Kimwana wa Ngwasuma 2009 yaanza

January 13, 2009

.

.

Shindano la kumtafuta kimwana wa Ngwasuma kwa mwaka huu wa 2009 limeshaanza, na vimwana wapo kambini hivi sasa pale katika ukumbi wa Meeda Club Sinza.


Kilimanjaro Connection

January 11, 2009

Bango la Kilimanjaro Connection

Bango la Kilimanjaro Connection

Bendi ya Kilimanjaro Connection ipo jijini Kuala Lumpur Malaysia kwa ajili ya kutoa burudani, Kilimanjaro Connection watakuwa wakipiga Club ya Rum Jungle kuanzia jumatano hadi jumapili.

Katika show ya jana Viajana hawa wamezikongonga nyoyo za mashabiki wa burudani na kufanya ukumbi kujaa hakuna hata pakuweka mguu.

Wakiwa wanapiga nyimbo zao maarufu na zingine copy toka Ngwasuma hadi ABBA group jamaa wamekamilika kinoma na kufanya usiku kuwa mfupi. PAmoja na kiingilio kuwa kikubwa (50 Rm kwa mtu) sawa na Tsh. 15,000/= na kwa mujibu wa meneja wa Club hiyo anasema walijaribu ku adjust kiingilio ili angalao ku control watu lakini kila siku wanazopiga watu wanajaa na kwa sasa wataongeza maonyesho na kupumzika mara moja tu kwa wiki siku ya Alhamisi. Kwa zaidi ya miaka 10 bendi hii imekuwa ikitoa burudani jijini Kuala Lumpur na show zake kupendwa na watu wote.

Haya wadau wa Malaysia kazi kwenu

The Kilimanjaro Connection wakiwa jukwaani.

The Kilimanjaro Connection wakiwa jukwaani.

Kankukely, Dr Kiiza and I

Wadau na Kankukelly kabla ya show kuanza

watu wamokazini

watu wamokazini

Mdau akiwa na mmoja wa waimbaji na wacheza show wa Kilimanjaro Connection BAnd

Mdau akiwa na mmoja wa waimbaji na wacheza show wa Kilimanjaro Connection BAnd

Jamani dada anacheza huyu wamalay wote hoi

Jamani dada anacheza huyu wamalay wote hoi


Nawapa shavu wazee wa Ngwasuma….!

September 8, 2008
Waimbaji wa FM wana Ngwasuma wakiwajibika Jukwaani kijiji cha Makumbusho

Waimbaji wa FM wana Ngwasuma wakiwajibika Jukwaani kijiji cha Makumbusho

Either Hot or Not!! Jamaa wako juu, Mukubwa Maghambo tuko pamoja?

Either Hot or Not!! Jamaa wako juu, Mukubwa Maghambo tuko pamoja?

Pamoja na kuibuka Bendi nyingi bado Wana ngwasuma wanatamba na kujaza mashabiki lukuki, Pichani ni Wanamuziki na wachezaji shoo wakiselebuka na kupagawisha vilivyo kwenye kijiji cha Makumbusho. Picha zote kwa hisani kubwa ya Dar411.com

Pamoja na kuibuka Bendi nyingi bado Wana ngwasuma wanatamba na kujaza mashabiki lukuki, Pichani ni Wanamuziki na wachezaji shoo wakiselebuka na kupagawisha vilivyo kwenye kijiji cha Makumbusho hivi kribuni. Picha zote kwa hisani kubwa ya Dar411


Yu wapi King Blaise??

August 11, 2008
King Blaise

King Blaise

Mtunzi na mwimbajiwa Bendi ya Muziki wa Dansi nchini FM Academia King Blaize inadaiwa ameikacha Bendi hiyo na kutimkia Majuu, chanzo chetu cha habari kinasema Blaize kwasasa yupo nchini Uholanzi kwa kile kinachodaiwa kwenda kutafuta Maisha.

Ni karibia muda wa mwezi mmoja washabiki wa FM wamekuwa hawamuoni jukwaani walipotaka kujuwa ni wapi yupo Mkali huyo wa sauti ya kulalamika msemaji mmoja kutoka katika bendi hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema Blaise kwasasa yupo Uholanzi akisaka maisha baada ya kuona mambo hayamuendei sawa hapa Tanzania. Read the rest of this entry »


Mambo ya Ngwasuma Miss Tanzania

August 4, 2008
Ngwasuma

Ngwasuma

Bendi ya FM academia kama kawaida usiku wa jana walipagawisha wadau mbalimbali kwenye shidano la kumtafuta Miss Vodacom Tanzania 2008 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam wakiongozwa na kiongozi wa Mkuu Nyoshi El-Sadaat wa kwanza Kulia pichani wakifanya vitu vyao jana. Picha na Haki Ngowi


%d bloggers like this: