Manchester “Sasa Ligi ndio imeanza”

January 18, 2009
Dimitar Berbatov

Hatimaye yakalia kiti cha enzi.

Goli la dakika ya mwisho toka lililofungwa na Dimitar Berbatov kwa kichwa baada ya kupata cross dakika ya 89 liliwabeba MAn U na kuwafanya kufika kileleni mwa ligi usiku wa leo, Huku wakicheza ugenini na Bolton ambao walionyesha kufa kiume dakika zote 90 za mchezo.

Huku wakicheza bila ya Rooney ambaye anaumuhimu mkubwa mashambulizi ya Manchester mara kwa mara yalikutana na ukinzani wa kipa aliyekuwa akikatisha tamaa wa Bolton, Kross nyingi za Ronaldo ziliishia miguuni mwa beki za Bolton ama kupanguliwa na kipa wao na hivyo kufanya Man U kuongeza mashambulizi na nguvu zaidi Manchester walihitaji ushindi huu kufa na kupona walao kuwapa matumaini ya Ubingwa mwaka huu mashabiki wao, na wao wanasema sasa ligi ndio imeanza.

Wakati huo huo: huku wakicheza uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki 41,000 timu ya Chelsea liiponea chupuchupu kuvikwa nepi nyumbani na Stoke City,Chelsea nayo iliponea mdomo wa Mamba kupata kichapo iliporudisha goli dakika za mwisho kabla ya Frank Lampard (90) kufunga bao la pili dakika ya 90 na kufanya Chelsea kumaliza kwa 2-1.

Rory Delap

Rory Delap fires home Stoke’s shock opener

Stoke City walipata goli la kuongoza dakika ya 60 ya mchezo kupitia kwa Rory Delap, goli ambalo liliipeleka Chelsea mchaka mchaka kabla ya kusawazisha dakika ya 88 ya mchezo kupitia kwa Juliano Belletti na hatimaye Frank Lampard kuongeza goli la ushindi dakika 2 baadaye. Chelsea wamekuwa wakiozongwa na shetani mbaya kwenye game za karibuni na kipigo kibaya ni cha MAnchester cha 3-0 ambacho kiliwaumiza sana mashabiki.

MAtokeo mengine na story zake ni kama ifuatavyo, gonga link kupata story:-


Masikini Ronaldo

July 21, 2008
Masikini Ronaldo
Masikini Ronaldo

Timu ya Manchester United imemwambia mchezaji wake Cristiano Ronaldo kuwa hakutakuwa na mabadiliko yeyote yamshahara kutegemeana na deal ya kwenda Real Madrid kutofanikiwa, Real Madrid ambao walikuwa wameweka dau kubwa kwa Ronaldo ambaye aliwekewa ngumu na timu yake, wamesema kuwa walitaka kumsajili Ronaldo na walikuwa tayari kumpa mkataba mnono lakini kama imeshindikana basi ni heri akabaki huko.

Kwa kiasi fulani Manchester hawakupendelea kitendo cha Ronaldo kutoficha hisia zake kuhusu hamu yake ya kujiunga na Real Madrid na wao wameichukulia hii kama ilikuwa njama ya Ronaldo kuongezwa mshahara alisema Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo David Gill.

Aidha Gill alisema kuwa Ronaldo atabakia kwenye mkataba wake wa awali wa dila 240,000 kwa wiki ambao bado una miaka minne kumalizika.


%d bloggers like this: