Ushindi una utamu wake bwana!

September 30, 2008
.

.

Bayern Munich’s coach Juergen Klinsmann jumps with joy as Bayern Munich’s Brazilian midfielder Ze Roberto scored the 1-1 during their Champions League group F Bayern Munich vs Olympique Lyonnais football match at the Allianz-Arena in the southern German city of Munich today September 30, 2008


Deplaizir nakati ya bongo…

September 29, 2008
Jose na Deplaizir

Jose na Deplaizir

Mwanamuziki Jose Mala wa FM Academia akiwa na mwanamuziki Deplaizir Mcongo anayeishi Uingereza walipokutana juzi usiku , Deplaizir yuko Tanzania akifanya Recording na wanamuziki kadhaa wa Tanzania, lengo likiwa kujitambulisha Afrika ya mashariki na kati akiwa chini ya Meneja wake wa ukanda huu Sophia Kessy wa Africa Bambataa.


Lucille ‘out’, washiriki wapanga mgomo

September 29, 2008

Namibia’s Lucille Naobes

Mshiriki wa Big Brother Africa kutoka Namibia, Lucille amekuwa mshiriki wa pili kufuata nyayo za Latoya kutolewa kwenye shindano hilo. Lucille amekumbwa na tatizo hilo baada ya TK ambaye alikuwa mkuu wa nyumba kuamua kumbadili Lucille na yeye katika orodha ya washiriki wa kupigiwa kura za kutolewa.

Mshiriki huyo alikuwa akipambana na Mnigeria Uti na Ricco wa Angola ambao waliangusha kilio baada ya KB kutangaza kuwa Lucille ndiye anayeondoka katika shindano hilo. Uti alifanya uharibifu kabla ya Ricco kumtuliza. Awali TK alimchagua Lucille kuchukua nafasi yake kwa madai kuwa anaamini binti huyo asingetolewa kwenye shindano hilo.

Aidha, mara baada ya kutolewa, Lucille alipigwa na butwaa kugundua kuwa TK ndiye alimembadilisha jina lake na kudai amefanya hivyo akiamini kuwa yeye (Lucille) ndiye aliyeiba sigara zake. Lucille alipigiwa kura kutoka Botswana, Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Zambia, Zimbabwe na kura moja ya nchi ambazo hazina mshiriki wakati Uti akipigiwa kura na Angola na Namibia na Rico akiwa hajapata kura hata moja.

Wakati huo huo, kutokana na kitendo alichokionyesha Uti jana aliadhibiwa na Big Brother kwa kupelekwa kwenye chumba cha adhabu. Wakati huo huo, washiriki wa waliobakia kwenye jumba hilo wamepanga kugoma na kumpa saa 24 Big Brother kutekeleza ombi lao la kuongezewa pombe kwenye jumba hilo.

Washiriki hao wamepanga kuwa hakuna hata mmoja atakayekwenda kwenye chumba cha mahojiano na Big Brother na kutofanya mazoezi asubuhi, kukataa kuamka na kutofuata maagizo yake. TK na Thami ndio walioongoza mipango ya kufanya mgomo wakidai kuongezewa pombe na kusema: “Akituita kwenda chumba cha mahojiano tutakataa na pia adhabu yake tutaikataa,” alisema TK.


“Nimeimba kwa Niaba ya wanandoa” Inspector

September 29, 2008
Inspector

Inspector

Msanii mahiri wa kizazi kipya Haruna Kahena maarufu kama Inspekta Haruon amesema aliamua kuujibu wimbo wa nyota ‘Mwana FA’kwa ajili ya kuwatetea wana ndoa.

FA hivi sasa anatamba na wimbo wake wa Bado nipo nipo kwanza, ambao ndani yake anaelezea kukerwa kwake na tabia zake za wanawake kutokuwa waaminifu,kiasi cha kuwafanya wajibu wanaomuliza siku ya kuoa kwamba kwa sasa bado yupo yupo sana, kwani hata akiamua kuoa,bado haoni mwanamke wakumfanya kuwa mkewe.

”Ni kweli,nimeimba ili kumjibu kwa niaba ya wanandoa sio wanawake wote walio sio waaminifu katika ndoa zao kwani kuna watu wapo katika ndoa kwa miaka 50 na bado wana pendana.

Wapo ambao sio waaminifu lakini sio kila mtu kwa hiyo kwa maoni yangu alicho kiimba kina hitaji kukosolewa alisema Inspekta ambaye pia anafahamika kama Babu.

Baada ya wimbo huo wa FA,Inspekta alikuja na wimbo wake unaoenda kwa jina la ndoa haina doa.

Mapema mwaka jana Inspekta aliimba wimbo ambao ilikuwa ni majibu ya wimbo wa Mh. Temba usemao Hakuna mwaka wa Shetani,baada ya mkali huyo wa TMK wanaume Family kuibuka na kibao chake cha mwaka wa shetani.

Alipoulizwa kuhusu madai ya baadhi ya wadau kwamba ameishiwa mashairi kiasi cha kusubiri kuwajibu wenzake,Babu alisema “Hii ndiyo sanaa wanaosema hivyo hawaelewi kazi ya msanii sio tu kuburudisha bali pia kukosoa kufundisha na kuonya”.

Source: Dar411


Wanigeria wakomaa kuichukua Newcastle

September 29, 2008

.

Mmiliki wa Newcastle Mike Ashley, anataka £400m kuuza klabu.

Kundi la wafanya biashara wa Nigeria limewakilisha rasmi nia yao na ofa yao kwa kuichukua timu ya New Castle United.

Kundi hili ni moja wapo ya wadau walionyesha nia ya kuinunua Klabu hii lakini mpaka sasa wao ndio wamekuwa wa kwanza kuweka wazi nia yao ya kuichukua klabu hii.

Mfanya biashara wa Nigeria ambaye anamakazi yake Uingereza Chris Nathaniel ndiye anayeongoza kundi hilo la wafanyabiashara, alipooulizwa ni kiasi gani wamebid kwa ajili ya kuichukua Timu hiyo ya Newcastle, Nathaniel alikataa kuweka wazi kwa kile alichosema kuwa hapa ni ushindani kwani wengine nao wanataka kujua ili wabid juu yao.

“hatuwezi kuweka wazi kwa wakati huu, hii ni siri kati yetu na Newcastle, lakini tumewakilisha ijumaa, inshalla tunawza kupita.” alisema.

“Newcastle hawajatoa muda maalum lakini wamesema itakuwa karibuni.”


Bosigwa, Anelka waibeba Chelsea dhidi ya Stoke.

September 28, 2008
Bosigwa akipiga kiufundi kutoka chobingo!

Bosigwa akipiga kiufundi kutoka chobingo!

Magoli mawili yaliyofungwa na Bosigwa na Anelka yaliipa ushindi wa 2-0 Chelsea usiku wa leo na kufanikiwa kuongoza ligi kwa muda. Goli la kwanza lilifungwa dakika ya 36 ya mchezo na mchezaji Bosigwa na baadaye alifamnikiwa kumtengenezea pande Anelka na kupachika bao la pili dakika ya 76 ya mchezo. Hili ni goli la kwanza kwa Bosigwa baada ya kusajiliwa akitokea FC Porto.

Stoke hawakuonyesha upinzani mkali sana kwa Chelsea ambao waliumiliki mchezo kwa zaidi ya asilimia 60 huku wakifanya jumla ya mashambulizi 20 langoni mwa Stoke dhidi ya 8 tuu kwa upande wa goli la Chelsea.


Man wapata ushindi wa kwanza nyumbani…

September 28, 2008
Ronaldo akipachika Penalti yake

Ronaldo akipachika Penalti yake

Goli la penati ambalo Ronaldo alifunga kwa hakika lilikuwa mwiba kwa Bolton ambao walilalamika kitendo cha refa  Rob Styles kutoa Penati isiyohalali ambayo ilipelekea kupachikwa goli la kwanza lililofungwa na Ronaldo. Huu ni ushindi wa kwanza wa Man U nyumbani,

Hata hivyo Man U walifanikiwa kuongeza goli la pili lililofungwa na Wayne Rooney, mchezo wa jana Man U waliutawala kwa 75% huku Bolton wkionyesha kujihami zaidi. Mpaka mwisho wa mchezo Man Utd 2 – 0 Bolton.


%d bloggers like this: