Mahakama ya Biashara yatupa ombi la EATV

July 30, 2008
Ze Comedy wacheka kudadaadeki

Ze Comedy wacheka kudadaadeki

Pichani ni Kundi la Ze comedy wakishagilia kwa pamoja muda mfupi baada ya Mahakama kuu kutupilia mbali ombi la EATV dhidi ya kikundi hicho..
——–

Na Rabia Bakari wa gazeti la Majira

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imetupa maombi ya kituo cha televisheni cha EATV, ambao ni walalamikiwa katika kesi iliyofunguliwa na kundi la wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Ze Comedy ya kuiomba mahakamani itupe kesi dhidi yao kwani haina madai ya msingi. Read the rest of this entry »


Ze Comedy watinga Bungeni

July 15, 2008

Ze Comedy wakiwa katika moja ya maonyesho yao jijini.

Ze Comedy wakiwa katika moja ya maonyesho yao jijini.

Waigizaji wachekeshaji maarufu Ze Comedy jana walivamia ukumbi wa Bunge na kufanya kila mmbunge kutaka kuongea ama kupiga nao picha ya kumbukumbu.

Ilikuwa ni kipindi cha asubuhi cha Bunge kama kawaida Naibu Spika Mheshimiwa Anne Makinda alikuwa akisoma majina ya wageni waliokuwemo ukumbini humo kama ilivyoada na ndipo aliposhtuliwa kuwa miongoni mwa majina aliyosoma ni wanachama wa kikundi cha Ze Comedy na kushtuka na wabunge kulipuka kwa kicheko.

Kwa mujibu wa Naibu Spika kundi hili lilihudhuria kwa mualiko maalum wa wabunge wa majimbo ya mkoa wa Dar Es Salaam.

Nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya kipindi cha Bunge cha Asubuhi wabunge na maofisa wengine wa Bunge waliungana kwa pamoja na wasanii hao kwa maongezi ya hapa na pale na kupata picha kadhaa za kumbukumbu, Akiongea na waandishi wa habari kiongozi wa kundi hilo Wakuvanga alisema wameamua kwenda Dodoma ili kujua ni jinsi gain Bunge linafanya Kazi zake.

Miongoni mwa waliokuwepo ni Masanja, Joti, Mpoki na Seki.

Hivi karibuni serikali kupitia Wizara ya habari ilitoa tamko la kuingilia mgogoro uliopo kati ya kikundi hicho na tajiri yao wa zamani EA Television na kuagiza asasi zinazohusika kukaa pamoja na kulitolea maamuzi suala hilo haraka inavyowezekana.
Akiongea bungeni Naibu waziri wa Habari Utamaduni na Michezo bwana Joel Bendera alisema suala hilo limekabidhiwa kwa Chama cha Haki Miliki (Cosota) na kuongeza kuwa mkataba kati ya Ze Comedy na EATV umekwisha na kundi hilo limeingia mkataba mpya na TBC1 lakini wameshindwa kuendelea kwa sababu ya SAGA hilo. Spoti Starehe inawatakia kila la heri.


%d bloggers like this: