Queen Suzy avishwa pete ya Uchumba!!

May 29, 2009

DSC02238

Mnenguaji wa FM Academia Queen Suzy ambaye kwa sasa yuko Malaysia ziarani na Bendi ya The Kilimanjaro Connections amepata mchumba ambaye anatarajia kufunga naye ndoa baadaye mwaka huu. Suzy ambaye amevalishwa pete ya uchumba na Mchumba wake huyo raia wa Uingereza anayeishi na kufanya kazi nchini Malaysia.

DSC02239

Awali Queen Suzy alivalishwa pete hiyo kwenye sherehe ndogo iliyofanyika kwenye Jengo la KLCC na kuhudhuriwa na baadhi ya Wanamuziki na marafiki wa karibu wa pande zote.

Suzy anatarajia kurejea nyumbani baadaye mwezi ujao baada ya mkataba wao kumalizia na amesema mchumba wake pia anatarajia kwenda Tanzania mwezi July ambapo taratibu nyingine zitafuatwa.

Suzy ambaye yuko Malaysia tangu mwezi wa december mwaka jana akiambatana na wana mkorogo, pia amepiga mafanikio kwenye sekta nzima ya muziki kwani kwa sasa pamoja na kucheza pia ameanza kuimba chini ya gwiji muimbaji mkufunzi Delphinus Mununga (mdogo wa marehemu Kasheba), “kwakweli nafurahi mafanikio yangu kimuziki ningependelea kuimba zaidi kwani sasa nakiona kipaji changu cha muziki” alisema Suzy alipokuwa akiongea nami katika kiota chao cha Rum Jungle.

DSC02147

Queen Suzy akiwa na mpenzi wake kisiwani Lang’kawi-Malaysia.

DSC02139


Nawapa shavu wazee wa Ngwasuma….!

September 8, 2008
Waimbaji wa FM wana Ngwasuma wakiwajibika Jukwaani kijiji cha Makumbusho

Waimbaji wa FM wana Ngwasuma wakiwajibika Jukwaani kijiji cha Makumbusho

Either Hot or Not!! Jamaa wako juu, Mukubwa Maghambo tuko pamoja?

Either Hot or Not!! Jamaa wako juu, Mukubwa Maghambo tuko pamoja?

Pamoja na kuibuka Bendi nyingi bado Wana ngwasuma wanatamba na kujaza mashabiki lukuki, Pichani ni Wanamuziki na wachezaji shoo wakiselebuka na kupagawisha vilivyo kwenye kijiji cha Makumbusho. Picha zote kwa hisani kubwa ya Dar411.com

Pamoja na kuibuka Bendi nyingi bado Wana ngwasuma wanatamba na kujaza mashabiki lukuki, Pichani ni Wanamuziki na wachezaji shoo wakiselebuka na kupagawisha vilivyo kwenye kijiji cha Makumbusho hivi kribuni. Picha zote kwa hisani kubwa ya Dar411


King Blaise si huyu!

August 25, 2008
FM Academia

FM Academia

Mwanamuziki wa FM Academia King Blaise wa kwanza kushoto anaonekana walipokuwa kwenye onyesho kwa ajili ya vunja jungu huko Tabata, onyesho ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo. King Blaise alisemekana kutimlia Uholanzi (gonga hapa uisome) na baadaye habari toka kwa mshabiki nambari One wa FM Academia Big Producer Maghambo aliniahakikishia kuwa King Blaise atarudi na ataonekana jukwaani muda si mrefu na anakuja na Albamu yake (solo) inakwend kwa jina la Tumpokee Mfalme. (Picha na Muhidini Issa Michuzi).


Mambo ya Ngwasuma Miss Tanzania

August 4, 2008
Ngwasuma

Ngwasuma

Bendi ya FM academia kama kawaida usiku wa jana walipagawisha wadau mbalimbali kwenye shidano la kumtafuta Miss Vodacom Tanzania 2008 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam wakiongozwa na kiongozi wa Mkuu Nyoshi El-Sadaat wa kwanza Kulia pichani wakifanya vitu vyao jana. Picha na Haki Ngowi


%d bloggers like this: