Tour Eiffel ya Wenge BCBG na Weekend njema

Moja kati y wanamuziki wa Wenge ya JB Mpiana ambao waliondoka na bado nawalilia Allain Mpela, Huyu bwana alikuwa anauwezo mkubwa si tu wa kutunga bali alikuwa anakarabati Verse, yaani wimbo ukitungwa wakisikilizishana yeye huwa anazirekebisha na akirekebisha na kuzitengenezea mtiririko wa sauti hakuna anayepinga na moja ya albamu ambazo alishiriki kwa kiasi kikubwa kuiratibu ni hii ya Titanic (Titanike) ambayo waliitoa baada ya kuparaganyika na akina Werason na wao kuunda WMMM.

Japokuwa wimbo huuu ulitungwa na mpiga drums maarufu Titina Alcapone ukisikiliza beti ya Allain Mpella Afande utakubaliana na mimi kuwa alikuwa jembe, msikilize kuanzia 3:20 kisha unipe maoni yako.

Mwingine ambaye kwa sasa mepotezwa kabisa na hajawahi kuwika tangu atoke kundini ni Aimelia Lyase Doming’ong’o ambaye kwa kiasi kikubwa JB Mwenyewe ameweza kuziba pengo lake kwa kuimba sauti yake ingawa ya Aimelia ni kali na nyembamba zaidi lakini pengo lake haijaonekana sana.

Wimbo huu ni kwenu Jay Single Suvereigh Mukullu, Papaa Mabamba Maregesi pamoko sana mkuu (Full Mzaire), Papaa Julie We Ston Presidaa Bana Kongolee na Darisalama, Papaa Sultan ndani ya jiji la Dar, Engineer Mboneka Mwana BCBG, Juma Mukulu nakati ya Airport, Hadji Le BeeCeeBeeGeeque Nambari wani, Mapenzi Club tuko pamoja, Muzee ya Tunduma sina haja ya kukutaja, Papaa na kati ya Muscat unajijua, Wenge BCBG Arusha Club pamoja sana.

Weekend njema.

Advertisements

5 Responses to Tour Eiffel ya Wenge BCBG na Weekend njema

 1. Anonymous says:

  mdau hii TOUR EIFFEL ule mnara mkubwa uliopo paris ndio umeimbwa hapa UKIWA NI UTUNZI WA titina alcapone, Sio SERGE PALMI ambapo ameimbwa mtoto wa mjini mmoja anaejulikana pia kama play boy de brussels

 2. Anonymous says:

  Mdau hapo hujaeleweka, vizuri unamaanisha nini? Papa Pius ameeleza vizuri, na huo Serge Palmi ni utunzi wake Burkina faso Kasongo.

 3. Shaibu Mwambungu says:

  Papa Pius Natafuta Lyrics yake kwenye Maktaba yangu nikipata nitaitandika hapa barazani Shaibu Thabit Mwambungu – Mbinga,Ruvuma

 4. Cora Downy says:

  a great deal of good facts and inspiration, each of which I want, because of give this kind of a beneficial details right here.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: