Habari za Afya ya Uzazi

.

.

Ungana na tovuti hizi kwa maswala mbalimbali kuhusu afya ya uzazi:

.

HIV na Ukimwi barani Afrika

aids ribbon graphic

Afrika kusini ya jangwa la Sahara, ndilo eneo lililoathiriwa zaidi na janga la Ukimwi. Eneo hili lina asilimia 10 tu, ya jumla ya idadi ya watu kote duniani, lakini ndilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu waishio na virusi vya HIV.

Yaani – theluthi mbili (2/3) za watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kote duniani.

Ukimwi husababisha vifo vya watu takriban watu 6,000 kila siku barani Afrika.

Pindi mtu anapoambukizwa virusi vya HIV, huishi navyo kwa maisha yake yote kwani hakuna tiba, lakini siku hizi yapo madawa speshei ya kupunguza makali ya ukimwi hivyo basi kusaidia walio ambukizwa kuishi kwa muda mrefu.

HIV na Ukimwi barani Afrika
Ukweli ni kwamba: Zaidi ya watu milioni mbili nchini Kenya wameambukizwa virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi.
Ukweli ni kwamba: Nchini Uganda Ukimwi ndio unaoongoza kwa kusababisha vifo kwa wale wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 49.
Ukweli ni kwamba: Ukimwi umewaathiri zaidi wanawake kuliko wanaume hasa vijana walio kwenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 24.
Ukweli ni kwamba: Maambukizo ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watu wazima katika sehemu za mijini ni karibu mara mbili zaidi kuliko sehemu za mashambani.
Ukweli ni kwamba: Karibu wakenya 150,000 hufa kwa ukimwi kila mwaka.
UNAIDS report 2004

HIV ni nini?
ni ufupisho wa Human Immunodefeciency Virus yaani virusi vinavyoua kinga ya mwili. Ni HIV ni kirusi kinachoharibu uwezo wa mwili wako wa kujihami dhidi ya maambukizo.

Watu wengi hufikiria kwamba watu ambao wana virusi hivyo, wana Ukimwi, ukweli ni kwamba virusi vya HIV ndivyo vinavyosababisha Ukimwi, yaani yawezekana mtu akawa na virusi vya ukimwi kwa muda mrefu bila ya kuugua ukimwi. Hii inamaanisha anaweza kuwa na HIV bila kujua, wala kuona dalili zozote – Wakati huo iwapo tahadhari hazitachukuliwa anaweza kumwambukiza mtu mwengine .

Ukimwi ni nini?
Neno Ukimwi lina maana ya Ukosefu wa Kinga Mwilini. Hapa virusi vya HIV huwa vimeshambulia kinga ya aliyeambukizwa kiasi kuwa, mwili wake wauwezi tena kujipa ulinzi dhidi ya maambukizo.

Hivyo huonyesha dalili za magonjwa tofauti tofauti na hata saratani, hapo ndipo wanasemekana kwamba wana ukimwi. Wakati huo ndipo kinga yao ya mwili huwa ni dhaifu sana, na magonjwa alo nayo yanakuwa vigumu kuyatibu na ndipo hapo ukimwi unasababisha kifo.

Fahamu kuwa kila mtu hukumbana na viini ambavyo husababisha magonjwa, lakini kama kinga yako ni imara si rahisi kupata maambukizo na hata ukipata ni rahisi kuyatibu lakini kwa wale waishio na virusi vya ukimwi kinga yao huwa imedhoofishwa sana kiasi kuwa akikumbana na viini ni rahisi kwake kupata maradhi na hata akitibiwa inachukua mda kupona.

Lakini ni vyema kufahamu kuwa siku hizi kuna dawa spesheli kwa watu wenye virusi vya HIV ambazo hupunguza makali ya ukimwi. Dawa hizi husaidia kuzuia kuzaana kwa virusi vya HIV mwilini. Hata hivyo hadi kufikia sasa kwa hakika hakuna chanjo dhidi ya virusi vya ukimwi, na hakuna dawa ya kutibu Ukimwi.

Lakini kwa jinsi matibabu yalivyoimarika katika miongo michache iliyopita, inamaanisha kwamba maisha ya baadhi ya watu walio na virusi vya Ukimwi yanaweza kurefushwa kwa miaka kadhaa.

Jinsi maambukizo ya HIV yanavyotokea.

Virusi vya HIV husambazwa kwa njia zifuatazo:

 • Kufanya ngono bila kinga.
 • Kuchangia sindano.
 • Mama aliyeambukizwa anaweza kumwambukiza mwanawe wakati wa uja uzito, kuzaa au kunyonyesha.
 • Kutangamana kwa damu au majimaji mengine ya mwili – mfano damu iliyo na virusi ikipenya kwenye jeraha au mchubuko.
 • Kuongezewa damu iliyo na virusi.

Huwezi kuambukizwa virusi kupitia:

running character by Tayo

TAYO
 • Kupigana busu, kugusana, au kuamkiana kwa mikono.
 • Kutumia kwa pamoja vifaa vya kulia chakula.
 • Kukohoa au kwenda chafya.
 • Kuumwa na wadudu kama kunguni au mbu au wanyama.
 • kupitia Vidimbwi vya kuogelea.
 • Kula chakula kilichotayarishwa na mtu aliye na virusi vya ukimwi.

Dalili za virusi vya Ukimwi?

Watu wengi walioambukizwa virusi vya HIV, huwa hawafahamu kama wameambukizwa, kwa sababu hakuna dalili zinazotokea mara moja baada ya kuambukizwa.

Watu wengine hupata homa, vipele, maumivu ya viungo na uvimbe mgumu, lakini dalili hizi zinaweza kutokea kati ya wiki sita na miezi mitatu, baada ya kuambukizwa.

Hii ni kusema mara nyingi mtu aliyeambukizwa virusi vya ukimwi huenda asionyeshe dalili zozote, lakini tahadhari isipochukuliwa wanaweza kuwaambukiza watu virusi hivyo.

Matibabu ya kupunguza makali ya ukimwi

Bado hakuna tiba ya ukimwi, lakini kuna dawa spesheli ambazo zinaweza kusaidia waishio na virusi kwa kuimarisha afya hivyo basi kuongeza umri.

Nifanyeje kama nahisi nimeambukizwa virusi vya HIV?

Njia ya pekee ya kugundua kama una virusi vya hiv ni kwa kufanyiwa uchunguzi wa HIV.

Kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya HIV si vigumu.

Unachotakiwa kufanya ni kutembelea kituo cha afya ya uzazi au (VCT). Hapa utapata ushauri – Kisha kama uko tayari kuendelea na uchunguzi huo, Utatoa damu ambayo inapelekwa kufanyiwa uchunguzi, kuona kama ina virusi. Matokeo hayachukui muda mrefu kutolewa, na waweza kuyasubiri.

Tayo cartoon

TAYO

Pengine itahijitaji uchunguzi kama mara mbili tatu hivi kubainisha kwa yakini iwapo mtu ameambukizwa au la. Hii ni kwa sababu inachukua kipindi cha kama miezi mitatu kuanzia siku ya kuambukizwa kwa virusi kuweza kuonekana wakati wa uchunguzi.

Pengine swala la kusubiri kwa mda huu ndiyo sehemu ngumu zaidi ya utaratibu wa kuchunguza virusi vya ukimwi, lakini kusubiri kuna maanisha kwamba utakuwa na uhakika wa matokeo.

Huduma za uchunguzi wa virusi vya ukimwi zinapatikana kwa urahisi. Wasiliana na daktari wako au tembelea tu kituo cha huduma za afya ya uzazi kwa vijana kama vile VCT. Kama una wasi wasi kuhusu kuhifadhiwa kwa siri zako, usiwe na hofu.

Katika kliniki nyingi kuna utaratibu kabambe wa kuhifandhi siri za wateja. Haya yote utafahamishwa na mshauri wako, ikiwemo ni vipi uchunzguzi huo unafanywa, vipi utapokea majibu na hata kupata ushauri zaidi wa jinsi ya kuishi na virusi iwapo kwa bahati mbaya itabainika kuwa tayari umeambukiza.

Kumbuka Kama umefanya mapenzi bila kinga, ama unafikiria kuna uwezekano wowote kwamba umeambukizwa virusi vya HIV ni vyema kufanyiwa uchunguzi huo.

Usiendelee kuhatarisha maisha yako na ya wengine – Uamzi wa kwenda kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya HIV unaweza kuwa mgumu, lakini ni busara kwako na kwa wengine kutafuta usaidizi na ushauri wa kitaalam mapema iwezekanavyo.

Jinsi ya kuepuka maambukizi ya HIV.

 • Usijihusishe na ngono isiyo salama. Tumia kinga kila mara unapofanya ngono. Ukweli ni kwamba hakuna tendo la ngono lililosalama kwa asilimia 100. Kutumia kinga ni kupunguza hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV ukimwi, na magonjwa mengine ya zinaa. Kwa hivyo daima tumia kondom na uyafuate maagizo kikamilifu.
 • Usichangie sindano.

Jinsi mtu anavyoambukizwa virusi vya HIV.

Mtu huambukiwa virusi vya HIV kama kirusi cha HIV kitaingia kwenye mishipa yake ya damu, wakati majimaji yake ya mwili yatatangamana na yae ya mtu ambae tayari ameambukizwa.

Virusi vya HIV hupatikana kwa wingi kweye majimaji haya ya mwili wa mtu ambae tayari ameambukizwa.

 • Damu
 • Manii/ Shahawa
 • Majimaji ya ukeni, ikiwa ni pamoja na hedhi
 • Maziwa ya matiti

Kwa kawaida majimaji mwengineyo ya mtu aliyeambukizwa kama mate, jasho na mkojo huwa hayana idadi kubwa ya virusi, kutosha kumwambukiza mwingine.

Ndio sababu maambukizo ya virusi vya HIV hutokea zaidi kupitia ngono na aliyeambuzwa, kuongezwa damu iliyo na virusi, mama aliyeathirika kumnyonyesha mtoto, au kuchangia sindano na mwathirika nk. Na hali yenginezo kama hizo.

Wakati wa kufanya ngono virusi hivyo huweza kupenya na kumwingia mtu mwengine kupitia maeneo nyororo ya ukeni, uumeni, sehemu ya kupitisha haja ndogo na hata njia ya kupitisha haja kubwa kwa wale wanaotumia njia hiyo kufanya ngono.

Kufanya mapenzi katika hali ya kuwa sehemu za siri ni kavu huongeza hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV pamoja na magonjwa mengine ya zinaa.

Ngono kavu

Hii ni katika ile hali ya kufanya ngono ilhali eneo la ukeni halina ule unyevu nyevu wake wa kawaida. Hali hii huongeza hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV na pia magonjwa mengine ya zinaa. Baadhi ya watu, wana itikadi kwamba wanawake wenye unyevu unvyevu mwingi ukeni, wanapenda mno kufanya ngono hivyo basi ni mzinzi.

Ukweli ni kwamba wanawake kimaumbile hutoa majimaji hayo wakati miili yao inajitayarisha kufanya mapenzi. “Kuwa tayari kwa mapenzi” hakumaanishi kwamba uko tayari kufanya ngono na mtu yeyote tu! Na kama wanamke hayuko “tayari kufanya mapenzi”, na akaendelea na kufanya ngono kavu, (iwe kwa kulazimishwa au kwa hiari) husababisha maumivu makali kwa mwanamke, na kumsababishia pia kupujuka hali inayozidisha hatari ya kupata maambukizo.

Kuwa na Virusi vya HIV ilhali u-mja mzito

Hatari kwa mtoto wako

Imekadiriwa kwamba asilimia kati ya 25 na 45 ya wanawake wenye virusi vya ukimwi, na wamepata pia mimba, wanaweza kuwaambukiza watoto wao ambao hawajazaliwa. Kwa hivyo wanahitaji ushauri wa kitaalam na dawa spesheli ili kupunguza hatari kuwaambukiza watoto wao.

Virusi vya ukimwi vinaweza kusambazwa kutoka kwa mama mja mzito aliyeambukizwa, hadi kwa mtoto tumboni kwa njia tatu:

 • Wakati mtoto yungali tumboni mwa mama, ambapo virusi vinaweza kusambaa kutoka kwa mama hadi kwenye nyumba ya uzazi.
 • Wakati wa kujifungua, ambapo mtoto anaweza kuingiwa na majimaji ya ukeni au majimaji mengine kutoka kwa mama.
 • Wakati wa kunyonyesha, ambapo virusi vinaweza kuambukizwa kupitia maziwa anayonyonya.

Uwezekano wa kumwambukiza mtoto, wakati wa kujifungua ni mkubwa zaidi kama mama ana ujazo mkubwa wa virusi mwilini mwake na kinga yake tayari ni dhaifu. Kabla ya wanamke aliyeambukizwa kupewa usaidizi wowote wa kimatibabu kwanza atafanyiwa uchunguzi wa damu kuona kima cha virusi ndani ya mwili na hali yake ya kinga kwa ujumla.

Kama kinga yake itakuwa thabiti na idadi ya virusi ni ndogo mwilini, huenda hatahitaji dawa mpaka kipindi cha mwisho mwisho cha uja uzito yaani baada ya wiki ya 24.

Lakini kama ujazo wa virusi ni mkubwa na kinga mwili ni dhaifu, huenda italazimu kutumia madawa spesheli ya kupunguza makali ya ukimwi, mapema ili kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtoto.

Hatari ya kumwambukiza mtoto virusi vya ukimwi inaweza kupunguzwa hadi kufikia kati ya asilimia, moja na asilimia mbili tu kama hatua zifuatazo zitazingatiwa.

Kupata matibabu ya kupambana na virusi vya Ukimwi

 • Kwa sasa hivi hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba kutumia madawa ya kupambana na makali ya virusi vya HIV (ARV), kunamletea madhara mama na mtoto ambaye hajazaliwa.
 • Madawa ya kupambana na virusi vya ukimwi haswa AZT, yamethibitishwa kupunguza kwa asilimia kubwa, hatari ya mama kumwambukiza virusi hivyo mtoto wake wakati wa uja uzito .
 • Kama tayari unatumia madawa hayo ya ARV, kisha ukagundua kuwa u-mja mzito, mfahamishe daktari wako haraka iwezekanavyo. Kwa kawaida huwa ni vyema kuendelea na matibabu, lakini huenda ikakulazimu kubadilisha madawa. Kwa vyovyote vile, usisite kutumia madawa hayo bila ya ushauri na daktari.
 • Siku hizi inawezekana kupewa madawa ya ARV, ili kukabiliana na virusi vya ukimwi, kupitia kwenye mishipa ya damu wakati wa uchungu wa kujifungua. Inaaminika kwamba kufanya hivyo kunapunguza hatari ya kumwambukiza mtoto virusi hivyo wakati wa harakati za uchungu wa kujifungua.
 • Pia, ni kawaida mtoto wako kupewa madawa ya kupambana na virusi vya ukimwi ili kuzuia uwezekano wowote wa kuambukizwa.

Kuzaa kwa njia ya upasuaji

 • Ukichagua njia ya kuzaa kupitia upasuaji, yaani caesarean section kwa kimombo, kwaweza kupunguza kwa asilimia kubwa, hatari ya mama kumwambukiza mtoto wake virusi vya ukimwi.
 • Utaratibu huu humkinga mtoto asiingiwe na damu ama majimaji mengine ya mwilini na pia inamaanisha kwamba hutapata maumivu yanayoandamana na uchungu wa mda mrefu wa uzazi, hali inayoaminika kuchangia uwezekano wa mama kumwambukiza mtoto.

Kutonyonyesha

 • Inapendekezwa kwamba wanawake wenye virusi vya ukimwi wasiwanyonyeshe watoto wao bali watumie maziwa mbadala, kama ya ngo’mbe au maziwa maalum ya unga kwa watoto.
 • Hilo pekee linasadikiwa kupunguza hatari ya mtoto kuambukizwa virusi kwa kati ya asilimia 10 hadi 20.

89 Responses to Habari za Afya ya Uzazi

 1. salma says:

  sina comment yoyote ila natoa shukurani zangu kwa kutuelimisha jinsi gani unaambukizwa lakini sisi wengine bado hatuna waume na tayari tumeambukizwa sijuwi itakuaje maana bado hutujawa wazi katika hili

 2. piusmickys says:

  Pole sana Dada Salma
  Lakini si hoja bado kuna maisha hata kama umeambukizwa bado unaweza kuishi maisha marefu kama utatimiza yafuatayo:
  1. Kupima CD4 zako na kujua ziko ngapi
  2. Kuhakikisha haupati maambukizi mapya
  3. Kula vizuri mlo kamili
  4. Kufanya mazoezi na kuhakikisha hauchoshi mwili unapata muda wa kupumzika na kupunguza mawazo kwani wengi wanaathirika na mkengeuko wa mawazo na hili ni tatizo kubwa si kwa waliombukizwa badi linaathiri kiafya hata kwa wale ambao hawajaambukizwa msongo wa mawazo ni tatizo sugu. unaweza kuepeuka hili kwa kufanya yafuatayo:-
  1. Kujisomea vitabu vya hadithi
  2. Kuangalia sinema muda wa ziada
  3. Kujijumuisha na marafiki
  4. Kujishughulisha na kazi zozote za ujasiliamali au kusaidia nyumbani nk
  KAribu kwa ushauri zaidi dada Salma.

 3. CM says:

  Mi nauliza je inakuwaje kama mume wangu ameathirika na mi sijaathirika
  Nampenda Mume wangu na bado tunaishi pamoja anang’ang’ania tuongeze mtoto lakini najua hapo na mimi nitapata virusi nataabika sana ukiweza naomba email yako ili nikuandikie binafsi tutaelewana zaidi.
  Dada CM

 4. ally says:

  kwakweli nimefurahi sana kwa ushauri wako ni mzuri sana,mi naswali 1tu kwanini virusi vya onekana baada ya miezi 3 kwa nini sio baada ya mwezi 1 nilikuwa napenda unipe ujuzi kuhusu ili suala

 5. ally says:

  na nashkuru mungu nimepima zaidi ya mara tatu nimekutwa salama kabisa coz napenda sana kujua afya yangu

 6. piusmickys says:

  Bwana Ally nashukuru kwa kutembelea ukurasa huu.
  Kimsingi Virus vya ukimwi vinatofautiana kutokana na mahali hadi mahali, Sababu za kijiografia, kibailojia na kadhalika,
  Vile vile inategemea na Immune za mtu (uimara wa chembe hai kwenye mwili wako kupigana na maradhi).

  Kwanza elewa kuwa kuna tofauti kati ya Mtu mwenye Virusi vya Ukimwi na mtu anayeugua Ukimwi. unaweza kuwa na virusi vinavyosababisha Ukimwi na usiwe na mgonjwa wa Ukimwi.
  Upungufu wa Kinga mwilini ni matokeo ya chembe hai nyeupe kushambuliwa na kushindwa kuulinda mwili kutokana na aradhi. Yale maradhi ndio ugonjwa wenyewe.
  Nije kwenye swali lako:-
  Ndio Bw. Ally, virus vinaweza kuingia mwilini lakini suala la lini vitaonekana kama nilivyosema inategemea na uhimili wa chembe hai mwilini mwako lakini kwa Technolojia ya sasa unaweza kujua mapema zaidi kama mtu ameathirika va Virusi vya Ukimwi hata baada ya masaa 72 tangu ajamiiane au kuongezwa damu yenye virus vya ukimwi. lakini ndio maana kwa uhakika huwa wanataka kupima baada ya muda huo na wakati mwingine kuta kukupima mara tatu ikiwa na tofauti ya miezi mitatu mitatu.

 7. josephine says:

  nashukuru kwa ushauri wenu mzuri, lakini mimi nina swali ambalo linanisumbua sana nimepima 2007 nikaonekana nina virusi kwenye kituo kimoja hapa mjini iringa lakini mtu aliyenipima sikumuamini ata kidogo na hata vifaa alivyotumia kunipimia sikuvielewa kwakua mi nimuoga wa sindano sikuviangalia kwa muda ule lakini baada ya kunichoma nikaangalia sikuelewa kitu, nikamuuliza naweza kurudia tena kwa mara nyingine ili niwe na uhakika akanikatalia, minikaamua kwenda kupima sehemu nyingine nikaonekana sina, nikashangaa nikamua kurudi tena kwenye kituo cha kwanza baada ya miezi 4, sikumkuta yule dada aliyenipima nikamkuta muhudumu mwingine, sikupima nikaondoka, mpakaleo sipati jibu na nashindwa kuelewa inakuwaje. naomba ushauri na msaada wa mawazo kwasasa mi nimeolewa na ni mjamzito wa miezi 2, sijaanza bado klinic na sijapima tena toka nipate majibu ya mara pili

 8. piusmickys says:

  Josephine, ni case chache zilizoripotiwa kama zako, na ndio maana unashauriwa kupima mara tatu kwa interval at least ya miezi mitatu mitatu!!.
  Hii inakupa uhakika zaidi, ni vizuri kupima hasa wakati huu wa ujauzito kwani itakupa uhakika zaidi na kuchagua maisha ya kuishi, Mara nyingi watu wengi wanaogopa kupima na wengi wao wakipima wanajikuta wako salama, Kupima kutakupa uchaguzi wa maisha yako, mumeo na mtoto mnayemtarajia.
  Kwa ushauri wangu ni vizuri ukapime, kama sehemu hauiamini jaribu kwenda kwenye kituo kingine kwani kwa sasa kuna vituo vingi vinavyotoa ushauri nasaa na kupima.

 9. Hilda says:

  Kaka Pius, Nimependa jinsi unavyotusaidia hasa ktk huu ugonjwa.
  Mimi nilipima VVU wakati nikiwa mja mzito na kwa bahati mbaya ilithibitika kuwa nimeathirika. kwa wakati huo nilikuwa na mimba ya miezi 4, nilikuwa na CD4 112, kwahiyo nilianza kutumia ARVs kipindi hicho. Nilijifungua kwa oparesheni, na sikumnyonyesha mtoto kabisa. Mtoto ameshafikisha mwaka 1 sasa na kwa kweli hajapata tatizo lolote na anaendelea vizuri kabisa. Nina hofu sana kama atakuwa hajaambukizwa virusi? kwa vile CD4 zangu zilikuwa chini sana. Daktari anayenihudumia kwa mtoto alinishauri nisubiri mpk mtoto afikishe miezi 18 ndo nikampime. We unasemaje kwa hilo kaka Pius?

 10. piusmickys says:

  Dada Hilda kwanza nashukuru kwa kutambua msaada wa maelezo yangu.
  Pili napenda kukupa hongera kwa kujifungua na mtoto kufikisha mwaka mmoja.
  Ni kweli kuwa kitaalamu mtoto anaweza kugundulika kama ana virusi ama la akiwa na miezi 18, mwaka mmoja na nusu, Kwani kuanzia muda huo mtoto anakuwa na kinga zake mwenyewe tegemezi ambazo kwa kiasi kikubwa kama ameathirika ni rahisi vipimo kuonyesha.
  Sio tuu kumnyonyesha bali kuna njia nyingine ambazo kama hautkuwa muangalifu pia zinaweza kumuambukiza mtoto, Ni kawaida kwa mama Kuonyesha mapenzi kwa mtoto lakini unapokuwa kwenye hali ya kuishi na Virusi vya Ukimwi inabidi uwe muangalifu, wakati mwingine unaweza kuwa na kijipele ambacho kikitumbuka uwezekano wa kutoa damu au maji maji ni mkubwa na ikumbukwe kuwa ngozi ya huyu mtoto bado ni laini na hivyo inaweza kupata mchubuko kirahisi wakati mwingine hata na nguo au kutegemeana na utundu wa mtoto. Kama hilo linatokea jaribu kuwa muangalifu hasa napomkubatia mtoto na kadhalika.
  Hii itasaidia kumlinda mtoto na Contamination ya aina yeyote.
  Vinginevyo na kupongeza kwa kuniandikia na usikate tamaa

  Pia kumbuka kula vyakula vya kujenga mwili mboga mboga na nyama nyeupe (samaki au Kuku).
  Fanya mazoezi hata kwa kutembea tu unaweza hata kushuka kituo kimoja na unapokwenda kwenye daladala kama umbali si mrefu, usifanye sana mazoezi ukauchosha mwili.

  Jiangalie ujikinge na magonjwa yanayoepukika yanayoweza kupunguza kinga zako za mwili kama Malaria, Mafua, Kifua kikuu na mengineyo.

  Fuata maelekezo ya dawa kama unavyoambiwa na Dr. na usibadilishe muda wa kunywa dawa labda inapobidi sana kama unakwenda nje na nyumbani pendelea kuweka tembe kadhaa kwenye Pochi yako ili usiweze kupitisha kunywa dawa. na Pia usibadili aina ya Dawa bila ushauri sahihi wa Daktari.

  Kama kuna jingine ambalo huwezi kuandika hapa nitumie email: piusmicky@yahoo.co.uk

 11. Anonymous says:

  Nisingependa kutaja jina langu hapa lakini tatizo langu liko sawa na huyo dada hapo juu nami nina mtoto wa miezi 6 sasa asante nimepata point kwenye maelezo yako ambayo pia zilikuwa zinanitatiza. Kingine ndugu zetu hatujawajulisha kuwa tuko kwenye hali hii kwani tumetoka kuoana mwaka mmoja uliopita lakini mume wangu bado analazimisha tusitimie kinga nifanyeje?

 12. piusmickys says:

  Dada yangu nashukuru kama umepata Point mbili tatu. Naomba pia uzingatie hayo niliyoyasema pia unaweza kusoma majarida mbali mbali na kusikiliza mara kwa mara kipindi cha Kimasomaso ambacho huwa pia kinachambua habari mbalimbali kuhusu UKIMWI.

  Pili nasikitika kuwa mume wako bado “ANAKULAZIMISHA” kufanya mapenzi bila kinga, hii ni hatari sana kwenu wote wawili, kwani inafanya mnazidi kupata Maambukizi mapya ambayo kwa hali ya mtoto mdogo utafupisha siku za kushi.
  Nafikiri mshauri mumeo muende kwa mshauri nasaha na anahitaji kupatiwa ushauri nasaha, Mara nyingi wanaume huwa hawapendi kwenda sehemu kaama hizo ila kwa vile ni mumeo unaweza kutumia njia mbadala na ikiwezekana ongea na Dr. kwanza muelezee hali halisi kabla ndio uende na mumeo ila Dr/Mshauri ajue ni nini cha kusema na wapi ahimize. Kumbuka hii kwa ajili ya Maisha yenu na Mtoto wenu ikizingatiwa ndio kwanza mna mwaka mmoja kwenye ndoa yenu.

  • hilda says:

   Naomba nisitaje jina langu hapa, nipo kwenye ndoa zaidi ya mwaka sasa, ni wiki moja tu imepita tangu tulipopima VVU, na mume wangu amekutwa na maambukizi.
   Hatujapata mtoto bado na tunahitaji sana mtoto.Je, kuna uwezekano wa kupata mtoto bila mimi na mtoto huyo kupata maambikizi yoyote?

 13. KSA says:

  Nimependa maelelekezo uliyonipa kupitia Email nimeweza kumshawishi na tumekwenda kupima nashukuru sana tena sana Mungu akujalie sana kwa ushauri ulionipa kama nilivyokwambia nimekuta ameathirika na kama nilivyokwambia mwanzo sikuwahi kufanya naye tendo la ndoa kwani ndio alikuja likizo ili tuongelee mipango ya ndoa yetu baada ya kufahamiana kwa mwaka takribani mmoja.
  Nimeona niandike hapa kama ulivyosema kwa faida ya wengine, tusiamini mtu kwa kumuangalia jamani huyu kaka Pius alinishauri niende kupima kamba hatujafikia kwenda kwa wazazi na kweli nimekuta mchumba wangu ameathirika hivyo jamani msipuuze.
  Mimi KSA
  Ngarenearo – Arusha

 14. maisha says:

  mimi naogopa kupima huwa nasemanitaenda lakini sijaenda,mpaka nilipata safari ya Ulaya, mpaka sasa ipo huku. nauliza je kubabuka mdomo wa chini inaweza kuwa dalili? sivuti sigsra, tangia nitoke Africa huu mwaka na nusu sijawahi kufaya tendo la ndoa. je hiv husababisha dalili hizi za kubabuka mdomo?

 15. samir says:

  mimi naonaona unajidaganya na unadaganya jamii,uko ulaya,kwanini usipime ukajua? wakati huku kila kitu kipo na wanacho jali sana ni afya utakaaje siku zote hizo bila pima? ulishajua ukimwi si lazima kutiana ,kuna njia nyingi ambazo wewe unaweza kupata nenda pima ujue tena ulaya ndo poa hakuna hata gharama ya matibu wala ya upimaji yote bureee.

 16. Anonymous says:

  Mimi naitwa Fatma au mama Fety na London wa Moshi University naomba mtupe njia au vyakula vya kula ili mtu aweze kupunguza uzito

 17. Anonymous says:

  mimi ni mama fetty na london nifanye nini ili niweze kupata mtoto wa kiume nimejaza mijike

 18. piusmickys says:

  Mama Fetty Kwanza nashukuru kwa kutembelea Blog yangu
  Kuna njia nyingi za kupunguza uzito ila moja wapo ni kubadilisha vyakula na kufanya mazoezi.
  Lakini kwa sababu umeulizia zaidi vyakula inaonyesha kuwa umelijua tatizo lako (hehehee)
  Kwa haraka haraka vipo vitabu vingi sana vinaongelea mlogani muafaka ila kwa leo naomba nikupe Article hii:

  “I Cut Down on Junk Food and Lost 70 Pounds”

  How Christi Lee Palas triumphed over a pantry full of junk food, upped her exercise, and lost 70 pounds.

  By Charlotte Latvala
  Getting Out of Junk Food Paradise

  Name: Christi Lee Palas
  Age: 22
  Height: 5’8″
  Weight: 145 pounds
  Pounds Lost: 70
  At Current Weight: 4 years

  Christi Lee Palas grew up in a junk-food paradise. “My mom kept the kitchen stocked with chips and ice cream,” says the MBA student and Pittsburgh native. “If it was in the house, I ate it. So did my brother and sister, and all three of us got huge.” By the age of 18, Christi weighed more than 200 pounds.
  A Takeout Diet

  Extra heft was an asset on Christi’s high school softball team (helping her hit the ball farther), but she was always conscious of her size. “The coach only ordered one or two larger uniforms, and I was afraid I wouldn’t get one, since there were several bigger girls on the team,” she says. Practicing four days a week wasn’t enough activity to burn off the takeout or spaghetti she’d eat afterward. Still, Christi didn’t realize how heavy she was until she got weighed for her physical in February of her senior year. “Usually, I would glance away from the scale. But this time I looked and was shocked to see it read 215 pounds,” she says. “I thought, What will I be in 20 years — 300?”
  Changing Her Exercise Regimen

  Christi was motivated to start walking to and from school and around her neighborhood: four and a half miles a day. “By May, I could fit into size 18 jeans again, instead of just wearing sweatpants,” she says. Then she reduced portion sizes and cut out soda, high-fat condiments like mayo and butter, and fast-food standbys like General Tso’s chicken. When she weighed herself again in September, she discovered that she’d lost almost 40 pounds. Inspired, she hit the campus gym for 40 minutes four times a week and added weight training to her routine to drop another 30 pounds by the end of her freshman year.

  Now a grad student, Christi has kept the weight off and maintained the same size for four years. In addition, she’s been a mentor to brother Caleb, 21, and sister Brandi, 25 — they’ve lost nearly 100 and 30 pounds, respectively. “We trade fitness tips and go on hikes together now, instead of eating junk food in front of the TV.”

 19. Dear says:

  mimi nilipima mwaka elfu mbili nilikutwa mzima na tangu hapo sijafanya tendo la ndoa na ninaogopa mno mno. niko masomoni nategemea kumaliza mwakani ili nirudi nyumbani na kufunga ndoa na mchumba wangu. Sasa huyu mtu hatujawahi pima wala kufanya naye tendo la ndoa, wala kuzungumzia swala la kupima je ni vibaya nikimshawishi tukacheki afya zetu kabla ya mambo yote kuanza. maana mimi naogopa sana sana ugonjwa huu.
  dear

 20. piusmickys says:

  Ni uamuzi wa busara kupima kabla ya Ndoa.
  Maranyingi vijana tumekuwa na kasumba ya kupima kwa macho na kujipa moyo kwa kudhani mtu mnene yuko salama!! La hasha vipimo vya hospital ndio sahihi na at least mnapima mara tatu kuwa na uhakika zaidi.

  Nakushauri endelea kujitunza na kumshauri mpenzi wako mpime kabla ya ndoa kwa uhakika wa usalama wenu na kiumbe mtakachojaaliwa hapo baadaye kama mk na mume,
  Hiyo inakupa uhuru zaidi na kupanga maisha yenu na mpenzi wako, Inakupa uhakika wa maisha na kukuondoa wasiwasi zaidi.

  Nakutakia kila la heri kwani kwenye hoja yako mkazo wangu ni kukusihi mpime kabla ya ndoa.

  Pius

 21. Anonymous says:

  Kaka salama?
  Mimi nina swali moja nina miaka 24 nimekuwa nikipiga nyeto almost three years now, kwangu mi naona ni njia salama ya kupuguza hamu zangu na kwa sasa napiga hata mara 2 au tatu kwa siku, Je ina madhara yeyote hii? Naomba unisaidie isije ikawa najipalilia moto bure
  B.M

  • Denis kamagi says:

   kaka me nilivyosikia masterblation inaifanya misuli ya uume kukomaa na hivyo kukuletea madhara pindi utakapotaka ku do kwasababu tayari itakuwa imezoea kitu kidumu kama kiganja lakini ile sehemu ya mwanamke ni laini sana so ni vema ukaacha.

 22. piusmickys says:

  Duh kaka BM
  Asante kwa swali lako.
  Katika hali ya afya bado sijawah kusoma mahala kwamba kuna effects za moja kwa moja, lakini ki saikolojia hilo lina utata kwani mara nyingi nimewahi kusikia kuwa mazoea ya kujichua yanapelekea kuwa na riziko la nafsi kila mara ucheuapo, hii upelekea kutuliza hamu zako kwa njia ya mkato, sasa utakapo kuja kuwa na mahusiano ndani ya ndoa akili yako inakuwa imejiweka kuridhika kila ucheuapo na hivyo kukufanya kuwa mnyimi kwenye tendo zima la ndoa ambalo maratajio yake ni kuwaridhisha nyote wawili.

 23. kareni says:

  Mimi ni msicha mwenye umri wa maka ishini na moja naishi mkoa wa Klimanjaro Moshi nilibeba mimba ikafikisha miezi minne ikiwa imeharibika nikatoa mpata sasa damu zinatika mpaka sasa ni vipaya naomba ushauri wako naomba unisaidie ilikuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka jana

  • piusmickys says:

   Dadaa Karen
   Kwanza pole sana, inaelekea umepatwa na tatizo, matatizo ya namna hiyo ysnasababishwa na mambo mengi inategemea na kwanza historia atakayotoa mgonjwa mwenyewe pili vipimo baada ya uchinguzi. Kwa kuwa hilo ni la kitaalamu zaidi
   Nakushauri haraka uende hospotal na umueleza Daktari tatizo lako atakusaidia. Pole sana

 24. Anonymous says:

  tunakushukuru sana kaka kwa kutuelimisha, hapa nimejifunza mengi, mie naswali langu naishi na mtu aliye tayari kuambukizwa na choo chetu nikile cha kukaa je mtu huyo hawezi kutuambukiza sie wengine?

 25. Habari za afya ya uzazi.. May I repost it? 🙂

 26. usp says:

  can you go in to greater depth with this particular content? i would certainly like to study a lot more about it, specifically the 2nd part

 27. Oliver maina. says:

  je nauliza hivi kuhisi mwaasho sehemu za siri ni dalili za ukimwi?

 28. Caroline says:

  Samahani Mimi naomba kutoka nje ya mada . Swali langu ni kwanini mama mjamzito uvimba miguu au wakati mwingine mwili mzima? Naomba usioweke e-mail yangu hasante

 29. anita mbigu says:

  daktari mm nimekuwa muoga kwenda kuchec hiv na isitoshe nimeshawahi kusexy bila kinga na kuugua ugongwa wa zinaa

 30. Anonymous says:

  pole sana Anita usiwe mwoga juu ya kucheck afya yako ukishajua Afya yako itakusaidia kujilinda zaidi tafadhali nenda katika kituo cha Afya na ucheck Afya yako.

 31. Denis kamagi says:

  Mdudu anayeeneza ugonjwa wa kisonono anaiteaje?

 32. John's to't says:

  Natakakujua njiaambazo zinaweza kueneza ungojwa wa kisonono

 33. Iddi mafta says:

  Nashukuru sana kwakuelimisha watu

 34. DVD says:

  Nimekuwa mwenye furaha sana, kwa kuingia kwenye blog yenu. Nimekuta mambo mengi ya mafunzo, basi nawatakia la heri.

 35. Rodrick al says:

  Naweza sex na mwanamke mwenye vvu nisipate vvu sababu nyingine ukiacha ya ukavu ukeni na kama nina vvu kuna ulazima wa kunywa dawa…

  • Brown tinda says:

   Mie napenda kutoa ushauri ni kwamba watu wote tupende kwenda kwenye vituo vya afya ili kucheki afya zetu kwani kufanya hivyo inatuweka kuwa salama wakati wowote na kujiamini,mungu atusaidie atuepushe na janga hili.

 36. Anonymous says:

  je ukimwi unasababisha mimba kutoka?

 37. sety sanga says:

  Thanks for this education

 38. Anonymous says:

  MI NAULIZA , HIV IMEGAWANYIKA KTK AINA NYINGNE NDOGONDOGO? MAANA NIMEWAH SIKIA HIV C, HIV F…nk

 39. Marwa Nyabuchigira says:

  Mimi Kwajina Naitwa MARWA NYABUCHIGIRA mtazamo wangu ukimwi ndio unaogopeka hapa dunian lakini hawajali unambiwa fuata nyuki ule asali matokeo yake unapata ukimwi nimezaliwa serengeti mara katika kijiji cha kisangula tujirinde na ukimwi

 40. andrew says:

  nikweli mnafundisha jaman tuache ngono zembe

 41. kwahiyo virus can be transfered through viginal vapour but not blood only.?

 42. ag says:

  jaman mi naogopa kwenda kupima tena nikisikia swala la ukimwi natetmeka kabisa nifanyaje jaman nateseka?

 43. Annie says:

  Well done!!

 44. Adams says:

  nashukuru kwa mafundisho mazur

 45. Pascal Bujimu says:

  Asante kwa wako ushauri

 46. bacar says:

  shkran sana kwa elimu yenu,

 47. bacar says:

  shkran sana kwa elimu yenu,
  nimepitia matukio kama mawili ya ngono zembe napata hofu sana nikitaka kwenda kupima ,naomba ushauri.

 48. Johnson says:

  Asante sana dr. napenda kuuliza hv.. unaweza kutambulika mda gan baada ya kusex na muathirika wa VVU

 49. niko says:

  nakua na wasi wasi pale mtu akinitemea mate au kubadilishana mate mabaki ya chakula nikiwa nakula nae sasa najiuliza naomba msaada kama ana UKIMWI na mm nitaupata?

 50. zaujiare says:

  yn ukimw unaogopesha waambukizaj hasa ni vbaba vynye hela zao kwnda kwa mtt wdago nawachukia sana

 51. Mlyani wa mwanza says:

  Ahsante dr.kwa maelezo yako,hakika unaelimisha BY JOSEPH MLYANI

 52. Anonymous says:

  Uncle ningependa kujua kwa mfano mtu umeenda kupima kwa mara ya kwanza ukaambiwa umeathirika kuna haja tena kurudia hizo mara tatu

 53. Anonymous says:

  Hivi mfano mtu ukiwa unamiwasho sehemu za siri ni dalili za HIV ukiwa ushapima kaswende, kisonono na huna.?

 54. angela john says:

  Dr ninasumbuliwa na kuharisha na kuwashwa na mwiii na pia kusikia vitu vikitembea kuelekea moyoni na moyo kuuma sana na kutoka vioele jifuani,nilipima full blood picture nikaambiwa kinga zangu zimeshuka sana zilikuwa ni 1.1mm3.Ukimwi sijapima naogopa je hizi zaweza kuwa nidalili za HIV?

 55. Job Richard says:

  Ahsanteni kwa elimu yenu nzuri

 56. Emmanuel Ochieng says:

  thankz 4r ur advice.

 57. Agnessy Bern says:

  Habari za kazi Dr. kiufupi nimecheki afya na kujikuta nimepata tatizo la maambukizi ya Virus vya Ukimwi. Tatizo kubwa lipo kwa mwenza wangu maana siri si nzuri, baada ya kupata majibu nilimjulisha hali ambayo nimekutwa nayo lakini ana wasiwasi mkubwa je unanishauri nifanye nini ili awe katika hali ya kawaida. A.B From
  Njombe

 58. Abigail says:

  Asante sana unatusaidia wengi sana kwa majibu yako mazuri, tutawasiliana zaidi kwa email

 59. Mponeja D Ntugwa says:

  Ukweli Wangu Mm Siyo Mtaalam Lakini Na Kiswahili Changu Kutoka Bara, Kuhusu Mambukizi Ya Vvu Yaani Njia Za Mambukizi Zipo Zingine Ambazo Wataalam Wanazikanusha Kwa Mfano:kuchangia Sabuni,dodoki,mawe Ya Kuogea,vyombo Vy Kuogea,vyombo Vya Kulia,kunywea, Chakula Alichoandaa Mgonjwa Km Maziwa Ya Ng’ombe Na Chakula Kingine Kama Mgonjwa Atajikata Na Kutoa Damu Na Kuchanganyikana Na Chakula Hicho,halafu Kuhusu Kuandaa Mgonjwa Maziwa Ng’ombe Huambukizwa Virusi Hivyo Familia Au Mtu Yoyote Akitumia Mazw Hupata Vvu Na Kama Watatumia Watu Wengi Kwa Mkupuo Tayari Wana Vvu Na Hiyo Mimi Nimeona Kwa Macho Yangu Koo Zinateketea Hadi Vijiji Siku Hizi Watu Wanapata Vvu Bila Kujua Kautoa Wapi Usihangaike Ulitumia Vitu Hapo Juu. Virusi Ukvichemsha Havifi,labda Utumie Murefu.Kote Duniani Tutakwisha Kama Hawajagua ,hilo.Ahsante Anayebisha Anitafute Nimpeleke Walikoambukizwa Hao Ng’ombe Kwa Namba Kubwa Na Wananchi Wanavyofurukuta Vvv Kwa Namba Kubwa.Hakikisha Uje Na Dkr.Nitafute 0716043836.

 60. habali zenu wapendwa mimi naswali kidogo, nihivi niugua fangus sehemu za sili nimetumia dawa hila sasa nimepona lakini nakua mkavu sana na sipati hamu ya tendo nifanyeje na huku nilipo pemba hakuna ma doctar wa kunitibu naomba msaada plz

 61. Anonymous says:

  hv,chanzo cha ukimw ni nin hasa,hv ni kwel dawa imepatikana,au watu wanafanya biashara tu.

  • Anonymous says:

   Habar zenu jaman,ninaitwa ally husein,nilikutana na na mtu mweny virus nilipoenda kupima baada ya miez mitat sikuonekana na tatz.baada ya miezi sita nikapimwa kwa kutumia unigol hakukuwa na tatz.mwanzon wa mwez wa saba nikajipima mwenyewe kwa kutumia detamine test.ikaonyesha mistar miwili.lkin ule wa patient umefifia sana.je nitakuwa na maambukiz.??naomben jib ndg zang

 62. micky says:

  jaman naombeni ukishajua una ugonjwa wa ukimwi usisambaze chakufanya pata mwenzio mwenye ukimwi achana na wazima ok

 63. Habari yako, samahan eti mtu anaweza kukaa zaid ya miez mitatu bila kuona dalili yoyote ya ukimwi?? Mafua yasiyopona ni dalili ya ukimwi??

 64. Anonymous says:

  mfano ume fanya ngono lkn ukapata goli mojatu kwa mariziano je hapo waweza kupata ukimwi

 65. Anonymous says:

  Nafurah kwa maelezo dock swali mate yanaweza kuambukiza ukimwi

 66. habby says:

  nashukulu kwa kutuelimisha nipo nje ya mada nilikuwa nauliza siku yangu ya kupata hedhi tarehe 14 namaliza tarehe 16 je sku ya hatari kupata mimba ni hipia

 67. Anonymous says:

  Kwel kabisaa by a.mukandala

 68. dan po says:

  asante

 69. Anonymous says:

  Sitaki Nitaje Jina Langu ,dr Mim Nikijana Mwe Umri 23 Nimetembea Na Mama Mwenye Vvu zaidi ya kumi na mbili Na Mwisho Nikakuta anatumia vidonge vyaARVs ndipo nikaamua kwenda kupima ,sasa inachua miez mitano sijakutwa na maambukizi ya ukimwi,je nikienda kupima mara ya tatu naweza kukutwa na vvu?maana sina raha kabisa juu ya msahala huu,naomba ushaur wako dr .

 70. Frank says:

  Dr Naomba Ushauri Wako Mm Nimetembea Na Mwanamke Anaetumia ARV Na Nimepima Mara Mbili Sijagundulika Na Maambukiz Yeyote, Na Tangu Niache Kufanya Mapenz Na Mama Huyo Sasa Inachukua Muda Wa Mwez Sita Je Nikienda Kupima Naweza Kukutwa Na Vvu,hata Hivo Nafsi Yangu Inakosa Raha (msongo)tangu Nipite Mahali Pabaya Huwa Najihis Kuwa Mim Niwakufa Tu!

  • Hussein Rashidy says:

   Dr. Pole na kaz naomba kuuliza mtu mweny dalili za ukimwi anaweza kumwambukiza mwengne akiwa yey ndy yupo stage za kwanza

 71. Sarah says:

  Naombeni Ushauli Mimi Nimeolewa Ila Kila Mwezi Napata Siku Zangu Tarehe 3mpaka 7 Na Mwezi Mwengine Napata Tarehe 3 Mpaka 7 Alafu Ikifika Tarehe 27 Nazipata Tena Asa Nashindwa Kuelewa Na Mda Mwengine Nakuaga Nakosa Mwezi 1alafu Ikifika Tarehe 19 Napata Nakuna Mda Mwengine Na Kuna Siku Moja Nimejistukia Nanatoka Uchafu Mzito Warangi Nyeusi Asa Naombeni Ushauli

 72. maria says:

  kwakwer nimekifatilia kipindi chako kwa uzuri zaidi Doctar mm naomba ushauri nimdada nilieolewa tokea niolewe Nina kama miaka 3 tulibahatika kupata motto mmoja ila kwa sasa huyo motto ana miaka4 na ivi salsa ni mjamzito wa miez5 nikaenda hospital kuanza klinik mimba ikiwa name miez minne na kwa bah at mbya nikapima HIV nikakutwa nimeathilika dicta nikalud kumwambia muwe wangu atak kabisa kwenda kupima doctar nimeumia sana kwann atak kwenda kupima je nikijifungua nimnyonyoshe iyo miez sit a mana naopa Doctar naomba ushauri wko

 73. Anonymous says:

  kwakwer nimekifatilia kipindi chako kwa uzuri zaidi Doctar mm naomba ushauri nimdada nilieolewa tokea niolewe Nina kama miaka 3 tulibahatika kupata motto mmoja ila kwa sasa huyo motto ana miaka4 na ivi salsa ni mjamzito wa miez5 nikaenda hospital kuanza klinik mimba ikiwa name miez minne na kwa bah at mbya nikapima HIV nikakutwa nimeathilika dicta nikalud kumwambia muwe wangu atak kabisa kwenda kupima doctar nimeumia sana kwann atak kwenda kupima je nikijifungua nimnyonyoshe iyo miez sit a mana naopa Doctar naomba ushauri wko

 74. elizabeth says:

  kwakwer nimekifatilia kipindi chako kwa uzuri zaidi Doctar mm naomba ushauri nimdada nilieolewa tokea niolewe Nina kama miaka 3 tulibahatika kupata motto mmoja ila kwa sasa huyo motto ana miaka4 na ivi salsa ni mjamzito wa miez5 nikaenda hospital kuanza klinik mimba ikiwa name miez minne na kwa bah at mbya nikapima HIV nikakutwa nimeathilika dicta nikalud kumwambia muwe wangu atak kabisa kwenda kupima doctar nimeumia sana kwann atak kwenda kupima je nikijifungua nimnyonyoshe iyo miez sit a mana naopa Doctar naomba ushauri wko

 75. rey says:

  Dr mi naomba ushauri wako nlikua ktk uhusiano na mpenzi wng lkn kwa sasa atuko pamoja ni km mwaka sasa umepita!.lkn sasa nmempata mpenzi mwingine tumepanga kuoana miez michache ijayo lkn mi nkaona vema nkapime kabla atujafanya chochote mana nlikua na wasiwasi na mpenz wng wa mwanzo bahati mbaya nmekutwa na maambukizi ya UKIMWI!sasa nashndwa kumwambia mchumba angu mana tunapendana aswa moyo wng unaumia mno kumkosa jmn na nna hamu ya kuolewa na kupata watoto ushauri wako Dr pls!!!!!naomba km utaeza unijibu ktk email yng Dr.

 76. Nissah says:

  Je maziwa ya mama aliyeambukizwa yakimgusa mtu mwenye mchubuko, mtu huyo anaweza kuambukizwa na yeye?

 77. brenda says:

  Nashukuru sana kwa ushauri wako. Mm nipo kweny mahusiano na mpenz wang tumeenda kupima mm sina na yeye ni hiv positive, nampenda ila naomba kukuliza inawezekana kuwa nae bila kupata maambukizi? Na njia zipi ni Salama zitazonisaidia nisipate maambukizi? Je naweza kuendelea kuwa nae na tukapata watoto wakiwa hawana maambukizi?

 78. Maige Herry says:

  Nashukuru kwa elimu ni watu wachache wanao elewa kutofautisha kati ya UKIMWI na VIRUSI VYA HIV

 79. ramia says:

  mm nimetembea na mwanamke alie adhirika nimepima sina lakini ninamawozo mpaka mwili unaishiwa nguvu nimekonda nifanyaje

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: