais alitambulishwa wili iliyopita kwenye onyesho la kila jumapili la WMMM na kwa sasa ndiye kiongozi mkurugenzi wa Bendi (Directeur artistique).

Kabla Japonais hajarejea kwenye bendi nafasi hiyo ya uongozi ilikuwa kwake Papii Kakol ambaye atapewa madaraka mengine. Japonais ambaye alitamba kwa upigaji gitaa la solo atasikika kwenye nyimbo mpya ambazo WMMM wanazifanyia mazoezi na pia umati ulilipuka kwa mayowe. Japonais alisikika vyema kwenye Solola Bien na aliamua kuondoka mwenyewe ili akafanye kazi yake yeye kama yeye na baada ya mambo kutomuendea vizuri ameamua kurejea kwenye bendi yake akiwa ni mmoja wa waanzilishi wa WMMM.

Kwa sasa WMMM wameingia Studio kwa ajili ya albamu yao mpya itaitwa « Flash India ».


Buriani mwanamuziki NDOMBE OPETUM…!! Ni Baba yake Mzazi Baby Ndombe.

June 12, 2012

DRCongo imempoteza mwanamuziki mkongwe NDOMBE OPETUM wa Bendi Bana OK, Huyu ni Baba mzazi wa BABY NDOMBE aliekua Wenge Maison Mere ya Werrason, Mzee Ndombe alifariki May 24 anazikwa leo June 12.


Yuko wapi Allain Konkou?

June 11, 2012

Unamkumbuka Alain Kounkou alivyowasha moto Africa nzima 1992 na hii kitu ?? wewe ulikuwa wapi wakati huo na unakumbuka nini ukisikiliza hili Generique la ukweli????

Sijui yuko wapi huyu mtu alikua na masebene ya ukweli.


Foundation Solomon Kalou, Thank you..

June 11, 2012

Huwa nasikia raha sana ninapoona mtu mweusi anapata mafanikio katika shughuli zake halafu anaamua kurudisha sehemu ya kile alichokipata kwa watu wake. Leo tumtizame mwanandinga Solomon Kalou wa timu ya soka ya Chelsea ya Uingereza anapoamua kushare kile alichokipata kupitia kipaji chake na watu wake wa nyumbani kwao alikozaliwa Ivory Coast kwa kuzindua Foundation yake kwa ajili ya watu wa Ivory Coast.

Hafla ya uzinduzi wa foundation hiyo ilifanyika katika jiji la Abidjan na kuhudhuriwa na watu mbali mbali mashughuli wa Ivory Coast ambapo ulikua ni usiku mzuri sana uliombatana na burudani kibao… pata picha ya kilichojiri kwa uchache na hii iwe ni changamoto kwa watu wote wa hapa nyumbani wanapopata mafanikio makubwa ya kimaisha na kiuchumi kujaribu ku share mafanikio yao hayo na jamii inayowazunguka..


Foundation Solomon Kalou, Thank you..

June 11, 2012

Huwa nasikia raha sana ninapoona mtu mweusi anapata mafanikio katika shughuli zake halafu anaamua kurudisha sehemu ya kile alichokipata kwa watu wake. Leo tumtizame mwanandinga Solomon Kalou wa timu ya soka ya Chelsea ya Uingereza anapoamua kushare kile alichokipata kupitia kipaji chake na watu wake wa nyumbani kwao alikozaliwa Ivory Coast kwa kuzindua Foundation yake kwa ajili ya watu wa Ivory Coast.

Hafla ya uzinduzi wa foundation hiyo ilifanyika katika jiji la Abidjan na kuhudhuriwa na watu mbali mbali mashughuli wa Ivory Coast ambapo ulikua ni usiku mzuri sana uliombatana na burudani kibao… pata picha ya kilichojiri kwa uchache na hii iwe ni changamoto kwa watu wote wa hapa nyumbani wanapopata mafanikio makubwa ya kimaisha na kiuchumi kujaribu ku share mafanikio yao hayo na jamii inayowazunguka..


Werrason na watu wake

June 9, 2012

Niliwahi kuandika kuhusu Werrason na nafasi yake kwa jamii, Kiukweli Werrason anakubalika sana kwenye miji ya Congo, hii inatokana na kujiweka kwake karibu na jamii hasa watu wa chini, inasema Werrason hupendelea sana kukaa vijiweni na kupiga story zile za mitaani bila kuwatenga watu wake wa Chini na mara nyingi huwa akifurahi huwa anafanya Show za bure bila malipo, hii imemfanya kuwa karibu sana na mashabiki wake tofauti na wanamuziki kama Koffi, Fally, Jb Mpiana na wengineo ambao wanasemwa kunata sana kwenye makundi haya ya jamii.

Huu ni mmoja wapo wa nyimbo ambazo zilikuwa kwenye albamu ya Solola Bien, moja ya kazi za Werrason ambazo nazikubali sanaaaa kwenye albamu za Wenge Musica Maison Merre enzi hizo kikosi kikiwa bado kimetimia watu kama Ferre, Mabiala, Lacoste, Adjani, Baby, Bill, Celeo, Japonais, Kapaya, Dominguez etc, wenyewe waliwaita le barça de la zik congolaise. Barcelona ya Muziki wa Congo.


%d bloggers like this: