ICE BLACK MAGIC DAR – 17th DEC 2010

November 30, 2010

...


Simulizi ya Kweli ya Kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa 1971 Dr. Kleruu.

November 29, 2010

 

Mnara wa Kumbukumbu ya alipouawawa Marehemu Kleruu.

Kwa wapenda Historia nadhani wanakumbuka hadithi ya mauaji ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr. Kleruu kwa kupigwa Risasi na mkulima mmoja huko Isimani Iringa siku ya Christmas Desemba 25 1971.

Mwanaharakati, Bloga na Muandishi wa kujitegemea Majid Mjegwa amefanya mahojiano na mtoto wa kiume wa Kiume wa mtuhumiwa wa mauaji hayo Mwamindi. Kujua nini wameongea bofya hapa.

 


Cheka Ki-Spoti na Alamba Arab Version!

November 29, 2010

Soso Fresh RudMixxTape ya BUREE!!

November 29, 2010

...

katika kuondoa mipaka ya kimuziki,noizmekah studios imeunda rudmixxes kadhaa zenye mix up ya tz na mamtoni,suitable material for club & radio available for free kabisa,rudmixx hizi ni kwa lengo la ku hype radio & club dj’s wa2patie live mixing za style hizi na kuzoesha watanzania kwamba muziki we2 waweza kwenda international tukijitahidi maana wanyamwezi jinsi wamekaa vema kwenye beat ze2 humu ndani ya rudmixtape ni ucpime.

Bonyeza Hapa Kudownload

 


Afande Kova, Hata Mbuyu ulianza kama mchicha!!

November 29, 2010

 

Jangwani jana Jumapili

Kibaka akiwa taabani

Kijana akiwa hoi hajitambui baada ya wananchi kumshambulia kwa kosa la kuiba simu ya mkononi katika eneo la Jangwani kisha kutimua mbio lakini alikamatiwa kwenye geti la shule ya Sekondari ya Jangwani na kupata kipondo hadi mauti kumkuta.

Tatizo la vibaka limekuwa kero na yapo maeneo sugu ambayo yanajulikana kabisa, ni ukweli kuwa yanajulikana sio siri na kama sisi raia tunayajua na imani kabisa hata wenye kazi yao Jeshi la Polisi wanajua pia.

Hainiingia akilini kuwa kunapokuwa na kitu Polisi wanamwagwa mitaani na kunakuwa shwari, siku za sikukuu au kama kuna tukio kubwa wale Polisi wanatoka wapi? Si lazima hawa Polisi wawe kila mahali ni zile sehemu korofi tu.

Kujichukulia sheria mikononi ni wazi kuwa raia wamechoka, hebu fikiria wale vibaka wa Ubungo mataa wanang’oa vioo vya magari au wheel capes huku gari inatembea hii si dharau tena mchana kweupee!!. Kibaka kama huyo ukimshika hasira zake hazikingiki.

Maeneno kama hayo ya Ubungo Mataa, Ubungo Darajani, Tabata Relini, Tazara, Chang’ombe Mataa pale, Jangwani, Bonde la Mkwajuni, Salenda Bridge na sehemu nyingine hizi zinajulikana kuwa ni korofi siku zote, inashindikana nini Polisi kuweka Doria maeneo haya?

Eneo la Ferry zamani lilikuwa na matatizo sana, Mkuu wa Kituo pale aliwashirikisha wafanya biashara na wapiga debe katika Ulinzi shirikishi kwa ushirikiano wa Polisi na hao wafanyabiashara na wapiga debe wakimuona kibaka wanamkamata na kumpeleka Polisi leo hii Pale Ferry vibaka wamepungua kwa kiasi kikubwa sana.

Mheshimiwa Kamanda wa Polisi hata mbuyu ulianza kama mchicha, tunazipongeza juhudi zako kwa kupambana na Majambazi na kwa siku za karibuni kwakweli matatizo na matukio ya ujambazi yamepungua kwa kiasi fulani kutokana na habari hizo kupungua kuandikwa magazetini (sina takwimu sahihi).

Lakini ninachotaka kukutahadharisha ni kuwa hata Mbuyu ulianza kama mchicha, hawa majambazi nao walianza kama vibaka tu ndio leo wamekuwa majambazi. Inawezekana kama tu kila mmoja akitimiza wajibu wake.

 


Tusker Project Fame; Msechu ala Shavu kwa Ian!!

November 28, 2010

 

Msechu

Baada ya kuponea kwenye tundu la sindano kwenye shindano la Tusker Project Fame wiki hii, mwakilishi pekee wa TAnzania Msechu leo (Jumapili) alikonga nyoyo za wengi baada ya kuimba wimbo wa Hasira Hasara ambao alionyesha kipaji cha hali ya juu.

Huku akiimba kwa kujiamini kama kawaida yake Msechu ambaye amejizolea sifa kem kem kwa kusakata Sebene vilivyo na majibu yake ambayo yako kama comedian fulani humfanya awe na nasaba ya kipekee.

Baada ya kuimba ma jaji wote walimpa comment nzuri Msechu, “Ulipoanza kuimba niliona ni Msechu anamuigiza Kidumu lakini baadaye kidogo nimeona kuwa ni Msechu ana Muigiza Msechu, Umefanya vizuri sana…” alisema Jaji Ian. Si kawaida kwa Ian kumsifia mtu kirahisi, kwani alionyesha kuutambua uwezo wa Msechu na kushangiliwa sana.

“Leo nitalala vizuri baada ya kupata comment nzuri toka kwa Ian…” alisikika akisema Msechu kwa furaha.

Jaji Ian ni mmoja wa majaji ambaye mashabiki wengi wa Tusker Project Fame hasa wa Tanzania wamekuwa wanamchukia kiasi fulani kwa comments zake kuhusu washiriki wa TAnzania na amechangia kwa kiasi kikubwa wao kutoka.

Ni ukweli kuwa Ian akikukubali ujue na mashabiki watakukubali tuu.

Kwa wiki ijayo Majaji waliawaamulia washiriki nyimbo za kuimba wiki ijayo. na ndipo Msechu alipoambiwa kuwa ataimba wimbo wa Show Me The Way wa kwake Papa Wemba.

 

Probation

...

Wiki hii washiriki wote wamewekwa kwenye Probation huku watazamaji wakihamasishwa kupiga kura, ni kweli watanzania ni wavivu kupiga kura, shime jamani tumpigie kura Msechu.


Ali kiba alia na “Ally Kiba” feki wa Facebook

November 28, 2010

 

Kurasa mbalimbali za Ally Kiba ndani ya Mtandao wa kijamii wa FAcebook.

Wanamuziki wa kizazi kipya Ali Kiba ameonyesha masikitiko yake kwa wale aliwaita Ally Kiba “fake” ndani ya mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa wanamchafulia.

Akiongea na Mtangazaji wa kituo cha Clouds Fm, Dj Fetty aka Fee eh!  jana Ali Kiba alisema kuwa amesikitishwa na habari za uwepo wa Ali Kiba hao ambao kwa siku za karibuni amekuwa akipata kesi mbalimbali.

“Nimesikia wanachat na watu huko Kenya na Kuchukua hela kwa ajili ya Show ambazo baadaye hatokei kwenye show kisha hunitafuta mimi baadaye…” alisema Ally Kiba kwenye mahojiano hayo.

Wiki iliyopita moja ya magazeti yaliandika kuwa Ally Kiba amefiwa na mtoto jambo lililo[elekea mtangazaji huyo kumtafuta Ally kiba ambaye alikana habari hizo na kumbe Ally Kiba huyo Feki amekuwa akichangisha pesa kwa ajili ya msiba huo.

“Si tu kuchangisha fedha kwa ajili ya msiba bali pia aliwahi kusema kafiwa na mama yake watu wakamchangia” aliongeza Ally Kiba.

Kuthibitisha hilo Spoti na Starehe iliamua kujaribu kumtafutta ukurasa wa Ally Kiba kwenye mtandao wa kijamii wa FAcebook na zilikuja Kurasa tano ambazo zote zilikuwa na picha ya mwanamuziki huyo na jina lake pia, Kwa njia hii ni vigumu kujua kama mwenye jina ni mtu halali ama lah.

Ally Kiba alisema kuwa yeye huwa hachat na mtu kwenye facebook kwani si yeye anayesimamia ukurasa wa facebook ye huwa ana update profile yake tuu.

NINI CHA KUFANYA LILIKUTOKEA?

Facebook walilijua hilo ndio maana katika kila ukurasa wa mtu (profile) ama awe ni rafiki yako au sio rafiki yako moja ya vitu unavyoweza kuviona ni kitufe kinachokuwa wewe uwezo wa kubonyeza na kumripoti mtu ambaye unahisi anatumia jina la mtu mwingine, ama lako au hata kama ameweka picha ambazo haziendani na maadili basi umripoti mtu huyo kwao na wao kuchukua hatua.

Chini kushoto kwa ukurasa wa mtu husika kuna sehemu imeandika “Report/Block this person”, Bonyeza hapo kisha jaza hiyo fomu ambayo inamaswali kadhaa kama inavyoonekana hapo chini.

 

...

Chagua moja wapo ya unachohisi si sahihi kuhusu ukurasa huo kisha bonyeza “Submit”. Ingawa inaweza kuchukua muda lakini ndani ya masaa 24 mtandao wa facebook ukijiridhisha na maelezo yako hatua za kinidhanimu huchukuliwa.

 

Kisheria.

Nilimuuliza mwanasheria Herry wa H&M Advocates juu ya suala hili akasema ni kosa kisheria kwani ushahidi upo lakini alisema kuwa mitandao pia ina wanasheria wake na akasema Ally Kiba kama akimtumia mwanasheria wake anaweza kumshitaki huyu tu anayetumia jina lake kama tu akiwa na ushahidi wa kutosha.

Hivyo basi Ally Kiba unapaswa kuchukua hatua za kinidhamu la sivyo jamii haitakuelewa, na masuala haya si wewe wa kuyafatilia hapa ndio mameneja wenu wanapoonyesha umuhimu wao kwenu, Kama ulivyokaririwa mwenyewe ukisema kuwa unalijua hili na ukakaa kimya jamii haitakuelewa inamaana bila jitihada binafsi za Dj Fee eh! kukutafuta basi ungekaa kimya na jamaa angeendelea kuvuta mkwanja wa watu kwa jina lako sivyo? haii haijakaa sawa kimtindo fanya jitihada za makusudi si kwa Ally Kiba tu bali kwa mtu yeyote ambaye atatokewa na kitu kama hiki.


%d bloggers like this: