Anaitwa AY wa Commercial!!

July 31, 2008
AY Aka Ambwene Yesaya

AY Aka Ambwene Yesaya

Ukiongelea mafanikio ya Muziki wa Bongo Flavour basi hutosita kumuongelea kijana Ambwene Yesaya au kama alivyozoeleza kwa jina la AY, Spoti na starehe katika kukuletea habari za wanamuziki na wanamichezo mbali mbali wa ndani na nje ya Tanzania wiki hii tunakuletea kijana nguli wa burudani katika sekta ya muziki wa kizazi kipya. ama kwa hakika hakuna mwanamuziki wa Bongo Flava aliye wahi kuwa nominated kwenye award za Kora isipokuwa yeye, AY alikuwa ndio mwanamuziki wa Bongo Flava wa kwanza kutajwa kugombea Award hiyo akiwa ni kwenye kundi la kutoka Afrika Mashariki na kati amblo lilikuwa ni Mwanamuziki bora wa Kiume (the best male artist) hii ilikuwa ni mwaka 2005. Baada ya hapo pia AY aliingia kwenye Kisima Award ikiwa ni kwenye kundi la wimbo bora toka Tanzania, akiwa na hit single yake ilokuwa inatamba kipindi hicho ya “Inategemea na mtu”. Read the rest of this entry »


Burudani kedekede Miss Tanzania 2008

July 30, 2008

Twanga, Minanawe, Chameleon, Wanaume, Wazee wa Ngwasuma kutumbuiza

Vimwana wanaowania kinyang'anyiro cha miss Tanzania 2008, wakiwa katika picha ya pamoja kambini kwao Bagamoyo, Picha na GPL

Vimwana wanaowania kinyang'anyiro cha miss Tanzania 2008, wakiwa katika picha ya pamoja kambini kwao Bagamoyo, Picha na GPL

Bendi za bendi za FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ na African Stars ‘Twanga Pepeta, Mina Nawe kutoka Afrika Kusini, Jose Chameleon wa Uganda, Wanaume Family, Wanne Star na kikundi cha THT. ni vikundi ambavyo vitatoa burudani wakati wa kilele cha mashindano ya Miss Tanzania 2008.

Wakiongea wakati wa kutaja viingilio kwa mtanange huo, Kamati ya Miss Tanzania ilisema viingilio cha kuona fainali za mashindano hayo Agosti 2 mwaka huu kitakuwa sh. 100,000, sh. 80,000 na cha chini kitakuwa sh. 35,000. Read the rest of this entry »


Mahakama ya Biashara yatupa ombi la EATV

July 30, 2008
Ze Comedy wacheka kudadaadeki

Ze Comedy wacheka kudadaadeki

Pichani ni Kundi la Ze comedy wakishagilia kwa pamoja muda mfupi baada ya Mahakama kuu kutupilia mbali ombi la EATV dhidi ya kikundi hicho..
——–

Na Rabia Bakari wa gazeti la Majira

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imetupa maombi ya kituo cha televisheni cha EATV, ambao ni walalamikiwa katika kesi iliyofunguliwa na kundi la wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Ze Comedy ya kuiomba mahakamani itupe kesi dhidi yao kwani haina madai ya msingi. Read the rest of this entry »


Tampere African Sports ya Finland yainyuka 3-1 Vaasa

July 30, 2008
Kikosi madhubuti cha TAS kilichowatoa kamas Vaasa

Kikosi madhubuti cha TAS kilichowatoa kamas Vaasa

Timu inayoundwa na wabongo wanaoishi jiji la Tampere finland(Tampere African Sports-TAS) jana imewachapa magoli 3-1 majirani zao wa mji wa Vaasa.

Mchezo ulikuwa wa ushindani vuta nikuvute katika mashindani ya ‘summer heat’. Tampere walijipatia magoli 2 kupitia kwa mshambuliaji wake Mark Mhekwa na Ngasa Ambrose kupigilia msumari wa tatu kwa njia ya penati.

Vaasa wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi kupitia mchezaji wao raia wa kenya Sospeter,huku wakikosa kufunga penati baada ya kipa wa tampere Edo Ndaki kufanikiwa ‘kuifuta’.

Kikosi cha Vaasa ambacho kilicheza na TAS

Kikosi cha Vaasa ambacho kilicheza na TAS

Mpaka mwisho wa mchezo TAS 3-Vaasa 1.

TAS sasa wanawasubiri ‘mahasimu wao’ BONGO fc kucheza mchezo wa marudiano.Ikumbukwe mchezo wa kwanza BONGO FC walichapwa nyumbani kwao magoli 3-1.

Nikiripoti kutoka ufini,  Mdau wa Spoti na starehe

Spoti na Starehe inawapongeza wadau wa TAS kwa ushindi huo


Chelsea yaishinda Malaysia kwa 2-0

July 30, 2008
Toka kulia ni Mimi na anayefuata ni Mh Zungu, Mbunge wa Ilala tukiwa uwanja wa Shah Alam tukifuatilia mechi ya Chelsea na Malaysia

Toka kulia ni Mimi na anayefuata ni Mh Zungu, Mbunge wa Ilala tukiwa uwanja wa Shah Alam tukifuatilia mechi ya Chelsea na Malaysia jana usiku. Chelsea ilishinda 2-0.

Magoli yaliyofungwa na Nicolas Anelka na Joe Cole yaliwapa ushindi wa 2-0 dhidi ya timu ya All Star ya Malaysia ambayo inajumuisha wachezaji wa wanaunda timu ya Taifa, Timu ya Chelsea huku ikichezesha kikosi chake cha kwanza jana iliifunga kwa Taabu timu ya Malaysia katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Shah Halam jijini Kuala Lumpur hapo jana usiku. Timu ya Malaysia ndio iliyoanza mchezo kwa kasi na kukosa mabao mawili ya wazi dakika ya saba ya mcezo na dakika ya kumi ya mchezo. Baadaye mpira ulibadilika na Chelsea kucheza kwa kuonana zaidi huku Anelka akionyesha kuinyanyasa zaidi ngome ya Malaysia ambao walikuwa wakicheza kwa kuogopa majina. Goli la kwanza lilifungwa na Nicolas Anelka dakika ya 27 ya kipindi cha kwanza.

Mchezaji wa Chelsea Frank Lampard akiwa katikati ya wachezaji wa Malaysia Omar na Fauzie Nan wakati wa mchezo wa kirafiki jan.

Mchezaji wa Chelsea Frank Lampard akiwa katikati ya wachezaji wa Malaysia Omar na Fauzie Nan wakati wa mchezo wa kirafiki jan.

Kipindi cha pili kilianza kwa mchezo wa kasi huku ngome ya Malaysia ikijiimarisha zaidi na lakini Joe Cole alifanikiwa kupenya na kupachika goli dakika ya 53 kipindi cha pili. Kwa ujumla mchezo ulikuwa mzuri na timu ya Malaysia huku ikicheza ndani ya joto kali ambalo lilikuwa 29c kwa usiku huoilicheza mchezo wa kujihami zaidi huku ikifanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kushtukiza ambayo yalivunjwa moyo na juhudi za golikipa wa Chelsea ambaye alicheza vizuri usiku huo,


Tanzia

July 29, 2008
Marehemu Jackson Goa - Jack Bai

Marehemu Jackson Goa - Jack Bai

Familia ya Mikongoti wa Dar Es Salaam na Familia ya A.Goa wa Ifakara – Kilombero, Inasikitika kutangaza kifo cha ndugu yao Jackson Goa au Jack Bai kilichotokea leo katika hospitali ya buruhani. Mipango ya mazishi inafanya nyumbani kwa Kaka wa Marehemu Dar es Salaam. Habari ziwafikie ndugu jamaa na marafiki popote pale walipo.

E. Mikongoti – 0784 431154


Mamiss na mguso wa jamii…

July 29, 2008
Mamiss na mguso wa jamii

Mamiss na mguso wa jamii

Washiriki wa Miss Tanzania 2008 wakizungumza na mtoto aliyejitambulisha kwa jina moja la Josephine, aliyekuwa anatoka kuokota kuni katika vichaka vya Mjimwema Kigamboni Dar es Salaam juzi. Warembo hao walikuwa kwenye ufukwe wa South Beach katika maandalizi ya shindano lao linalotarajiwa kufanyika Agosti 2, mwaka huu. (Na na HabariLeo).


%d bloggers like this: